Mpasuko bungeni
na Charles Mullinda
TAnzania Daima~Sauti ya Watu
SASA kuna kila dalili kuwa hatua ya Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumzuia Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni ya kutetea hoja zake zote alizozitoa dhidi ya Kamati Teule iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, inaweza kuligawa Bunge.
Dalili hizo zimeanza kuonekana baada ya wabunge kuanza kuonyesha tofauti za wazi za msimamo kuhusu hatua hiyo, huku baadhi wakikubaliana nayo kwa maelezo kuwa ni kwa masilahi ya CCM na kulinda hadhi ya Bunge, na wengine wakionekana kuipinga.
Wabunge kadhaa waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili walieleza kuwa, hatua hiyo ya kamati ya CCM inatoa picha kwamba sasa Bunge limeanza kuyumba na kutumika vibaya baada ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuonyesha mwelekeo wa kuyumba.
Aidha, kundi hilo la wabunge limekwenda mbali zaidi na kueleza kuwa, hatua hiyo ya uongozi wa CCM ambao umekubaliwa pia na Sitta, unalenga kuficha siri ya mkakati uliotumika kuwaangusha baadhi ya mawaziri, akiwemo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kwa sababu za kisiasa kwa kutumia kashfa ya Richmond.
Kwa mujibu wa wabunge hao, hatua hiyo inathibitisha kuwepo kwa mkakati maalumu wa kuwanyamazisha ama kuwamaliza kisiasa baadhi ya wanasiasa, unaoendeshwa na kundi moja la wanasiasa ndani ya CCM kwa kutumia kivuli cha Bunge.
Habari zaidi zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa, baada ya kuvuja kwa habari kuwa Rostam amezuiwa kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni, baadhi ya wabunge wameanza kujipanga kumshinikiza Spika Sitta kutoa nafasi kwa mbunge huyo kutoa maelezo yake ili ukweli ufahamike.
Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa ambaye jana alizungumza na Tanzania Daima Jumapili kupitia simu yake ya kiganjani, alisema Bunge limeanza kupoteza mwelekeo na sasa linaelekea pabaya.
Dk. Slaa alieleza kushangazwa kwake na hatua ya Spika wa Bunge, kuanza kuwa na maamuzi ya kutatanisha, ambayo yanaonyesha dhahiri kuwagawa wabunge.
"Tunaelekea pabaya, Spika anashangaza, anaanza kuwa na maamuzi ya kutatanisha ambayo ni dhahiri yanawagawa wabunge. Rostam alitakiwa ndani ya Bunge na Spika mwenyewe kutoa maelezo ya kutetea hoja zake, leo anakuja na maelezo yanarudishwa kwenye Kamati ya CCM wakati wengine wanapelekwa kwenye Kamati ya Maadili!
"Tunarudi nyuma kwenye Bunge kuwa chombo cha CCM. Spika anakubali kutumika, tunajua aliitwa Butiama na kuagizwa mambo yote yanayohusu chama chao yajadiliwe kwanza ndani ya chama. Maagizo hayo yanadhihirishwa na hiki anachokifanya sasa," alisema Dk. Slaa mmoja wa wabunge makini na wenye msimamo thabiti katika masuala ya msingi.
Alisema ingawa Spika amekwishatamka kuwa ameacha kuhudhuria vikao vya chama chake, hilo halitoshi, anachotakiwa kufanya ni kuachia nyadhifa zote alizonazo katika CCM ili awe na uwezo wa kukataa kutumiwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid (CUF) ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, naye alisema Spika Sitta ameanza kuyumba na kueleza kuwa asidhani kwamba limekwisha kwa sababu anatarajia kulifufua tena kesho (Jumatatu) kwa kuomba mwongozo wa Spika kuhusu kanuni iliyotumika kumzuia Rostam kutoa maelezo yake kama alivyotakiwa katika kikao cha Bunge kilichopita.
Alisema hatua iliyofikiwa na Kamati ya Uongozi ya CCM dhidi ya Rostam si sahihi, kwa sababu inamnyima haki yake ya kikatiba, kisheria na kiraia ya kujitetea dhidi ya tuhuma alizoelekezewa, na pia ufafanuzi aliotakiwa kuutoa na Spika.
