Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Maji ukiyavulia nguo hunabudi kuyaoga. CCM wameshavua nguo zao ktk ripot ya mwakyembe sasa maji ya rostam lazima wayaoge. wasingevua (kuzuia ripoti ya kamati) wasingeoga
 
Hii ishu haijakaa sawa, tunahitaji ukweli zaidi, swali langu ni kwa nini Rostam alikwepa kwenda mbele ya kamati ya Mwakyembe aliyoitwa kwa mujibu wa sheria? sasa eti anataka kusema mbele ya bunge bila kuwa under oath?

Rostam na Six, ndio mtandao wenyewe haswa, the matter of fact ni Rostam, ndiye aliyemtaka Six kuchukua fomu ya u-spika, na ndiye aliyemuomba Marehemu Akukweti, ambaye originally ndiye aliyekuwa designated kuwa spika, akae pembeni, sasa wanapoanza kukaangana mbele ya public, na hasa ndani ya chombo muhimu cha taifa kama bunge, huku rais amekaa pembeni akiangalia, exactly wanafikiria na kutuambia nini sisi wananchi at at large?

Mimi nilifikiri kuwa Rostam, na huo ukweli wake angekuwa in the good hands kuusema under oath, au mbele ya sheria, kuliko kwenye kikao cha kawaida cha bunge, na kama kweli ameamua kusema ukweli, basi angetoa nafasi kwa public au wanasiasa wenziwe kuanzia upinzani mpaka CCM, wampe maswali maana najua yako mengi sana, na hasa kutoka kwetu wananchi, I mean huyu amekataa kwenda mbele ya kamati ya Mwakyembe, alichofanya ni kuvunja sheria ya jamhuri yeye na Yona, sasa here he comes na agenda ya kutaka ku-dictate his political fate kwa ku-strike a confusion political bomb,

Yes, Rostam has all the rights kuamua kusema ili kuweka mambo wazi tena hadharani, na ikiwezekana apewe, lakini kwa sababu maelezo yake ni muhimu sana kwa taifa, basi kuwe na some kind of understanding, either politically au legally, kwamba:-

1. Kwa sababu nia ipo on his side kujisafisha mbele ya umma, yaani sisi wananchi, basi apewe maswali au topic za kuziongelea kwenye maelezo yake, ili aguse kila kona ya tuhuma dhidi yake, ikiwa ni pamoja na ushiriki wake kwenye kumchafua Salim kwenye uchaguzi wa rais, na what was his role kwenye kumshinikiza Mkapa, kupindisha katiba za CCM, ili kumpitisha mgombea wake Rostam, na wale wazee Darwesh na mwenziwe walipewa na nani zile SUV mbili mpya kuzunguka Tanzania nzima kuelezea role ya Salim kwenye kifo cha Karume, pamoja na zile shillingi millioni 20.

2. Maelezo yake yote yawe under oath, meaning kwamba atakapomaliza kutakuwa na special follow up ya bunge kuhakikisha kuwa kila alilosema ni ukweli under sheria za jamhuri.

3. Asichague topic ya kuongelea au hata kama amechagua basi aongezewe upana wa field ya ku-cover maana yeye anahusika tuhuma nyingi sana, na akimaliza kuongea yaani ndani ya bunge kuwa na kipindi cha maswali na majibu yake kutoka kwa wabunge, na haya yote yaonyeshwe live au wazi ili wananchi tujue mchele na pumba vilipo,

Anything less, ni yale yale ujanja ujanja wa baadhi ya viongozi wetu, kuanzia Rostam mwenyewe na wanaomkinga sasa hivi asiseme, Spika na CCM, ndani ya bunge wanatakiwa kuitumia nafasi hii ya uamuzi wa Rostam, kuamua kusema voluntarily kwa faida ya taifa zima, na hasa sheria yetu, maana huyu akisema yote anayoyajua, basi anatusaidia taifa na kamati zisizoisha za uchunguzi kila siku na kupoteza hela za walipa kodi bure,

Ninasema hivi kwenu viongozi wa CCM, huyu Rostam aruhusiwe kusema, lakini iwe under oath ndio njia pekeee itakayotuhakikishia kuwa anaongea ukweli, na akimalaza kuongea ndani ya bunge kuwe na kipindi cha maswali kwake kutoka kwa wabunge, msilichezee hilo bunge hapo sio mahali pa mchezo ni mahali pa kutunga sheria za jamhuri, na one does not need to be a priest kujua kuwa kuwa Mungu anaheshimu sana haki na sheria na hasa zinapotengenezwa.

