Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Nadhani watanzania wana masikio na macho, taarifa muhimu zinatolewa dhidi ya hawa wachache wanaotumia madaraka yao kujinufaisha kwa jasho la wananchi na raisi na vyombo kama bunge vinatetea/kukaa kimya. 2010 itakuja ambapo watahitaji kueleza sera zao .... hapo ndipo tutakapowashika sehemu mbaya ... BOT, RICHMONd, TCTS, bado tu wahusika hawashughulikiwi??? Au raisi wetu amepigwa limbwata na wahusika ili asiseme chochote???

Kuna kitu hakiko sawa ...tena fununu ni kwamba RICHMOnd ni jamaa mkuu mwenyewe ndo maana hasemi kitu
 
It seems kanuni zinamzuia Rostam kusema alichotaka,na yeye akatingsha kiberiti kuwa ana resign ubunge,ili akayaongelee haya kama raia wa kawaida>Yeye alidhani jamaa wangetishika,lakini wakamwambia a-resign kama anataka.
 
Na Mwandishi wetu
MBUNGE wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, ametishia kujiuzulu ubunge kutokana na hatua ya Kamati ya Uongozi ya Bunge kumzuia kuwasilisha hoja yake bungeni, MwanaHALISI limedokezwa.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Kamati hiyo, zinasema Rostam alitoa tishio hilo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Uongozi ambao ni pamoja na Spika wa Bunge, Samwel Sitta na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Inaelezwa kwamba baada ya Rostam kutoa kauli hiyo, Waziri Mkuu na Spika kwa pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.

“Kabla Rostam hajamaliza kulalama, Spika hakumkawiza. Alisema, “Andika barua ya kujiuzulu sasa hivi. Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya Bunge…,” alinukuliwa na mjumbe mmoja wa Kamati.

Mjumbe huyo alisema kauli ya Rostam iliwaudhi wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwani haraka Waziri Mkuu alitoa tamko la kuungana na Sitta kumtaka Rostam ajiuzulu ubunge.

Wiki iliyopita, Spika alimzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni, baada ya kubaini kuwa aliyoyaeleza katika kile alichoita “hoja yake” hayakustahili kuwasilishwa bungeni.

Katika Mkutano wa Bunge uliopita (wa kumi), Bunge lilimtaka Rostam kuwasilisha maelezo yake katika mkutano unaoendelea sasa mjini Dodoma, baada ya kusikika akituhumu kwamba Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond, “iliendelea na kazi zake hata baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Spika.”

Rostam, kwa mujibu wa taarifa, alitaka Spika, kwa kutumia hoja za Rostam, amwamuru Dk. Mwakyembe kumsafisha ndani ya Bunge.

Hata hivyo, shinikizo lake hilo lilikataliwa na Kamati ya Uongozi.

Taarifa za ndani ya Bunge, zinasema kukataliwa kwa maelezo binafsi ya Rostam kumetokana na kuonekana yamejaa tuhuma, shutuma na dharau kwa Bunge na Kamati Teule ya Mwakyembe.

Spika wa Bunge amekiri kupokea hoja binafsi ya Rostam, lakini alisema ameshindwa kuruhusu iwasilishwe bungeni kutokana na kwenda kinyume na Kanuni za Bunge.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya Uongozi amemkariri Spika akisema Bunge halikujadili hoja ya Rostam, siyo kwa kumwogopa, kama baadhi ya magazeti yanavyotaka kuonyesha, bali kwa sababu hoja yenyewe inakiuka Kanuni za Bunge.

Alipopigiwa simu na gazeti hili kupata undani wa taarifa hiyo, Sitta alielekeza mwandishi awasiliane na Rostam mwenyewe ambaye, Spika alisema tayari amejulishwa uamuzi huo.

MwanaHALISI halikuweza kuwasiliana na Rostam kupata upande wake.

