Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Katika suala la kupambana na UFISADI kuna waliofikiria wakati MAFISADI wanajibu mapigo, wataonekana kirahisi. Lakini mpaka sasa lazima watu wajue mafisadi ni watu hatari sana wanaweza kutokea usipotegemea.

Mafisadi wanajua loop hole zilipo na kwa Chadema naona waliijua mapema, hata kabla Chadema hawajajua.

Sasa hizi tuhuma za aliyekuwa Makamu mwenyekiti kuiba sijui nini hii tumefika mbali!!.
 
Kwani mkimripoti huko bungeni hawawezi mpiga child support? you have lots of alternatives kuliko huku kumwaga mambo yenu ya ndani mnakokufanya sasa. Yaani data za makamu mwenyekiti wa chama chako unatafuta hapa JF, this is serious. Okay, do as you like.

Lingine, mbona hujanijibu mna wanachama wangapi Tanzania nzima???just curious. Mwanachadema Yyeyote anayejua anaweza nijibu tafadhali, hata kwa PM.

CHADEMA imekuwa ikishughulikia mambo yake ndani. Mambo mengi tu ya mazito na ya siri. Bila hayo kutoka nje.

Lakini katika hili la Chacha naona mambo mawili:

1. Chacha mwenyewe ameamua kuwamwaga hadharani kupitia Mtanzania na Rai kabla na kupotosha mijadala ya vikao; hivyo Mbowe na Tundu Lissu ilibidi wajitokeze kumwaga hadharani ukweli kwa niaba ya chama.

2. Hapa huyu mtu anayeitwa Paparazi Muwazi ndiye aliyemwaga haya ya Chacha na UDSM na Chacha na Mkewe. Na huyu si mwanaCHADEMA. Sasa kama mambo yamemwaga hapa, sisi kama wanaCHADEMA tunakosa gani kuuliza kama ni ukweli au uwongo ili tupate maoni ya watu wengine ikiwemo viongozi wetu wa CHADEMA wanaopita hapa? Wasipojibu hapa nitawauliza vikaoni

Asha
 
Si unaweza ukampigia simu ukamuuliza chacha mwenyewe, au waogopa?

Hivi wakati mwanachama wenu anapojaza form za kuomba uongozi, hakuna swali la kuuliza criminal hitory yake. Kama lipo Chacha alilijaza vipi? kama aliandika hakuwa na criminal history yeyote, je alidanganya? na mwanachama anapodanganya sheria za chama chenu zinasemaje?
 
Simaanishi wewe uchukue hatua, ila kwa vile wewe ni kada huko Chadema, wapelekee ujumbe wangu huu tafadhali kama unavyowapelekea jumbe nyingine. Samahani kwa kukutuma. Waambie Mama kule JF anauliza hakuna uwezekano wa kumshtaki Chacha kwa Sitta ili akatwe nusu ya mapato yake kwa ajili ya kulea familia, ikiwezekana hata akatwe robo tatu kwani familia yake ni kubwa!

Halafu Asha, na ukada wako wooooooooooooote hujui chama chako kina wanachama wangapi? Haya tuseme chadema wanawanachama millioni moja na wote hao wakapiga kura kumchagua rais kwa ticket ya chadema, je wana uwezo wa kuwaondoa CCM madarakani?. Nadhani kuna haja ya nyie wanachadema kufanya kazi ya ziada kutafuta wanachama wa kutosha kwanza.

Nitawafikishia ujumbe wako.

Kwani uliambiwa wanaopiga kura ni wanachama tu? CCM yenyewe ina wanachama milioni 4 tu. We uliambiwa watakaompigia kura Obama ni wanachama wa Democrat tu? Suala la kuangalia ni jinsi gani CHADEMA itawatumia wanacham wake milioni moja kupata kura milioni 10. Kila mwanachama akitafuta kura kumi tu, tayari CHADEMA inachukua dola.

Asha
 
Si unaweza ukampigia simu ukamuuliza chacha mwenyewe, au waogopa?

Hivi wakati mwanachama wenu anapojaza form za kuomba uongozi, hakuna swali la kuuliza criminal hitory yake. Kama lipo Chacha alilijaza vipi? kama aliandika hakuwa na criminal history yeyote, je alidanganya? na mwanachama anapodanganya sheria za chama chenu zinasemaje?

