Rostam Aziz: Mjadala wa Bandari unajadiliwa kishabiki. Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana

Rostam Aziz: Mjadala wa Bandari unajadiliwa kishabiki. Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Mwekezaji ambaye Mkurugenzi wa Taifa Group, Rostam Azizi amesema kuwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi Nchi imekubaliana Serikali hisifanye biashara kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na kuchochea maendeleo.

Amesema kwa upande wake hana tatizo na mjadala wa Bandari lakini katika kufuatilia mjadala huo anachukizwa mjadala huo kuwa wa kishabiki na kuibua udini na ubaguzi "Unamuona kiongozi mkubwa anaanza kuzungumza Uzanzibar na Utanganyika"

Amesisitiza kuwa mjadala huo umekuwa ukijadiliwa kishabiki sana huku akidai kuwa Bandari kuendeshwa na wawekezaji ni jambo la busara sana.

Ameyasema hayo katika mjadala unaendelea Serena Hoteli leo Jumatatu, ambao umeandaliwa na taasisi ya Media Brains “Kulinda na Kuendeleza Umoja wa Kitaifa Wakati wa Mageuzi ya Kisiasa na Kiuchumi” (Protecting and Promoting National Cohesion in Times of Political and Economic Reforms).

Baadhi ya washiriki katika mjadala huo ambao wanatarajiwa kutoa maoni ni Katibu wa TEC, Padre Kitima, Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe, Godbless Lema, Steven Wasira, Prof. Kitila Mkumbo

(Taarifa zaidi katika mjadala huu zitaenedelea kukujia).

IMG-20230619-WA0000.jpg
 
Huyu ni kabila gani? Hana uraia nchi nyingine?. Haya ndo maswali ya wazalendo ajiandae kama anataka kuyajibu.
Mnyamwezi wa Igunga Tabora

Ndiyo mbunifu alieifanya serikali kuanzisha mfumo wa Bima ya Afya

Mwaka 1995 akiwa mbunge wa Igunga alianzisha mfumo wa Bima ya Afya, mkapa aka copy kwake na kuuingiza serikalini.

Wewe mzalendo umefanya nini kwa Tanzania?
 
Back
Top Bottom