kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
LONDON, England
WINGA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema Barcelona ni klabu kubwa duniani lakini inaongoza kwa kubebwa.
Ronaldo anaungana na kocha wake, Jose Mourinho kuilaumu timu hiyo baada ya kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Camp Nou juzi.
Barca ilishinda mabao 2-0 mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Bernabeu huku beki wake, Pepe na kocha Mourinho wakipokea kadi nyekundu.
Madrid ilifunga bao kupitia kwa Gonzalo Higuain lakini lilikataliwa na Ronaldo alisisitiza kusema Barcelona si timu ya kutisha na kucheza katika kiwango chake.
"Hii ni mipango," Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari baada ya mechi.
Tulijua mambo haya yatatokea. Tumekuwa tukiishi na vitu hivi. wamepora haki yetu kucheza fainali kwenye Uwanja wa Bernabeu. Hata hapa, mambo ni yale yale.
"Kuna vitu vingi. Vilivyotokea Bernabeu, vilivyotokea hapa, Ni vitu vya kutafakari. Barcelona ni klabu kubwa, lakini kuna vitu nyuma yake. Ni ngumu kucheza mkiwa 10 baada ya kadi nyekundu na Barcelona, leo hii unakataliwa bao."