Ahsante Wakuu.
 
RA ana kiburi, kiburi cha pesa, pesa aliyotuibia, baada ya kutuibia akawafadhili CCM na CCM inamwabudu RA na pia kamati ile ilikuwa na wanaCCM hivyo RA kwa mazoea yake ya kulindwa na CCM alijua all gonna be ok hata asipotoa maelezo mbele ya kamati.
 
lo! natamani ipatikane manma ya kuvichomoa hivyo vielelezo toka kwenye birefcase ya Rostam,halafu tuvitundike hapa hadharani ili vitusaidie kulisambaratisha hilo lisisiemu ufisadi
 
Mitego waliyowategea wengine, inawanasa wenyewe. Kama walifungana kamba ili wasipoteane katika safari yao, wakumbuke kuwa kamba hukatikia pabovu, nadhani tunakaribia kuona kamba ikikatika
 
Unajua bongo bado tunao viongozi wenye akili na uwezo wa kuona mbali, maana ninakumbuka jinsi kigogo mmoja alivyokuwa akimwambia muuungwana, baada ya uchaguzi kuwa "...please usiulete mtandao wako ndani ya ccm, maana kwanza ninaupa huu mtandao miaka miwili tu....." na here we go!
 
Kwa mara nyingine tena CCM imeonyesha woga kuumbuka! Walitoka Butiama kwa mikogo, kumbe ni mafisi! ukweli ni vibaka watupu!

Kama kuna watakaodai wao ni CCM asili ni wapinga Ufisadi, basi nao waondoke na kuanzisha chama chao na kuwaachia mafisadi CCM koko!

Ngoma ikilia sana hupasuka.
 
maelezo ya Rostam yatapatikana..
Rostam usihofu..Tupo na wewe..Hakuna atakae Kutishia na ane kutishia yeye ndio muoga...tuna kulinda wakati wote...

viongozi acheni UKUDA
 
Ninasema hivi kwenu viongozi wa CCM, huyu Rostam aruhusiwe kusema, lakini iwe under oath ndio njia pekeee itakayotuhakikishia kuwa anaongea ukweli, .
Ahsante Wakuu.

Nadhani haitatuhakikishia kuwa anasema kweli bali itatupa haki ya kumchukulia hatua za kisheria kama amedanganya.
 
Hawataweza kuzima kila kitu kila siku, siku itafika tuu moto utawaka tena utakuwa mkubwa sana...
 
kwa CCM huu usemi wa za mwizi arobaini na kila uovu una mwisho wake haliko kabisa vichwani mwao, trust mii hawa jamaa hawako dunia yetu kabisa bado wanaamini kuwa wako safe na kuwa waTZ bado ni wajinga na hawajui vitu
 
Mwenye Makosa hapa ni spika, kwani alipodai hivyo vielelezo alisema anataka kuwapa wataalamu wake wavipitie halafu wamshauri. sasa hao wataalamu ni kamati ya Uongozi ya CCM?

Alafu mbunge anapokuwa Bungeni muda wote anakuwa under Oarth, kwa hiyo ukisema uongo bungeni kunasheria ambazo huwa zinawabana kam vile walivyozipindisha kumbana Zitto.

