Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’

Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’

Ombi langu mh Rais tunaomba msaidie mwimbaji wa injili aweze kurudia hali yake msaidie kwa matibabu tunaambiwa hali yake hairidhishi

Dada rose ameitangaza sana hii nchi anastahili msaada wako mh Rais naamini kwa moyo wako wa upendo utamsaidia
 
Mungu amponye kwakweli huyu anahitaji counseling na rehab ya hayo madawa ya kulevya
 
Wachungaji wa siku hizi wanajua kuombea mapepo tu.. Sio magonjwa.
Hivi wajua hata kifo ni kupona pia? Ndo maana tunasema R,I,P usiwalete wachungaji humu kwenye madawa ya kulevya. Unataka kuniambia kuwa utaenda kunywa sumu kwa sababu upo karibu na kanisa ili uje kuombewa? Waza kabla hujaandika
 
Wachungaji wa siku hizi wanajua kuombea mapepo tu.. Sio magonjwa.
Unajua pepo likishakuingia huwa linacheza na akili yako tu huwenda lilikuwa linamzuia kwnda rehabu mapema kwahiyo kuombewa sio ndio kupona ni hatua ya kwanza ya kupona
 
Mungu akuponye dada Rose

Such a good woman, moyo wa upendo, moyo wa kujali wengine kuliko hata kujijali wewe
Muda wote unatabasamu kumbe ulikuwa unawachekea mashtwani yaliyotaka kukuangamiza

Feel so disapointed
Ndiyo ajue kuwa 'Ngada'si glucose!
 
Hivi ule mkataba na Sony uliisha wadau?Maana ndipo alipoanza kujichanganya
Yeah ni kweli hapo ndo alipoanza kuiimbia Album(hela) lakini Bado Mungu ni mwaminifu atamsadia Rose
 
Dr. Mwakiembe na kampeni ya kutetea maslahi ya wasanii Kanumba, Majuto and the like imefia wp?
 
uuutamaduni wa kibongo ni kuwa awakuchangiii ukiwa hai,ukiwa mgonjwa watatamani wakuongezeee mzigo mwingine wa ugonjwa,mgonjwa akifa watabuni project ya kupiga pesa kama tshet na makofia huku wakiweka ringtone ya wimbo wa WIZ KHALIFA WA SEE YOU AGAIN,kwa uhalisia rose ajiombeee tu mwenyew asiwategeemeee hawa wanafiki
 
So where's Jesus Christ to save her now?
 
DUA zinahitajika kutokana na madai kwamba, nyota wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amelazwa hospitalini nchini Kenya, katika chumba cha uangalizi maalum ‘ICU’, Vyanzo vya habari vimedokezwa.

Chanzo makini kutoka nchi hiyo jirani kilieleza kuwa, hali ya mwanamuziki huyo aliyewahi kutamba na nyimbo kibao kama Nibebe, Nipe Uvumilivu na nyingine nyingi kwa sasa yupo hospitali akisumbuliwa na maradhi ikiwemo mikono inayotajwa kuwa imeharibika. Kilieleza kuwa, baada ya Rose kushindikana kupata nafuu kanisani alikokuwa anafanyiwa maombi, mwenyeji wake ambaye naye ni mwimbaji wa injili pamoja na wenzake walimpeleka hospitali (haikutajwa) kwa tiba zaidi.

“Kwa sasa yupo ICU huku Kenya ambapo suala la afya yake liko mikononi mwa baadhi ya waimbaji Injili wa huku ambao wamekuwa wakifanya siri ili watu wasijue kama Rose kalazwa. “Ukweli haujulikani kalazwa hospitali gani, lakini kuna madai kuwa ameathiriwa sana na madawa ya kulevya hivyo wanahofia wakitaja jina la hospitali kila mtu atajua chanzo cha kuumwa kwake.

“Mimi nimeambiwa kinachomsumbua ni mikono ambayo hata kwenye video iliyosambaa hivi karibuni mitandaoni ilionekana kama imeungua moto, yapo madai kuwa mikono imeanza kuoza na hawezi kufanya kitu chochote,” kilidai chanzo. Inaelezwa kwamba, hapo hospitali ameambiwa atakaa kwa siku 30 kwa ajili ya matibabu na ushauri, hivyo hawezi kurudi Tanzania hadi apate nafuu.

Ili kuujua ukweli wa habari hizo,chanzo hicho Cha habari kilimtafuta kiongozi wa chama cha waimba Injili cha Tanzania Music Foundation ‘TAMUFO’, Stella Joel ambaye alisema, wamesikia taarifa hizo za kulazwa kwa Rose lakini wao kama chama wanafuatilia zaidi. “Tumesikia Rose amelazwa Kenya hivyo tunafuatilia na tukishapata ripoti kamili tutatoa taarifa zaidi,” alisema Stella.

TUJIKUMBUSHE

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimuonyesha Rose akiwa amedhoofu mwili huku mikono na uso vikiwa kama vimeungua moto ambapo mchungaji alikuwa akimuombea na Rose kuonekana amepagawa na mapepo.
Hujafa hujaumbika...
aaaah
 
Ombi langu mh Rais tunaomba msaidie mwimbaji wa injili aweze kurudia hali yake msaidie kwa matibabu tunaambiwa hali yake hairidhishi

Dada rose ameitangaza sana hii nchi anastahili msaada wako mh Rais naamini kwa moyo wako wa upendo utamsaidia
aaaah mbona uongo jamaani
 
Amkubali Yesu Kristo kikamilifu, aachane na ustaa.

Wamemtumia sasa wamemuacha ili ateseke.

We love you Rozi but Jesus Christ anakuhitaji mno.

Mungu akuponye dada yangu.
Kiaje? Mumwambiw Msami ndio amkubali Mungu
 
Back
Top Bottom