Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
naomba hicho kichwa ch ahabari kiwe hivi
RICHmond:Ikulu ya Rostam then nitaanza kuchangia kwanini Rostam wala hatishwi na haya mambo
Reliable Sources Zinasema Kuwa ..hii Richmond Wote Walikuwepo[muungwana ,rostam,na Lowassa]...muanzilishi Rostam Na Ndie Aliyewauzia Wenzake Idea...
Muungwaana Alimuweka Rizwan Kama Msimamizi Wake Na Mwenzake Akamuweka Richard...rostam Alimuweka Mfanyakazi Wake Mmoja....
Muungwana Alishtuka Mapema Akaamua Kuuondoa Rizwan Haraka ....na Kipindi Hiki Ndipo Faili Lenye Majina Ya Wakurugenzi Lilipotea Brela....na Wala Halijapata Kuonekana...
lowassa Alichelewa Kushtuka ...na Wakati Anashtuka Na Kumuuandikia Muungwaana Kusudio La Kuachana Na Richmond...mwenzake Alishashtuka Kabla Na Lishaamua Richmond Imfie Lowassa Mkononi....aondoke...na Afe Kisiasa!!!..lakini Hata Hivyo Naye Lowassa Alishajitoa Ricmond Akamuachia Rostam..
Rostam Naye Ameshtuka Late Na Kuwapa Zigo Dowans ...lakini Bado Hawezi Kujitoa Dowans Kwa Kuwa Kila Mtu Anajua Ni Yake ..na Hata Vifaa Na Baadhi Ya Wafanyakazi Wametoka Caspian....
Hakuna Namna Ambayo Muungwana Naye Na Ikulu Yake Wanaweza Kujitenga Na Richmond...kwani Kama Hakuwa Na Nia Ya Kutumia Richmond Kama Mtaji Wa Kumuangamiza Lowassa...kama Rais Alikuwa Na Uwezo Toka Awali Wa Kuikataa Richmond ...baada Ya Kuwa Ameshtuka...tusingefika Huku....
Dr. Ringo Tenga ndio alihusika na hiyo mikataba na wala si Ridhwani.Kwanza Ridhwani hajafaulu Mtihani wa kuwa Advocate.ni mwanasheria tuInasemekana kuwa huyo mtoto wa JK ndie aliyekuwa shahidi katika mkataba wa kuhamisha shughuli za Richmond kwenda Dowans,akiwa kama mwanasheria kwenye kamapuni ya IMMMA.
Inasemekana kuwa huyo mtoto wa JK ndie aliyekuwa shahidi katika mkataba wa kuhamisha shughuli za Richmond kwenda Dowans,akiwa kama mwanasheria kwenye kamapuni ya IMMMA.
Mchungaji Kishoka tutafasirie maandiko:
"Hakuna ushkaji mkubwa kuliko huu, wa fisadi mmoja kuutema ulaji kwa ajili ya washkaji zake" (Richmonduli 8:18)
"Kwa maana jinsi hii Lowassa alimpenda JK, hata akautema u-PM, ili kila aliyerichimondi asilowaswe bali awe na ulaji wa milele" (Bangusilo 3:16)
"Kwa kujiuzuru kwake nasi tumepona" Kilongola 5:9
Baada ya kusanuka ndiyo maana Lowasa kaambiwa jiondoe mapema ili issue ife lakini wameishia bango sana Bungeni kwa kuwa sasa wengi wanataka jambo hili liende Mahakamani .Na huko tutasiia mengi na Muungwana sasa tutaona kama kweli issue itaenda mbele hakutakuwa na wa kubakia katika kutajwa sawa na BoT ambayo inataka kumezwa na Richmond lakini watu wanasema next ni BoT .
nDUGU TUANDAMANE WEWE HUKJUA TOKA ZAMANI HAYA?ILA MWISHO WA HAO WAHINDI UMEKARIBIA KABISA KAMA JINA LAKO TUTAANDAMANA KUCHUKUA MALI ZAO KOTE NCHINIKweli bwana hata mimi sasa naona IKULU NI YA ROSTAM NA WAHINDI WOTE
Teh teh LOWASSA akwaambia wenzIe nami nakwenda mtaani kuwaandalia makao ili nitakapo kuwepo nanyi muwepo,ili tume zikiundwa mjue muda wa mavuno ya mafisadi umewadia.kisha akapanda ikulu kuomba JK ASIMFILISI.KAMATI ya mwakyembe ikatokea na jeshi ikamwabia NITAKAEMBUSU HUYO NDIYE.....yaaani teh teh he he he.