Katibu wa wabunge wa CCM, Ali Ameir Mohammed, alipoulizwa juu ya suala hilo alisema, “Sijui kilichojadiliwa. Sifahamu Kamati ya Uongozi ya Wabunge wamesema nini. Sikuwapo Dodoma, na wala sijakutana na mwenyekiti wangu (Waziri Mkuu) wala Rostam.”

Hata hivyo, imefahamika kuwa wajumbe wa Kamati Teule, walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia Taifa kuwa Rostam ndiye mwenye Richmond na Dowans.

Uchunguzi wa MwanaHALISI umeonyesha kuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kilichoitwa “misumari ya mwisho wa kumpigilia Rostam.”

Wiki iliyopita Rostam alimweleza Spika wa Bunge, nia yake ya kutoa maelezo binafsi kuhusu madai ya Kamati Teule kuwa alihusika na njama za kifisadi za kuibeba Richmond.

Taarifa za Bunge zimesema hakukubaliwa kwa mujibu wa Kanuni za 53( na 54(4) za Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007 zinazingatia kuwa “Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo Bunge lilikwisha kuliamua ama katika Mkutano huo au ule uliotangulia ....”

Imefahamika kuwa Rostam, katika hoja iliyokataliwa na Spika, aliwaita wabunge kuwa ni wasanii na wababaishaji kwa sababu tu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusika na mkataba wa kifisadi wa Richmond/Dowans.

Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa Viti Maalum (majina tunayo), ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kuwasilisha maelezo yake.

Kuna madai pia kuwa “aligawa fedha nzuri” kwa baadhi ya waandishi wa habari (majina tunayo), ili kuipunguza makali Ripoti ya Kamati Teule.

Pamoja na jitihada hizo, bado zaidi ya asilimia 95 ya wabunge wanaiunga mkono Kamati Teule na wangetaka wahusika wote katika kashfa ya Richmond wachukuliwe hatua kali.

“Hawa watu hawajui kusoma mood ya wabunge. Wengi tuna hasira naye; tungemchanachana baada ya kuwasilisha utumbo wake. Sauti za Viti Maalum zingemezwa na sauti za wabunge wazalendo,” amesema mbunge kijana na machachari.

Alipoulizwa Dk. Mwakyembe kama kweli Kamati yake ilikuwa na ushahidi wa ziada unaoonesha Rostam ndiye Richmond/Dowans, alisema kwa ufupi, “Tumwombee tu mwenzetu aruhusiwe kutoa dukuduku lake. Tutakayoyasema sisi yatajulikana palepale ulingoni.”


Source: MwanaHalisi
 
Huyu ni mtu muhimu sana katika kuiangusha CCM. Nimefurahishwa sana na PM na Spika kwa kuwa majasiri kumwambia ajiuzulu hawakujua kama alikuwa anawatishia wakubwa NYAU.

Inabidi ifike wakati Mr JK awe na moyo wa paka afanye kweli asafishe Chama lakini hili kwake ni kama kukutanisha mbingu na ardhi(yaani ni jambo gumu kulifanya) tungoje tuone!
 
Haya maelezo ya huyu Muajemi tutayapataje tuyachambue au atutumie hapa JF tumpatie ushauri unaofaa
 
wanaosubiri 2010 ni sawa na mtu anayejifariji baada ya kukosa kile alichokitegemea na sasa anasema wacha tusubiri mechi ya marudiano.jamani aliyetangulia ametangulia tu,na ukitaka kumkaribia anza sasa sio kusubiri lalasalama eti ndio uanze kumkimbilia.hapa watu wamesahau kuwa wagombea wa ccm wote majina yao upitiswa na vikao vyao vya juu,sasa ni nani aliyesema kuwa hatagombea 2010.hii ndio siri ya wabunge wa ccm kuwa wanyonge.lakini kama ile sheria ya mgombea binafsi ikianza kutumika hapo ndio mwisho wa ccm na makamba wao.
 
Mnachekesha sana ninyi watanzania, nani wa kumnyamazisha Rostam, serikali hii ana hisa nayo?
 
