Root simu ya android yoyote ukitumia magisk

Root simu ya android yoyote ukitumia magisk

Umefanikiwa kuroot?


  • Total voters
    24

Jury

Senior Member
Joined
Feb 6, 2018
Posts
196
Reaction score
153
MAANA YA ku-ROOT

ku-ROOT maana yake ni kuweza kupata uwezo au access ya system files zilizopo kwenye simu yako ambazo kwa kawaida zinakuwa zimejificha au kuzuiwa kwa mtumiaji ili asiweze kuzifikia , kwa kiingereza naweza kusema its an ability to obtain administrative access or rights on the file system of your phone. ku-Root simu yako sio dhambi ila pia kuna matokeo mazuri na mabaya lakini maranyingi matokeo huwa ni mazuri yale mabaya husababishwa na uzembe au mtu kuto fuata maelekezo anayopewa, Tunavyo root simu tunakuwa tunapewa uwezo wa ku-contol simu zetu katika kila upande, kwa mfano kama una simu ambayo ina internal GB4 pengine umeinstall baadhi ya applications tu simu yako ikajaa sasa ukiwa umesha root simu yako utakuwa una uwezo wa kuongeza nafasi katika simu yako na baadae ukaweza kuinstall apps ambazo zilishindikana wakati hauna root

JE NI MUHIMU KU-ROOT SIMU YAKO?
Jibu ni Ndio na Hapana, Kwa wanao penda utundu wa simu au customizations basi jibu ni ndio kwasababu kuna mengi unayakosa, ila kwa ambao wanatumia simu na wameridhika na wanachokikuta kwenye simu jibu ndi Hapana sio lazima,
Tunapo Root simu zetu tunafanya kitendo ambacho ni kinyume na makampuni walichotuwekea ndio maana unaambiwa uki root simu basi umesha futa warrant yako, ingawa kuna njia pia ya ku-unroot na warrant yako ikarudi lakini hilo litakuwa somo la siku nyingine...tufahamu kuwa waliweka uwezo wa ku-root haswa kwa wale "Developers" ambao wanafahamu madhara na mazuri ila kutokana na faida zake imekua ikitanuka siku baada ya siku na hatimaye hata kama hauna skills sana unaweza ukafanya.

FAIDA ZA ku-ROOT SIMU YAKO
Kuna faida nyingi sana katika swala la ku-rot simu yako, ila nitaongelea chache ambazo ni muhimu na nzuri

  • Uwezo wa Kuongeza nafasi ya simu yako na kusave uishaji haraka wa chaji

Ukijiuliza memory inaongezekaje unaweza usipate jibu ila jibu ni kwamba unapo root simu yako ule uwezo unaokuwa nao unaweza ukafuta Apps ambazo zimekuja na simu na ambazo zinakuawa hazifutiki sasa kwa mfano simu yako ina GB 8 internal lakini kwenye Apps wamekutengea GB 1 alafu OS nzima inachukua GB 4.5 alaf nafasi inayobaki ambayo ni 2.5GB inakuwa kwaajili ya miziki, videos, na mdeia files nyingine. Sasa ukiwa na root nafasi ambayo utafanikiwa kuongeza ni kutoka kwenye hiyo OS ambayo ina GB 4.5 kwasababu hiyo 4.5 imebeba apps ambazo zinakuwa pre-installed sasa unapokuwa na Root unakuwa na uwezo wa kuzifuta hizo apps ili upate nafasi mfano mzuri unaweza kuona simu hii ya samsung -:



sasa katika simu hii kama unavyoiona hapo juu, apps nyingi unaweza usiwe na umuhimu nazo kwahiyo ukiwa na root unaweza kuzifuta zote na kubaki na zile ambazo unazihitaji kutumia.


  • Uwezo wa kuremba simu yako ipasavyo

Hakuna kitu ninachopenda kwenye simu kama kuwa na uwezo wa ku customize muonekano wa simu ninayo tumia, njee mpaka ndani... Sasa ukiwa na root unaweza ukabadili muonekano mzima wa simu yako kama ni themes au baadhi ya shortcut kuzipaka rangi tofauti tofauti na kila siku unakua unaiona simu yako ni mpya bila kuichoka, tuongee ukweli kama simu yako imekaa namna fulani kilasiku unaiona hivyo hivyo nadhani utaichoka tu mapema, angalia mfano wa simu ambayo
Imekuwa customized muonekano mzima





Kama unavyoona hapo juu kuna rangi ambazo njano na hiyo background transparent ambayo ime affect hadi kwenye Apps kama instagram pia ukiona chini hapo katika Home, recent na back buttons zimebadilika zimekaa design kama ya windows 10, yote hayo na mengine mengi utaya pata uki-root simu yako..


