Rostam Aziz kugeukia Waislamu, Kuibua wengine CHADEMA

Tatizo watu wakipewa vimisaada vya unga na vijisima tunaona ndo misaada ya nguvu!wakati zahanati tu zenyewe huko igunga ni taabu!Rostam hakuna alilofanya ukilinganisha na utajiri wake!
 


Umasikini sidhani kaka/dada, miundombinu yes, na hii inachangiwa na miji yake ilivyokuwa scattered. Ndugu yangu upo Tanzania au ulaya?

Mnyonge mnyongeeni lakini haki yake mpeni.

Sawa mama nikipata muda nitakushushia.
 
Sio Kwa Igunga Tu Bali Sehemu Nyingi Sana Amesaidia, Mfano Mashule N.k Hadi Tabora Mjini Wanamtegemea Rostam.
 
Hakuna mtu ambaye anachochea matatizo kama mtu anayejitahidi kutoa misaada tu! Kama ni misaada tu waache wawe wa kwanza. Ningeona mtu anasifika kwa kusema amefanya nini kusaidia kufungua ajira, kuleta mashule n.k kwenye jimbo lake ili watu waweze kujiletea maendeleo yao wao wenyewe. Leo anatukuzwa kwa kuleta Misaada!? Kwa umasikini gani wa ubongo na viungo walionao wana Igunga na Tabora "anakotegemewa"!?
 
jamaa anaongoza kutoa misaada ya kijamii na kimaendeleo jimboni kwake. Labda ni mmoja wapo wa wabunge wanaosaidia wananchi wao. Ipo mingi sana sijui unataka specifics?, kama ni hivyo sema tuziandae na kukumwagia umu.

FairPlayer

ANZA UONGO WAKO NA
1 Maji Igunga mjini hakuna, Vijijini ndio kabisa na marambo yote yamekakauka wakati bwawa la Mwanzugi maji tele lakini ameshindwa kusimamia mradi huo
2 Barabara za Igunga hazifai hata kwa mkokoteni, lakini hapo nyuma akiwa na BMW wakifungua barabara ya lami Nzega-Malendi (mpakani mwa Tabora na Singida) RA aliahidi kuweka lami barabara za Igunga, leo nashangaaa ghafula anakuwa mwanamziki wa KKKT?wakati hajatimiza ahadi hizo
3 Zahanati hazina dawa, Hazina wataalamu, kina mama wanafia huko Makomero. Igogo, Kininginila, etc hata gari ya wagonjwa hawana.

TAFADHALI BWANA ACHA UJINGA WAKO NENDA IGUNGA UONE GHARAMA YA KUWA NA MBUNGE FISADI
 

Kajenga Shule Na Barabara Fanya Utafiti Kwanza.
 

Jamani kuna mtu alikuwepo UDSM kati ya 1978 na 1979 atueleze nini hasa nilitokea kwa Chacha Wangwe?

PM, kwanini usitutajie jina la huyo mwanamke mwenzetu wa Dar es salaam aliyemshika Chacha masikio? Mi nitafurahi nikipata namba yake ya simu. Na namba ya simu ya mwanamke mwenzetu aliyetelekezwa Tarime!

Asha
 

Asha, usiingilie mambo ya mapenzi ya watu, labda kama wewe ndio mke halali wa Chacha uliyemzalia watoto 12. Lakini kama chacha mmekutana hapo chadema.....hayo mambo yake ya ndani yawache yatakutokea puani bure. Endelea kuikuza Chadema, uchaguzi Mkuu uko around the corner.
 

Kama ni kweli mtu anaweza kumtelekeza mkewe mwenye watoto 12 aliyekuwa sambamba naye kwenye kampeni za uchaguzi mara tu baada ya kushinda ubunge na kulowea Dar es salaam kwanini tusiamini kwamba anaweza kuitelekeza CHADEMA kwa kuwa sasa ameshakutana na kipya kinyemi Rostam Aziz? Haya mambo yana uhusiano kwa kweli. Maadili hupimwa kwa njia nyingi. Wala sina nia ya kuingilia mapenzi yao, nina nia ya kumshauri tu mbunge wetu kupunguza kashfa jimboni kwake. Ni vyema akarudi kwa wananchi wake huko Tarime. Unajua huko ni kijijini kitendo cha mke kukaa maisha ya tabu wakati mumewe mbunge haionekani Tarime kinasambaa jimbo zima. Nyinyi wakina Mama na Wakina baba wa Dar es salaam mnaweza kufanya hayo kwa kuwa every body has own bussiness but not in tribal communities.

Na hilo la UDSM 1978-1979 mbona hujasema chochote jamani?

Cha tunajenga, huko Zanzibar tumefanya kazi nzuri sana na umewasikia Zitto na Mnyika wakiwa Tanga. Dr Slaa yeye anafanya kazi nzuri bungeni. Tundu Lissu yeye yuko Singida anakata pori tu, anaandaa majimbo kwa ajili ya watu wengi sana huko mpaka Dewji ameshaanza kupanic, alifanya mkutano Singida Mjini akaanza kuropokaropoka

Asha
 

Ahh kumbe wengine wako majimboni na wewe unamshupalia Chacha na personal issues zake. Okay..mgawanyo mzuri wa kazi. Sasa kwa nini msimpige huyo Chacha child support, mnamkata mshahara wake anapelekewa Mama watoto wake huko kijijini, huoni kuwa huyo mama angekuwa amesaidiwa kuliko kubaki kutangaza kuwa kamtelekeza mkewe huko kijijini. Akikujibu kuwa hamtaki tena na akaamua kumtaliki je, utamlaumu na kumtangaza kwa kumtaliki mkewe?


Hivi Asha, Chadema ina wanachama wangapi kwa ujumla Tanzania?
 