hii hap ya moto toka kwangu
Teh teh LOWASSA akwaambia wenzIe nami nakwenda mtaani kuwaandalia makao ili nitakapo kuwepo nanyi muwepo,ili tume zikiundwa mjue muda wa mavuno ya mafisadi umewadia.kisha akapanda ikulu kuomba JK ASIMFILISI.KAMATI ya mwakyembe ikatokea na jeshi ikamwabia NITAKAEMBUSU HUYO NDIYE.....
Ikulu: Richmond anaijua Rostam
· Ndiye aliyeileta nchini
· Lowassa alimuingiza
Na Saed Kubenea
KAMPUNI ya Richmond Devolvement Company (RDC), ni mali ya mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, imefahamika.
Taarifa za kuaminika zinamtaja Rostam kuwa kinara mkuu katika Richmond; waziri mkuu aliyengolewa na Bunge, Edward Lowassa, aliingizwa na mwanasiasa huyo.
Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Bunge iliyochunguza mkataba kati ya serikali na Richmond zinasema kwamba Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Salva Rweyemamu, ndiye aliyethibitishia Kamati kuhusu kuhusika kwa Rostam na Richmond.
Akizungumza 18 Desemba, 2007 katika kikao cha Kumi na Tano cha Kamati ya Bunge saa 10:23 jioni, Rweyamamu alilithibitishia Bunge kwamba anafahamu kampuni ya Richmond tangu Desemba 2006.
...Mwaka jana, tuliombwa na watu wa Richmond, tuwasaidie katika ku-menage media katika matatizo yao kama yalivyokuwa na kwa kweli kazi hiyo tuliianza bila mkataba, tukaifanya, alisema.
Alisema wakati huo ofisi za kampuni hiyo zilikuwa katika jengo la Mkadamu House jijini Dar es Salaam; alitukutanishwa na Gire kwa ajili ya kufanikisha kazi hiyo.
Mheshimiwa mwenyekiti our main contact person alikuwa ni mtu mmoja anayeitwa Gire nafikiri ni Mohamed, sina uhakika na jina la kwanza, Salva alikiambia kikao cha Kamati ya Bunge.
Alisema, Gire ndiye alikuwa representative wa Richmond hapa Dar es Salaam. Gire alipewa namba yangu na rafiki yangu Rostam, I have that feeling. Kwa hiyo, baada ya hapo nikawa na-deal na Gire throughout."
Katika ushahidi wake huo uliochapishwa kuanzia ukurasa 955 hadi 964 katika kitabu cha Hansard za Bunge Sehemu ya Tatu, Salva anakiri kwamba Richmond ilikuwa ni kampuni ya kitapeli.
Ushahidi huo wa mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu unathibitisha madai kwamba Richmond haikuwa kampuni ya Marekani, bali kikundi cha watu wa hapa nchini kilichokuwa na lengo la kukamua uchumi wa nchi.
Vilevile ushahidi huo unathibitisha kwamba wakubwa ndani ya serikali, akiwamo waziri mkuu aliyejiuzulu, Lowassa, alijua kila jambo kuhusu Richmond.
Huu ni ushahidi mkubwa sana na ambao hauwezi kupuuzwa hata kidogo. Kwanza, ni kwa sababu, Salva ni swahiba mkubwa wa Rostam na ni mtu wa ikulu. Ushahidi wake, lazima uwe na ukweli, alisema mbunge mmoja wa CCM, juzi mjini Dodoma.
Wakati Salva akizungumza hayo, Rostam alikanusha kuifahamua kampuni hiyo, lakini alikiri kwamba alimtambulisha Salva kwa Gire.
Mimi nawafahamu Dowans, si Richmond. Hawa nawafahamu kwa sababu kampuni yangu ya Caspian inafanya kazi pale, alisema Rostam mjini Dodoma.
