Ufunuo wa Yohana
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 319
- 72
Maji ukiyavulia nguo hunabudi kuyaoga. CCM wameshavua nguo zao ktk ripot ya mwakyembe sasa maji ya rostam lazima wayaoge. wasingevua (kuzuia ripoti ya kamati) wasingeoga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ishu haijakaa sawa, tunahitaji ukweli zaidi, swali langu ni kwa nini Rostam alikwepa kwenda mbele ya kamati ya Mwakyembe aliyoitwa kwa mujibu wa sheria? sasa eti anataka kusema mbele ya bunge bila kuwa under oath?
Rostam na Six, ndio mtandao wenyewe haswa, the matter of fact ni Rostam, ndiye aliyemtaka Six kuchukua fomu ya u-spika, na ndiye aliyemuomba Marehemu Akukweti, ambaye originally ndiye aliyekuwa designated kuwa spika, akae pembeni, sasa wanapoanza kukaangana mbele ya public, na hasa ndani ya chombo muhimu cha taifa kama bunge, huku rais amekaa pembeni akiangalia, exactly wanafikiria na kutuambia nini sisi wananchi at at large?
Mimi nilifikiri kuwa Rostam, na huo ukweli wake angekuwa in the good hands kuusema under oath, au mbele ya sheria, kuliko kwenye kikao cha kawaida cha bunge, na kama kweli ameamua kusema ukweli, basi angetoa nafasi kwa public au wanasiasa wenziwe kuanzia upinzani mpaka CCM, wampe maswali maana najua yako mengi sana, na hasa kutoka kwetu wananchi, I mean huyu amekataa kwenda mbele ya kamati ya Mwakyembe, alichofanya ni kuvunja sheria ya jamhuri yeye na Yona, sasa here he comes na agenda ya kutaka ku-dictate his political fate kwa ku-strike a confusion political bomb,
Yes, Rostam has all the rights kuamua kusema ili kuweka mambo wazi tena hadharani, na ikiwezekana apewe, lakini kwa sababu maelezo yake ni muhimu sana kwa taifa, basi kuwe na some kind of understanding, either politically au legally, kwamba:-
1. Kwa sababu nia ipo on his side kujisafisha mbele ya umma, yaani sisi wananchi, basi apewe maswali au topic za kuziongelea kwenye maelezo yake, ili aguse kila kona ya tuhuma dhidi yake, ikiwa ni pamoja na ushiriki wake kwenye kumchafua Salim kwenye uchaguzi wa rais, na what was his role kwenye kumshinikiza Mkapa, kupindisha katiba za CCM, ili kumpitisha mgombea wake Rostam, na wale wazee Darwesh na mwenziwe walipewa na nani zile SUV mbili mpya kuzunguka Tanzania nzima kuelezea role ya Salim kwenye kifo cha Karume, pamoja na zile shillingi millioni 20.
2. Maelezo yake yote yawe under oath, meaning kwamba atakapomaliza kutakuwa na special follow up ya bunge kuhakikisha kuwa kila alilosema ni ukweli under sheria za jamhuri.
3. Asichague topic ya kuongelea au hata kama amechagua basi aongezewe upana wa field ya ku-cover maana yeye anahusika tuhuma nyingi sana, na akimaliza kuongea yaani ndani ya bunge kuwa na kipindi cha maswali na majibu yake kutoka kwa wabunge, na haya yote yaonyeshwe live au wazi ili wananchi tujue mchele na pumba vilipo,
Anything less, ni yale yale ujanja ujanja wa baadhi ya viongozi wetu, kuanzia Rostam mwenyewe na wanaomkinga sasa hivi asiseme, Spika na CCM, ndani ya bunge wanatakiwa kuitumia nafasi hii ya uamuzi wa Rostam, kuamua kusema voluntarily kwa faida ya taifa zima, na hasa sheria yetu, maana huyu akisema yote anayoyajua, basi anatusaidia taifa na kamati zisizoisha za uchunguzi kila siku na kupoteza hela za walipa kodi bure,
Ninasema hivi kwenu viongozi wa CCM, huyu Rostam aruhusiwe kusema, lakini iwe under oath ndio njia pekeee itakayotuhakikishia kuwa anaongea ukweli, na akimalaza kuongea ndani ya bunge kuwe na kipindi cha maswali kwake kutoka kwa wabunge, msilichezee hilo bunge hapo sio mahali pa mchezo ni mahali pa kutunga sheria za jamhuri, na one does not need to be a priest kujua kuwa kuwa Mungu anaheshimu sana haki na sheria na hasa zinapotengenezwa.
Ahsante Wakuu.
Kwa mara nyingine tena CCM imeonyesha woga kuumbuka! Walitoka Butiama kwa mikogo, kumbe ni mafisi! ukweli ni vibaka watupu!
Kama kuna watakaodai wao ni CCM asili ni wapinga Ufisadi, basi nao waondoke na kuanzisha chama chao na kuwaachia mafisadi CCM koko!
Ninasema hivi kwenu viongozi wa CCM, huyu Rostam aruhusiwe kusema, lakini iwe under oath ndio njia pekeee itakayotuhakikishia kuwa anaongea ukweli, .
Ahsante Wakuu.
Mimi naomba bunge liwaeleze wabunge nao watueleze sisi ni kwa sababu zipi huyo Rostam anakatazwa kuongea, na ni kwa maslahi ya Taifa au watu binafsi??
na pia tuelezwe je kamati aliyosema huyo Fisadi spika ndio viongozi wa CCM au??
Mimi sielewi kwanini mambo ya Bunge yanaingizwa na ya chama cha CCM, hayo mambo yao, na haya ni ya maslahi ya Taifa
Vipi hivi bado dhana ya haki ya myonge itapatikana kwa hoja na sheria inafanya kazi katika nchi yetu ya Tanzania?