Wakurya ni watu wa MITAALA mama. Wao wanaamini kuwa na mke mmoja ni sawa na kuwa jicho moja, likiingia hata mchanga tu wewe ni KIPOFU (sorry, asiyeona) siku nzima.
 


Ahhha Sasa sister, CHADEMA itamkata vipi mshahara wakati mshahara analipwa na Bunge? Sasa ndio maana nataka wenye data wamwage hapa ili pengine uwekwe utaratibu wa yeye kukatwa na Spika Sitta.

BTW: Watu wa Tarime wamelalamika kuwa CHADEMA inawapa ruzuku ya laki nne kila mwezi. Lakini Mbunge wao pamoja na kuwa anapata ruzuku ya milioni moja kila mwezi ya mbunge kwa ajili ya kuhudumia jimbo, haonekani jimboni wala fedha hizo hapeleki kwenye ofisi yake ya chama na hata ofisi ya mbunge Tarime imeshafungwa. Sasa kama anaweza kutelekeza chama chake na ofisi yake jimboni sitashangaa kama akimtelekekeza mkewe. What goes around, comes around!

Asha
 
Chama Ni Lazima Kiwe Na Uwezo Wa Ku Screen Wanachama Hususani Ktk Rank Za Wilaya Mpaka Taifa, Huwezi Ku Recruit Watu Hovyohovyo Tu Ailimuradi Kesho Upate Kura Za Wananchi, Ni Makosa Makubwa Sana Ktk Siasa Za Ushindani Hasa Ktk Nchi Yenye Mafukara Wengi.

Chadema Wajipange Na Kutafakari Kabla Ya Kuenda Mbele.

Ccm Nao Uchaguzi Uliopita Umeingiza Watu Kama Akina Jah People Wa Pale Makambako Eti Ndiye M/kiti Wa Chama Wa Mkoa Mzito Kama Iringa!! Jah People Anamshinda Aliyekuwa General Secretary Of Ccm (mangula) , What A Shame Way Of Dying!!!!!

Tujitizame Na Tuambizane Ukweli Mapema , Too Late Is Too Late
 

Hivi hii ruzuku ilisha kubalika? I mean tayali inatolewa? na je mbunge anapewa in person ama kuna ofisi ya mbunge ampapo pesa hiyo hutumwa?
(sorry mkuu just to know)
 

Kwani mkimripoti huko bungeni hawawezi mpiga child support? you have lots of alternatives kuliko huku kumwaga mambo yenu ya ndani mnakokufanya sasa. Yaani data za makamu mwenyekiti wa chama chako unatafuta hapa JF, this is serious. Okay, do as you like.

Lingine, mbona hujanijibu mna wanachama wangapi Tanzania nzima???just curious. Mwanachadema Yyeyote anayejua anaweza nijibu tafadhali, hata kwa PM.
 
Hivi hii ruzuku ilisha kubalika? I mean tayali inatolewa? na je mbunge anapewa in person ama kuna ofisi ya mbunge ampapo pesa hiyo hutumwa?
(sorry mkuu just to know)

Acha ile ya CDF bado haijaanza kutolewa. Nazungumzia ile posho ya milioni moja ambayo ipo siku zote, nje ya mshahara wa mbunge kwa ajili shughuli za jimbo

Asha
 

Wanachama kati ya laki 8 na milioni moja. Mama unavyosema utafikiri mimi ni Dr Slaa mwenye mamlaka ya kuwasiliana na bunge na kuchukua hatua. Mi ni kada tu hapa tunajadili tu. Viongozi wa CHADEMA wakipita wakipata hoja wafanyie kazi. Na nikikutana nao huwa nina kawaida ya kuwapatia.

Mbona hujasema chochote kuhusu Chacha kutoroka nchi mwaka 1978-1979 kwa tuhuma ya wizi? Hivi ni kweli jamani?
Asha
 

Tukubali kusaidiwa na Idara zinazoheshimika kama TISS kwenye SCREENING ya viongozi wetu hasa wa KITAIFA. Naamini hili lingefanyika tusingekuwa na watu kama LOWASSA, KARAMAGI, WANGWE,... Kwani MWALIMU alikuwa anafanyaje enzi za Urais wake?
 

Simaanishi wewe uchukue hatua, ila kwa vile wewe ni kada huko Chadema, wapelekee ujumbe wangu huu tafadhali kama unavyowapelekea jumbe nyingine. Samahani kwa kukutuma. Waambie Mama kule JF anauliza hakuna uwezekano wa kumshtaki Chacha kwa Sitta ili akatwe nusu ya mapato yake kwa ajili ya kulea familia, ikiwezekana hata akatwe robo tatu kwani familia yake ni kubwa!

Halafu Asha, na ukada wako wooooooooooooote hujui chama chako kina wanachama wangapi? Haya tuseme chadema wanawanachama millioni moja na wote hao wakapiga kura kumchagua rais kwa ticket ya chadema, je wana uwezo wa kuwaondoa CCM madarakani?. Nadhani kuna haja ya nyie wanachadema kufanya kazi ya ziada kutafuta wanachama wa kutosha kwanza.
 
Tukubali kusaidiwa na Idara zinazoheshimika kama TISS kwenye SCREENING ya viongozi wetu hasa wa KITAIFA. Naamini hili lingefanyika tusingekuwa na watu kama LOWASSA, KARAMAGI, WANGWE,... Kwani MWALIMU alikuwa anafanyaje enzi za Urais wake?

Hao TISS wanafanya kazi kwa maslahi ya sisiemu? kama sivyo basi wanaweza kusaidia kufanya hiyo screening ya viongozi wa vyama vya upinzani. Vinginevyo olalaaaaaaaaaa, upinzani utakufa kifo cha mende miguu juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…