WembeMkali
JF-Expert Member
- Jun 16, 2007
- 282
- 3
Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond na Dowans Holdings S.A, baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo.
Aidha, alitakiwa aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd, ilitumiwa na Dowans.
Lakini alipoulizwa na Mtanzania jana, Rostam alisema yeye ana kampuni ya ukandarasi na amekuwa akifanya kazi na makampuni mbalimbali bila kujali mambo ya kisiasa.
Mimi ni mkandarasi, nimefanya kazi na nitaendelea kufanya kazi na makampuni mengi, sina la kuficha katika hilo, kwani kila mtu anajua kampuni yangu, alisema.
Sasa hapo ndiyo kajibu mapigo gani?.Huyu mtu siyo msafi ni mmoja wa mafisadi wakubwa na mtu wa karibu na JK. Si busara kwa Rostam Aziz kuendelea kushika nafasi katika serikali ya Tanzania kwa vile hayuko pale kwa ajili ya wananchi bali yuko pale kwa maslahi yake na wafanyabiashara wenzake wenye asili ya kiasia.
Ningeomba wanaJF kuweka mali zake hapa hadharani na kila aina ya biashara zake kwa kuwa magazeti mengi ameshayanunua.
-Wembe.