Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Rose Muhando, ametoa msimamo mkali na kuwakosoa wasanii wa Injili wanaofanya kazi za muziki na wasanii wa muziki wa dunia au Bongo Fleva.
Kauli hii imekuja mara baada ya kuwepo kwa mjadala mkali mtandaoni uliochochewa na hatua ya mwimbaji wa Injili, Joel Lwaga, kufanya wimbo wa ushirikiano na nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Mjadala huo uliosema na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Instagram, umeibua maoni tofauti kati ya mashabiki wa muziki wa Injili na Bongo Fleva.
Akieleza sababu za msimamo wake, Rose Muhando amebainisha kuwa lengo kuu la mwimbaji wa Injili linapaswa kuwa kumtumikia Mungu na kulinda huduma yake badala ya kusaka views na umaarufu wa muda mfupi.
Alisisitiza kuwa kabla ya msanii kuchukua hatua ya kufanya kolabo kama hiyo, anapaswa kushauriana na mchungaji wake wa kiroho au kuongea na Mungu.
Rose aliongeza kuwa yeye mwenyewe amewahi kufuatwa na wasanii wengi wa kidunia wakitaka wafanye naye wimbo, lakini Mungu alimkataza na hawezi kukiuka katazo hilo kwa namna yoyote ile.
Kupitia ujumbe wake huo, Rose alieleza namna anavyoipigania huduma yake kwa kusema:
"Mimi nalinda huduma yangu kwa gharama yoyote na sifanyi ili nipate views nyingi na umaarufu bali kumtumikia MUNGU."
Alitamatisha kwa kutoa tahadhari kuwa ingawa views na umaarufu vinaweza kupatikana kwa muda kupitia kazi hizo, msanii anayeingia kwenye kolabo hizo anajikuta akiwapoteza na kuwajaza mashaka wale waliomwamini na kumfikisha hapo alipo tangu mwanzo.