Rose Mhando: Meneja wangu anataka kuniua

Rose Mhando: Meneja wangu anataka kuniua

Hivi ni kitu gani kipo nyuma ya pazia kuhusu mtumishi wa Mungu Rose Muhando?

Ukitazama video hii, Rose anaropoka maneno ya kutisha.

Je, ni kweli kwamba waimbaji wa Injili wanaishi maisha ya kutisha namna hii?


Aliekuambia Rese Mhando ni mtumishi wa Mungu nani?
 
Sifa na utukufu ni kwako Bwana Yesu. Hakika Yesu unastahili kuabudiwa wewe pekee. Ila baaada ya kuangalia hii video kuna vitu vimenichanganya. Kabla ya kuangalia hii video, nilikuwa nafahamu kwamba mtu akiwa anafanyiwa au kutolewa mapepo huwa anakuwa sio yeye tena au hajitambui. Pia mara nyingi huwa anakuwa hana ufahamu wa mambo yanayo endelea kwenye zoezi zima, ndio maana mara nyingi watu wanao pagawa mapepo ujirusha rusha wengine paka wana jijeruhi basipo kujuwa. Wengine uchana mavazi na kubaki uchi pia hata kupigana na kutukana watumishi wa Mungu pasipo kufahamu.

Ukiangalia hii video, kuanzia 0.22 paka 0.23 unaweza kuona kama Rose anajaribu kushusha gauni au nguo chini kujisitiri. Tena 1.45 paka 1.48 Unaweza kuona kama mchungaji anamkandamiza kwa nguvu Rose mdomoni, lakini Rose anajaribu kumwondoa mkono mchungaji. nadhani hii ni ishara kwamba " tafadhali unaniumiza". Pia 2.00 paka 2.01 kuna mhudumu amemtupia Rose kitu kama khanga, alafu Rose akajaribu kama kuivuta kwa juu ili kujisitiri. Baada ya kusema hivyo, sina shaka dada yetu Rose alikuwa anajielewa kwenye zoezi zima. Je kitu kama hichi kinaweza kutokea? mtu kupagawa mapepo na wati huo huo kujitambua!

Nakaribisha watumishi wote na watu wenye uwelewa kwenye hii mada.
Mkuu Mkimagii, kama sio mwanasheria, unapaswa kuwa mwanasheria, mwandishi wa habari za investigative journalism or mwana saikolojia, Una kipawa au kipaji cha observation into little details, japo wote tumeona hiyo video clip, ni wachache wake observers details, hiyo inatokana na kuwa na IQ kubwa. Baada ya kukuona ndio nimeangalia tena nikaona.
Thanks for your observations
P
 
Mh, Rais kwanza natanguliza shukrani kwa kuwajali wasanii wetu kwa Taifa hili ahsante kwa mchango wako kwa Ruge wa Clouds ahsante kwa Wastara Juma.

Mh, Rais naleta ombi langu maalum kwa ajili ya Rose muhando. Tunajua ana mapungufu yake mengi sana kama Mwanadamu, tunafahamu amefanya mengi ya kufedhehesha, lakini Mh Rais

Dada huyu ni kioo kwa Taifa letu, ni nyota kutokea Tanzania popote atakapokuwa ama kwa wema au ubaya Jina la Nchi yetu linatajwa, Mfano niandikapo ujumbe huu kwako niko Nje ya Tanzania, kila gazeti limeandika "A star from Tanzania.."

Mh, nakuomba tusaidie kumvalisha nguo huyu dada, anapodharirika sisi pia kama Taifa tunadharirika, alipokuwa na sifa njema, nje ya mipaka yetu sisi pia kama Taifa tulipata Sifa njema.!

Mh, Rais Tafadhari nakuomba Mvalishe nguo Dada yetu. Huenda mamlaka yako ikasaidia janga hili, na wale walio nyuma ya Mchezo huu. Natumai hatua za kisheria zaweza kutumika kwao.
Ahsante nawasilisha..
Ihusike kwa Mh WHUM.
Ndugu Harrison Mwakyembe..
 
