Watadai barabara safi, hospital,mashule pamoja na huduma nyingi za jamii kwa mtaji wa kucheza bao na kunywa kahawa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watadai barabara safi, hospital,mashule pamoja na huduma nyingi za jamii kwa mtaji wa kucheza bao na kunywa kahawa.
How about this for Change:
Tuweke the 'alleged' ufisadi wa Rostam pembeni, halafu....
Tunajua Rostam anayo mapesa, haihitaji CCM ili apate mkate wake wa kila siku (ila labda kwa kuongeza uzito wa mkate huo. ila pengine CCM ndio inahitaji mapesa yake!
Sasa basi, katika hali hiyo Rostam ajitutumue na kuwaambia CCM kuwa liwalo na liwe, hata kama ni kumfukuza uanachama wamfukuze, lakini yeye anataka kusafisha jina lake kwa wananchi wake wa Igunga na waTanzania kwa ujumla - so he proceeds na kusema ukweli wake hadharani.
For one, mimi ntamheshimu sana kwa kitendo kama hicho, na utakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa. Wananchi tutayapima maneno yake na hata pengine kumrudishia kiasi fulani cha heshima yake kama ukweli umo katika maneno hayo.
Jambo la kusikitisha, hakuna mtu, hata hao wanaojiita 'safi' ndani ya CCM walio tayari kuonyesha ujasiri wao.
Unajua kuna kiongozi mmoja mzito wa serikali aliwahi kusema in private kuwa "....mtandao wamelikoroga hilo ni lazima walinywe...",
According to the dataz, ni kwamba wakulu wengi wasio mtandao wameamua kuakaa pembeni na kuwaangalia mtandao wakilikoroga, sasa wanawasubiri walinywe, mimi ninajiuliza swali moja muhimu kwamba hwa wakulu wanaohusishwa na ufisadi, kila kukicha tuhuma mpya, sasa wanawezaje kufanya kazi za taifa kwa ufasaha na huku pia wakishughulikia utetezi wa ufisadi wao?
I mean hivi ni kweli Rostam, sasa hivi anao muda wa kushughulikia taifa na hizi tuhuma? Mimi nafikri wale wote wanaohusishwa na tuhuma za ufisadi, ni vyema wakaanza kujiweka pembeni na uongozi, na ni wakati muafaka wananchi tukaanza kudai na hiyo sheria kwenye katiba yetu ya jamhuri!
Haihitaji ufahamu wa elimu rasmi kujua mchezo anaofanya rostam.huyu hana rekodi kabisa hata ya kusimama kuuliza swali la nyongeza bungeni tangu awe mbunge wa Igunga.ni mwoga kuongea hadharan! Kama hawez kusimama kuuliza maswali bungeni au hata kuzungumza kwenye vikao vya baraza la madiwan jimboni kwake sembuse kujibu tuhuma dhidi yake bungeni!! Tena za jinai! Hawezi.kajenga mazingira ya kuleta hofu juu ya alichotaka kusema ili hatimaye azuiwe kujieleza kama alivyotakiwa na bunge! Ni mpumbavu tu anaweza kusema namsikiliza spika na chama changu kuliko kupata nafasi ya kukanusha yale aliyotuhumiwa nayo mbele ya umma.kwa vile hata hao anaosema anawaheshimu wanawajibika kwa umma pia direct au indirectly! Heshima ipi ni bora ya spika na chama? au watu wa Igunga na watanzania wote waliompa hiyo dhamana aliyo nayo! Jambo hili liende mahakaman tu! Lakini ni dhahiri kabisa rostam hana sifa tena za kubaki kuwa kiongozi tanzania! Anaonekana laghai, tapeli na fisadi! Kwa vile profile yake yote ina walakin mkubwa, URAIA wake, ELIMU yake hata BIASHARA zake! ashukuru vile anaishi nchi isiyokuwa na uzalendo, watu ni mashabiki tu! na hata sheria zilizopo hazifuatwi! Lakini atabaki na natural dignity pale tu atazungumzia tuhuma za richmond dhidi yake kwa vielelezo siyo lazima bungeni! Hata ikibidi kuacha ubunge kwa gharama ya ukweli.