Hii commission ya Leadership ethics inafanya nini? Iko accountable kwa nani? Tuna viongozi ambao hawatakiwi kuwa kwenye leadership kabisa na yenyewe iko kimya. Bila ya mkwara wa upinzani kuandamana kwenda kuangalia record za Chenge jamaa bado angekuwa amedindisha!

Huyu Rostam inajulikana wazi alipakua hela za EPA lakini...KIMYA!! Viongozi ndio mifano ya taifa hili na hii ndio mifano tunayoifuga? No wonder wizi ulikuwa sifa kabla ya watu kufunguliwa macho...
 
Kuna kila aina ya ushahidi kwamba Rais JK alikutuma kutafuta a replacement ya mradi wake wa umeme toka Richmond ambao walivurunda.Nadhani hata kama JK anajuana sana na watu wa Richmond ama hata ana mkono huko mkubwa kwa maana ya share nia ilikuwa njema kwamba Richmond yenu imevurunda na sasa atatfutwe mwingine anunue .Ukaambiwa na Rais tafuta na wewe ukaja na Dowans .Nyie watu wale wale .Mwakyembe yeye maneno yake yaliishia kwa Richmond na si Dowans.bado tunataka useme ukweli .Je wewe nani alikutuma kuja na Dowans ambayo wewe ndiye mwenye nayo na ndugu JK ? Mlitangaza wapi tender ya take over hadi Dowans mkawa washindi ? Ndugu Rais si utueleze tu ukweli nasi tutakusamehe ?
 
Kwani huyu Rostam zamani alikuwa anaongea?? au ndo mambo ya bubu kujua kuongea basi balaa tupu?!!!?
 
Sasa ajiandae na anguko la tatu... teh teh teh teh

Mimi nilijua huyu hawezi kukaa kimya maana atathirika kwenye madeal yake machafu anayofanya, hivyo lazima atafute jinsi ya kujisafisha, je matope aliyonayo anampaka nani? lets wait and see.
 
Mimi nilijua huyu hawezi kukaa kimya maana atathirika kwenye madeal yake machafu anayofanya, hivyo lazima atafute jinsi ya kujisafisha, je matope aliyonayo anampaka nani? lets wait and see.

Ofcourse atawapaka CCM na watawala na Bunge pia. Hajui alifanyalo ila waswahili wanasema "mwenye kiranga haliliwi wala hawekewi matanga" Kitakachomfika kitakuwa funzo kwa mafisadi wengine na pengine itambidi akimbie nchi.
 
Ngurumo Ni Fimbo Ya Mbali Anapiga Kelele Weee Halafu Mwaka 2010 Atakuja Hapa Kuomba Uanachamahalafu Mwaka 2011 Tutampa Ukuu Wa Wilaya Au Aendeshe Kipindi Fulani Katika Tbc
 
Kama nilivyoshauri kwa Raia Mwema, wahariri wanatakiwa kuwashukia kikamilifu wale wote wanaotishia maisha yao ya kazi, na wataacha hiyo tabia, unless wawe wana uhakika na kesi zao.





Baada ya kumshtaki kubenea.. Wahariri sasa kumvaa Rostam

29.04.2008 0532 EAT

Na Said Mwishehe

WAKATI Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amefungua kesi Mahakama Kuu ya akidai fidia ya sh.bilioni 3 kutoka gazeti la Mwanahalisi akidai limempaka matope kuhusiana na kashfa ya Richmond, sasa Jukwaa la wahariri linaangalia namna ya kumsaidia apambane katika kesi hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Sakina Datuu, alisema taarifa za kushitakiwa kwa gazeti hilo linalomilikiwa na Saed Kubenea wamezipata na tayari wameanza kuzungumza ili kuona wanaweza kushirikiana vipi na uongozi wa gazeti hilo kuhusu kesi hiyo.

