Rostam Aziz: Historia ya Dkt. Slaa haimpi uhalali wa kujifanya anajali maslahi ya Mtanzania. Kampuni zangu hazihusiki na uwekezaji wa DP World

Sidhani. Ingawa anachosema Dr. Slaa ni kweli lakini sidhani kama ataweza kumjibu Rostam Aziz. Hawa watu wawili kati yao hakuna aliye msafi. Wanajuana sana. Anayoyasema Rostam anayafahamu.

Na kuna anayoyafaham Dr. Slaa kuhusu Rostam. Naye akiyaweka Mezani.... Huu mgogoro utaenda enda mwishowe utakuwa ni vita ya hawa wawili watahama kutoka kwenye DP World na Watanzania watasahau watabaki kusubiria episodes za watu hawa huku siku zikiendelea mbele.

Kama ungekuwa mshauri wa Dr. Slaa kitaalamu. Je ajibu au Anyamaze?
 
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

---

Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.

Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.

Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.

Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.

Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.

Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.

Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.

Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.

Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.

Huyu Bwana Dkt. Slaa anaangalia maslahi yake binafsi, hakuwa mwanachama wa CHADEMA bali alipoona jina lake limekatwa (alipogombea kupitia CCM) ndio akahamia CHADEMA

Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu

Historia ya Dkt . Slaa inatosha kabisa kueleza kuwa yuko tayari kupandikiza chuki na uhasama kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa Kiswahili kifupi huyu jamaa (Dkt. Slaa) ni 'kizabizabina' ni fitina, mbinafsi. Na ni mtu wa kusema chochote na lolote na wakati wowote kwa maslahi yake binafsi"

Dkt. Slaa ananiita mimi fisadi, sasa mimi (Rostam) nafanya kazi na sekta binafsi wala sifanyi kazi na serikali nakuwaje fisadi, kwa hiyo nawafisadi sekta binafsi wenzangu, je watakubali nao? Sijawahi kupata skendo ya serikali na wala sijawahi kuomba ku-supply hata sindano serikalini

---

My Take

CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani

Watatoka sana mapangoni 🤣🤣🤣!! Alietenda kosa haimaanishi hapaswi kukosoa mapungufu flani!!
 
Dalili ya hatari na nchi kuangamia ni pale mafisadi papa wanapopata nguvu ya kuongea na kujiita watakatifu. Hii ni ishara kua ufisadi umekubuu, hii ni sawa na mwizi sugu aliezoea kuiba inafika mda haibi tu bali hata anabaka mkeo, watoto na haitoshi anataka kukubaka na ww, hvyo anachofanya Rostam ni kutubaka kitu ambacho hatutakiwi kukubali. Mafisadi sasa wameota pembe.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
THAT PART OF AN EYE THAT DISTINGUISHES THE COLOUR ITSELF HAS NO COLOUR.SIO LAZIMA UWE NA RANGI ILI KUONA NA KUTAMBUA RANGI. KUTOKUWA MUADILIFU, HAKUKUZUII KUTOWAONA WASIO WAADILIFU. TUJIBU HOJA, ILA TUSIKWEPE KUJIBU HOJA ETI KWA KUWA ALIYESEMA SI MUADILIFU.
 
Mbona mambo mengine haongeleagi, why hili la bandari tu? Huyu asibishe.. hapa ana mkono wake.
 
Mi naelewa hivi JAL 2 ndio Hii ishaanza kutekelezwa mission!!

SASA nadhani Pengo kamtuma Dr.achokoze nyuki kwenye mzinga sio!? halafu nyuki waanze kushambulia wakutane na Moshi na moto mkali wafe!!

Hii move kama ipo hivyo bas the state wamechanga karata vizuri SANA!!

Ni kama lile gazeti la uhuru mnakumbuka!!?

Eti "mama hatogombea 2025" mama si akajibu!!?si ndio operation ya kumkwamisha ikaanza arasmi Ili HADI 2025 awe amepoteza mvuto !!?

Mawazo huru haya ya mlipa kodi asiekwepa!

Mungu IBARIKI Tanzania nchi yetu niipendayo SANA!
 
Rastam katoa utetezi dhaifu sana wa wawekezaji.

Kajibu maswali ambayo hayajaulizwa, wakati maswali yaliyoulizwa hajayajibu.

Kajaza ad hominem attacks, logical non sequitur na false dichotomies kwenye utetezi wake.
Hicho kithungu thatha dha
 
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

---

Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.

Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.

Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.

Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.

Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.

Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.

Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.

Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.

Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.

Huyu Bwana Dkt. Slaa anaangalia maslahi yake binafsi, hakuwa mwanachama wa CHADEMA bali alipoona jina lake limekatwa (alipogombea kupitia CCM) ndio akahamia CHADEMA

Watanzania wakumbuke kuwa, huyu mtu (Dkt. Slaa) alipokuwa CHADEMA mwaka 2015 alikisaliti chama chake wakati kukiwa kinaelekea kwenye uchaguzi, alikisaliti chama chake kwa kuhongwa, alihongwa ndipo akaasi na kukisaliti chama chake (CHADEMA). Alikaa zake pale Serena baada ya pale akapanda ndege kwenda Canada na kisha akapewa ubalozi

Kwa kifupi Dkt. Slaa hana uadilifu wala uaminifu wa kunisema, mtu ambaye hana msimamo, mbinafsi , anayeangalia maslahi yake na hajawahi kuchangia chochote katika uchumi wa nchi yetu kazi yake ni kupiga tu mdomo. Mtu wa namna hii kumjibu ni shida lakini ni lazima wakati mwingine umjibu

Historia ya Dkt . Slaa inatosha kabisa kueleza kuwa yuko tayari kupandikiza chuki na uhasama kwa ajili ya maslahi yake binafsi, kwa Kiswahili kifupi huyu jamaa (Dkt. Slaa) ni 'kizabizabina' ni fitina, mbinafsi. Na ni mtu wa kusema chochote na lolote na wakati wowote kwa maslahi yake binafsi"

Dkt. Slaa ananiita mimi fisadi, sasa mimi (Rostam) nafanya kazi na sekta binafsi wala sifanyi kazi na serikali nakuwaje fisadi, kwa hiyo nawafisadi sekta binafsi wenzangu, je watakubali nao? Sijawahi kupata skendo ya serikali na wala sijawahi kuomba ku-supply hata sindano serikalini

---

My Take

CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani
Kimeumana
 
Back
Top Bottom