Rostam amejiandalia anguko la pili?
Ansbert Ngurumo
NILITARAJIA kwamba Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ingemfunga mdomo Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, ili asijitetee kuhusu alivyohusishwa na kashfa ya Richmond.
Ni kawaida ya kamati hii kuziba watu (wabunge wake) midomo wanapokaribia kuibua mambo mazito yatakayoivua nguo. Lakini yawezekana kwamba katika hili, sasa ndiyo inamzibua mdomo Rostam Azizi.
Rostam Azizi hakuzuka tu. Alijipanga na alidhamiria. Anaijua kamati hiyo, na amekuwa akiitumia kuziba mengine. Alijua analeta mambo mazito dhidi ya Bunge na CCM yake; na alifanya mikakati na wadau wenzake kabla ya kwenda bungeni.
Alijua waziri mkuu angeitisha kikao hicho kumdhibiti. Nimeshangaa kwamba amekubali kudhibitika!
Zaidi ya hayo alijua kwamba Spika wa Bunge, Samuel Sitta, asingeipokea na kuipitisha hoja yake moja kwa moja. Anajua madhara yake. Hata Sitta alijua kuwa Rostam Azizi anaandaa mashambulizi, kwani ni mwendelezo ule ule wa utetezi wa kambi ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujitetea na kusafisha majina yao.
Sitta alijua fika kuwa wanaosafisha majina yao ndio hao wanaosababisha kile alichokiita siasa za maji taka, za kuibua kashfa zake.
Baadhi yetu tulishaonya kuwa suala hili la Richmond halikuwa la Lowassa na Rostam pekee; na kwamba haliwezi kwisha sasa. Tulisema pia kwamba kama Lowassa asingejiuzulu, tungejua mengi makubwa, iwapo wangeanza kutajana.
Lowassa alitunyima fursa hii. Alikataa kujitetea. Alikataa kusema anachokijua. Akajiuzulu. Naamini sasa kambi yake imejizatiti upya, na hoja zake zitapatikana katika utetezi wa Rostam Azizi.
Hapa katikati yametokea mengi ndani na nje ya CCM, ambayo hata Spika wa Bunge anayajua.
Kwanza, Rostam Azizi na Lowassa wamekuwa wakilalamika kwamba walihusishwa kimakosa. Alianza Lowassa, baadaye wakubwa wakamzima kama kibatari, baada ya kuona wana Monduli wamemwekea zulia jekundu!
Sasa ni zamu ya Rostam Azizi; na ujumbe wao ni ule ule. Napenda kusema kwamba si vema kuwaziba midomo. Waachwe waseme walichonacho. Wana haki ya kujitetea.
Imesemwa sana chini chini, sasa iachwe iwekwe wazi; kwani kina Rostam na Lowassa wanadai kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Richmond iliwaonea, na ilipewa maagizo maalumu; tena nje ya muda wake.
Katika hili, kambi hiyo inamtuhumu Spika wa Bunge moja kwa moja. Si siri kwamba wakati Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, anawasilisha ripoti ya kamati yake bungeni, na kutoa hitimisho lililolazimisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa; tayari kambi ya Rostam na Lowassa ilikuwa na mafaili ya ripoti mbili mkononi.
Kwa mujibu wa kambi hiyo, ripoti ya kwanza ya kamati ya Bunge haikuwahusisha kabisa Rostam na Lowassa.
Wanadai kwamba ilipowasilishwa kwa Spika, akaikataa kwa maelezo kwamba Bunge lisingeweza kupokea ripoti isiyokamilika.
Ripoti ya pili, iliyowahusisha, ndiyo iliyowasilishwa bungeni; na wao wanadai ilitengenezwa nje ya muda waliopewa, ikaongezewa vikolezo na majina yaliyokusudiwa.
Haya ni madai ya kambi ya Rostam na Lowassa. Na ndipo hapa wanapoanzia kudai kwamba muda unaodaiwa kutumika kukamilisha ripoti ya pili haukuwa rasmi!
