Rose Muhando: Nafikiria kurudi kwenye Uislamu

Rose Muhando: Nafikiria kurudi kwenye Uislamu

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi' wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.

Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

"Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti' tu.

"Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja," alisema Rose.

Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.


Chanzo: GPL
 
Hajashiba din huyo hayo ni majaribu mpango wa mungu unataka utimie
 
Japo siamini chanzo cha habari lakini kuna ukweli kuwa Rose amekuwa tapeli na sio mara moja.
 
Naamini alikuwa kafungua duka sasa kaamua kufunga duka lake yupo sawa kwanza hakumfuata mungu wa kweli alienda Kwa kuahidiwa upendo wa kibinadamu sasa kaukosa bora arudi Kwa mungu asie na shaka ndani yake na mungu atamsamehe yote aliyomkosea baada tu ya kurudi na kumuomba msamaha
 
Hili Gazeti liliuza sana,na yeye sijui alipewa kiasi gani.
 
Back
Top Bottom