fuateni ubatizo wa maji mengi, mtu azamishwe kama Yesu alivyobatizwa katika mto yordani. Enyi wakatoliki na walutheri ni nani aliyewaloga mbatize kwa maji kidogo?
Umekalili vibaya mnoo
Ngoja nikuulize maswali matatu ya ubatizo afu nyie wote mnaofanana mnijibu.
Kwanza ni kweli ubatizo ni neno la kigreek lenye maana ya kuzamishwa- kwa kiswahili kisicho fasaha sana.
Hata neno pentecoste mnalodhania ni siku ya Roho Mtakatifu maana ake ni siku ya 50.
Eti kanisa la kipentekoste, kanisa la kihamsini guys amkeni. Anyways hili tuliache.
Ubatizo wa maji mengi au machache ulianza kuwa practiced lini? Hapa kama hujui historia ya kanisa hutakaa uje ujibu hili swali. Hapa ni lazima usome Church Fathers au Apostolic Father lazma tena uwasome Apologetic Fathers. Otherwise huwezi jibu hilo swali.
Twende kibiblia maana utasema hayo ni mapokeo ila naomba twende polepole tujibu huu ubatizo ulikuwa wa aina gani.
1. Kuongoka kwa Sauli/ Paulo na kubatwa kwake. Nitanukuu...
Ukiweza soma Matendo 9 yote upate context.
Kisha Anania akaenda kwenye ile nyumba, akaingia ndani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.” Ghafula vitu kama magamba vikaanguka chini, kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa.
Matendo 9:17-18
Mwenye akili aniambie huyu Mtume Paulo alibatizwa mto gani hapo kwenye nyumba? Na je kama ubatizo ulifanyika kwenye nyumba maji yalikuwa madogo au mengi?
Kama ubatizo wa maji ya mtoni ungekuwa lazma huyu Anania angeongozana na wenzake kwenda mtoni na huyo kipofu sauli akambatize huko ila hilo halionekan apo.
2. Ubatizo wa Mrumi Kornelio
Na nukuu kama ilivoandikwa.
Kwa kuwa waliwasikia wakinena kwa lugha mpya na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akasema, “Je, kuna mtu yeyote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.
Matendo 10:46-48
Naomba jina la huu mto nyumban kwa huyu mtu wa mataifa.
3. Paulo na Sila kumbatiza askari wa gereza walimokuwa wamefungwa.
Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako.” Wakamwambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake. Wakati ule ule, yule mkuu wa gereza akawachukua, akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa.
Matendo 16:31-33
Hii familia ya huyu askari walienda kubatizwa mto gani?
Je. Maji yalikua mengi au madogo/machache?
Swali chokonozi. Ubatizo wa watoto wa dogo ni ruksa au sio? Maana hapo walibatizwa yeye na familia yake yote 😆 au hii familia haikuwa na watoto? Au kama walikuwepo mbona hatusikii wakisema watoto waliachwa hawakubatizwa?
Zingatia Jeografia ya Israel haina mito mingi tangu zamani hadi leo
Basi hii ni mifano michache kibiblia ambayo majibu unayo wewe msomaji