Tuwaamini Rostam na Lowassa? Tuiamini ripoti ya kamati ya Bunge? Lakini hatuwezi kujibu vema maswali haya hadi kwanza utetezi wa Rostam uwasilishwe na usikilizwe.
Sana sana, kambi ya kina Rostam inatufanya tujiulize leo. Mbona wanataka kujitetea leo wakati walikuwa na muda wa kufanya hivyo na kutoa vielelezo wakati wa mjadala wa ripoti hiyo katika kikao kilichopita? Je, baada ya miezi miwili kupita, jamii itaamini maelezo wanayokuja nayo sasa? Utetezi wao utaaminika kwa Bunge na mamlaka nyingine zinazohusika? Utawasafisha?
Hata hivyo, habari za kuaminika zinasema kwamba muda huu waliopewa, umewasaidia kuwasilisha vema utetezi wao kwa Rais Jakaya Kikwete, kabla ya kuupeleka bungeni.
Ni wazi kwamba rais naye ni mhusika mkuu katika mradi wa Richmond tangu mwanzo, bali hapa katikati mawimbi ya kisiasa yalimzidi nguvu.
Na kwa kuzingatia ukaribu wa watatu hao (Kikwete, Lowassa na Rostam) kisiasa na kifamilia, rais amewasikiliza na kuahidi kusaidia kuwasafisha. Kisichojulikana ni kama walidhani njia mwafaka ya kujisafisha ni kupitia bungeni.
Maana, ili wajisafishie bungeni, inabidi Bunge lifike mahali likiri kwamba liliwaonea. Maana yake, kamati ya Bunge ilikosea; hivyo hata mapendekezo iliyotoa, ambayo serikali iliahidi kuyatekeleza yalivyo, yasitishwe.
Je, watawala wako tayari kulidhalilisha Bunge kuwasafisha marafiki wa wakubwa? Lakini wengine wanasema katika siasa za Tanzania lolote linawezekana.
Kwa maana hiyo, yawezekana hata jitihada za sasa za kambi ya Rostam na Lowassa zina baraka kutoka juu. Maana baadhi ya wachunguzi na wafuatiliaji wa mambo wamegundua kuwa katika siku za karibuni, uhusiano kati ya Kikwete na Sitta umechafuka kwa sababu ya Richmond.
Niliandika suala hili kwa kifupi huko nyuma, kwamba sasa Kikwete ameogopa athari ya kujitenga na kina Lowassa na Rostam, kwa hiyo anawatafutia fursa wajisafishe; na kwamba ndiyo maana hata vikao vya CCM Butiama vilikwepa kabisa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.
Hili liliwaudhi baadhi ya wajumbe; na liliwagawa wastaafu kila mtu akajitengenezea sababu ya kutokwenda Butiama.
Walitaka Kikwete achukue msimamo wa Bunge, asikilize maoni na hisia za wananchi juu ya ufisadi.
Alikataa, kwani alishapewa dozi ya siri ambayo ilikuwa katika mafaili ya Rostam na Lowassa, akajua akiruhusu chama kiwaguse tu, watakitesa; maana wana mengi ya kuanika.
Lakini hili linawatia watawala katika mtihani mgumu. Yawezekana ni kweli kwamba hoja ya Rostam na Lowassa dhidi ya kamati ya Bunge ni kweli. Na kama ni kweli, hasira za rais dhidi ya Spika zitathibitishwa siku si nyingi.
Maana kama si kamati ya Bunge, Baraza la Mawaziri lisingevunjwa; rais asingeingizwa katika wakati mgumu unaotishia kukigawa chama chake na serikali yake.
Hata hivyo, itabidi achague moja; ama kuwasikiliza kina Rostam na Lowassa au kulisikiliza Bunge. Je, yuko tayari kutosa taasisi za utawala na kuwakumbatia marafiki? Yuko tayari kuliaibisha Bunge na kujenga heshima ya watu binafsi?
Lakini wapo watu wanaodhani kwamba lolote linawezekana. Wanaosema hivi wapo ndani ya mfumo wenyewe, na wanakumbuka kwamba miaka miwili iliyopita, Rais Kikwete alishauriwa na kuonywa kuhusu uhusiano wa serikali yake na Rostam.
