Ronaldo atoa msaada wa fedha kwa familia za wachezaji waliofia katika ajali ya ndege

fungi

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014
Posts
2,539
Reaction score
4,672
Bado dunia na ulimwengu wa soka kwa sasa unaomboleza msiba wa msafara wa timu ya Chapocoense ya Brazil uliyopata ajali wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege wa Medellin Colombia.

Ajali hiyo ya ndege imehusisha watu 81 kati ya hao 76 wamepoteza maisha huku 72 kati ya hao walikuwa ni sehemu ya msafara wa timu hiyo na wachezaji wakielekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa America dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia

Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya mastaa wa soka walioguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huu, Ronaldo ameamua kuchangia euro milioni 3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.6 kwa timu ya Chipacoense na familia za wachezaji wa timu hiyo waliyopoteza maisha.
 
Upendo safi sana . ..RIP kwa marehemu . ..
 
manchester UnitedOfficial have informed FIFA that they will donate €89M to Chapecoense
@FC Manchester cityofficial have informed FIFA that they will donate €390M to Chapecoense
Arsenal fc has informed FIFA and the Brazil Football Association that they will donate £67million to Chapecoense and the families of the victims
 
mkuu rekebisha hapo ni fainali ya kwanza klabu bingwa amerika ya kusini na sio afrika kama ulivyoandika wewe.
 
manchester city kiboko
wenger bahili kama kawaida yake
 
Ronaldo ana moyo wa kusaidia sana ..tena hio kwake ni kama buku tu alikua na uwezo wa kutoa zaidi
 
Halaf wenzetu bwana hawana longolongo na tamaa za kijinga kama kwetu afrika..hela ikitolewa zinaenda direct kwa wahusika kama ni familia zinaenda huko familia zote za wachezaji waliopoteza maisha zinakusanywa data zao za kibenki kwaio misaada ikija tu na information zinarushwa kwao ...kama ni timu basi zinaenda kwenye akaunt ya timu, ila ingekua huku kwetu zile 80 percent zinapigwa na wadau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…