Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
- Thread starter
- #121
PM,
Nashukuru kuweka wazi wewe sio Chadema. maana ningekushangaa. Halafu hao hao Chadema wanakubali vipi kumweka kiongozi kihiyo kwenye umakamu mwenyekiti tena wa taifa?
Ufisadi sio wa CCM tu kumbe....
FairPlayer
Fair Player
Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA haina nguvu wala watumishi wengi kama Usalama wa Taifa wa nchi. Hivyo hawana system ya kufanya vetting ya viongozi wao. Kurugenzi kwa habari nilizonazo ina mtumishi mmoja tu wa kufanya uchunguzi, awali alikuwepo pia Kampeni mmoja wa Jeshi akiitwa Eugine Maganga, lakini baada ya Kikwete kushinda bwana huyu kwa kuwa alisoma na Kikwete, kikwete akamuita na akarudi CCM.
Kwa hiyo, Chacha aliwadanganya CHADEMA kuhusu elimu yake na CHADEMA wakadanganyika, wakaona wamepata kumbe wamepatikana.
Naamini kabisa CHADEMA hawalijui ili suala la uongo wa Bwana Chacha kuhusu elimu yake, wangelijua lazima lingejitokeza katika mijadala ya Kamati Kuu yao kuhusu nidhamu yake kama ambavyo lilijitokeza hilo la kumtelekeza mkewe.
Lakini kwa maoni yangu kama mchambuzi wangeligusa hilo wangeonekana tu kwamba wanamchimba, wangeulizwa mbona mlimpitisha kugombea ubunge?
Kwenye fomu za ubunge za kiserikali suala la elimu lilishaondolewa hivyo wasingeliona kwenye fomu za wagombea.
Mkakati wa Rostam umefanya kazi vizuri sana, Chacha amesimamishwa kwa sababu za kinadhamu lakini kupitia Mtanania, Majira, Rai na baadaye magazeti mengine ameweza kutengenezewa ujumbe kuwa amesimamishwa sababu ya hoja zake za kupinga ukabila na kutaka ruzuku ipelekwe wilayani. Na umma watanzania ukaamini kuwa Chacha ndio Mkweli na Mbowe ndio Muongo na kwamba viongozi wa Kamati Kuu ya CHADEMA wanaburuzwa na Mbowe kumwonea Chacha. Hiyo ndio nguvu ya Vyombo vya habari Tanzania.
Sasa tusubirini mikakati inayofuata ambayo nimeshawaeleza tayari kuwa itafanyika. Tusubiri pia jinsi ambavyo Chacha ataanza kumshambulia Zitto, and at one point he will get it personal.
Wachunguzi wa mambo wanasema hali hii isingejitokeza kama CHADEMA ingekuwa na kitengo thabiti cha ushushu(intellegence) cha kuweza kupata habari zote za mipango inayofanywa na Bwana Rostam, Ballile na Chacha Wangwe bila kusubiria hisani ya mtu mmoja wa nne anayetumiwa ambaye ameamua kuvujisha hizi habari zote(jina lake nalihifadhi kwa kuwa ndio source wangu mkuu)
PM