"Chombo kilichotoa uamuzi huo si cha kikatiba, hakihusiani na Bunge. Spika anapaswa alete hoja ya kumzuia Rostam bungeni na Bunge ndiyo liamue, anachoogopa ni nini? Nina shaka na maamuzi hayo.
"Hili halijaisha, Jumatatu (kesho) nitamuomba muongozo Spika kuhusu kanuni iliyotumika kumzuia Rostam, na ninamshauri arudi kwenye kanuni na hansard aache kuyumba," alisema Rashid ambaye anaheshimika kutokana na kuwa na misimamo isiyoyumba.
Mbunge mwingine aliyezungumzia suala hilo ni William Shelukindo (CCM) wa Bumbuli ambaye alisema uamuzi uliochukuliwa na kamati hiyo ya CCM ni sahihi kwa sababu, suala la kamati teule iliyochunguza Kashfa ya Richmond lilishamalizika baada ya kamati hiyo kukabidhi ripoti yake kwa Spika, hivyo haliwezi kujadiliwa tena.
Alisema anazifahamu vyema kanuni za Bunge kwa sababu ni mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge na kusisitiza kuwa, uamuzi huo wa kuzuiwa kwa Rostam kutoa maelezo yake ni sahihi.
"Mimi ni mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge, ninazifahamu vyema kanuni, hii Richmond basi jamani imekwishafika mwisho. Jambo likishapitishwa na Bunge haliwezi kurudishwa tena. Kamati teule haipo tena, ilishamaliza kazi zake, hivyo hata kama Rostam atasimama na kutoa maelezo yake, hakuna mtu wa kujibu. Labda Rostam kama bado anataka kulizungumzia hili alilete kwa njia nyingine, lakini hii ni wazi Spika hatamruhusu, na ni sahihi," alisema Shelukindo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), alieleza kuwa jambo hilo ni zito, hivyo halipaswi kuongelewa ovyo ovyo.
Alisema binafsi hayuko tayari kulizungumzia, lakini kama litafikishwa bungeni wabunge wataonyesha msimamo wao.
Mwanasiasa mmoja aliyedai kutokuwa upande wowote katika suala hili alieleza kuwa, Spika Sitta ameonyesha wazi kulinda jambo fulani katika suala hili, kwa kutoa kauli zinazotafautiana kila anapokuwa akizungumzia au kuulizwa kuhusu Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni.
"Huyu mtu ni mwanasheria, amekaa bungeni siku nyingi, inawezekana kweli hajui vizuri kanuni za Bunge, mwanzo alitangaza bungeni kuwa Rostam anawajibika kuwasilisha maelezo yake binafsi kuhusu kile alichokisema bungeni katika kikao hiki cha Bunge.
"Muda umefika, ameulizwa na vyombo vya habari, mwanzo alisema amemzuia kwa sababu alitaka kuwasilisha maelezo hayo bila kumpelekea ayapitie na kwamba alimuagiza ayaandike ampelekee, ayasome ndipo amruhusu, baadaye kasema wataalamu wake wanayapitia, kisha ameibuka na hii mpya eti haruhusiwi kwa sababu kanuni za Bunge zinamzuia kuyawasilisha, huyu ni mtu wa kutilia shaka," alisema mwanasiasa huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Katika kipindi kisichozidi siku tano, Spika Sitta ametoa kauli kadhaa katika vyombo vya habari kuhusu Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni.
Jumatano wiki hii, alilieleza gazeti dada la Tanzania Daima kuwa, amemzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake binafsi bungeni kwa sababu alikuwa hajatimiza masharti ya kanuni za Bunge.
Alisema mbunge huyo wa Igunga alikwenda ofisini kwake Jumatano ya wiki hii akiwa hajaandika maelezo yake na akiuliza ni lini atapangiwa kujieleza na ndipo yeye akamweleza kuwa, hawezi kumruhusu kusimama bungeni kuyawasilisha mpaka atakapoyaandika na kumkabidhi ili ayapitie kwanza.