Wakati tume ya Mwakyembe inateuliwa wengi tulidhani itakuwa kama tume za Mr. Clean kwa hiyo huenda hata RA hakuwa na imani nayo kuwa itatumia vielelezo vyake vizuri, lakini pia Inawezekana kuwa yeye na rafiki zake walimbakiza RA kwa makusudi ili aje atumike kuwasafisha hapo baadaye yaani sasa ili wawe clean for 2010 au 2015 (kuna ajenda ya Siri hapa)
 
Mimi naomba bunge liwaeleze wabunge nao watueleze sisi ni kwa sababu zipi huyo Rostam anakatazwa kuongea, na ni kwa maslahi ya Taifa au watu binafsi??
na pia tuelezwe je kamati aliyosema huyo Fisadi spika ndio viongozi wa CCM au??
Mimi sielewi kwanini mambo ya Bunge yanaingizwa na ya chama cha CCM, hayo mambo yao, na haya ni ya maslahi ya Taifa

Vipi hivi bado dhana ya haki ya myonge itapatikana kwa hoja na sheria inafanya kazi katika nchi yetu ya Tanzania?

Mimi pia ninakumbwa na mshangao kama wako.
Ni kwa nini mambo ya Bunge yanaamuliwa na Waziri mkuu?(Waziri Mkuu ni Kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni)Yeye sio kiongozi wa shunguli za Bunge.

Kwa nini mambo ya Bunge yanaamuliwa na CCM na vikamati vyake??? Maelezo aliyotaka kuyatoa RA ni kwa Bunge na si kwa Kamati Za CCM.
Kwa muono wangu CCM hawana mamlaka ya kumzuia RA kama Mbunge kuongea bungeni zaidi ya kumvua uanachama kwanza.Wanweza kukshauri kama mwanachama wa CCM atoe hoja yake lakini sio kumzuia kama mbunge.
 
Hata tukiing'ang'ania CCM kama chama tawala - hakuna siku hata moja watanzania walio vijijini watapata auheni ya maisha yao - hawa watu wote ni mafisadi kuanzia kwa mshikaji hadi ngazi ya chini kabisa na ni wasaani wa kutupwa

Mnyonge mnyongeni ila sasaaaaaaa,haki yakeeeeeeee MPENI jamaa!!ebo
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Rostam ni mwakilishi wa watu Igunga bungeni , swali jee atawawakilisha vipi kama amenyimwa kuongea ? ...Jamani hii habari kweli ina ukweli ?

Halafu najua waziri mkuu atasema anakatazwa kuongea kwa maslahi ya taifa , ni maslahi gani hayo ? Kuna ujinga unaoendelea pale chini kutaka kuwafanya watanzania kama watoto wadogo , kwamba kuna baadhi ya habari inabidi ziwe filtered kwanza . Mimi namchukia Rostam ila kwenye hili niko naye , ni lazima tumentain same standard not only to our friends but also to our advesaries.
 
Mgaya Kingoba, Dodoma
Daily News; Saturday,April 12, 2008 @00:01

Rostam apigwa stop

MAELEZO ya Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM) kuhusu kuhusishwa kwake na kashfa ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond sasa hayatawasilishwa bungeni, imefahamika.

Akizungumza mjini hapa jana, Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema Mbunge huyo wa Igunga hataweza kutoa maelezo yake tena kwa sababu Kanuni za Bunge zinamzuia kufanya hivyo. "Kanuni ya 54, kifungu kidogo cha nne, kinamzuia kufanya hivyo.

Kanuni inaeleza wazi kuwa jambo likishazungumzwa na kutolewa maamuzi haliwezi tena kuletwa hoja kuhusu jambo hilo," alisema Sitta na kuongeza kuwa jana alikuwa anaandaa barua ya kumjibu Mbunge huyo.

Alisema kwa mujibu wa maelezo aliyoyasoma katika maandishi ya Rostam, anaona kuwa yatazua mjadala mwingine kwani itabidi Kamati Teule nayo ijibu; jambo alilosema itakuwa ni kuleta vurugu bungeni.

