Ronaldo de Lima abatizwa na kuwa Mkristo!

Ronaldo de Lima abatizwa na kuwa Mkristo!

Mshambuliaji mashuhuri duniani Ronaldo de Lima amebatizwa katika Kanisa la Sao Jose do Jardim Europa Parish huko Sao Paulo.

Ronaldo de Lima ame post picha kwenye Instagram page yake na kusema "Imani ya Kikristo imekuwa msingi muhimu wa maisha yangu toka utoto ingawa nilikuwa sijabatizwa. Kwa sakramenti hii najisikia kuzaliwa upya kama mtoto wa Mungu kwa namna mpya, kihisia na kwa undani kabisa."

Hongera kwake kuamua kujikabidhi kwa Kristo.

Aisee
 
Usijali...huo ni mwili tuu...na mwili hauna manufaa yoyote mbinguni..

Ile roho ndio dhahabu ya mbinguni...au ww unahisi viwete wataenda mbinguni wakiwa viwete...acha hizo mkuu...

Maji mengi au kidogo haijalishi, mbinguni kwa Baba yake kuna makao mengi...ukiweza kufafanua hapo basi swala la yeye kunawa kichwa litafutika akilin mwako
Nini maana ya Ubatizo au Babtism?
 
kidogo kulinganisha na nini? Maji ni ishara, ubatizo upo rohoni (kwa moto na Roho Mtakatifu). Sisi mafundisho yetu yanaangalia context ya maandiko, sio word to word, ni vizuri ukajua maudhui. Hiyo ni hasara ya kila mtu kujiona anajua maandiko badala ya kwenda shule.

Sisi hata ikitokea mtu asiyewahi kubatizwa akatamka kuwa anaomba afanyiwe ubatizo, na bahati mbaya katika maandalizi ya ubatizo ikatokea amefariki, basi huyo anachukuliwa amepata ubatizo (kwa nia yake). Hapo hata maji ya mto au bakuli hayajatumika, ila anazikwa kama Mkatoliki aliyebatizwa
fuateni biblia katika ukamilifu wake, msichepushe uhalisia wake
 
fuateni ubatizo wa maji mengi, mtu azamishwe kama Yesu alivyobatizwa katika mto yordani. Enyi wakatoliki na walutheri ni nani aliyewaloga mbatize kwa maji kidogo?
Umekalili vibaya mnoo


Ngoja nikuulize maswali matatu ya ubatizo afu nyie wote mnaofanana mnijibu.


Kwanza ni kweli ubatizo ni neno la kigreek lenye maana ya kuzamishwa- kwa kiswahili kisicho fasaha sana.

Hata neno pentecoste mnalodhania ni siku ya Roho Mtakatifu maana ake ni siku ya 50.
Eti kanisa la kipentekoste, kanisa la kihamsini guys amkeni. Anyways hili tuliache.

Ubatizo wa maji mengi au machache ulianza kuwa practiced lini? Hapa kama hujui historia ya kanisa hutakaa uje ujibu hili swali. Hapa ni lazima usome Church Fathers au Apostolic Father lazma tena uwasome Apologetic Fathers. Otherwise huwezi jibu hilo swali.

Twende kibiblia maana utasema hayo ni mapokeo ila naomba twende polepole tujibu huu ubatizo ulikuwa wa aina gani.


1. Kuongoka kwa Sauli/ Paulo na kubatwa kwake. Nitanukuu...

Ukiweza soma Matendo 9 yote upate context.

Kisha Anania akaenda kwenye ile nyumba, akaingia ndani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani amenituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.” Ghafula vitu kama magamba vikaanguka chini, kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa.
Matendo 9:17‭-‬18


Mwenye akili aniambie huyu Mtume Paulo alibatizwa mto gani hapo kwenye nyumba? Na je kama ubatizo ulifanyika kwenye nyumba maji yalikuwa madogo au mengi?

Kama ubatizo wa maji ya mtoni ungekuwa lazma huyu Anania angeongozana na wenzake kwenda mtoni na huyo kipofu sauli akambatize huko ila hilo halionekan apo.


2. Ubatizo wa Mrumi Kornelio

Na nukuu kama ilivoandikwa.


Kwa kuwa waliwasikia wakinena kwa lugha mpya na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akasema, “Je, kuna mtu yeyote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.
Matendo 10:46‭-‬48



Naomba jina la huu mto nyumban kwa huyu mtu wa mataifa.


3. Paulo na Sila kumbatiza askari wa gereza walimokuwa wamefungwa.

Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako.” Wakamwambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake. Wakati ule ule, yule mkuu wa gereza akawachukua, akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa.
Matendo 16:31‭-‬33


Hii familia ya huyu askari walienda kubatizwa mto gani?
Je. Maji yalikua mengi au madogo/machache?