Nimempigia jana, ameniuliza kwani wewe ni nani na kwanini unataka kujua hayo? Amesema nimpigie akiwa na nafasi. Labda jaribu na wewe kumpigia au Mwanakijiji ampigie amhoji hayo. Maana naona wanapatana

Asha
 
Nitawafikishia ujumbe wako.

Kwani uliambiwa wanaopiga kura ni wanachama tu? CCM yenyewe ina wanachama milioni 4 tu. We uliambiwa watakaompigia kura Obama ni wanachama wa Democrat tu? Suala la kuangalia ni jinsi gani CHADEMA itawatumia wanacham wake milioni moja kupata kura milioni 10. Kila mwanachama akitafuta kura kumi tu, tayari CHADEMA inachukua dola.

Asha

Suala la wanachama ni muhimu, kama CCM wana wanachama 4000 tu, kwa nini nyie msiwe na wanachama 5000 au 6000. Hii itawasaidia kupata wabunge wengi pia. Independents wengi si wapiga kura! jengeni chama, bla bla zimeshatosha sasa na Mbowe asigombee tena urais 2010, ameshachuja kama alivyochuja Lipumba na maalim Seif.
 
wewe wala usishangae ya chadema na wangwe,hayo madogo tu na yataisha soon, wanagombana mke na mume au wazazi na mtoto ije kuwa chadema na wangwe. Watamalizana ndani ya familia yao ya chadema. Cha muhimu wewe shangaa ya ufisadi na sisiemu na ujadili suluhisho, je unafikiri ufisadi utaisha vipi tanzania?

Vita ya panzi, furaha ya kunguru. Chadema waache porojo zao kwenye media, wakae chini na kutatua matatizo yao ndani. Hii inatuletea wasiwasi sisi ambao tumekiamini chama na tunaona kwamba ni mtetezi wa wanyonge. Sasa leo wanaanza kutupiana matusi. Je tutafika kweli?
 
Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Nilisema hapa miezi mingi nyuma kuwa Rostam kumtumia Chacha Wangwe kuibomoa CHADEMA. Watu wakasema nasema udaku. Leo CHADEMA ineshavikwa ukabila na ubadhirifu wa ruzuku. Ni matokeo ya kikao cha RA na Wangwe Kempinsiki Hoteli na baadaye kikao kwenye ile nyumba ya Kinondoni mitaa ya jirani na Balozi Wa Marekani hapa Tanzania. Nilesema hapa Rostam alivyomnunua yule aliyejiita kiongozi wa CHADEMA Igunga kutoa tamko la kumwuunga mkono kugombea Ubunge 2010, lakini nikaweleza kwamba baada ya hapo mkakati utakaofuata ni wa kuwatumia viongozi wa dini. Maneno yangu yamedhihirika kwa Rostam kulitumia kanisa la KKKT Kinondoni. Sasa habari kutoka duru la wanamkakati wa Rostam ni kwamba sasa atawatumia Viongozi wa Kislamu hivi karibuni na atahamia kwa watu mashuhuri Tanzania. Na katika mkakati wake huo amefanikiwa kuwanunua hata baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi katika vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikimuanika zaidi vya Thisday/Kulikoni na Tanzania Daima. Na vile vilivyokuwa katikati vya Mwananchi na Nipashe. Na ameongeza nguvu zaidi katika vyombo anavyovitawala vya Majira na Mtanzania. Kwa upande mwingine, ule mkakati niliousema siku nyingi wa kumtumia Chacha Wangwe umefanyiwa marekebisho kwa kuwa malengo hayafukiwa kama ilivyopangwa. Awali ilipangwa Chacha Wangwe atumie kikao kilichofanyika Dodoma 28 Juni, 2008 kutoa hoja ya kutaka Kamati Kuu ipige kura ya kutokuwa na imani na Dr Wilbroad Slaa kama Katibu Mkuu, ili akiondolewa Slaa aondoke na Sekteratiati yake yote wakina Zitto, Tundu Lissu, Mnyika, Tumbo na wengineo; Mbowe abaki mwenyewe na iwe rahisi kummalizia. Katika Mkakati huo ilipangwa kama kura za kutokuwa na imani hazitatosha ilikuwa Chacha Wangwe atoke nje na kusema kuwa Mbowe ametumia udikteta kuzuia hoja hiyo, na ajitokeze mbele ya umma na hoja hizi hizi ambazo ameumua kuzitoa sasa. Angefanya kama anavyofanya sasa lakini ujumbe wake ungekuwa ni kuwa Mbowe anamlinda Dr Slaa ambaye ameshindwa kazi na anaruhusu ubadhirifu. Lengo la Mkakati mzima likiwa ni Dr Slaa kupoteza imani kwa wananchi na hatimaye mjadala wa ufisadi kuonekana hauwahusu watu 11 wa CCM aliowataja kwenye list of shame bali hata yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya au nzuri, mtu mmoja wa Rostam ambaye ni mpenzi wa Dr Slaa akatoa siri nyingi kwa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA. Suala hili likaingizwa kwa Kamati ya Wazee wakina Mtei, Profesa Baregu, Balozi Ngaiza, Makani na Ndesamburo, hata hivyo wazee wakaamua yote yawekwe kama kumbukumbu na kuamua kupatanisha hasa baada ya Chacha kuonyesha urafiki na kujirudi. Nyuma ya pazia Chacha akaendelea na mpango wake kwa kwenda kumng’oa Dr Slaa Dodoma, na tayari Ballile alitumwa Dodoma na Rostam kuratibu habari hiyo. Lakini mambo yakabadilika Dodoma pale ripoti ya Kamati ya Wazee ilipowasilishwa Dodoma, Chacha akawageuka Wazee kuwa hakukubaliana nao yaishe, akatoa hoja ya kumshambulia Dr Slaa; kikao kikamgeuka yeye. Akachukia na kumtukana Baregu. Akamtukana pia Mama Chiku Abwao matusi ya nguoni kwa kutangaza kuwa pamoja na kuwa alimuunga mkono na kumpigia debe kuwa Makamu katika hilo hakubaliana nao. Matusi yake yakamuudhi Tundu Lissu aliyetaka achukuliwe hatua za kinidhamu, Chacha akainuka na kumvamia Tundu Lissu kutaka kumpiga- Board Guard wa Mwenyekiti akapambana nae na kumzuia. Ndio maana mtakumbuka kuwa habari ya Mtanzania iliyoandikwa kabla ya Chacha kusimamishwa, huku Ballile akijua kuwa matarajio ni Slaa kusimamishwa, wakati kikao kinaendelea mpaka usiku wa mananeo Ballile akaandika Habari ya Mambo ambayo alitarajia yangetokea kikaoni lakini hayakutokea. Alitarajia pangekuwa na mjadala mkali kuhusu hoja ya Ruzuku lakini kwa bahati mbaya suala hilo halikujadiliwa kama ilivyotarajiwa. Baaada ya Mkakati huo kushindwa, Rostam na Ballile wakaamua kutumia mkakati wa “CHADEMA yamwaga Mboga, Chacha Amwage Ugali”. Pamoja na Mkakati huo kufanikiwa kuichafua CHADEMA, bado haujaweza kutimiza malengo ya awali. Hivyo, wakabadili Mkakati na kukubaliana kwa Chacha Atangaze Wazi kuwa lengo lake ni Kugombea Uenyekiti na Kumwondoa Mbowe na Dr Slaa. Mkakati huo umeanza ku-back fire’ kwa kuanza kuwaunganisha waCHADEMA wote makini na hata wapenzi kwa kuanika rangi halisi za Chacha Wangwe. Jana kimefanyika kikao kingine, tathmini imefanyika ya jinsi Mkakati wa kuwatumia KKKT Kinondoni ulivyofanikiwa. Kwa ujumla imeonekana Mkakati umefanikiwa lakini kuna hofu viongozi wa juu wa kanisa la KKKT hususani Askofu Malasusa wanaweza kuchukia na kutoa onyo kali kwa wenzao wa Kinondoni. Suala hili linajengwa uzito zaidi kwa jinsi ambayo Spika Sitta amechukizwa na habari za kanisa hilo kutumika. Ili kuzuia hali hiyo, imekubaliwa Rostam afanye kwa haraka tukio na Waislamu ili Wakristu waoone dini zote zinakubaliana nae na kumuona ni mtu msafi. Kwa upande mwingine, sasa Rostam Aziz ameamua kubadili mkakati wa jinsi ya kuwabomoa CHADEMA na sasa pamoja na Chacha Wangwe kukusudia kwenda mahakamani na kukata rufaa kwenye baraza kuu, Rostam Aziz amepanga mkakati mwingine unaoitwa “GAWA, TAWALA”, chini ya mkakati huu ‘mashujaa’ kadhaa watalipwa kujitokeza kuwa mstari wa mbele kuungana na Chacha, tayari Wangwe na Ballile wamepewa fungu la fedha kuingiza watu kuunda kundi lao. Mpaka sasa katika Orodha wako Mziray, Shilembi. Lyimo, Shilungushela. Chini ya azma hiyo, kikwazo kikubwa ni kukosa home base baada ya Tarime kutoa msimamo wa wazi wa kumpinga na kueleza wazi kuwa wao wanapokea ruzuku ya Laki Nne kila mwezi kutokana na moja ya wilaya iliyofanya vizuri zaidi katika matokeo ya uchaguzi 2005. Baada ya Habari hiyo ya Nipashe, Chacha Wangwe alipiga simu kuwatisha viongozi hao lakini viongozi hao wakamweleza kuwa msimamo wao ni msimamo pia wa madiwani wengi wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Halmashauri(Kama Meya) wa Tarime ikikumbukwa kuwa CHADEMA ni chama tawala huko. Baada ya Kadhia hiyo, Jana Rostam alimwelekeza Chacha Kufanya mapinduzi Tarime kwa kuwaondoa viongozi hao. Jana hiyo hiyo Chacha Wangwe akampigia simu Chacha Okong, yule aliyekuwa kampeni manager wake kwenye uchaguzi mkuu 2005 ambaye pia alikuwa katibu wa wilaya a;iyehama toka CHADEMA kwenda CCM baada ya Chacha Wangwe kushindwa kuendeleza kazi za chama na pia kuwatelekeza kabisa wapiganaji wenzake na kukaa Dar es salaam. Chacha Wangwe amemuahidi milioni 10 kama atarejea chama chake cha awali cha CHADEMA na atahakikisha kuwa anarudi kwenye nafasi yake ya Katibu wa Wilaya na kutoa kauli ya kuumuunga mkono. Fedha hizo ni chini ya kiwango ambacho Rostam aliahidi kitolewe kwa ajili ya zoezi hilo. Kuna mengi yanaendelea hivi sasa, na tutarajie mengine zaidi wiki hii. Mkakati huu ni sehemu ndogo tu ya mpango kabambe wa Rostam wa kujisafisha na kuwaita watu wengine zaidi mafisadi ili kugeuza mjadala wa ufisadi nchini Tanzania.