Siku moja baadaye, Sitta alilieleza gazeti hili kuwa alikuwa ameshapokea maelezo ya Rostam na akayakabidhi kwa washauri wake kwa ajili ya kupitiwa na kupatiwa ushauri kabla ya kumpangia tarehe ya kuyawasilisha au la.
Aidha, siku hiyo hiyo, Sitta alikiri kuhusu uamuzi wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuitisha kikao cha Kamati ya Uongozi ya CCM kujadili masuala mbalimbali, likiwamo hilo la Rostam.
Taarifa ambazo Tanzania Daima ilizipata kutoka ndani ya kikao hicho, zilieleza kuhusu kufikiwa kwa uamuzi wa Rostam kuzuiwa kuwasilisha hoja yake na habari hiyo ikaandikwa katika toleo la jana gazeti hilo dada la hili.
Jana hiyo hiyo, Sitta alikaririwa na gazeti moja (si Tanzania Daima) la kila siku akieleza kuwa, alikuwa amemzuia Rostam kutoa maelezo yake kwa sababu maelezo aliyoyaandika yangeweza kusababisha vurugu bungeni.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 12 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
eeh nashangaa haman bado maoni watanzania bado hamjaamka. nayi wa USA semeeni hili.
Ya kwangu mafupi ni haya; watanzania tupo kwenye njia panda ambayo inabidi tuamue kunyoa au kusuka.Namkumbuka mzee ruxa wakati ule alisema klorokwini ni chungu ila lazima tuimeze ii tupone malaria. Tukubali tukatae huu ndio muda rasmi wa wa kuweka mambo wazi Spika anajaribu kuzima moto kwa kufunika na nyasi kavu. Hii si sawa na ni hatari zaidi.Lowasa alijitoa kafara akijua itakuwa mwisho na watanzania wataridhika na kuiacha serikali kuendelea kula kimya kimya.Huu ulikuwa mtazamo mbovu wa jambo kubwa la kitaifa kama hili la maslahi ya taifa.
Ni vyema ROSTAM akaeleza alishiriki vipi na nani kuhujumu nchi yetu. CCM wasimpikie cha kusema kwani maswali yataendelea tu. pia MASABAHA naye aeleze kwa nini alijiuzulu na wengine wote ili tuamue cha kuwafanya sisi kama watanzania tunaobeba mizigo ya ufisadi.Iweje mtu aombe msamaha kama hana kosa? watuambie makosa yao wameyajua?
Huu uwe mwisho wa serikali ya siri siri has akuhusu maslahi ya taifa.WABINGE MUWE NA MSIMAMO ILI TUANZE UPYA . NI BORA SASA BUNGE LIKAVUNJWA NA TUANZE UPYA NA SERIKALI MPYA . HILI HALIKWEPEKI KWANI SASA MAMBO YA CCM HAYABEBEKI TENA.
HUU NI MTAZAMO WANGU.
na emmanuel , Sweden, - 13.04.08 @ 10:33 | #6294
Hivi hakuna njia yeyote ya kumtoa huyu spika wa Bunge na akachaguliwa mwingine? Watu wanaotaka kuiyumbisha nchi hii nimeshaamini ni huyu spika, huyu ataleta machafuzi makubwa katika nchi hii.
Hivi ninyi Wabunge mlimchagua kwa kufuata vigezo gani? Mbona hamna kitu ktk akili yake jamani!! anatuaabisha kabisa.
Mimi nahisi ktk ripoti ya Rostam, nafikiri Spika na Kikwete wake watakuwa wamehusishwa na hataki wajulikane.
na Amani, Yemeni, - 13.04.08 @ 10:55 | #6298
Kwanza huo mpasuko wa Bunge uundiwe serikali ya Mseto kama anayoitaka Seif Sharifu na ******* wenziwe.Pili mliambiwa zamani kuwa huyo Mwakiembe katumiwa kuwaumiza wengine kisiasa, hamkusikia na mlimpigia makofi kwa ripoti yake ya ki-aina-aina!
Mimi nahisi hii Tanzania yote imejaa mafisadi hata waandishi wa habari nao wamo kwani hawajui hata kupima mambo.Wao ni kuandika tu ili gazeti linunuliwe.
