Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Daa!! hii nayo kali, ila kama inawezekana wahariri mnaweza mkamuomba Mungu ili awaepushe na hili, kwani huyu Mbunge wa Igunga anaweza kuondoa shitaka mahakani, lakini Kubonea kama akimuomba Mola yote yanawezekana kuepukika, hakuna anayependa kesi hata kidogo, lakini Kubenea asisahau hii ndiyo changamoto ktk maisha. Mungu akusaidie ndugu yangu.
 
Mimi ni mmoja kati ya watu ambao simpendi kabisa RA, lakini lazima nibaki kwenye ukweli tu. Napenda magazeti yanayoandika ukweli na si kufurahisha wasomaji na kuuza tu.

Je, Mwanahalisi ana ushahidi wa ku-back maandishi yake in court?
Sipendi kuamini kuwa hawana.
 
Huo ni mkwara tu, anatikisa kiberiti. jipangeni vizuri mtashinda tu. Ukweli mara zote ni mmoja lakini uongo upo wa aina nyingi.Aluta continua, please keep up informing us Mungu hayupo na watu wabaya
 
Raia Mwema, kwa "kumwomba radhi" Rostam Aziz, wamedhihirisha ukweli kwamba wao ni wale wale wa Rai ya Rostam Aziz. Hakuna kipya. Usanii ndani ya usanii! Ndio maana sikulipenda hili gazeti!

Kaeni mkao wa kula, kitu kipya kikali zaidi ya MwanaHALISI kiko jikoni, karibu kitatoka. Utakuwa wimbo mtamu sana... yaani albam itauza kopi zote na chenji hairudi!

./Mwana wa Haki!

Mwanahaki,

Ulitaka hata wakikosea wasiombe msamaha? Nimeisoma hiyo article kwa kweli
sehemu ambako wamemtaja Rostam huenda walienda mbali zaidi hata kama hatumpendi Rostam.

Naamini magazeti ya TZ sasa yanajitahidi sana tena kwenye mazingira magumu, ila wakikosea ni muhimu kukubali na sio kung'ang'ania tu kwa faida ya kung'ang'ania.

Katika nchi inayhofuata sheria, hata mvunja sheria naye ana haki zake.

Mimi nawapenda thisday jinsi wanavyoandika habari zao. Wanachambua hasa lakini pia wako makini kuhakikisha hawaachi mwanya wa kuburuzwa mahakamani.
 
Ulitaka hata wakikosea wasiombe msamaha? Nimeisoma hiyo article kwa kweli sehemu ambako wamemtaja Rostam huenda walienda mbali zaidi hata kama hatumpendi Rostam.
Mtanzania asante mkuu.

Mwanahaki anapaswa kujua kuwa hata kama RA angekaa kimya, serikali ya JK ingeweza kulishitaki 'Raia Mwema' kutokana na hiki walichoandika hapa chini na mengine!

“Serikali” hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.
Ni somo; yatupasa kuwa huru LAKINI makini!
 
RA is done! I have said this several times!

Haoni!! Is Totaly Blind

Hawezi kusoma nyakati! haoni upepo unapulizia kutoka wapi kwenda wapi!

RA traits hazikubaliki kwenye hali ya sasa ya kisiasa Tanzania!hali imekaa KIUTU Mno! Imekaa kimaadili mno! Imekaa KIMIIKO MIIKO MNO!

Angekuwa smart enough kuona hivyo na kuwa kimya kwa muda kubahatisha kama mawimbi hayatambeba kwa hicho kinachofuatia karibuni.

Spirt ya nchi imebadilika! Nobody can explain this clearly.

Hata Raisi mwenyewe is out of control of what is taking place!

Ni kama NGUVU YA UTU wa watu Ndio inaogoza na kuelekeza nchi!

Saa yeyote mahali popote mtanzania yeyote anaweza kuandaa maandamano na kutoa maoni yake kwenye chombo chochote cha habari na kuamsha moto wowote kama anavyoona yeye na ikalete impact.

Waalmu,wanafunzi,vyama vya upinzani, wanahabari, shirika lolote,wanabogo flav, Ngos etc.... wote hawa wanaweza kuweka IMPACT isiyotegemewa ... na isiyo weza kuyumbishwa na serekali au Fisadi yeyote! HILI HAWALIONI!

Simply .... slowly thigs are geting on hands of THE PEOLPLE!

RA akae chochonjo akiteleza kidogo..moto unaweza kumuwakia labda kama kiwango cha UTU wake kiko juu na kuweza kuteka nyoyo za watanzania walioamka kwa namnafulani.

Katika viongozi wote waiojiuzulu karabuni...wote hawakuamini kuwa kwa muda mfupi tu wangewezakuwa walipo sasa!

Ni hali halisi ya kisiasa inawezesha hayo kutokea!

