Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’

Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
3,367
Reaction score
4,067
DUA zinahitajika kutokana na madai kwamba, nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’, Vyanzo vya habari vimedokezwa.

Chanzo makini kutoka nchi hiyo jirani kilieleza kuwa, hali ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kibao kama Nibebe, Nipe Uvumilivu na nyingine nyingi kwa sasa yupo hospitali akisumbuliwa na maradhi ikiwemo mikono inayotajwa kuwa imeharibika. Kilieleza kuwa, baada ya Rose kushindikana kupata nafuu kanisani alikokuwa anafanyiwa maombi, mwenyeji wake ambaye naye ni mwimbaji wa injili pamoja na wenzake walimpeleka hospitali (haikutajwa) kwa tiba zaidi.

“Kwa sasa yupo ICU huku Kenya ambapo suala la afya yake liko mikononi mwa baadhi ya waimbaji Injili wa huku ambao wamekuwa wakifanya siri ili watu wasijue kama Rose kalazwa. “Ukweli haujulikani kalazwa hospitali gani, lakini kuna madai kuwa ameathiriwa sana na madawa ya kulevya hivyo wanahofia wakitaja jina la hospitali kila mtu atajua chanzo cha kuumwa kwake.

“Mimi nimeambiwa kinachomsumbua ni mikono ambayo hata kwenye video iliyosambaa hivi karibuni mitandaoni ilionekana kama imeungua moto, yapo madai kuwa mikono imeanza kuoza na hawezi kufanya kitu chochote,” kilidai chanzo. Inaelezwa kwamba, hapo hospitali ameambiwa atakaa kwa siku 30 kwa ajili ya matibabu na ushauri, hivyo hawezi kurudi Tanzania hadi apate nafuu.

Ili kuujua ukweli wa habari hizo,chanzo hicho Cha habari kilimtafuta kiongozi wa chama cha waimba Injili cha Tanzania Music Foundation ‘TAMUFO’, Stella Joel ambaye alisema, wamesikia taarifa hizo za kulazwa kwa Rose lakini wao kama chama wanafuatilia zaidi. “Tumesikia Rose amelazwa Kenya hivyo tunafuatilia na tukishapata ripoti kamili tutatoa taarifa zaidi,” alisema Stella.

TUJIKUMBUSHE

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha Rose akiwa amedhoofu mwili huku mikono na uso vikiwa kama vimeungua moto ambapo mchungaji alikuwa akimuombea na Rose kuonekana amepagawa na mapepo.
Hujafa hujaumbika...
 
pale unapoumwa Ebola halafu unaenda kanisani kuombewa upone Kifafa.
 
Rose harafu uniambie kiongozi wa dini anawezaje saidi wafuasi
 
Drug barons. Sasa mnachekelea ? Hela yake imeishia kwenu sasa mnammaliza na mwili
 
Kwahiyo yale maombi ya mchungaji ndo kusemaje?[emoji56]
 
Hivi ule mkataba na Sony uliisha wadau?Maana ndipo alipoanza kujichanganya
 
Amkubali Yesu Kristo kikamilifu, aachane na ustaa.

Wamemtumia sasa wamemuacha ili ateseke.

We love you Rozi but Jesus Christ anakuhitaji mno.

Mungu akuponye dada yangu.
 
akipata nafuu awaambie nduguze yeye ni dini gani maana story zimekua mingi sana.
 
Mungu akuponye dada Rose

Such a good woman, moyo wa upendo, moyo wa kujali wengine kuliko hata kujijali wewe
Muda wote unatabasamu kumbe ulikuwa unawachekea mashtwani yaliyotaka kukuangamiza

Feel so disapointed
 
Back
Top Bottom