PM

Nimerudia tena kuusoma huu uchambuzi. Haya ni maneno mazito

Asha
 
Asha
Suala la kuangalia ni jinsi gani CHADEMA itawatumia wanacham wake milioni moja kupata kura milioni 10. Kila mwanachama akitafuta kura kumi tu, tayari CHADEMA inachukua dola.

Duh!! Chadema ina wanachama 1m!!!! Hawa si kama wale clayanti wa Voda???

Mama
Suala la wanachama ni muhimu, kama CCM wana wanachama 4000 tu, kwa nini nyie msiwe na wanachama 5000 au 6000. Hii itawasaidia kupata wabunge wengi pia. Independents wengi si wapiga kura! jengeni chama, bla bla zimeshatosha sasa na Mbowe asigombee tena urais 2010, ameshachuja kama alivyochuja Lipumba na maalim Seif.

Nawe!??! nani kakwambia milioni nne inaandikwa 4000!!!!
 
Duh!! Chadema ina wanachama 1m!!!! Hawa si kama wale clayanti wa Voda???

Nawe!??! nani kakwambia milioni nne inaandikwa 4000!!!!

Nilikuwa nawaza kipesa pesa, hebu zidisha mara elfu moja hapo chap chap!
 
si Unaweza Ukampigia Simu Ukamuuliza Chacha Mwenyewe, Au Waogopa?

Hivi Wakati Mwanachama Wenu Anapojaza Form Za Kuomba Uongozi, Hakuna Swali La Kuuliza Criminal Hitory Yake. Kama Lipo Chacha Alilijaza Vipi? Kama Aliandika Hakuwa Na Criminal History Yeyote, Je Alidanganya? Na Mwanachama Anapodanganya Sheria Za Chama Chenu Zinasemaje?
Umemaliza Kila Kitu.
 
