Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hii source ni ya moja ya gazeti la global publishers?DUA zinahitajika kutokana na madai kwamba, nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’, Vyanzo vya habari vimedokezwa.
Chanzo makini kutoka nchi hiyo jirani kilieleza kuwa, hali ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kibao kama Nibebe, Nipe Uvumilivu na nyingine nyingi kwa sasa yupo hospitali akisumbuliwa na maradhi ikiwemo mikono inayotajwa kuwa imeharibika. Kilieleza kuwa, baada ya Rose kushindikana kupata nafuu kanisani alikokuwa anafanyiwa maombi, mwenyeji wake ambaye naye ni mwimbaji wa injili pamoja na wenzake walimpeleka hospitali (haikutajwa) kwa tiba zaidi.
“Kwa sasa yupo ICU huku Kenya ambapo suala la afya yake liko mikononi mwa baadhi ya waimbaji Injili wa huku ambao wamekuwa wakifanya siri ili watu wasijue kama Rose kalazwa. “Ukweli haujulikani kalazwa hospitali gani, lakini kuna madai kuwa ameathiriwa sana na madawa ya kulevya hivyo wanahofia wakitaja jina la hospitali kila mtu atajua chanzo cha kuumwa kwake.
“Mimi nimeambiwa kinachomsumbua ni mikono ambayo hata kwenye video iliyosambaa hivi karibuni mitandaoni ilionekana kama imeungua moto, yapo madai kuwa mikono imeanza kuoza na hawezi kufanya kitu chochote,” kilidai chanzo. Inaelezwa kwamba, hapo hospitali ameambiwa atakaa kwa siku 30 kwa ajili ya matibabu na ushauri, hivyo hawezi kurudi Tanzania hadi apate nafuu.
Ili kuujua ukweli wa habari hizo,chanzo hicho Cha habari kilimtafuta kiongozi wa chama cha waimba Injili cha Tanzania Music Foundation ‘TAMUFO’, Stella Joel ambaye alisema, wamesikia taarifa hizo za kulazwa kwa Rose lakini wao kama chama wanafuatilia zaidi. “Tumesikia Rose amelazwa Kenya hivyo tunafuatilia na tukishapata ripoti kamili tutatoa taarifa zaidi,” alisema Stella.
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha Rose akiwa amedhoofu mwili huku mikono na uso vikiwa kama vimeungua moto ambapo mchungaji alikuwa akimuombea na Rose kuonekana amepagawa na mapepo.
Hujafa hujaumbika...
Mimi nimeambiwa kinachomsumbua ni mikono ambayo hata kwenye video iliyosambaa hivi karibuni mitandaoni ilionekana kama imeungua moto, yapo madai kuwa mikono imeanza kuoza na hawezi kufanya kitu chochote,” kilidai chanzo. Inaelezwa kwamba, hapo hospitali ameambiwa atakaa kwa siku 30 kwa ajili ya matibabu na ushauri, hivyo hawezi kurudi Tanzania hadi apate nafuu.
Drug abuse inawezaje kufanya mikono ipate matatizo Mr King Kong LA familia?Kwasasa yupo strong ila kweli mikono kama imeungua flani hivi ila ipo active.
Drug abuse inawezaje kufanya mikono ipate matatizo Mr King Kong LA familia?
Chidi benzi sauti yake dhaifu?La Familiaaaa ILALA ILALA Mikono Mfululu yaani Pa papa papaaa wamekaaaaa!!! Atakuwa alikuwa na shida nyingine na wala sio Unga!!! Sauti yake ni strong ambayo inaonyesha haijawahi kupitisha VILEVI vya aina yeyote!!
Huyu ana ugonjwa wake wa siku zote anausema kwa kila mtu. Akiongeza comment lazima autajeChidi benzi sauti yake dhaifu?
Whitney Houston?
Amy Winehouse?
Na walikua hawajapitisha vilevi vya aina yeyote?
Yeye Na Genta sio?Huyu ana ugonjwa wake wa siku zote anausema kwa kila mtu. Akiongeza comment lazima autaje
Chidi benzi sauti yake dhaifu?
Whitney Houston?
Amy Winehouse?
Na walikua hawajapitisha vilevi vya aina yeyote?
Pigia mstari. Ni sawa na Gsam yeye kila anayekufa anadai ni coronaYeye Na Genta sio?