Kama kweli Rostam kazuiliwa basi wabunge wahoji hilo.Tumechoka na hizo kelele za kila siku. Nyote wezi nyie!
na ABDI JUMA IBRAHIM, Tanga, - 13.04.08 @ 11:28 | #6311
Jana nilisema huyu Spika mbali ya kuwa mwanasheria na mzoefu,maji yamemzidi,yamefika shingoni,amejitahidi kuficha na kudhibiti lakini wapi,sasa ndio kajichanganya kabisaaa na amedhihirisha alivyo na mapungufu makubwa,uwezo mdogo wa kuamua na kujua aseme nini kwa wakati upi,haswa kwenye mambo mazito ya kitaifa.
Baada ya Dr mwakyembe kuliomba bunge litake maelezo dhidi ya shutuma zilizotolewa na Rostam, Spika kwa kauli yake mwenyewe alimtaka Mbunge huyo(Rostam) kutoa maelezo, "la sivyo utakuwa umeridhalilisha bunge" alisema spika wetu.
Sasa nashangaa mtu huyo huyo anasema Rostam haruhusiwi kutoa ufafanuzi wa alichokisema.Hivi huyu ni spika kweli.Tatizo letu mtu akikaa serikalini kwa muda mrefu tunaona anafaa,ukweli kuhusu capability na uwezo wake mdogo wa kufikiri na kufanya maamuzi umeonekana(critical thinking and prompt decision making).
Sishangai,huyu Spika alipewa nafasi hiyo kama hatua ya CCM kujirudi,ni fadhila ya mpasuko wa kimtandao ndani ya Chama cha mapinduzi.hana uwezo,maamuzi yake hayaendeni na CV yake,kabakia kujigamba kama mwana ngonjera. Watanzania wa sasa hawataki porojo na majigambo,wanataka kazi na tija,wanaujua ukweli na wanataka bunge lisimame kwenye ukweli.
Kama ni kweli kuna hujuma zilikuwepo, kuwatenga baadhi ya wanamtandao tunataka tujue,si haki,na ni hatari kubwa kwa usalama wa nchi,ni kuidhalilisha hiyo demokrasia mnayoimba kila kukicha ,ripoti ya Dr Mwakyembe niliipenda sana na nafikiri ni ripoti ya kwanza nzuri,iliyotolewa na kamati lukuki zilizokwishaundwa hapo zamani.Lakini sitapenda watuhumiwa wazuiwe kutoa ukweli na kujitetea.Ndiyo! Rostam alikuwa akitafuta ushahidi kama kamati ilivyotafuta ushahihidi,Je? haki iko wapi? sheria iko wapi? narudia tena demokrasia tunayoimba kila siku iko wapi?
Huyu fisadi wa kihindi(nitabadilisha sifa yake nitakaporidhishwa na utetezi wake)apewe nafasi,tena ya kipekee.Penye ukweli huongo ujitenga.Tena ni wakati muafaka wa kujikaanga yeye mwenyewe kwa mafuta yake.
Kwa muono wangu kuna kitu kikubwa zaidi ya sisi tunavyofikiria.kuna siri kubwa inayofichwa,maadam,ndio kumekucha siri itavuja na hapo ndipo tutajua ukweli halisi wa sakata zima la ufisadi.
Eti wanalinda masilahi ya chama.Ufisadi ni kosa la jinai,ni kosa kwa jamhuri na si chama tawala.je siku CAFU au Chadema wakichukua nchi nao wachote uchumi wetu na wawafunge watu midomo eti ni kwa ajili ya masilahi ya chama.Kwanza mi sielewi masuala ya bunge chama kinaingia vipi.