Tukubali kusaidiwa na Idara zinazoheshimika kama TISS kwenye SCREENING ya viongozi wetu hasa wa KITAIFA. Naamini hili lingefanyika tusingekuwa na watu kama LOWASSA, KARAMAGI, WANGWE,... Kwani MWALIMU alikuwa anafanyaje enzi za Urais wake?

Wilcard,
TISS haiheshimiki tena. Kumejaa watetezi wa ufisadi kule.
 
Moderators

Mpaka sasa kuna thread zaidi ya tano zote zinamzungumzia Chacha Wangwe na CHADEMA. Naona zinajaza uwingi hapa. Nashauri zote ziunganishwe chini ya thread moja ili mjadala uweze kufuatiliwa kwa urahisi

Asha
 
Rostam ni mtu hatari sana, na kuendelea kusubiri ni sawa na kusubiri janga ama balaa. Hivi anatoroka lini? kama bado sana inabidi atimuliwe, ni mnafiki, mfitini, fisadi, ndumilakuwili and so on. Hivi wataallam hakuna namna yeyote legal inayoweza kumuwajibisha Rostam? anatuchezea akili watanzania na kibaya zaidi anacheza na akili ya Rais!

hakuna kumsubiri atoroke mi naona tuandamane ili akamatwe achukuliwe hatua za kisheria (nimesema tuandamane ili kushinikiza maana tukisubiri hawatamkamata si tunajua uswaiba wake na kikwete) hawezekani kwenye soo zote kama richmond na EPA tukose ushahidi wa kumtia hatiani huyu.
 
PM

Kila nikiangalia bungeni simuoni Chacha. Yuko wapi? Anawawakilishi vipi wananchi wa Tarime kama haendi bungeni?

Sasa mbona kiongozi wa upinzani Hamad Rashid wa CUF aliposema Chacha ni mtoro Chacha alikanusha?

