Ronaldo: Barca inabebwa

Ronaldo: Barca inabebwa

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
LONDON, England
WINGA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema Barcelona ni klabu kubwa duniani lakini inaongoza kwa kubebwa.

Ronaldo anaungana na kocha wake, Jose Mourinho kuilaumu timu hiyo baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Camp Nou juzi.

Barca ilishinda mabao 2-0 mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Bernabeu huku beki wake, Pepe na kocha Mourinho wakipokea kadi nyekundu.

Madrid ilifunga bao kupitia kwa Gonzalo Higuain lakini lilikataliwa na Ronaldo alisisitiza kusema Barcelona si timu ya kutisha na kucheza katika kiwango chake.

"Hii ni mipango," Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.

“Tulijua mambo haya yatatokea. Tumekuwa tukiishi na vitu hivi. wamepora haki yetu kucheza fainali kwenye Uwanja wa Bernabeu. Hata hapa, mambo ni yale yale.

"Kuna vitu vingi. Vilivyotokea Bernabeu, vilivyotokea hapa, Ni vitu vya kutafakari. Barcelona ni klabu kubwa, lakini kuna vitu nyuma yake. Ni ngumu kucheza mkiwa 10 baada ya kadi nyekundu na Barcelona, leo hii unakataliwa bao."
 
Barca wanabebwa saana tu

kwa timu inayocheza kwa kiwango cha juu kama barca, their players always need to be protected by match officials. it's not a rule of thumb but it makes a lot of sportmanship sense!

mchawi wa r madrid ni mourinho mwenyewe. style aliyoi-impart kwa wachezaji wake ni kucheza negatively and kutumia a lot of muscles na kiugomviugomvi tu - which makes their football extremely ugly to watch whenever they meet the best.

tunaoijua r madrid from time memorial, pride and tradition ya bernabéu ni kushinda with style....so i can see Mourinho's kibarua kikiota nyasi next summer, for the true bernabéu faithfuls will never put up with his crappy approach!
 
Raha ya kubebwa kubebeki mwingine, hivyo barca uzuri wao wanapobebwa wanakunja miguu na kujilegeza/wakati mwingine wanaingia ndani ya mbeleko:bange:
 
With this, Barca won't win the title.
It's another time for Man U to shine on UEFA's champs final at Wembley.
 
Kweli wanabebwa kwnn walalamikiwe wao tu,tuliona kwa arsenal then r madrid uefa should explore this.
 
ni aibu kwa timu kubwa kama barca kubebwa...! waachwe wacheze kwa uwezo wao wakimbana na maadui wenye mbinu tofauti tuwaone ubora wao
 
Ndio tunabebwa
Uone aibu kwa kubebwa,huo ni ufisadi katika kabumbu,Barca wamekuwa kama wanashindia uji au mdebwedo wakiguswa tu chali chini kama mende,na kuanza kulia kuanzia mchezaji aliyejiangusha hadi kocha hadi kwa mashabiki wote hao hulazimishwa refa atoe adhabu,hiyo ni tabia mbaya hadi Mascherano nae kafundishwa kujirusha na kulia kulia kama mtoto,udume wote kaucha Liverpool sasa kawa mdebwedo
 
hahaaaaaaaa kazi ipo siku ya fainali

Mtachonga sana, lakini ukweli ni kuwa Barca ni Barcelona. Hakuna wa kumsimamisha!
 
sio mnazi wa real madrid per say lakini ukweli upo wazi kabisa BARSA WANABEBWA SANA TU.....!

BARSA WAMEUTIA DOA KUBWA SANA MCHEZO WA SOKA
 
Man U nao wanabebwa sana tu. Sasa tuone nani atakayebebwa zaidi Wembley.:third:
 
mtoto wa nyumbani lazima apewe kipaumbele ukizingati fainali

Hehehehe...haya bana..

Ukiangalia sana wanaochonga sana Real Madrid ni wareno Maurinho na C Ronaldo. Wanachonga sana hawa....Ingekuwa soka ni kuchonga, Ureno ingetawala soka la Dunia.
 
ha ha ha!
too personal!

na liverpool nayo inabebwa sana

Hehehehehe...Hatari sana hii...

Hii fainali ingefanyika O Trafford, Man U wangeuchukau ubingwa kilainiiiii.....lakini Wembley si mbali sana.... Sitashangaa wakibebwa...Tatizo linabaki...watabebeka?
 
Back
Top Bottom