Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
- Thread starter
-
- #121
PM,
Nashukuru kuweka wazi wewe sio Chadema. maana ningekushangaa. Halafu hao hao Chadema wanakubali vipi kumweka kiongozi kihiyo kwenye umakamu mwenyekiti tena wa taifa?
Ufisadi sio wa CCM tu kumbe....
FairPlayer
FAIR UNASHANGAA HIO?...kwanini hushangai ya Mwenyekiti wa Chadema...? tuna kazi kufika huko tunapokwenda..kihiyo akiwa CCM atasemwa, lkn kihiyo akiwa mpinzani utaambiwa hao Wasomi ndio mafisadi...PM,
Nashukuru kuweka wazi wewe sio Chadema. maana ningekushangaa. Halafu hao hao Chadema wanakubali vipi kumweka kiongozi kihiyo kwenye umakamu mwenyekiti tena wa taifa?
Ufisadi sio wa CCM tu kumbe....
FairPlayer
Basi huyu chacha ni mtu hatari, duh anawatukana matusi ya nguoni na kutaka kuwapiga baadhi ya viongozi wenzake! Kama hii habari ni ya kweli na kweli tupu basi huyo sio kusimamishwa tu, bali anafaa kufukuzwa hata uanachama.
Hafai kuwa kiongozi wa wananchi, kiongozi mzuri haongozwi na jazba, bali ni msikivu, mvumilivu na anayeshaurika.
Mimi bado nasisitiza kwamba tunapotaka kumteua, kumchagua mtu kwenye ngazi nyeti hasa za kitaifa tuutafute UNDANI wake vizuri. Gharama za kumwondoa au kutengua uteuzi huwa ni kubwa sana; CHADEMA wajiandae sasa kwa gharama nyingi tu ikiwemo kulipoteza jimbo la TARIME, kupoteza MADIWANI wengi tu huko TARIME.
Nilikuwa huko mikoani na niliporejea nimekuta jambo hili ni hot katika vyombo vya habari. Jana nilimwona Rostam ITV akitetea na kuchangia "mlungula wa shilingi milioni 7". Nilisikitika sana na jinsi alivyokuwa akishangiliwa na kulishangaa Kanisa kwa kumualika mtu ambaye integrity yake kwenye jamii ni questionable kwa sasa na haikushangaza alipotumia nafasi ilie kujaribu kujisafisha. Nilikusudia palepale (pengine kwa haraka na hasiri) moyoni kwamba sitanunua CD/Album ya hiyo kwaya!
Paparzai Muwazi, si jambo kla kushangaza kuwa Spika amekasirika kwa hilo maana habari nilizo nazo ni kuwa Spika Sita ni muumini wa Usharika huo wa KKKT Kinondoni na zaidi yeye alikuwa Mdhamini (Trustee) wa KKKT (sina hakika kama bado ni Trustee wa KKKT), kwa hiyo kwa Rostam kutinga MAdhabahuni ambapo Spika ni muumini na Mtu wa muhimu ni kutaka kumuonyesha Spika kuwa yeye Rostam ni gari kubwa na ni ule Mkakati wa "Mafisadi" kutaka kumwondoa Spika.
Wito wangu kwa Kanisa ni kuwa liwe makini sana maana Ufisadi unaanza kufunguliwa milango na kutumia Madhabahu kujisafisha ni sawa na kuukaribisha Ushetani mahali patakatifu. Siamini kama Kanisa halijui kuwa Rostam ndiye mmliki wa ile Kampuni ya Dowand/Richmond isipokuwa kuna watu na uongozi wa KAnisa pale KKKT Kinondoni ambao wanatumiwa au kutumika kimkakati kwa kutoa Jukwaa na Madhabahu kwa Watuhumiwa wa Ufisadi kujisafisha kwa rushwa ya Vijisenti. Kanisani ni vema likumbuke maadniko kuwa "kupenda pesa ni chanzo cha maovu yote" (1Tim. 6:10) Ole wako Kanisa!