Jamani PM uko wapi? Hebu endelea kutumwagia mambo

Asha
 
Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Nilisema hapa miezi mingi nyuma kuwa Rostam kumtumia Chacha Wangwe kuibomoa CHADEMA. Watu wakasema nasema udaku. Leo CHADEMA ineshavikwa ukabila na ubadhirifu wa ruzuku. Ni matokeo ya kikao cha RA na Wangwe Kempinsiki Hoteli na baadaye kikao kwenye ile nyumba ya Kinondoni mitaa ya jirani na Balozi Wa Marekani hapa Tanzania. Nilesema hapa Rostam alivyomnunua yule aliyejiita kiongozi wa CHADEMA Igunga kutoa tamko la kumwuunga mkono kugombea Ubunge 2010, lakini nikaweleza kwamba baada ya hapo mkakati utakaofuata ni wa kuwatumia viongozi wa dini. Maneno yangu yamedhihirika kwa Rostam kulitumia kanisa la KKKT Kinondoni. Sasa habari kutoka duru la wanamkakati wa Rostam ni kwamba sasa atawatumia Viongozi wa Kislamu hivi karibuni na atahamia kwa watu mashuhuri Tanzania. Na katika mkakati wake huo amefanikiwa kuwanunua hata baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waandamizi katika vyombo vya habari ambavyo vilikuwa vikimuanika zaidi vya Thisday/Kulikoni na Tanzania Daima. Na vile vilivyokuwa katikati vya Mwananchi na Nipashe. Na ameongeza nguvu zaidi katika vyombo anavyovitawala vya Majira na Mtanzania. Kwa upande mwingine, ule mkakati niliousema siku nyingi wa kumtumia Chacha Wangwe umefanyiwa marekebisho kwa kuwa malengo hayafukiwa kama ilivyopangwa. Awali ilipangwa Chacha Wangwe atumie kikao kilichofanyika Dodoma 28 Juni, 2008 kutoa hoja ya kutaka Kamati Kuu ipige kura ya kutokuwa na imani na Dr Wilbroad Slaa kama Katibu Mkuu, ili akiondolewa Slaa aondoke na Sekteratiati yake yote wakina Zitto, Tundu Lissu, Mnyika, Tumbo na wengineo; Mbowe abaki mwenyewe na iwe rahisi kummalizia. Katika Mkakati huo ilipangwa kama kura za kutokuwa na imani hazitatosha ilikuwa Chacha Wangwe atoke nje na kusema kuwa Mbowe ametumia udikteta kuzuia hoja hiyo, na ajitokeze mbele ya umma na hoja hizi hizi ambazo ameumua kuzitoa sasa. Angefanya kama anavyofanya sasa lakini ujumbe wake ungekuwa ni kuwa Mbowe anamlinda Dr Slaa ambaye ameshindwa kazi na anaruhusu ubadhirifu. Lengo la Mkakati mzima likiwa ni Dr Slaa kupoteza imani kwa wananchi na hatimaye mjadala wa ufisadi kuonekana hauwahusu watu 11 wa CCM aliowataja kwenye list of shame bali hata yeye mwenyewe. Kwa bahati mbaya au nzuri, mtu mmoja wa Rostam ambaye ni mpenzi wa Dr Slaa akatoa siri nyingi kwa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA. Suala hili likaingizwa kwa Kamati ya Wazee wakina Mtei, Profesa Baregu, Balozi Ngaiza, Makani na Ndesamburo, hata hivyo wazee wakaamua yote yawekwe kama kumbukumbu na kuamua kupatanisha hasa baada ya Chacha kuonyesha urafiki na kujirudi. Nyuma ya pazia Chacha akaendelea na mpango wake kwa kwenda kumng’oa Dr Slaa Dodoma, na tayari Ballile alitumwa Dodoma na Rostam kuratibu habari hiyo. Lakini mambo yakabadilika Dodoma pale ripoti ya Kamati ya Wazee ilipowasilishwa Dodoma, Chacha akawageuka Wazee kuwa hakukubaliana nao yaishe, akatoa hoja ya kumshambulia Dr Slaa; kikao kikamgeuka yeye. Akachukia na kumtukana Baregu. Akamtukana pia Mama Chiku Abwao matusi ya nguoni kwa kutangaza kuwa pamoja na kuwa alimuunga mkono na kumpigia debe kuwa Makamu katika hilo hakubaliana nao. Matusi yake yakamuudhi Tundu Lissu aliyetaka achukuliwe hatua za kinidhamu, Chacha akainuka na kumvamia Tundu Lissu kutaka kumpiga- Board Guard wa Mwenyekiti akapambana nae na kumzuia. Ndio maana mtakumbuka kuwa habari ya Mtanzania iliyoandikwa kabla ya Chacha kusimamishwa, huku Ballile akijua kuwa matarajio ni Slaa kusimamishwa, wakati kikao kinaendelea mpaka usiku wa mananeo Ballile akaandika Habari ya Mambo ambayo alitarajia yangetokea kikaoni lakini hayakutokea. Alitarajia pangekuwa na mjadala mkali kuhusu hoja ya Ruzuku lakini kwa bahati mbaya suala hilo halikujadiliwa kama ilivyotarajiwa. Baaada ya Mkakati huo kushindwa, Rostam na Ballile wakaamua kutumia mkakati wa “CHADEMA yamwaga Mboga, Chacha Amwage Ugali”. Pamoja na Mkakati huo kufanikiwa kuichafua CHADEMA, bado haujaweza kutimiza malengo ya awali. Hivyo, wakabadili Mkakati na kukubaliana kwa Chacha Atangaze Wazi kuwa lengo lake ni Kugombea Uenyekiti na Kumwondoa Mbowe na Dr Slaa. Mkakati huo umeanza ku-back fire’ kwa kuanza kuwaunganisha waCHADEMA wote makini na hata wapenzi kwa kuanika rangi halisi za Chacha Wangwe. Jana kimefanyika kikao kingine, tathmini imefanyika ya jinsi Mkakati wa kuwatumia KKKT Kinondoni ulivyofanikiwa. Kwa ujumla imeonekana Mkakati umefanikiwa lakini kuna hofu viongozi wa juu wa kanisa la KKKT hususani Askofu Malasusa wanaweza kuchukia na kutoa onyo kali kwa wenzao wa Kinondoni. Suala hili linajengwa uzito zaidi kwa jinsi ambayo Spika Sitta amechukizwa na habari za kanisa hilo kutumika. Ili kuzuia hali hiyo, imekubaliwa Rostam afanye kwa haraka tukio na Waislamu ili Wakristu waoone dini zote zinakubaliana nae na kumuona ni mtu msafi. Kwa upande mwingine, sasa Rostam Aziz ameamua kubadili mkakati wa jinsi ya kuwabomoa CHADEMA na sasa pamoja na Chacha Wangwe kukusudia kwenda mahakamani na kukata rufaa kwenye baraza kuu, Rostam Aziz amepanga mkakati mwingine unaoitwa “GAWA, TAWALA”, chini ya mkakati huu ‘mashujaa’ kadhaa watalipwa kujitokeza kuwa mstari wa mbele kuungana na Chacha, tayari Wangwe na Ballile wamepewa fungu la fedha kuingiza watu kuunda kundi lao. Mpaka sasa katika Orodha wako Mziray, Shilembi. Lyimo, Shilungushela. Chini ya azma hiyo, kikwazo kikubwa ni kukosa home base baada ya Tarime kutoa msimamo wa wazi wa kumpinga na kueleza wazi kuwa wao wanapokea ruzuku ya Laki Nne kila mwezi kutokana na moja ya wilaya iliyofanya vizuri zaidi katika matokeo ya uchaguzi 2005. Baada ya Habari hiyo ya Nipashe, Chacha Wangwe alipiga simu kuwatisha viongozi hao lakini viongozi hao wakamweleza kuwa msimamo wao ni msimamo pia wa madiwani wengi wa CHADEMA na Mwenyekiti wa Halmashauri(Kama Meya) wa Tarime ikikumbukwa kuwa CHADEMA ni chama tawala huko. Baada ya Kadhia hiyo, Jana Rostam alimwelekeza Chacha Kufanya mapinduzi Tarime kwa kuwaondoa viongozi hao. Jana hiyo hiyo Chacha Wangwe akampigia simu Chacha Okong, yule aliyekuwa kampeni manager wake kwenye uchaguzi mkuu 2005 ambaye pia alikuwa katibu wa wilaya a;iyehama toka CHADEMA kwenda CCM baada ya Chacha Wangwe kushindwa kuendeleza kazi za chama na pia kuwatelekeza kabisa wapiganaji wenzake na kukaa Dar es salaam. Chacha Wangwe amemuahidi milioni 10 kama atarejea chama chake cha awali cha CHADEMA na atahakikisha kuwa anarudi kwenye nafasi yake ya Katibu wa Wilaya na kutoa kauli ya kuumuunga mkono. Fedha hizo ni chini ya kiwango ambacho Rostam aliahidi kitolewe kwa ajili ya zoezi hilo. Kuna mengi yanaendelea hivi sasa, na tutarajie mengine zaidi wiki hii. Mkakati huu ni sehemu ndogo tu ya mpango kabambe wa Rostam wa kujisafisha na kuwaita watu wengine zaidi mafisadi ili kugeuza mjadala wa ufisadi nchini Tanzania.