Narudia kusema.Hiki chama cha mapinduzi hakina jipya,na natabiri mwisho wao unakaribia.Vitabu vyote vya dini vinasema Hata Mungu hapendi kuona watu wake wakiteseka kwa sababu ya watu wachache.Wezi, majangiri,wauaji,Kaeni chonjo,kwani mwenye nguvu anawaletea mtafaruko na mgongano ili wananchi wanaonyanyasika lakini wagumu wa kimaamuzi waamke,waone kwamba sasa basi,liwalo na liwe.Hakika mtaripa madhambi yenu hapa hapa,mmefanya kufuru kujitengenezea maisha ya peponi kwa mgongo(on expence of)wa wananchi fukara,sasa jehanam inanukia,itawakuta hapa hapa,masaki,osterbay,ocean road,upanga nk.
Hakika nchi itatamalaki,ukweli unaofichwa utakapokuwa wazi.nasema mtaficha sana lakini utatoka tu kwani upepo wa mageuzi umeanza, na umeanzia ndani,umeanzia chunguni,ukitoka utakwenda kwa wananchi,watu ambao siku zote mnawarubuni waendelee kunyanyasika,waendelee kutaabika.Hakika mlikuwa mkiwapa matumaini hewa.
Wakati wa kuwadanganya sasa utakwisha kwani wameujua ukweli.hapatakuwepo porojo za kasi mpya au kasi ndogo!hapatakuwepo na njozi za uchumi umepanda kwa kasi ya asilimia 6.1% wakati hali yao ya maisha inaendelea kudhorota!hapatakuwepo na kupaa au kushuka kwa ndege ya maendeleo!Nasema ni wakati huo hakutakuwepo na tupeni mda kidogo,tunajenga mikakati mipya.
Sijui sasa mtakuja na slogan(kauli mbiu) gani ili kuendelea kuwarubuni, kuwatia hofu na kuwajengea matumaini ya kufikirika hao wapiga kura.Hata mkija na " maendeleo ya sunami",Kasi ya upepo!maendeleo ya kimbunga!", nasema hakuna atakayewasikiliza.
Mimi sina chama na katika uongozi wa juu wa vyama vyote,sioni kiongozi wa kutukomboa.angalau naona mwanga kwa baadhi ya viongozi wa chini wa baadhi ya vyama vya upinzani.ndiyo! sioni wa kutuongoza na tunataka wa kutuongoza na kutukomboa, tunataka wa kufanya mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi.Ebu angalia bahati waliyopata majirani zetu Rwanda.Hakika wamempata wa kuwakomboa,tunataka watu kama kagame,Kiongozi ambaye akiwa anakula, anafikiria maendeleo ya wananchi wake,akiwa amelala anaota njozi za kimaendeleo na anazitekeleza hata kama ni chungu kama chroloquine kwa viongozi wenzake,yeye cha kwanza ni maendeleo na maisha bora kwa wananchi wake.Hatutaki Raisi mtalii, kila kukicha yeye yuko ughaibuni.Ni wakati gani atakaa chini.atakaa kitako,kuona na kutafakari maisha ya anaowaongoza.ndio maana anaishia kupokea taarifa zilizotengenezwa kumridhisha,si wamekwisha jua ni mpokea taarifa.
Nasema,wananchi hawatataka mkwala na mbwembwe za kutembelea mawizarani.Eh!jamani,viongozi wetu kwa usanii kweli awajambo.uko ni kudhihirisha kuendeleza utalii,lakini huo nauhita utalii wa ndani.wananchi hawatataka hotuba za kila mwezi,hotuba zisizo na mantiki,hotuba za kuwapumbaza.kwani watakuwa wameujua ukweli,wameangaziwa mwanga mpya.
Nawaona(I can see)(I ENVISION) wananchi wakijutia makosa waliyokuwa wakiyafanya kwa miongo mingi.wakitaka mapinduzi sasa,wakitaka mapinduzi katika box la kura.Nawaona wananchi wasioambilika tena,hawaelewi la mkwezi au mgema au mpanda nazi,wananchi waliotayari kujitoa muhanga kwa ajili ya masilahi ya nchi yao.Hakika hayo ndio maono yangu na hayako mbali.ndio kwanza yananza kufukuta ndani ya chama cha wabadhirifu.kupitia kwa kinara wao Rostam na Lowassa.