I am sure RA is DONE!!!!!!

why?

Ni anavyojiweka,

Hali imekaa Ki Julius Nyerere sana sasa hivi na yeye na wenzie ni kinyume kabisa na traits hizo! hata alipokuwahai Nyerere aliwaambia wazi kuwa hawafai!

RA he has to be realy good kujinasua!
 
Wayao,

Hawashindwi vita, babu anaweza kukimbia lakini mjukuu atarudi kupambana vita vilivyoachwa na babu yake.

Walikubali kupanda pamba mchana kutwa, giza lilipoingia walirudi wakang'oa kazi yao yote ya mchana.
 
Raia Mwema, kwa "kumwomba radhi" Rostam Aziz, wamedhihirisha ukweli kwamba wao ni wale wale wa Rai ya Rostam Aziz. Hakuna kipya. Usanii ndani ya usanii! Ndio maana sikulipenda hili gazeti!

Kaeni mkao wa kula, kitu kipya kikali zaidi ya MwanaHALISI kiko jikoni, karibu kitatoka. Utakuwa wimbo mtamu sana... yaani albam itauza kopi zote na chenji hairudi!

./Mwana wa Haki!

Angalia ile BARUA YA KILA WIKI KICHWA CHA HABARI NIMEKISAHAU NA NIKO MBALI NA ILO GAZETI KWA SASA(yule bint anaye mwandikia mpEnzi wake Frank.kuhusu USHAMBENGA WA VYOMBO VYA HABARI.ILA HII NI DHAHILI HAWA NI WALE WALE.)
 
Raia Mwema walichofanya ni kuepusha malumbano........cha msingi.......message SENT!!!
 
Kufikiri kwamba wasomaji wa gazeti ni "timu" ya gazeti hilo si sahihi, unaweza kuwa supporter na mwanaharakati wa gazeti fulani lakini ultimately kama kuna litigation atakayekuwa responsible ni mhariri labda na wandishi wake.

Unachoweza kufanya ni kuwaelewa, ku protest kwa njia nyingi ikiwa pamoja na barua za wasomaji au barua personal kwa mhariri/muandishi au kuonyesha kutoridhika publicly kama unavyofanya hapa.Kama yote unaona hayafai unaweza kuacha kununua hilo gazeti au hata kuanzisha lako.

Walioandika habari hiyo ni waandishi/ timu ya gazeti na wenye wajibu wa kuomba au kutoomba radhi ni wao wenyewe, sisi wengine ni waangaliaji na kama tutawajudge itakuwa ni kwa wallets zetu.

Tatizo la sheria, kwa mtu anayeelewa sio kweli kwamba mara zote inasimamia ukweli.Unaweza kusema ukweli kwamba fulani ni mwizi lakini kama huna ushahidi wa kuthibitisha hivyo anaweza kukupiga libel charges ikabidi uombe msamaha.Wenye kuelewa wataelewa nini kinachoendelea.

Tanzania ingawa tunahitaji "exposee journalisms" pia tunahitaji a balanced approach na responsible journalism ili tusiwape hawa mafisadi ushindi unaotokana na legal technicalities.Kitu kikiandikwa watu wawe tayari kwenda mahakamani kukitetea, ama sivyo hata kama tuna habari za nguvu hapa, na tunajua ni za kweli, lakini kama tunakosa ushahidi unaoweza kusimama mahakamani hatuchapishi ng'o!
 
Jamani sielewi..................!!!!!!!!!!!!!!!!


Tusimbeze Rostam, hatikisi kiberiti

Joseph Wambura Aprili 23, 2008



WIKI iliyopita nilikusanya magazeti yote ya wiki. Niliyasoma kijuu juu, ila nilipata fursa ya kuyapitia kwa ufasaha Jumapili nilipotoka kanisani.

Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wanahabari kwa kazi nzuri wanayofanya kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha jamii. Kimsingi nimekuta magazeti mengi kwa asilimia kubwa yakilifahamisha Taifa letu nini kinaendelea katika jamii.

Hata hivyo, wakati napitia gazeti la Raia Mwema, toleo namba 025, nilikutana na makala ndefu iliyochapishwa ukurasa wa nne na kuendelea ukurasa wa 22. Mwandishi wa makala hii ni Lula wa Ndali Mwananzela.

Makala hii ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho: "Sipendi Rostam Aziz atikise kiberiti bungeni." Alichambua na kuhoji Rostam alitaka kuzungumza nini bungeni hadi nchi nzima ikatetemeka.

Katika moja ya aya zake anasema: "Kitu gani hasa alitaka kusema kiasi kwamba kwa nyakati tofauti imeonekana kana kwamba ana ‘jambo' kubwa ambalo lingeweza kuleta vurugu bungeni?"

