Ronaldo wa kombe la dunia kama mchezaji wa ureno anaonekana ni tofauti kabisa na yule Ronaldo wa EPL kama mchezaji wa Man U: Hii imekaaje?

Ronaldo wa kombe la dunia kama mchezaji wa ureno anaonekana ni tofauti kabisa na yule Ronaldo wa EPL kama mchezaji wa Man U: Hii imekaaje?

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Pamoja na ukweli kuwa R7 kwa sasa hana kasi yake ile ya zamani lakini Ronaldo wa kwenye kombe la dunia ameonekana kuwa tofauti sana na yule Ronaldo wa EPL kama mchezaji wa Man U.

Jana R7 kaibuka man of the match (mchezaji bora kwenye mechi)!!. Mchango wake kwenye mechi ulikuwa mkubwa sana ukiachilia mbali goli alilofunga kwa tuta!

Nadhani pamoja na kuwa na miaka 37, timu itakayomchukua bado ataifanyia makubwa kama watamheshimu na kumpatia nafasi!

1669360700136.png

1669360788452.png

1669360892668.png

Ronaldo na miaka 37 lakini bado anawakimbiza vijana ni hatari!! Ukiwauliza mabeki wa Ghana watakuambia Ronaldo msikiage tu!!
 
Haya ni mahaba yako yaliyokutopea kuhusu Ronaldo. Zaidi ya penati kuna kipi zaidi alichofanya?
Basi tuseme hiyo penati umefunga wewe!! Unachofumbia macho ni kuwa hiyo penalti ni yeye amefanyia faulo na mlinzi wa mwisho!! Alikuwa anaenda "kumsalimia" golikipa!! Penati haikushuka bure toka hewani!! ni jitihada zake!!
 
Haya ni mahaba yako yaliyokutopea kuhusu Ronaldo. Zaidi ya penati kuna kipi zaidi alichofanya?
Ni chuki yako kwa Ronaldo zinakufanya usione anachokifanya uwanjani!! Ila namba hazidanganyi! Ni mchezaji wa kwanza duniani kufunga katika kila kombe la dunia mfululiuzo michuano mitano ya kombe la dunia! Ni mchezaji mwenye magoli mengi zaidi ya kimataifa duniani!! Hata kama humpendi, rekodi zake zitakusuta!! Ni mchezaji wa pili kufunga goli kombe la dunia nyuma ya Roger Miller wa Cameroon (42 yrs)!! Kwa umri ule bado anatesa!!
 
Ni chuki yako kwa Ronaldo zinakufanya usione anachokifanya uwanjani!! Ila namba hazidanganyi! Ni mchezaji wa kwanza duniani kufunga katika kila kombe la dunia mfululiuzo michuano mitano ya kombe la dunia! Ni mchezaji mwenye magoli mengi zaidi ya kimataifa duniani!! Hata kama humpendi, rekodi zake zitakusuta!! Ni mchezaji wa pili kufunga goli kombe la dunia nyuma ya Geoge Weah (42 yrs)!! Kwa umri ule bado anatesa!!
george weah ajawahi kucheza kombe la dunia...
 
Man utd toka amestaafu alex ferguson imekuwa ni timu ya kuharibu viwango vya wachezaji wazuri

Pogba, mephis depay, lukaku, ronaldo, angel di maria, Harry Maguire , Aaron Wan-Bissaka, Anthony Martial, Eric Bailly na wengine kibao wameonekana wabovu kipindi wanachezea man utd ya baada ya ferguson
 
Pamoja na ukweli kuwa R7 kwa sasa hana kasi yake ile ya zamani lakini Ronaldo wa kwenye kombe la dunia ameonekana kuwa tofauti sana na yule Ronaldo wa EPL kama mchezaji wa Man U.

Jana R7 kaibuka man of the match (mchezaji bora kwenye mechi)!!. Mchango wake kwenye mechi ulikuwa mkubwa sana ukiachilia mbali goli alilofunga kwa tuta!

Nadhani pamoja na kuwa na miaka 37, timu itakayomchukua bado ataifanyia makubwa kama watamheshimu na kumpatia nafasi!

View attachment 2427016

View attachment 2427019

View attachment 2427024

Ronaldo na miaka 37 lakini bado anawakimbiza vijana ni hatari!! Ukiwauliza mabeki wa Ghana watakuambia Ronaldo msikiage tu!!
Hiyo mechi Kuna wachezaji wa Ureno walikiwasha kuliko Ronaldo, hiyo tuzo ya MOTM sijui huwa wanaangalia nn? Juzi KDB mwenyewe kashangaa kupewa wakat alikir mwenyewe kwamba hakuwa Na mchezo mzuri hata Modrick pia.
 
Katika tuzo za mchongo wakati mwingine ni pamoja na hii ya MOTM.
Mara nyingi huwa inatolewa kwa upendeleo kuelekea wale watu wenye majina makubwa.
Ikitokea mwenye jina kubwa akashiriki tukio lolote la ushindi hata kama ni mara moja tu basi nyie wengine tambueni hilo tuzo haiwahusu tena.
Watu wanaangalia biashara zaidi kwa sasa kuliko kitu kingine
 
Back
Top Bottom