Naona mpasuko mkubwa unaoambatana na anguko la dola linalotoa kishindo kikubwa.Hakika anguko la dola yenye nguvu kama ile ya kirumi.Ni suala la muda,labda dola ilyopo ifanye mapinduzi ya ndani,itubu,iwarudie ilyowakosea na kuwaambia sasa basi,hatuwaibii tena na mabilioni tuliyoiba haya hapa,chukueni.Najua hiyo ni ndoto na haiwezekani,kinachobakia ni kutimilika kwa ndoto yangu ya kwanza ya mapinduzi ya kifikra vichwani kwa walala hoi na hatimaye kwenye box la kura.
na romwald, USA, - 13.04.08 @ 11:37 | #6314
kama Lowasa,Karamagi, na Msabaha walijitetea, kwa nini huyu Rostam ambaye ni mtuhumiwa mkuu asijitetee?
Kwa nini tutoe uamuzi wa upande mmoja tu (uliotolewa na Kamati ya Mwakyembe) na upande mwingine hatujausikia utetezi wake? Hata mahakamani huwa wanasikiliza pande zote mbili. Sasa hii hali hii nfio inaitwa ni Udikteta ndugu yangu Sitta. Sitta sisi sio watoto na usitubuluzebuluze sisi tumechoka.
na jandu, msumbiji, - 13.04.08 @ 11:53 | #6320
Si haki hatakidogo kumyamazisha Rostam kutoa utetezi wake kwani huyu ndiye kinara wa ufisadi wote uliofanywa dhidi ya nchi yetu! Naamini utetezi wake kaandikiwa na washauri wake ambao nadhani watamuingiza matatani zaidi kuliko kumponya.Ujanja atakaotumia ni kutaka kuongopa kuwa kulikuwa na ripoti mbili moja ikiwa ni hiyo yeye na wenziwe wameighushi kuonesha kwamba kamati iliiandika baada ya muda wake kwa maelekezo ya spika!! Kote huko ni kutapatapa kwake na rafikiye Lowassa. Ukweli ni kwamba kama hivyo ndivyo mbona hakumpa rafikiye atumie ushahidi huo alipoitwa kujitetea? Mafisadi maji yamewafika shingoni waacheni wajizamishe wenyewe wao wakidhani wanajibu mapigo.
na Bulesi, Tanzania, - 13.04.08 @ 12:18 | #6323
JAMANI MUSISHANGAE YANAYOTOKEA CCM UKWELI NI KUWA SERIKALI BADO NI LOWASA ROSTAM NA KIKWETE:
Fukuto la fukuta, moshi wafoka, mapovu yanamwagika, CCM imefika njia panda! Ama isuke au inyoe!
Hili vurugu la Richmond, likizingirwa na BOT EPA, BOT CIS, BOT Minara, Rada, Kiwira, Buzwagi na moto kutoka Upinzani, unafanya mambo kadhaa tujiandee kutokea.
1. Wabunge ambao si mtandao, wenye uchungu wa kweli wa CCM, kuendelea kusulubisha viongozi wao na Serikali yao iwe wazi. Hawa wabunge, mwokozi wao na nguzo yao ni Wastaafu Malecela, Kawawa, Mwinyi, Salim na Msuya. Huku wako hawa walioshupalia RDC;-Mwakyembe, Kilango-Malecela, Seleli, Kimaro, n.k.
2. Team Mkapa; huku ni wale wajanja wa Che-Nkapa ambao bado wanatibu majeruhi ya mchakato wa kugombea Urais 2005 na kunyang'anywa tonge la Hatamu za Chama. Hapa kuna Mang'ula, Ngwilizi, Kigoda, Kinana, Warioba na Ruhinda. Katika kundi hili, pia wapo wale waliotajirika na mradi wa Ujasirimali Ikulu; Yona, Mramba, Mgonja, Mkono n.k.
