unayoyasema ni kweli kabisa lakini naweza kukuhakikishia kuwa PR machine ya CHADEMA haiko as effective kama ambavyo unavyofikiria au wanavyotaka kuimply.Ni kweli wana network nzuri na haswa toka kwa watu wa kaskazini ambao wako kwenye idara nyeti za serikali hivyo kupata "MABOMU" si tatizo lakini sasa hawawezi kukaa kutegemea mabomu tuuu. Wao ilitakiwa wawe wana ikosoa serikali kupitia mawaziri vivuli walionao.Nitakupa mfano mdogo tuuu. Unakumbuka yale maneno ya Mbowe kwenye Uwanja wa mashujaa kuwa bora serikali ya mkoloni? ili ilikuwa ni political suicide na walikuwa na nafasi nzuri ya kuirekebisha ile on the next day kuwa Mheshimiwa Mbowe alikuwa quoted out of context and so on na haikuwa nia yake kusema maneno yale katika uwanja ule...
Vile vile wanaye huyu kijana ZITTO KABWE ambaye ni avarage tuuu lakini hawawezi kumtegemea ZITTO pekeyake inabidi wawe na akina ZITTO 10 lakini tatizo ni kuwa Zitto yuko prone to gaffes, Na kama ZITTO anaweza kumoutshine leader wake kwa nini CHADEMA wasimpe specia ssistants ambao watakuwa wanampa hayo MABOMU ambayo hayatopelekea kusimamishwa au kupewa onyo?
Na yule Mzee SLAA kupeleka e-mail bungeni kutaka uchunguzi ufanywe bila ya yeye kuwa na enough materials kuback up motion yake ilikuwa ni makosa makubwa kisiasa, japo inawezekana ikawa kuna dalili za ukweli kwenye ile e-mail lakini still PR MACHINE ya CHADEMA ilifail kucapitalise na waliprove kuwa hata hizo source za "MABOMU" yako haziko that effectivekama ambavyo wengi wanafikiria.
Hivi unaweza kuniambia mara ya mwisho CHADEMA kama leading opposition paty Tanzania walitoa tamko ya Foreign Policy yetu kuhusu Majeshi yetu kuwepo SADC au kupelekwa LEBANON au performance ya balozi zutu nje?
We! we! we! we!
Nguvu ya PR machinery ya CHADEMA siwezi kuisemea kwani simo, nawe (kutokana na mtiririko wa hoja zako hapo juu) nadhani humo, ni obsever kutoka nje. NInachotaka kukueleza hapa ni kwamba CHADEMA hawafanyi kazi peke yao, kuna mtandao mkubwa unaokerwa na usanii huu na unaojua kwa kina wapi muungwana na watu wanakosea, wapi wana nguvu na wapi wana udhaifu. Upo mtandao wa watu wanaoipenmda nchi hii na walio tayari kuwekeza nguvu na akili katika kuleta mabadaliko. Hilo nalijua fika, sihisi; na ningekushauri usiidharau nguvu hiyo.
Pili, kauli ya Mbowe kuhusu serikali ya mkoloni haikuwa political suicide kam unavyodhani. Huu ni mwaka 2007 siyo 1970. Ni wananchi wangapi wanaoishi leo, wanaotegemewa, waliomuona mkoloni wakaumizwa naye kiasi cha kumuona Mbowe mbaya? Hawa anaowaaddress leo wanaishi katika mateso ambayo yanafanana na yale waliyosoma vitabuni kuhusu ukoloni. Wanaona watawala wanavyoishi kwa kutumbua na wao wanavyohangaika, na wana hasira zile zile tulizokuwa nazo dhidi ya mkoloni.
Kumbe hujajiuliza kisa cha umma kuamka sana leo na kuunga mkono hoja ya Zitto? Ni kwa sababu wananchi wanaona wanaishi maisha ya kitumwa wakatyi raslimali zao zinawatajirisha walio madarakani. Hisia zao zimejikita katika dhana ya chuki dhidi ya ukoloni mweusi, tena mbaya kuliko ule uliokuwapo - ambao hata hivyo wengi wa vijana wa leo hawakuuona. Hiyo ni political capital, sio suicide.
Kusema Zitto anamu-outshine mkubwa wake ni dhana ya ki-CCM. Katika CHADEMA wanatambua talent za watu na kuzikuza, wanajenga chama taasisi kwa nguvu ya kila mmoja, leo huyu kesho yule. Katika suala hili, aliyefukuzwa na Bunge ni Zitto kwa kile alichokisimamia, lakini alikuwa anazungumza siyo kwa ajili ya CHADEMA ila kwa niaba ya upinzani. Hamad Rashid ndiye kiongozi wa upinzani Bungeni, lakini halalamikii kuwa outshined kwa sababu hoja yao imekua. Bahati kwa CHADEMA ni kwamba hoja imesaidia kuwasha moto nchi nchi nzima na chama kinakua, hivyo njia inapatikana, na viongozi wanaitumia. Ukilitazama kwa macho ya ubinafsi, ndo utasema amemu-outshine mkubwa wake, Ni kweli kwamba kama angekuwa CCM wangeishamnyamazisha maana ndiyo system yao. Je, na sisi tujiruhusu kufikiri na kutenda kama CCM?
Tatu, kuhusu Dk. Slaa. Kumbe hujajua kinachoendelea. Hakupeleka tu internet sources bali alitumia hoja ya sources hizo kutaka serkali itoe majibu, halafu wenye sources wenyewe wakanza kufumuka. Lile likitabu limejaa documents ambazo hata kina EL wanashangaa amezipata wapi, na nyingine alikuwa hajawakabidhi anasubiri waruhusu hoja yake.
He is very well informed, na wakubwa wanajua hilo, la sivyo ndiye wangeanza naye kabla ya Zitto. Ushahidi wa hili ninao lakini sio kwa ajili ya kumwaga hapa sasa hivi. Subiri tu siku zisogee utajua ninachosema.