  • Uwezo wa kuweka Custom-Roms

Kwanza Rom(Read-Only-Memory) ndio ambayo inatumika kuwekewa Operating system katika simu yako sasa Custom- Roms zinakuwa zina replace ile OS ambayo tayari ipo katika simu yako na hii ni kutokana na mambo mbalimbali ambayo yanakuwa limited katika OS ambayo imekuja na simu yako. Fahamu kuwa Custom Rom inatengenezwa na madevelopers ambao wanatoa sample za OS katika Android kwa sababu Android inafahamika ni Open source code, ikiwa ni open source code inamaana kuwa una uwezo wa kutumia code zinazopatikana katika Android na kuziongezea na kupunguza baadhi ya mambo mbalimbali.
Custom rom zina kazi nyingi sana ikiwemo kubadirisha muonekano wa simu yako pia upande wa speed za hapa na pale kama simu yako inakuwa slow hizo custom rom hua zina saidia kuboresha , pia baadhi ya apps zinakuwa designed kwa style nyingine kutegemea na aina ya Rom, pia kusaidia katika games ku perfom vizuri bila kusahau kusaidia upande wa Cpu na katika betri wengi hua wanatumia Custom roms kutokana na ukaaji wa betri kwa namna flan hua zina saidia ingawa sio zote.
Kikubwa zaidi watu wanapenda kuweka Custom roms kwasababu wanataka ku run ile update mpya ambayo inakuwa imetolewa na Google, kwa mfano makampuni ya simu baadhi wanakuwa wana deley kwenye ku-update simu zao OS mpya ikitoka kama vile kutoka Android 7 mpaka Android 8 simu ambazo zimetoka na Android 5 au 6 baadhi zitakuwa ngumu kupata Android 8 kwahiyo hapa ndipo unapotafuta Custom rom ambao wao wana uwezo wakukupandishia simu yako mpaka juu zaidi.

FAHAMU: Sio custom-rom zote utakazo ziona zinakuwa Stable, nyingine nyingi zinakuwa katika matengenezo ya kilasiku kwahiyo kama ni unapenda kuweka hakikisha unasoma maoni mbalimbali kuhusu hiyo Rom
Uwekaji wa rom kama hautafuata masharti unaweza kuua simu yako ikafa kabisaa kwahiyo unashauriwa kuwa muangalifu au kama sio mzoefu mtafute mzoefu akusaidie.



HASARA ZA KU-ROOT

Siwezi kusema kuwa kuna hasara sana kwenye ku-root simu yako, kwasababu kila hasara ina hepukika, Hasara mojawapo ni kama vile kupoteza warrant ya simu yako lakini uzuri ni kwamba unaweza ku nu-root na ukapata warrant yako kama kawaida ingawa sio kwa simu zote... Hasara nyingine ni kma usipokua muangalifu unaweza ukaaribu simu yako na isifanye kazi kabisa kikubwa hapa ni kuhakikisha unakua makini kila upande.

TUENDELEE...

Simu nyingi hasa zilizopo kwenye soko la Afrika mfano tecno hazina dedicated developers kwa ajili ya kutengeneza custom recovery kuwezesha kuziroot kwa njia rahisi pia ata apps zinazotengenezwa kwa kiasi kikubwa zimeshindwa. Hii imepeleke watu wengi wanaotamani kuziroot sim zao kushindwa kufanya hivyo.
Kuna njia kadhaa za kuweza kuroot ambazo ni,
-kupitia apps kama king root
-kupitia custom recovery
-kupitia magisk n.k

Nitaelezea njia ya magisk ambayo unaweza root simu yoyote ya android bila kutegemea twrp wala kuport stock image.

ANGALIZO
Rooting ni process ngumu inayoitaji angalau maarifa kidogo ya jinsi ya inavyotekelezwa.Kama huna uelewa wowote usifate njia hizi ninazoandika hapa maana Rooting inaweza fanya ukapoteza data zako,ukaua simu yako pia inavoid warrant yako.Sitahusika kwa lolote lile endapo utaharibu simu yako kwa kutofuata hatua hizi kwa makini.Hii ni kwa nia ya kujifunza.
Tuendelee...