PM

Lile shinikizo la Sitta nililowaeleza limefanya kazi na wote mmeshuhudia jinsi KKKT walivyomkana Rostam. Kutokana na KKKT kumwahi Rostam kabla ya yeye kufanya tukio na waislamu sasa amesitisha mpango huo, badala yake amejizatiti kupingana na tamko la KKKT kiufundi. Amejiandaa kufanya propaganda kupitia Majira na Tanzania Daima kwamba tamko la KKKT limetokana na inda ya bwana Sitta na Mwambalaswa. Bila kuwashambulia moja kwa moja ataeleza wazi michango ambayo ameitoa kwa KKKT siku za nyuma na kueleza wazi kuwa wao ndio waliomualika wakati huo. Timu yake ya mkakati imechukua uamuzi huo baada ya ukweli kwamba baada ya KKKT kutoa tamko hata waislamu anawatumia nao wamesita sita. Wakati huo huo,timu ya mkakati ya Bwana Rostam inaendelea kutafakari jinsi ya kumwingiza Bwana Mengi kama mmoja wa watu waliofanya shinikizo zaidi ya Sitta kwa KKKT kutoa hilo tamko. Bwana Mengi ni mmoja wa waumini wa KKKT. Napo katika KKKT bado moto unafukuta Kinondoni, huku baadhi ya watu ikiwemo mchungaji wakipinga hatua za kinadhamu zilizochukuliwa. Na Bwana Rostam amekuwa katika mawasiliano nao wakati wote.