Swali chokonozi. Ubatizo wa watoto wa dogo ni ruksa au sio? Maana hapo walibatizwa yeye na familia yake yote 😆 au hii familia haikuwa na watoto? Au kama walikuwepo mbona hatusikii wakisema watoto waliachwa hawakubatizwa?


Zingatia Jeografia ya Israel haina mito mingi tangu zamani hadi leo

Basi hii ni mifano michache kibiblia ambayo majibu unayo wewe msomaji
 
fuateni biblia katika ukamilifu wake, msichepushe uhalisia wake
Kwani ubatizo wa Roho Mtakatifu na Moto alioutaja Yohana Mbatizaji, akasema huo ndio tutakaobatizwa na Kristo, haupo kwenye Biblia 'katika ukamilifu wake' unaousema? Yeye mwenyewe Yohana aliyebatiza kwa maji ya kwenye mto anakwambia waziwazi kuwa Yesu Kristo atawabatiza vingine, naye humuamini?
 
Porojo watu wanazidi kuingia kwa makundi.


Kila siku naweza kukuletea wapya hapa bongo tu wapo kibao ..


Porojo kibao naona umeumia tambua upo njia ya freemason jisalimishe na uingie kweny uislamu.
Mbona kuna makundi mengi tu ya watu wanaingi kwenye Ukristo kutoka huo uislam.Hakuna jambo la ajabu hapo.
 
Amemtaja Zakir Tena! Watu wasiomjua wameanza kumtafuta na kumjua ni nani zakri? Ajabu wamemkuta ni mtu mzuri, mwema na muongeaji mzuri kabisa.. muhubiri wa dini ya kiislamu mwenye kujuza uislam juu ya wale wasioujua..

Hapa umempiga chura teke kiongozi
Ni kawaida tu kama walivyokuwa kina Shekhe Aboud Rogo
 
Mkazikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo, ubatizo ni kuzika, au kuzamisha,kutosa kwa hiyo unaweza kujua ni maji kiasi gani yanahitajika,
Mbona huwa hamsulubiwi nae pia pale msalabani kama ndivyo hivyo ili tuone kweli mnafatisha kila kitu neno kwa neno? Au kwenye kusulubiwa ni pagumu mnaamua kuchagua tu kufuatisha kuzikwa/kuzamisha kwakuwa ni rahisi.
 
Kubatizwa ni kuzamishwa ndani ya maji yawe ya mto mfereji chemichemi au kisima.

Tofauti na hapo haya mengine ni mafundisho ya wanadamu na tamaduni za wazungu na kwa bahati mbaya ukirsto umeathiriwa sana na tamaduni za waUzungu.
 
Ubatizo gani huo? Alitakiwa abatizwe ubatizo wa maji mengi
Dini na maandiko vililetwa na wazungu, na ndio wanafanya hivo, eti mtu mweusi anajidai kujua kuliko aliyeanzisha hayo
 
Kubatizwa ni kuzamishwa ndani ya maji yawe ya mto mfereji chemichemi au kisima.

Tofauti na hapo haya mengine ni mafundisho ya wanadamu na tamaduni za wazungu na kwa bahati mbaya ukirsto umeathiriwa sana na tamaduni za waUzungu.
Before mzungu ni wapi mwafrika alikuwa na biblia yake na kusema kuna ubatizo wa maji mengi??
 
Kubatizwa ni kuzamishwa ndani ya maji yawe ya mto mfereji chemichemi au kisima.
Tofauti na hapo haya mengine ni mafundisho ya wanadamu na tamaduni za wazungu
Kuna nchi ambazo hazina hata mto. Lakini pia kuna maeneo ndani ya nchi ambayo mto upo umbali wa kutosha kutokea maeneo mengine. Hawa wanazamishwa wapi? Wafunge safari?
 
Wewe unataka battle za dini, kwenye ubatizo maji ni ishara tu na sio yanayotakasa. Hakuna andiko lolote linaloelekeza ubatizo uwe wa maji kiasi gani zaidi wengi mnakimbilia ku refer Yesu kubatizwa mtoni na maana ya ubatizo yaani kuzamishwa!

Kiasi cha maji hakijawahi kuwa issue toka enzi za mitume. Mkitoka kusema lazima yawe maji mengi itabidi tuulizane kiasi gani? Kwa maelekezo ya mapokeo au maandiko gani? Mkitoka hapo wengine watasema Yesu alibatizwa mtoni hivyo lazima ukabatizwe kwenye mto tu! Wengine watasema lazima uende mto jordan penyewe! n.k

Christianity sio imani ya juzi, tumepokezana miaka 2000 sasa kuanzia utaratibu wa ibada hadi masakramenti, you can't teach the church my friend! Hili sio Kanisa liloanzishwa na mtu tu.
Hakuna maji mengi kiasi chochote yanayoweza kusafisha roho! Naunga mkono, wingi au uchache wa maji siyo issue!
 
Back
Top Bottom