Rooting kwa kutumia magisk
kuna hatua kuu mbili
1 Kupatch stock boot image kwa kitumia magisk manager
2 kuflash patched stock boot image kwenye simu husika

Requirements
1 Uwe na computer
1 Backup data za simu husika
2 Unlock bootloader ya simu husika
3 Download usb drivers za simu husika
4 Download adb and fastboot tools
5 Download stock boot image ya simu yako NB hii utaipata kwenye stock firmware hakikisha inaendana na build number ya simu husika


HATUA YA KWANZA: Kupatch stock image kwa kutumia magisk manager
• Download latest magisk manager kwenye simu husika ( latest version ni muhimu sana)
• hakikisha stock boot image uliyodownload hapo mwanzo iko kwenye internal storage ya simu husika
• fungua magisk manager na kisha bonyeza Install>Install> Select and Patch a file
kisha select stock boot image

Hapo tayari,Magisk manager itapatch iyo stock boot image na kuihifadhi ndani ya downloads folder kwenye internal storage ya simu husika

HATUA YA PILI: Kuflash patched boot image kwenye simu husika
• Hakikisha ume exctract na kusetup adb and fastboot kwenye computer yako baada ya kuidownload
• Hamisha patched boot image kutoka kwenye simu yako na uiweke ndani ya folder la adb and fastboot tools kwenye computer yako
• Unganisha simu husika kwenye computer via usb
• wezesha usb debugging kwenye simu husika
• Boot kwenda kwenye Bootloader

code
-adb reboot bootloader
• Flash patched boot image na kisha ireboot kwa kuandika code zifuatazo na kubonyeza enter baada ya kila mstari
Code:
fastboot devices
fastboot flash boot patched_boot.img
fastboot reboot

Verifiy root kwa kutumia app ya root checker
Simu itakua rooted na utaweza modify software kwa kitumia magisk module au kutumia apps zinazohitaji root access pia utaweza kutumia magisk hide kuzuia root access kwa apps
Utaweza kuinstall TWRP,Custom Rom,Custom themes,Incompatible apps n.k utaweza kubadilisha boot animation,boot image n.k,utaweza fanya overclocking,optimize perfomance n.k

Feel free kuuliza swali lolote kuhusu hii rooting procedure

Tuendelee...


3.png

Eboot.jpg


Best magisk modules kuwa nazo

• Magisk Manager for Recovery Mode
• EdXposed
3 3. Volume Steps Plus
• Viper4Android FX
• CloudflareDNS4Magisk
• Camera2API enabler
• YouTube Vanced Magisk Module
• Universal GSM Doze
• App Systemizer
• Google Dialer Framework
Sony Device Dummy
xmplak
Disable Screenshot and Camera sounds
Audio Modification Library
Pixel Experience Magisk Module
ARISE Magnum Opus
Xposed Framework
 
kwa kingroot tulikuwa tunagusa mara moja tu,kitu imooo.

siku hizi ni kama watu wanapuuza hivi baada ya kuhitajika computer.hatua zimekuwa nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Now tuko android version ya 10,Kuanzia android version ya 5 apps za kuroot sio tegemeo tena vitu vimekua complicated hawadevelop recovery kwa simu zisizojulikana na kama zipo ni chache sana.

Android Version za zamani zilikua open Sana hazikua tight kwenye swala la ulinzi ndio maana ilikua kugusa tu

Njia pekee ya uhakika kama hamna custom recovery ya simu yako ni kupitia magisk
 
Ukitaka kuroot simu yako hakikisha umetenga kapesa ka kununua simu nyingine incase things go array.

Unforgetable
Cha msingi ni kuwa makini na kufata hatua zote bila kufoji ni makosa madogo madogo sana yanayopuuzwa hupelekea kubrick simu
 
Yes mkuu pia nmeipenda inakuja moja kwa moja na magisk hide....zile apps zisizo taka root ndio zimepigwa mtama
Acha kabisa Asee hii kitu upande wang ndio the best rooting method sababu kubwa ni modules zake pamoja na kua systemless kwamba haichange partition ya simu ivo baada ya kufanya tweaks unaweza unroot muda wowote bila shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes mkuu pia nmeipenda inakuja moja kwa moja na magisk hide....zile apps zisizo taka root ndio zimepigwa mtama

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah future nzur san pamoja na kuwa na uwezo wa ku Pass Google’s SafetyNet tests baada ya kuroot simu ivo kupelekea kuwa na uwezo wa kuinstall banking na security apps pia kupokea OTA updates
 
NIMEKUWA NIKISIKIA KU-ROOT SIMU LAKINI SIJAWAHIJUA INA MAANA IPI NA INAONGEZA AMA KUPUNGUZA NINI KWENYE SIMU.

NIFUNGUENI HIKI KIFUNGO CHA UJINGA TAFADHALI

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu hili hapa
MAANA YA ku-ROOT

ku-ROOT maana yake ni kuweza kupata uwezo au access ya system files zilizopo kwenye simu yako ambazo kwa kawaida zinakuwa zimejificha au kuzuiwa kwa mtumiaji ili asiweze ...
 
Back
Top Bottom