3. Mtandao; Kundi hili lina majeruhi wengi kutokana na kuvunjwa kwa baraza la mwazirina mwegemeo wa kashfa za ufisadi kuwa kwenye shingo zao. Kundi hili, limegawanyika katika sura mbili;
1. Team Kikwete ambayo wamebakia Makamba, Chiligati, Membe, Migiro, Karume
2. Team Rostwassa(Rostam/Lowassa); Karamagi, Msabaha, Nchimbi, Apson, Meghji, Kamala, Masha Diallo, Chenge,
4. Wasiofungamana lakini wana nguvu na ni tishio; Pinda, Mwandosya, Sumaye, Balali, Salmin, Magufuli, Msekwa na Sitta.
Serikali mpya na baraza lake la mawaziri bado ni ya Kikwete Lowasa na Rostam.
Masha-Mambo ya ndani, bila Lowasa Bw. Mdogo Masha asingekuwa hapo alipo, ni lowasa aliyemshika mkono na kumwingiza kwenye siasa, kwani yeye Masha na Business partner wake Magai walikuwa private lawyers wa mamvi, na hata Magai aliwahi kupatiwa ujumbe wa bodi ndani ya city water wakati huo Lowasa ni waziri wa maji. Je unategemea Masha atasahau alikotoka kama JK asivyomtupa Hussein Mwinyi???? Hao polisi, Manumba na Magereza vyote viko chini ya Masha. Sasa je, nani atamkoma Nyani giradi????
Ngeleja-Nishati na Madini- Huyu alikuwa mwanasheria mkuu wa Vodacom Tanzania LTD ambako Rostam na lowasa wana hisa japo mamvi ni silent share holder. Ni Rostam aliyemshika mkono Ngeleja akagombee Sengerema na kumpatia fungu la kutosha ashinde. Na ndio maana ameachwa madini ili aendelee kulinda migodi ya Rostam. Hivyo tusitarajie mabadiliko makubwa.
Mkullo-fedha- Huyu akiwa mkurugenzi wa NPF sasa NSSF alichota mapesa kibao kumuunga mkono JK mwaka 1995, hivyo ni senior mwanamtandao. Na ndio maana Mkapa alipoingia madarakani akamtema NSSF.
Chenge- Miundombinu, JK hana namna, hampendi Chenge lakini anakuwa forced na Lowasa na Rostam. Mikataba yote kuanzia IPTL n.k imesainiwa wakati wa Chenge na yeye anaelewa nani ni nani katika hayo makampuni yanayozidi kuutafuna utajri wa taifa hili na kutuacha watanzania tukilalia chips kavu. Eti JK atamtosa Chenge! THUBUTU! Atasema kila kitu ! Na ndio maana wakamuwahi Salome mbatia wakamuua ili asiendelee kutoa siri kwa wapinzani kuhusiana na pesa za BOT, kwani yeye ndo alikuwa Mweka hazina mkuu wa chama wakati wa uchaguzi
Kutokana na kuwepo makundi haya makubwa na utata unaotambaa angani hasa baada ya Lowassa kuangushwa na minong'ono kuwa naye Lowassa no Rostam ana ushahidi wa kujikosha, linalobakia kwetu watazamaji ni kupima upepo na kuomba dua wapigane na wagawanyike ili tujue nani ni kwa manufaa ya Taifa na nani ni mnyonyaji.Kutokana na kuogopa kumwagiana radhi ndo maana wanaanza kudhibitiana.
CCM si salama, na hata kama wakitoka nje ya ukumbi wakiwa wamekumbatiana, tusiwaamini.Hivyo si shangai kwa CCM kutumia bunge kumzuia Rostam kuwasilisha hoja.
na kimla, Tanzania, - 13.04.08 @ 12:38 | #6331
mwanangu usiseme sana chama cha mafisadi(CCM) ukijui watampeleka sasa hivi marekani watufunge kamba anaumwa na hata hospitali atakayolazwa tusiambiwe.twende nao taratibu kwa tahadhari sasa hivi maji yako shingoni we uoni fisadi balali hadi leo wanasema hajulikani haliko,kaa chonjo mpenda nchi
na chapakazi, tanzania, - 13.04.08 @ 12:39 | #6332
hawa wabunge ameingia mkenge, Rostam hana lolote zaidi ya kuleta mhcngangyiko huu ambao hata vyama vya upinzani na waandishi wa habari wmeingia mkenge.