Chadema imefanya makosa makubwa sana kutokumfukuza Wangwe uanachama . Ni lazima Chama kiwe na misimamo yake kama mtu amefika sehemu anafanya vikao na mtu kama Kaborou bila ya ridhaa ya chama , hilo tuu linatosha kumfukuza period . Ni lazima Chama kijenge misimamo thabiti ambayo wakati mwingine inaguwa ni vigumu kuitekeleza kutokana na kitu utakachopoteza ( kiti cha ubunge) , lakini ni lazima kufanya hivyo.
Ni lazima itambulike ya kuwa hakuna mtu wala kikundi cha watu ambao ni wakubwa zaidi ya chama . Chadema ni lazima wawe wakali katika hii ishu la sivyo itaset bad precedent ! Kuhusu Rostam mimi nimekasirishwa sana na kitendo cha KKKT kumruhusu huyu mtu kutumia platform ya kanisa kueneza siasa , don't we have separation of church and state (government) . Nadhani waumini wa hili Kanisa mtusaidie , muandikieni askofu mkuu barua kali kabisa na mumuambie ya kuwa mtajitoa au amtatoa dhaka (mavuno) kama wasipokuja forward na nakuomba msamaha . Swali ninalojiuliza hili kanisa litasemaje linampenda MUNGU ambaye awajawahi kumuona lakini haliwapendi watanzania ?
Ni lazima tukemee tabia ya Rostam " Divide and rule " , huyu mtu anataka kuinject mbegu mbaya sana jamii yetu .
Mama,ukipita Igunga na kukaa zaidi ya saa moja na ukijua ayafanyayo huyu RA utatoka Machozi. Huyu si Fisadi tuu ni zaidi ya shetani kama haya yasemwayo ni kweli.Hizo pesa anazotoa sadaka huko Dar, si angepeleka jimboni kwake jamanai. Hata Mungu hapendi watu wanaotoa sadaka kwa kujionyesha. Huko kwake Igunga kuna tokota kwa umaskini yeye anatoa sadaka kwa watu ambao wameshashiba! OOh lord of Mercy!
Mama,ukipita Igunga na kukaa zaidi ya saa moja na ukijua ayafanyayo huyu RA utatoka Machozi. Huyu si Fisadi tuu ni zaidi ya shetani kama haya yasemwayo ni kweli.
Mwalasusa anapaswa kutoa tamko juu ya hili la KKKT Kinondoni kabla mambo hayajawa mabaya zaidi
Wewe acha uongo na ku spin kiuanafunzi. Igunga Rostum ni kama Mfalme kwa jinsi alivyowasaidia wananchi wa kule. Hakuna mbunge TZ aliyetoa misaada kama Rostum kwenye jimbo lake, labda anafuatwa na Mkono.
Mkiwa hamna data msiandike, msiwe driven na maandiko ya kwenye net.
FairPlayer
Kwa ninavyowafahamu VIONGOZI wa Waislamu hapa Tanzania wameshakaa mkao wa kula kwa hili lakini Rostam asidhani kuwa atawazuga Waislamu kwani wao wenyewe hawana imani na Viongozi wao wanajuwa wemngi wapo kwa maslahi ya matumbo yao tu. Yeye acha ahonge hizo pesa.
Msaidie mtu kuweza kujitegemea huo ndio msaada sio sukari na viroba vya mchele kama afanyavyo RA.Wewe acha uongo na ku spin kiuanafunzi. Igunga Rostum ni kama Mfalme kwa jinsi alivyowasaidia wananchi wa kule. Hakuna mbunge TZ aliyetoa misaada kama Rostum kwenye jimbo lake, labda anafuatwa na Mkono.
Mkiwa hamna data msiandike, msiwe driven na maandiko ya kwenye net.
FairPlayer
Mama,
Ndo maana nikasema kama huna data akae kimya. Pamoja na shutuma zake kuwa ni fisadi (ambazo hazijathibitishwa mahakamani) jamaa anaongoza kutoa misaada ya kijamii na kimaendeleo jimboni kwake. Labda ni mmoja wapo wa wabunge wanaosaidia wananchi wao. Ipo mingi sana sijui unataka specifics?, kama ni hivyo sema tuziandae na kukumwagia humu.
FairPlayer