Rose Shirima hana kosa lolote, mwenye Makosa ni James Getogo kuibua makosa ya serikali/mwajiri wake

Kwenda huko maadili ya kazini hata uwe provoked vipi lazima uzingatie

Ndio maana private sector huwa kuna swali interview unaukizwa kuwa una uwezi wa kufanya kazi independently kwenye stressful condition?

Serikalini mnaleana sana wajinga nyie

Pili kum record mtu anayepanga mauaji ya mtu mwingine sio kosa .Huyo nesi alitaka vipimo vibovu vitumike ni muuaji huyo kamera za siri zilizofanya kazi hongera kwa wapigaji hizo picha za siri

Mtu anapanga luua mtu halafu unamwambia na kurekodi mipangi yako hakuna kitu kama hicho.Hongera kwa aliyerekofi
 
Huyo jamaa kavunja masharti ya mkataba yanayotakiwa utunze siri za kazi yako
 
James ana kosa kwann hakwenda kwa in charge kama alivyoelekezwa na Rose ili kupata ufumbuzi? Ila James alichofanya ni kumuudhi mwenzake tu ili amrekodi vizuri kutokana na tofauti zao kimtazamo. Mwaka huu naona ni wakusagiana kunguni tu.
 
Kosa la rose ni lipi?
Unajua ni mambo mangapi yanayofanyika kwenye nchi hii yanayohatarisha usalama wa Watu kisa umaskini wetu?
Au Kwa vile Rose karekodiwa tena bila ya kujua na aliyemrekodi ni mfanyakazi mwenzake
ni mambo mengi ndio yanafanyika,
lakini mambo yakiwa hadharani kama yalivyokuwa ya rose basi lazima hatua zichukuliwe,,hebu acha kutetea ujinga
 
We leo umekuwaje? Umelogwa siyo bure. Unataka kunifanya nianze kutia shaka makala zako ambazo mimi ni mfuatiliaji. Au una interest na huyo Rose? Umetoa wapi ujasiri wa kumtetea firauni km Rose? Unakatisha tamaa watumishi wazalendo. James amefanya jambo la kishujaa apongezwe. We na mimi tungejuaje ushenzi ule bila James au mtu mwingine kuufichua? Kuna jamaa moja alikuwa anakaimu nafasi ya ukuu wa chuo cha ufundi Arusha alirekodiwa na mtumishi wakiwa kwenye gari ya mkuu wa chuo akimkashifu Magufuli, ile video ilirushwa hewani haikuchukua muda yule bwana aliitwa Dodoma na kuondolewa moja kwa moja pale chuoni sembuse kimripoti nesi muuaji? Tuwe serious Rose ni muuaji hastahili kuendelea kuwa siyo tu mtumishi wa umma bali anyanganywe na vyeti maana amekiuka kiapo chake
 
Acha kulazimisha kufananisha vitu visivyofanana
 
James ana kosa kwann hakwenda kwa in charge kama alivyoelekezwa na Rose ili kupata ufumbuzi? Ila James alichofanya ni kumuudhi mwenzake tu ili amrekodi vizuri kutokana na tofauti zao kimtazamo. Mwaka huu naona ni wakusagiana kunguni tu.
Kwanini hakwenda kwa Incharge km alivyoelekezwa? Hivi unatumia nini kufikiri? Jaribu kutumia akili.
 
Brother umetumia hekima kubwa kulichambua ilo swala,,,ila kwenye kusema "nyokonyoko" nimecheka daah
 
Aliyerekod alifanya sahihi , video angeipeleka ngazi za juu ( mkuu wao wa kazi ) hapo kituoni Kwa ajili ya utatuz .... Kosa alilolifanya may be kuiweka video public .. hlo ni kosa kubwa sana
Mkuu nadhani haujafuatilia sakata zima namna lilivyokwenda.

Embu angalia hiyo video ya sakata kisha sikiliza video ya Ummi, mganga mkuu pamoja na mwanamke fulani mweny cheo hapo hosipitalini.

Ukishawasikiliza wote hao ndiyo utagundua stori na namna ya kubalansi maelezo ya pande zote.

Mimi nimeona kama mchezo mchafu huo uliandaliwa na mtu wa maabara kwa nia ovu.

Sitetei uozo wao isipokuwa yule boss wao wa kike aliyelitolea ufafanuzi sakata hilo, kasema expiry yake ipo ndani ya muda wa kutumika mpaka mwezi April na ni kawaida ya dawa zote kutotupwa siku hiyo hiyo ya expire iliyoandikwa kwenye kifungashio, huwa kuna muda wa mbele kitaalamu wanaoujua wafamasia.

Na kwamba walikubaliana kuendelea kutumia ili isije ikafika tarehe ya mwisho kabisa waka destroy.

Kwa hiyo huyo mfamasia anaufahamu muongozo huo, sasa kwanini aende kuvimba dirishani akizikataa dawa hizo kwa staff mdogo kabisa asiye na mamlaka yoyote?

Halafu tusi la nyo nyo nyo ni la kiuhawara zaidi, watani au ni kwa watu wanaodharauliana sana na kutafutiana kuharibiana.

Mwisho wa sakata hili waweza kuwa ni wa aibu kwa Lab tech aliyerusha.
 
James ni hafai kwenye kazi maana anaweza rekodi nyeti za mgonjwa ama akapiga picha majibu ya mgonjwa na akayasambaza
 
watanzania wengi hupenda kuficha madhaifu hata pale pasipofaa kufanya hivyo..nampongeza aliyerekodi na kutoa habari hiyo. watu wawe na hofu huko wanakoaminiwa....wasije wakaua taifa zima kwa ujinga ujinga wa watu wachache wachumia tumbo....sisi na ndugu zangu tunaunga juhudi za kuwarekodi waovu wote na kuwaanika mitandaoni
 
Ukiyachukulia mambo kimhemko hemko kama hivi utakwama sehemu nyingi.

Mada hujui hata inazungumzia kitu gani.
Wewe ukiulizwa kosa la Muuguzi ni lipi utajibuje?
Kulazimisha vitu vilivyo Isha muda kutumika. Au wewe unaandika tu Kwa sababu unajua kuandika
 
Ila wanawake wakipata kazi wanakua na vidharau vya kipuuzi sana mda mwingine huwa wanajisahau sana shenzi zao.
 
Kweli mkuu umesema vyema nimekupata uzuri sana.
 
Kwa kweli huyo mtu aliyemrekodi huyo mdada ROSE SHIRIMA kakosea sana yaani.
 
Uko biased very very bad, thats not critical analysis of the event, tumia kanuni husika na ufanye reference, duuh hii ni hatari sana sana
 
Uelewa wa uzalendo na kujitoa mhanga kuokoa taifa na watu wake ni mfinyu sana nchi hii Robert be careful hii issue ni sensitive sana hio analysis ni ya kitoto sana na haina maslahi mapana ya uhai wa raia wa nchi hii.
 
Getogo ni mbea. Mwanaume mbea anafaa kusutwa snitch.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…