Ni muda mrefu sana huyu mwimbaji wa nyimbo za injili yuko kimya na hasikiki tena kwenye game, lakini juzi tu nimekutana na hii video kwenye group moja la WhatsApp.
Je kuna ukweli wowote katika video hii?
Naomba kwa anayefahamu alipo msanii huyu kwa sasa na maisha yake kwa ujumla atueleze na kama kilichoonekana kwenye hii video ni kweli.View attachment VID-20181121-WA0000.mp4
 
Ni muda mrefu sana huyu mwimbaji wa nyimbo za injili yuko kimya na hasikiki tena kwenye game, lakini juzi tu nimekutana na hii video kwenye group moja la WhatsApp.
Je kuna ukweli wowote katika video hii?
Naomba kwa anayefahamu alipo msanii huyu kwa sasa na maisha yake kwa ujumla atueleze na kama kilichoonekana kwenye hii video ni kweli.View attachment 942330
Wakija nitag mkuu
 
Ni Kweli Mkuu.
Ameshambuliwa na Roho Chafu.
Ndio maana humwoni kwenye anga zake za mziki wa dini akifanya kazi.
Mara ya mwisho amethibitika akiwatapeli pesa waliokuwa wakimwalika kufanya matamasha au kuimba.
Na pia ameonekana akiishi maisha ya siyo ya Kikristo.
Alijiinua Juu na kujiona.
Wakristo wakamsusa kufanya naye kazi za dini.
Akaanguka peke yake bila msaada kwa walimu wake.
Ndipo alipofungua mlango wa kuingiliwa na Pepo wachafu au Majini.
Anahitaji msamaha kwa wote aliowaudhi.
Anahitaji msaada tena ili akae sawa.
Arudi kuomba msamaha na msaada atasaidiwa kama atajinyenyekesha na kujishusha na kuwa mwaminifu kama zamani.
 
Hivi ni kitu gani kipo nyuma ya pazia kuhusu mtumishi wa Mungu Rose Muhando?

Ukitazama video hii, Rose anaropoka maneno ya kutisha.

Je, ni kweli kwamba waimbaji wa Injili wanaishi maisha ya kutisha namna hii?

Unamzungumzia huyu rozi aliyehama kwa Yesu akahamia ccm?
 
Inavyomekana huyo Rose Mhando kapelekwa hapo kwa ajiri ya maombi kutokana na situation aliyokuwa nayo,i si yeye kajipeleka hapo, ila huyo jamaa ni tapeli tu, na ndio maana analazimisha mambo.
Naunga mkono hoja, kikawaida mtu mwenye mapepo, akiombewa na kugalagala, akitulia ni yametoka, nimenote Rose alitulia, yakawa kama yametoka, lakini alipoongea akaonekana kama bado yapo.

Halafu kuna kitu kama alikuwa anapuliziwa..
Haya mambo ya wahubiri wa miujiza tumeyazungumza sana humu
Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo! Adai yeye ni zaidi ya Rais... - JamiiForums

Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians! - JamiiForums

Vijana Waahidiwa Utajiri Kwa Shurti la Kuweka Agano la Kutohama Efata-Mtume na Nabii Mwingira!. - JamiiForums

Wosia wa Ask. Moses Kulola kwa Watanzania: Tuchague Rais kwa Kigezo cha Sifa Zake na sio Dini yake! - JamiiForums

P
 
Kila mtu anamapungufu yake,mi naona apewe tena mama yetu Rozi nafasi tena jamani ya kuihudumia jamii!
 
Pastor Nga'nga!!![emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]......kamutoa mapepopo
 
Tatizo la waimbaji injili wanapoinuliwa hujawa kiburi cha uzima. Wanakuwa na dharau kwa viongozi wao wa kiroho.Anguko lao ni baya sana. Ila si vema kufurahi juu yao waangukao maana wanaweza kuinuka tena wakiomba msamaha kwa makosa wanaowatendea watu wao
 
Mkuu Mkimagii, kama sio mwanasheria, unapaswa kuwa mwanasheria, mwandishi wa habari za investigative journalism or mwana saikolojia, Una kipawa au kipaji cha observation into little details, japo wote tumeona hiyo video clip, ni wachache wake observers details, hiyo inatokana na kuwa na IQ kubwa. Baada ya kukuona ndio nimeangalia tena nikaona.
Thanks for your observations
P

Nashukuru kaka ubarikiwe.
 
Hivi ni kitu gani kipo nyuma ya pazia kuhusu mtumishi wa Mungu Rose Muhando?

Ukitazama video hii, Rose anaropoka maneno ya kutisha.

Je, ni kweli kwamba waimbaji wa Injili wanaishi maisha ya kutisha namna hii?


I saw this and I cried, and have been emotional for Everytime I have watched it, Rose Muhando a servant of God whose Music brought so much Joy to us, through his Music many sought God, the messages she delivered through her song epitomizes what preaching through song is.
you may be down but not out,
may God's love and Kindness locate you, May you rise again.
#UtavumaTena
 
Back
Top Bottom