Waliomuonya waliona mbali juu ya ukweli ambao sasa ndio umedhihirika. Walitaka amshukuru Rostam kwa msaada wake kwao katika kampeni za urais, lakini asimweke karibu mno katika masuala ya utawala wa nchi.
Lakini Rais Kikwete alitaka kuwa muungwana kwa waliomsaidia. Ilifikia wakati, ingawa Rostam hakuwa serikalini, alikuwa akijihusisha moja kwa moja katika mipango ya serikali, hata katika mambo ambayo kimsingi yangefanywa na mawaziri.
Baadhi ya wanahabari wanakumbuka, na kumbukumbu bado zipo, kwamba hata baadhi ya taarifa za mikutano ya viongozi wa serikali na wanahabari kuhusu maamuzi kadhaa mazuri kwa serikali zilitoka kwake kwenda vyumba vya habari.
Ajabu, zipo taarifa za baadhi ya mawaziri ambao walifanikiwa kirahisi kumfikia rais kupitia nje ya serikali. Mtu mmoja aliyemuona kigogo mmoja wa usalama wa taifa ofisini kwa Rostam, tena wakijadili masuala ya taifa, aliwahi kudokeza kwamba sasa tunakoelekea utabiri wa Nyerere unakaribia kutimia, Rostam ataiweka nchi mfukoni.
Waliotaka kumtenga Rostam na Kikwete mwanzoni mwa utawala wa Awamu ya Nne, walijua kuwa Rostam ni mfanyabiashara mtafutaji na ana malengo mengi katika siasa, ambayo hawakutaka yamguse rais.
Kwa sababu hiyo, baadhi ya wanaojua vema uhusiano wake na Kikwete, waliokerwa na ukaribu wao huo, wanamuunga mkono mtu yeyote anayeweza kuwatenganisha kwa masilahi ya taifa.
Sasa leo yanapoibuka masuala nyeti kama haya, ni dhahiri rais anakumbuka ushauri aliopewa akaupuuza. Lakini anaona pia amechelewa kumtema Rostam, maana tayari anajua mengi yanayoweza kumuangusha Kikwete mwenywe. Amfanyeje?
Inaonekana kwamba hata katika sakata hili la Richmond, kama madai ya kina Rostam ni kweli, Sitta alidhamiria kutimiza azima ya kuwatenganisha Rais Kikwete, Rostam na Lowassa, kwa sababu binafsi au hizo hizo zilizotajwa hapo juu. Kwa muda sasa amefanikiwa. Je, utengano huu utadumu hadi lini?
Jambo linalojulikana pande zote ni kwamba Kamati ya Mwakyembe haikukuta faili la usajili wa Richmond; ikahitimisha kwamba Richmond ni kampuni feki.
Lakini wajuzi wa mambo wanajua kwamba faili hilo lilikwapuliwa muda mfupi baada ya kamati ya Bunge kuundwa na kupewa hadidu za rejea.
Bahati nzuri, waliolipoteza wanajulikana, na walidhani wangetumia kumbukumbu hizo kuonyesha udhaifu wa kamati ya Bunge, kuwatetea waliohusishwa na kashfa; jambo ambalo sidhani kama litasaidia sasa.
Haya yote yakiibuka, Bunge litapaswa kujadili na hatimaye kujua nani aliiba faili la usajili wa Richmond, na alitaka kuficha nini!
Bahati nzuri nyingine ni kwamba wenye Richmond wanajulikana. Hata Rostam Azizi anawajua. Lakini sidhani kama kwa ukweli wote wa moyo wake, anaweza kuwataja bungeni, ingawa ana vielelezo vya kuwachoma wengine.
Katika hili, Rostam hana ujasiri wa kunywa sumu! Hawezi. Hatathubutu! Sana sana, atakachofanya ni kujaribu kuonyesha kwamba yeye hayumo.
