Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. ROSE TWEVE APELEKA MILIONI 7 IRINGA, APINGA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Iringa Mhe. Rose Tweve amendelea na ziara yake ya siku tatu Wilaya ya Iringa mjini lengo likiwa ni uimarishaji wa Chama na Jumuiya, kutunisha mifuko ya wanawake, Elimu dhidi ya mikopo asilimia 4 ya wanawake, Uingizaji Wanachama wapya pamoja na uhakiki daftari la wanachama.
Katika hatua nyingine Mbunge Viti maalum, Mhe. Rose Tweve ametoa Tsh 7,200,000 kwa ajili ya Kata 18 za Iringa Mjini.
Zaidi ya yote Mhe. Tweve amepinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na kuwataka wanawake kufanya kazi ili kujenga uchumi imara katika Serikali hii inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.