Wakati huo huo, kile kikao cha Bwana Chacha Wangwe cha Dar es salaam kimefanyika, kwa kiasi kikubwa mjadala uliofanyika hapa ambao bwana Balille alipeleka nakala umeathiri mipango yao. Bwana Rostam ameanza kumwona Chacha Wangwe kama mzigo. Ule mpango wa kuwaibua mashujaa wengine unaendelea ingewaje uzito wa viongozi hao umeonekana mdogo sana. Mkakati unafanyika wa kujaribu kumweka upande wa Chacha kiongozi mmoja mwandamizi wa CHADEMA(jina nalihifadhi kwa sasa). Wakati hayo yakiendelea imekubaliwa kwamba Bwana Dr Paul Kyara, Mwenyekiti wa SAU, mchagga ambaye alinyimwa nafasi ya uongozi CHADEMA kuepusha ukabila na hatimaye akaamua kujitoa chama hicho na kuanzisha chama chake; amuunge mkono Chacha Wangwe katika kuishambulia CHADEMA. Tayari bwana Kyara amepewa fedha na Rostam kuzunguka kuunga mkono madai ya Chacha Wangwe kuwa CHADEMA kuna ukabila, wachagga wanapendelewa na kwamba yeye amewahi kuwa makao makuu ya CHADEMA na anajua kwamba ruzuku zinatumika vibaya. Bado Bwana Rostam amemtaka Chacha Wangwe kuendelelea kubaki Dar es salaam wakati wanaendelea kutafuta 'mashujaa' wengine wa kumuunga mkono. Katika kukaa kwake Dar es salaam, ilikubaliwa kwamba Chacha Wangwe aitishe maandamano ya wanaCHADEMA Dar es salaam ya kumuunga mkono kutoka Temeke Mwembe Yanga mpaka Kinondoni Ndugumbi ya kuunga mkono hoja yake kwamba ruzuku ya CHADEMA haipelekwi wilayani. Chacha Wangwe aliwasiliana na viongozi wa Temeke kuandaa maandamano hayo. Hata hivyo viongozi wa CHADEMA Temeke walichukizwa na uamuzi wa wanaojiita wanachama wa Dar es salaam 20 wanaomsaidia Chacha Wangwe ambao wamesambaza waraka kwamba Chama hakipo Dar es salaam kokote kwa kuwa watatu kati yao walisimamishwa kuwa viongozi wa CHADEMA Dar es salaam, na kwamba suala hilo limeua uhai wa chama Dar es alaam kiasi kwamba hata mikutano ya hadhara haifanyiki. Suala hili liliwaudhi watu wa Temeke badala ya kuandaa maandamano wakaandaa mkutano na waandishi wa Habari na kutangaza wazi kuwa Chacha na watu wake ni waongo, Mkoa wa Dar es salaam ulishavunjwa na kwa mujibu wa mabadiliko ya Katiba ya 2006 Dar es saalam ni Kanda, Mikoa yake ikiwa wilaya za sasa za kiserikakali na kwamba wao Mkoa wa Temeke wanapokea ruzuku ya chama kila mwezi, wanaofisi ambayo si ya kukodi inamilikiwa na CHADEMA yenyewe pamoja na kiwanja, na pia wana utaratibu wa kufanya mikutano ya hadhara kila weekend; hivyo madai ya Chacha na wanachama hao wa Dar es salaam yamelenga kugawa makundi katika chama. Mzee Kikoti Mwenyekiti wa Temeke akatoa mwito kwa chama kumvua uanachama Wangwe. Matokeo ya Tamko hilo ni Chacha kumpigia simu mratibu bwana Semkwai pamoja na Kikoti na kuwatukana matusi ya nguoni pamoja na kuwatisha. Kutokana na hali hiyo, Chacha amesimamisha maandamano hayo kutokana na kukosa mahali pa kuanzaia na anafikiria kufanya utaratibu mwingine.

Kikao kingine kati ya Chacha na Ballile bila ya Rostam kitafanyika tena Dar es salaam, nitawajulisha yatakayojitokeza

PM
 
Back
Top Bottom