Kanuni ya 54, kifungu kidogo cha nne, inasomeka; "Hoja ambayo, kwa maoni ya Spika ina lengo la kutaka jambo ambalo lilikwisha kuamuliwa na Bunge katika kipindi kilichopita, halitakubaliwa na Spika isipokuwa tu kama ni hoja ya kutaka uamuzi wa Bunge uliokwisha kufanyika ubadilishwe.
Kanuni ya 54, kifungu kidogo cha nne, inasomeka; "Hoja ambayo, kwa maoni ya Spika ina lengo la kutaka jambo ambalo lilikwisha amuliwa na Bunge katika kipindi cha kumi na miwili iliyopita kabla ya kikao kinachoendelea lifikiriwe tena,
halitakubaliwa na Spika, isipokuwa tu kama ni hoja ya kutaka uamuzi wa Bunge uliokwisha fanyika ubadilishwe.

Awali akizungumza na gazeti hili, Rostam alisema kwamba anamsikiliza Spika kwa sababu anamheshimu, anakiheshimu chama chake; lakini alisisitiza pia kuwa hahusiki na suala la Richmond; kwa vielelezo na uthibitisho alionao.

Katika mkutano wa 10 wa Bunge, Februari mwaka huu, Sitta alisema kwamba Rostam atawasilisha maelezo yake kuhusiana na suala hilo baada ya kuhusishwa nalo, lakini hakuwapo bungeni wakati huo.

Kashfa ambayo Rostam alitaka kuizungumzia iliundiwa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ambayo iliwasilisha ripoti yake katika mkutano huo na kusababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kutokana na ofisi yake kuhusishwa nayo.

Mbali na Lowassa, mawaziri wawili, Dk. Ibrahim Msabaha (Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Nizar Karamagi (Nishati na Madini), walijiuzulu baada ya wao pia kudaiwa kuhusika katika kuibariki kampuni hiyo ambayo Kamati Teule ilidai ilikuwa ya kitapeli na yenye utata.

Akizungumza jana, Rostam alisema kinachofanyika ni mchezo wa kuigiza na kwamba yeye anamsikiliza Spika, anamheshimu; anasikiliza maelekezo ya chama chake na akapuuza watu wanaoeneza umbea kuwa chama kitamdhibiti.

"Mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Nasikiliza maelekezo ya chama changu. Lakini pia mimi ni Mbunge niliyetokana na CCM. Mimi ni mtu mzito katika chama. Siwezi kudhibitiwa kwa umbea," alisema.

Baada ya kuijadili ripoti ya Richmond, wabunge walitoa mapendekezo 23 ambayo yalipelekwa serikalini kwa nia ya kufanyiwa kazi. Tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema yamekwisha kufanyiwa kazi na wanayo ripoti ya wataalamu iliyoyapitia mapendekezo hayo na kutoa ushauri.
 
tushaaambiwa hata kwenye misiba kila watanzania wanaozaliwa ni laan watarajiwa upo??????swala tufunge na kusali na kuomba niliomba siku moja kabla haya ya richmond ayajaj jf tufunge jumatano waliosikilza waliona =nguvu ya maombi hivyo swala ni kutenda hata nyie wa tanzania si mnasoma tu tufunge kweli ....nguvu za bwana zinatenda kazi....hata tukilazimishwa kurudi tanznaia kwa maombi rudi mtu
 
mi sijajua sheria na ibara zinazowalinda ila kama inawezekana jamani tufunge na kuomba inaonekana kuna mambo mkubwwa kwenye hayo melezo ambayo ama ingetishia uhai wa chama na amani nchin kama ndugu yetu mkuu mapinda anavyodai mafisadi hatari ukiwafatwa watakulipua looooooohhhhh
tuombe mungu kwa hili ajidhihirishe natumaini wabunge wakiomba maelzezo kama wao hawatanyimwa so hali alisi tutaifahamu tulisem ana tutasema kuna siri kubwa richmond na uko tunapoenda ni pabaya hata kuliko tulipotoka...,.,.,.........
 
rufiji kula hiyo

Mgaya Kingoba, Dodoma
Daily News; Saturday,April 12, 2008 @00:01

tanzaniadaima
12apr08 00:01:02
 
Back
Top Bottom