Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,925
Na Mwandishi wetu
12th August 2010
Barua mbili zilizoandikwa na Waziri Mkuu Pinda
Mbunge wa Igunga (CCM) mkoani Tabora aliyemaliza muda wake, Rostam Aziz, bila kujua au kwa sababu ya kutafuta kura tu, ameanika udhaifu wa kiutendaji wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Udhaifu huo unajieleza katika nyaraka za serikali ambazo Rostam kwa kutumia njia zake binafsi alizipata na kuzitumia kujinadi kisiasa katika jimbo la Igunga kuomba kura za maoni kutoka kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi hivi karibuni.
Rostam amechukua barua mbili zilizoandikwa na Waziri Mkuu Pinda kwenda kwa mawaziri wawili, akiwaagiza utekelezaji wa miradi ya umeme na barabara katika mkoa wa Tabora, wilayani Igunga, na kuzifanya vielelezo katika kitabu chake cha "Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi mwaka 2005 hadi 2010."
Katika kitabu hicho chenye kurasa 27 kikiwa na picha kubwa ya Rostam kwenye jalada, pia kinajieleza kuwa "Igunga ya mwaka 1964 si Igunga ya sasa Tuendelee kushirikiana kujenga Igunga yetu", barua hizo licha ya kutokunakiliwa kwa Rostam, zina kumbukumbu namba moja.
Barua ya kwanza ambayo iliandikwa na Waziri Mkuu Pinda na kuweka saini yake, ni ya Machi 8, 2010 ikiwa na kumbukumbu namba PM/P/567/31 kwenda kwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, ikiwa na kichwa cha habari; Ujenzi wa barabara ya Shinyanga – Igunga kupitia Ukenyenge.
Barua hiyo imenakiliwa kwa Rais Ikulu na kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa.
Katika barua ya pili ambayo pia iliandikwa na Waziri Mkuu Pinda Mei 6, 2010, miezi miwili baada ya ile ya kwanza, ina kumbukumbu namba ile ile yaani PM/P/2/567/31 ikielekezwa kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na nakala yake kupelekwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mwinyimsa. Barua ya pili ina kichwa cha habari; "Miradi ya umeme mkoani Tabora" kama ya kwanza nayo haikunakiliwa kwa Rostam, lakini amezitumia kwenye kitabu chake, akinakili kumbukumbu namba zake kama zilivyo bila kuonyesha kuwa zina mgongano.
Baadhi ya wakazi wa Igunga waliozungumza na NIPASHE juu ya kitabu hicho, walisema ndicho alikuwa akitumia Rostam kujinadi wakati wa kusaka kura za maoni katika jimbo hilo ambako aliibuka mshindi kwa kishindo.
Rostam katika sehemu ya utangulizi ya kitabu hicho, ameandika kuwa tatizo la muda mrefu la kijiji cha Simbo kutokuwa na umeme limepatiwa ufumbuzi, baada ya yeye kufuatilia kwa Waziri Mkuu ambaye alimwagiza Waziri Ngeleja ahakikishe umeme unafika kwenye kijiji hicho kama ilivyokusudiwa kwa barua yenye kumbukumbu namba MP/P/2/567/31 ya Mei 6, mwaka huu.
Kadhalika, aliandika kuwa kwa tatizo sugu la daraja la mto Mbutu lililoko Igunga, Waziri Mkuu alikwishamuandikia Waziri Kawambwa barua yenye kumbukumbu namba MP/P/2/567/31 ya Machi 8, mwaka huu ili wizara ichukue hatua za kuipandisha hadhi barabara hiyo kuwa ya Mkoa.
Alipotafutwa kuelezea utata wa barua hizo, Mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu, Said Nguba, alisema hawezi kutoa maelezo ya aina yoyote kuhusiana na barua hizo.
"Sina Comment (kauli) kabisa, mimi kama mwandishi wa Waziri Mkuu sina cha kukueleza kuhusu suala hilo na nisingependa uandike maelezo yangu ila kama unataka andika tu," alisema Nguba.
Alisema ni vyema mwandishi akawasiliana na Rostam mwenyewe kwani yeye hakuwa na jibu lolote kuhusiana na barua hizo mbili.
"Umeshawasiliana na Rostam Aziz, ni vyema ukamuuliza mimi sina cha kukueleza kabisa," alisema Nguba.
Hata hivyo, alipotafutwa kwa simu kwa wiki moja sasa, Rostam hakupatikana na simu zake zote zilikuwa zikiita bila kupokelewa. NIPASHE itimtumia ujumbe mfupi sms, lakini hakujibu.
Mkanganyiko wa barua hizi unaacha maswali kama Waziri Mkuu anaweza kuandika barua mbili tofauti kwa nyakati tofauti na zikawa na kumbukumbu namba moja. Hali hii pia inaacha maswali juu ya usahihi wa taarifa mbalimbali za serikali na jinsi zinavyoweza kutumiwa na watu ambao hawakulengwa, kama zilivyo barua hizi.
CHANZO: NIPASHE