"Ni kweli tumepata taariza za gazeti hilo kushitakiwa na Rostam hivyo kwa kuwa hivi sasa ni mapema mno kujua nini tunafanya, tumeanza kuzungumzia suala hilo. Jukwaa la wahariri tunatarajia kukutana haraka iwezekenavyo ili tuone tutashirikiana vipi na Saed Kubenea," alisema.

Sakina alikuwa akijibu swali aliloulizwa baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa kujadili wajibu wa vyama vya siasa, vyombo vya habari na asasi za kiraia katika kuendeleza demokrasia ya vyama vingi nchini.

Alisema binafsi anaamini wahariri watakapokutana wataweza kutoa mwelekeo mzuri zaidi wa kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri kwani wahariri wamekuwa wakishirikiana katika kushughulikia masuala mbalimbali yanayowabili wahariri na waandishi wao.

Alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa wajumbe waliokuwa katika mkutano huo kuuliza Jukwaa la Wahariri lina mkakati gani wa kumsaidia Saed Kubenea baada ya kushitakiwa mahakamani na Rostam Aziz.

"Tunataka kujua wahariri mmejipanga vipi katika suala la kumsaidia Kubenea ambaye amefunguliwa kesi na Rostam akidai kuwa gazeti la Mwanahalisi limemchafulia jina lake kwa sababu ya kumuandika kwa kumuhusisha na kashfa ya ufisadi.Tunaomba mtupe msimamo wenu kwa sasa,"aliuliza mjumbe huyo.

Katika kesi hiyo, Rostam anamshataki Mhariri Kubenea, na Pritench Company Limited wachapishaji wa gazeti hilo.

Kwa mujibu wa hati ya mashataka iliyosainiwa na Wakili wa Rostam, K.M Fungamtama, katika toleo namba 084, Februari 13 mwaka huu gazeti hilo katika ukurasa wa wake wa kwanza lilichapisha habari ikiambatana na picha ya Rostam yenye kichwa cha habari kisemacho"Richmondi ya Rostam Aziz-Ikulu",'Ndiye aliyeileta nchini', 'Lowassa alimuagiza'

Kubenea katika siku za karibuni amekumbwa na masahibu mengi ikiwa ni pamoja na kumwagiwa tindikali akiwa ofisini kwake pamoja na mhariri mshauri wa gazeti hilo, Ndimara Tegambwage ambaye alipigwa mapanga.

Baada ya mkasa huo, alipelekwa hospitali ya Muhimbili na kisha India ambako alitibiwa na kupewa miwani ya macho. Watuhumiwa walikamatwa na kesi bado inaendelea.


______________________
 
I know this will happen and Jk will take a move on it soon,

atamshauri atoe shauri lake
 
Kama Rostam akichomoa mashitaka, inatakiwa Wahariri wao waongeze kuni na kuhakikisha kuwa Rostam anapikika kwenye magazeti yote kabisa ili mwingine mwenye vibilioni vyake asije akawachezea tena.



_____________________
 
kama nikiangalia vizuri taharifa iliyoandikwa RA hakupata ushauri wa kutosha kabla ya kwenda mahakamani. Mwanahalisi alichoandika ni maoni yaliyotolewa kutoka vyanzo mbali mbali ikiwa ni pamoja na taharifa ya Rweyemamu (Ikulu) na Mwakyembe. Hakuongeza vitu ktk hili.

Rostamu alitakiwa kupeleka kamati ya mwakyembe(bunge) kama kweli ilikuwa inashitakika. Lakini Gazeti, naona kama mwanahalisi wakijipanga vizuri wanaweza kumuacha RA hoi. Labda kama anakwenda kutoa taharifa nyingine(Aliyotaka kuitoa bungeni). Lakini mwanahalisi hana cha kesi hapa. Ilitakiwa kama ni kushitaki vizuri ashitaki magazeti yote yaliyouzwa baada ya ripoti ya mwakyembe kutoa taharifa yake.

Hii ndiyo test ya mwisho kwa Rostamu Aziz ambayo itamwangusha milele katika siasa za Tanzania
 
Back
Top Bottom