NI DHAIRI ROSTAM ALIJUA MAELEZE YAKE HAYATAKUBALIWA BUNGENI KWA MUJIBU WA KANUNI ZA BUNGE(58-59).JAMBO LIKISHAJADILIWA HARIRUHUSIWI TENA, HIZI KANUNI ZIMEWEKWA TANGU ROSTAM HAJAZALIWA NA ANALIFAHAMU HILO.
AMEFANYA MAKUSUDI KUTUNGA TAARIFA YAKE NA KUPELEKA KWA SPIKA AKIJUA WAZI ATANYIMWA KUONGEA, HII NI NJIA YAKE Y KUJISAFISHA NA AMEWAPATA WENGI.
MAFISADI WANA AKILI SANA, HAO LAO MOJA SITTA,ROSTAM KIKWETE, LOWASSA, MTAFUNGUKA MACHO LINI???
na Imani - 13.04.08 @ 13:07 | #6337
hapa kuna usanii mkubwa kuliko kawaida ndo maana nilisema sitta achunguzwe .huyu si msafi ni kinyonga na kamwe hakuna mtu wa akili timamu anayeweza kukubali kumdhamini kinyonga kwa sababu anabadilika rangi kwa kila wakati.
wakati wabunge wa Cuf walipotoka nje waliambiwa haya ni mmasuala ya chama kwa hiyo walipewa adhabu lakini leo kamati ya chama inamzuia rostamu kujitetea haya si masuala ya chama!!!
Nilisemaq rostamu asiitwe fisadi kabla ya kujitetea na kama watu wako makini watajua kuwa huyu bwana ana washauri makini na ndo maaana alitaka kusemaq bila kuandika maana angeropoka na sitta ni mjanja anajua ambachoi angesema ndo maaana kaytaka maandishi.
hapa hakuna mtu safi labda ummma tutumie nafasi hii kuyajua mengi katika kipindi hiki cha mpasuko.
na wilibroad peter, sweden(örebro), - 13.04.08 @ 13:25 | #6342
Kila mwamba ngoma, ngozi huvutia kwake. Sitta mambo yamemfika shingoni, ama atetee maslahi ta CCM au ya TAIFA. Ni wazi ameamua kutetea maslahi ya CCM, sasa kazi ni kwetu sisi wananchi nini tufanye.
Rostam ameshatengeneza penati-maguu 12, refa ni wabunge CCM, washika vibendera ni wabunge UPINZANI, watazamaji ni wananchi. Sasa refa akipendelea wananchi ni lazima tuingie uwanjani na kuchukua sheria mkononi.
Unyerere warudi tena BUNGENI. Mlilala hundingwandingwa, mwimacho hambiwi tule!!!!!!!!!!!!!!!
na Zawadi Ngoda, Dar es salaam/ Tanzania, - 13.04.08 @ 13:52 | #6349
Rostam pia anahusika kwenye kashfa ya uchotaji wa mabilioni ya shilingi pale Wizara ya Kilimo,kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la MwanaHALISI,two weeks ago.Huyu mtu haridhiki! Kweli muonja asali haridhiki mara moja.But unfortunately mambo kama haya huwa hayawafikii wapiga kura mahalia,kwani huko vijijini kama Igunga huwa vyombo vingi vya habari huwa haviwafikii wananchi.Hata kama inatokea magazeti kuwa yanapelekwa huko,basi mabepari kama Rostam na Chenge huwa wanayanunua yote hata kabla hayajafika kwa wananchi.
Pia nashangazwa na ukimya wa serikali kuhusu huyu kupe Balali,je huo ugonjwa gani miezi yote hii?Au ana chronic terminal disease,(ingawa si vyema kuombea hivyo).Hapa kutakuwa na mchezo wa kijanja wa kumficha ili tusihoji,but serikali lazima itambue kuwa wananchi sasa wameamka,hatutasahau suala hili,tunajua anafichwa ili asiwataje wahusika wengine wa EPA.Mwalimu alipolazwa pale St Thomas tulikuwa tukipewa updates zake kila siku,sembuse huyu tapeli,"kuna siri gani kali" huko "sirikalini?"
na David, Dar, - 13.04.08 @ 14:12 | #6358