Lakini lolote atakalosema Rostam sasa, likijadiliwa vema na hadharani, likachunguzwa kwa macho ya akili ya watu makini na wazalendo, litaivua nguo serikali na CCM.
Na kama linaivua nguo CCM ili wananchi wapone, kwanini Rostam anazuiwa kusema? Kwani CCM ni bora kuliko Watanzania? Kwani wizi wa wakubwa ni baraka kwa taifa?
Hii ni fursa nyingine kwa wananchi kujua makubwa zaidi kuhusu Richmond; si kwa kusikia tu hoja ya Rostam, bali kwa kuifanyia pia uchambuzi wa kina na kuona kilichomo na kinachokusudiwa.
**** mambo mawili hapa. Kwanza, hoja ya Rostam ina nia ya kufichua udhaifu fulani ambao anadhani utamsaidia kusafisha jina lake na la Lowassa. Pili, hoja hiyo hiyo itafichua kingine asichokusudia, ambacho kitamvua nguo yeye, Lowassa na Kikwete; CCM na serikali.
Hapo ndipo utamu ulipo; mtego ambao kamati ya CCM inakusudia kuuruka. Hilo la kwanza, linalenga kutoboa matundu kwenye nguzo ya Bunge, kuonyesha udhaifu wa Spika na kamati zake, na kuwajenga waliohusishwa na kashfa ya Richmond.
Spika yupo tayari kudhalilisha Bunge kwa ajili ya kuwajenga washindani wake? Hapa ndipo ulipo woga wa Spika. Je, rais atamtosa Spika katika hili?
Hili la pili ndilo linalomsumbua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Ndio wasiwasi wa Kamati ya Uongozi ya CCM. Kwa sababu za kisiasa, ni wasiwasi wa Rais Kikwete pia. Sasa akae upande upi? Tusihukumu leo. Tusubiri.
Na inawezekana Rostam akafungwa mdono. Lakini je, Bunge litaikalia hoja yake hadi lini? Je, baada ya CCM kuingilia kati kumfunga mdomo asiliaibishe Bunge na CCM, ambalo Spika anaweza kulitumia kumnyima fursa ya kujieleza, Rostam atakuwa na ujasiri kama wa Dk. Willibrod Slaa, aliyechomoa hoja yake bungeni na kuimwaga hadharani?
Na je, hata akipewa muda atakuwa tayari kusema ukweli wote kuhusu Richmond na kujibu maswali yatokanayo? Kama ana uchungu na uwezo huo, kwa nini aliikwepa Kamati ya Mwakyembe, ndani ya muda iliopewa?
Mbona analeta utetezi wake nje ya muda wa kamati? Au aliamini kwa kuwa upotevu wa mafaili kilikuwa kisiki tosha kwa kamati ya Bunge kuhitimisha kazi yake?
Na je, anadhani iwapo Bunge litaruhusu hoja yake ijadiliwe kwa uwazi, hayatazuka mengine ambayo wajumbe wa kamati waliyafunika ili mwanaharamu apite na ambayo wanaweza kuyaibua leo kudhoofisha kabisa utetezi wa Rostam? Je, yuko tayari kwa anguko la pili? Tunasubiri matokeo.
ansbertn@yahoo.com
+447847922762
www.ngurumo.blogspot.com
Kwa kweli mambo bado ni magumu sana Rostam kwa namna yoyote ile ameiweka Serikali mfukoni mwake pamoja na CCM yake Makala hii imenifanya niamini kuwa Rostam alikuwa na ajenda yake kuingia kwenye siasa.
Rostam ndio chimbuko la siasa za maji taka kwani yeye ni muasisi wa kundi la mtandao.
Rostam ndie ataefanikisha anguko la CCM
Rostam ndie aliyefanikisha kumweka JK madarakani na ndiye atakae sababisha JK atoke pale alipo sasa.
Rostam, Rostam, Rostam
Mfanyabiashara mkuwa mwenye hisa 30% Vodacom Tanzania Ltd, yeye kuonana na Rais, Mkuu wa Usalama wa Taifa na top wa serikali wala ahitaji appointment. allaa awaweke yeye walipo halafu aombe apontment uliona wapi?