Ushahidi wa Salva katika kamati unavunja minongono kwamba Kamati ya Mwakyembe iliwazushia Rostam na Lowassa kuhusu kuifahamu kampuni ya Richmond.
Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu mkataba kati ya serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, iliwasilishwa bungeni Jumatano iliyopita na ilianza kujadiliwa Alhamisi, ambapo vigogo watatu wa ngazi ya juu katika serikali waliamua kuachia ngazi.
Vigogo walioachia ngazi ni Waziri Mkuu Edward Lowassa, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na mtangulizi wake, Dk. Ibrahim Msabaha.
Kabla ya kuingia ikulu, Salva alifanya kazi katika kampuni G&S iliyokuwa inajihusisha na ushauri wa habari.
Huko alikuwa pamoja na mwandishi wa habari mwandamizi Gedion Shoo, ambaye kwa mujibu wa Salva bado anaendelea na kazi hiyo mpaka sasa.
Hivi ninavyozungumza, sifahamu kama G&S wanaendelea na kazi hiyo, kwa sababu formally siko ndani ya G&S, nilijitoa baada ya kuanza shughuli yangu mpya. Siwezi kufanya kazi zote mbili, anafafanua Salva.
Akibanwa na mjumbe wa Kamati Injinia Stela Manyanya, Salva alisema, on one side, the company was not delivering on the other side, unapewa wewe jukumu la kuiambia media kusema hapa, hii delivery itakuja tu subirini wakati huo nchi iko kwenye matatizo makubwa sana. Matatizo ya giza.
Taarifa zinasema kujiuzulu kwa mawaziri hao kunafuatia shinikizo kubwa lililotokea ndani ya Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Imeelezwa kuwa baadhi ya wajumbe wa CC, walikuja juu, wakitaja majina na kushinikiza kwamba wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi unaohusu Richmond na Akaunti ya Fedha za Nje (EPA) waachie ofisi za umma na bila mjadala.
Imefahamika kwamba wajumbe waliokuwa wakishinikiza waliongozwa na Abdulrahaman Kinana na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela.
Bunge katika kikao chake kilichopita, liliunda Kamati teule kuchunguza mkataba kati ya serikali na kampuni ya Richmond.
Kamati hiyo iliongozwa na mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.
Reliable Sources Zinasema Kuwa ..hii Richmond Wote Walikuwepo[muungwana ,rostam,na Lowassa]...muanzilishi Rostam Na Ndie Aliyewauzia Wenzake Idea...
Muungwaana Alimuweka Rizwan Kama Msimamizi Wake Na Mwenzake Akamuweka Richard...rostam Alimuweka Mfanyakazi Wake Mmoja....
Muungwana Alishtuka Mapema Akaamua Kuuondoa Rizwan Haraka ....na Kipindi Hiki Ndipo Faili Lenye Majina Ya Wakurugenzi Lilipotea Brela....na Wala Halijapata Kuonekana...
lowassa Alichelewa Kushtuka ...na Wakati Anashtuka Na Kumuuandikia Muungwaana Kusudio La Kuachana Na Richmond...mwenzake Alishashtuka Kabla Na Lishaamua Richmond Imfie Lowassa Mkononi....aondoke...na Afe Kisiasa!!!..lakini Hata Hivyo Naye Lowassa Alishajitoa Ricmond Akamuachia Rostam..
Rostam Naye Ameshtuka Late Na Kuwapa Zigo Dowans ...lakini Bado Hawezi Kujitoa Dowans Kwa Kuwa Kila Mtu Anajua Ni Yake ..na Hata Vifaa Na Baadhi Ya Wafanyakazi Wametoka Caspian....
Hakuna Namna Ambayo Muungwana Naye Na Ikulu Yake Wanaweza Kujitenga Na Richmond...kwani Kama Hakuwa Na Nia Ya Kutumia Richmond Kama Mtaji Wa Kumuangamiza Lowassa...kama Rais Alikuwa Na Uwezo Toka Awali Wa Kuikataa Richmond ...baada Ya Kuwa Ameshtuka...tusingefika Huku....