Tatizo kubwa tulilonalo TZ na Africa kwa ujumla ni kwamba the so called wasomi, wengi wenu mnabwekea nje ya geti (ughaibuni) na hamko well informed na maisha ya wananchi wa kawaida wanao hangaikia mlo wa siku. Wengi wenu humu, mi nadhani its high time, muombe likizo muendee Kigoma, Buzirayombo, Shelui, Mpanda,Misungwi au Kasulu muone watu wanavyoishi na muache kutegemea internet na media za kitapeli za bongo. Njoo uone tunavyoishi huku na sio kutumia data za google kuangalia maisha ya watu ambao hawana uhakika wa aspirini. Huwezi pata picha sahihi kwa mtaji huo.
Jamaa hapo juu ameelezea safi kabisa, leo ni mwaka 2007 sio enzi za chama kushika hatamu, tatizo la wengi humu ni kuamini kwamba watanzania but tuko guided na sera za unyonge na ujamaa ndo maana wengi hamuishi kumnukuu Nyerere. Jmani fikra zinabadilika.
Mi personally nilimpigia kura JK, ila leo ukiniambia nikapige kura, I swear JK hawezi pata kura yangu na si mimi pekee yangu ni wengi humu kijijini kwetu! Kwa hiyo jua watu tunaamka taratibu. Kauli ya Mbowe, ingawa mimi si Chadema ila nakubaliana nayo Heri mkoloni mweupe kuliko mkoloni mweusi. Mi naamini aliyeko nje, anajitafutia Riziki kama mwana Adamu yeyote yule. Ila, tufike point tujue mageuzi ni jukumu LETU SOTE, Tanzania si ya Chadema wala CCM! Kwa nini inapokuja swala la kuilaumu CCM tuko pamoja, lakini likija swala la kutafuta njia mbadala ya haya matatizo, wote tunaelekeza shutuma kwa Chadema na CUF? huu ni ufinyu wa akili. Mara Zitto hana data, Slaa hana hiki, Seif hana hili, we jiulize we umefanya nini? atleast wao mchango wao umeonekana, wewe umefanya nini zaidi ya kukosoa tuu, tena kwenye internet ambayo mamilioni ya wapiga kura hawafiki? Kwa lugha nyingine mtu kama huyu ni irrelevant kwa harakati za kuikomboa Tanzania kwenye lindi la umaskini, maana huna link na walengwa.
Watu mnatoa hoja kwamba watu wanaendekeza njaa ndo maana hawatoki CCM, lakini mnasahau kwamba wenyewe mko ughaibuni, mnaogopa kurudi home kwa sababu mazingira yalipo hayawapi nafasi ya kuendeleza maslahi binafsi! What hypocricy?
Yaani watanzania tuichukulie TZ kama kampuni ambayo wote hapa ni shareholders not by any reason but by birth! Kwa hiyo kila mtu anajukumu la kutetea maslahi ya kampuni kwa sababu ni mwanahisa wa kudumu na hawezi kunyang`anywa hisa zake na mtu yeyote, kwa sababu alipata hizo hisa kwa sababu yeye ni mwanachama wa kampuni kwa kuzaliwa. I will be the last person to criticize Zitto au yeyote anayefanya kitu (hata kama kina mapungufu). Kila mtu aiulize nafsi yake. AMEFANYA NINI????
Nasema tena, nimekuwa MPIGA KURA wa CCM mda mrefu, ila nimegundua tunachezewa shere hapa. na hasira zangu nitazipeleka kwenye sanduku la kura 2010. Inshallah.