Rostam Aziz: Historia ya Dkt. Slaa haimpi uhalali wa kujifanya anajali maslahi ya Mtanzania. Kampuni zangu hazihusiki na uwekezaji wa DP World

Rostam Aziz: Historia ya Dkt. Slaa haimpi uhalali wa kujifanya anajali maslahi ya Mtanzania. Kampuni zangu hazihusiki na uwekezaji wa DP World



Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

Mimi sijui wamekosania nini. Rostam anasema Dr. Slaa historia yake haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya mzalendo. Siku zote anajijali yeye na tumbo lake.

Anaendelea...anasema aliacha utumishi wa Mungu kwa kuona maisha yake ni bora zaidi ya kumtumikia Mungu. Alijiunga na Chadema baada ya kukatwa CCM. Akajitoa Chadema baada ya kununuliwa na kupewa ubalozi. Anasema hana msaada kazi yake ni kupiga domo tu. Aiseee anamuita Kizabizabina ni mtu wa kuogopwa kama ukoma.

@Dr.W.P.Slaa tunasubiri majibu

My Take
CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani

Kati ya majizi yanayojianda kunufaika na ufedhuri wa huu mkataba wa hovyo wa bandari, Rostam ndiye kiongozi wao. Ni swala la mda tu majina yatawekwa hadharani
 
Asome hapa.

78F7C57B-1CBD-4A91-839F-23E0571CA5F7.jpeg
 
Binafsi siwezi msikiliza Dr Mihogo na Njaa zake badala yake nitamsikoliza na kumpa attention Rostam Kwa sababu kwanza ni mlipa Kodi na Mwajiri ila huyo mwingine ni njaa zinamsumbua ni WA kupuuzwa ,ameshazeeka hana jipya Kwa umri wake..

---

“Huyu ndugu yangu Dkt. Slaa sijui nimjibu nini maana historia yake haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania, siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.” – Mfanyabiashara Rostam Aziz

 


Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa.

---
Juzi katika mdahalo pale hoteli ya Serena nilisema kuwa sihusiki na hili jambo (mkataba wa bandari) kibiashara. Ningekuwa nahusika nisingekuwa jasiri wa kuyasema yale niliyoyasema katika mdahalo ule.

Unapohusika na jambo huwezi kulijadili, na pia huwezi kuwa na uwezo au neutrality (hali ya kutofungamana na upande wowote) ya kuzungumzia jambo lenyewe, hivyo ningekaa pembeni na kuacha wengine wajadili.

Mimi kama Rostam na kampuni zangu hatuhusiki na uwekezaji au utakaokuwa uwekezaji wa kampuni ya DP WORLD.

Mimi ni mfanyabiashara na nimewekeza ndani na nje ya nchi, na nimetangaza jina la Tanzania kote duniani kwa kuwavutia wawekezaji waje kuwekeza katika nchi yetu ili tuweze kupata ajira na tuimarisha uchumi wetu.


Watu wanapiga porojo na ninawapa changamoto waende mahakamani. Mimi ninaaminiwa na benki za ndani na za nje ndiyo maana wananikopesha,” amesema na kuongeza “Rais (John) Magufuli asigefungua viwanda vyangu kama mimi sio mfanyabiashara halali.

Mimi sifanyi kazi na serikali, huwezi kusikia Rostam anaomba tenda serikalini au anauza hata sindano serikalini. Mimi ni mfanyabiashara ninayefanya biashara na sekta binafsi ndio maana huwezi kunituhumu kuwa nimetoa rushwa au nimekula rushwa. Hayo maneno (ya Dkt. Slaa) ni ya uropokaji tu na yasiyifanyiwa utafiti.

Historia ya Dkt. Slaa haimpi heshima wala uhalali wa kujifanya eti yeye ni mtu wa kujali maslahi ya Watanzania. Siku zote amejijali yeye binafsi na maslahi yake binafsi.

Dkt. Slaa aliacha kazi ya utumishi wa Mungu kanisani baada ya utovu wa maadili kwa kuona maisha yake ni bora zaidi kuliko utumishi wa Mungu. Historia yake ni historia ya kukosa uaminifu an uadilifu.


Dkt. Slaa hakujiunga upinzani kutokana na imani yake kwa sababu jina lake lilikatwa alipogombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na sababu iliyotolewa wakati wa kukatwa jina lake ni sababu ya kukosa uadilifu alipokuwa mtumishi wa Mungu kanisani.




---

My Take
CCM na Team ya Magufuli mje na nyinyi mtujibu mlimnunua Dr. Slaa kwa bei gani

Aahaaaaaa,shikamoo Rostam
 
Mfanyabiashara mkubwa nchini Rostam Aziz amezungumza na waandishi wa habari Juni 26, 2023 ambapo ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo sakata la bandari ya Dar na kuhusika kwake kwenye uwekezaji huo mkubwa...
Rostam amerudia tena enzi za Mengi? Si aliita siasa zetu ni uchwara akasusa na ubunge akakimbia? Nani kazitakasa siasa zetu hadi zikamvutia kurudi?

Au ndo ule utatu umerudi rasmi? Hata hivyo Huyu ni gabacholi asiye na madhara kwenye siasa zaidi ya wizi.

Samia hatufai yule mwanamke tayari ametekwa!! TZ tuna state capture!!
 
Back
Top Bottom