Anafafanua kuwa Rostam alitaka kupeleka maelezo ya ufafanuzi kuhusiana na mkataba wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Makala hiyo inasema Rostam angetumia muda huo kujisafisha, na si ajabu angefika na vielelezo vyake zikiwamo fomu za BRELA zenye kuonyesha wamiliki halisi wa Richmond, na hivyo kujisafisha yeye na washirika wake.

Ameandika mengi, anayojua aliyatoa wapi, lakini pengine ninukuu aya ifuatayo iliyonifanya kuandika makala hii: "Hivi ni lini mara ya mwisho kwa Rostam kutoa mchango bungeni na alichangia nini? Ni kitu gani ambacho Rostam Aziz alisema bungeni katika mijadala ya bajeti au mingineyo ambayo inaweza kukumbukwa? Kama huko kote hajasema jambo lolote la kukukumbukwa, iweje leo tugwaye kama Taifa eti Rostam anataka kusema? Huku ni kujifanya duni kusiko na sababu."

Nimeamua kuijibu makala hii baada ya kuona tabia inayoibuka katika jamii yetu inastahili kukemewa vinginevyo itatupeleka pabaya. Namchukulia Rostam Aziz kama raia yeyote wa nchi hii mwenye haki ya msingi ya kujitetea anapokuwa ametuhumiwa.

Ni wiki iliyopita tu, tumeshuhudia Spika wa Bunge Samuel Sitta akijikanyaga juu ya uamuzi muhimu unaohusu kanuni za Bunge. Spika ni mhimili wa kanuni hizi, akijua kuwa jambo lililoamuliwa na Bunge haliwezi kujadiliwa katika muda wa miezi 12, katika mkutano wa 10, akasema Rostam angelazimika kuthibitisha tuhuma dhidi ya kamati ya Dk. Harrison Mwakyembe.

Rostam alikuwa akidai kutotendewa haki na kwamba kamati ilifanya kazi nje ya muda wake, hivyo aliamini kuwa ilifanya kazi kisiasa. Kama kweli wangekuwa na nia ya kumhoji wangeweza kumhoji, ila kumhoji kwao kungeweza kuvuruga mchezo wa kisiasa ulionuiwa.

Bunge la Mkutano wa 11 Sitta alikubali kumpa Rostam nafasi ya kutoa maelezo yake, lakini akatoa sharti kuwa shurti yaandikwe. Rostam alipoyaandika, Spika akabadili milingoti ya goli. Akasema kanuni za Bunge haziruhusu jambo lolote lililoamuliwa na Bunge kujadiliwa upya katika kipindi cha miezi 12!

Mwandishi wa makala ile anakiri nguvu na umuhimu wa Rostam Aziz katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kuwa nguvu kubwa aliyonayo ndani ya chama hicho ilimwogofya Spika Sitta,, pale anaposema: "Sasa kama mmoja wa mashabiki wake (Rostam) naye ataanza kumtwanga mangumi, basi si tu inawezekana kupata ufa mkubwa, lakini yaweza kabisa kusarambatika".

Mwandishi huyu huyu anayekiri nguvu ya Rostam, ndiye anadiriki kuhoji Rostam angesema nini na aliwahi kusema nini bungeni.




ROSTAM Aziz

Kilichonisikitisha zaidi, mwandishi wa makala hiyo naye ameangukia katika mkumbo. Anamwagia matope Rostam, bila kuchunguza na wala sijui kilichomtuma afanye hivyo.

Sitaki pia kuamini kama kweli mwandishi huyu anaishi nchini na ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya kisiasa.

Sina sababu ya kutumia nguvu kuonyesha ukweli umelala wapi katika kueleza Rostam alipata kuchangia nini akiwa bungeni. Kwa uchache niorodheshe matukio haya aliyotenda kwa ufasaha wa hali ya juu na kutikisa nchi akiwa bungeni.

Mwaka 1994 Taifa lilikumbwa na mfumuko wa bidhaa kutoka Zanzibar. Bidhaa hizo zilikuwa zikipita kwa njia ya panya, maarufu kama ‘Zanzibar route.' Zilikuwa azikiingia nchini bila kulipa kodi na kufurika madukani. Rostam alisimama bungeni, akajenga hoja na Serikali ikachukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo.

Alidiriki kuwatuhumu hata viongozi wa Zanzibar kuhusiana na biashara hiyo. Hapo alionyesha ujasiri wa kwanza akiwa mbunge kijana kuliko wote wakati huo.

Mwaka 1977 Rostam alikuwa mbunge pekee aliyekataa kuunga mkono muswada wa Sheria ya Madini. Alisema muswada huo ulikuwa na upungufu mkubwa wa msingi na akaonya kuwa iwapo ungepitishwa, vizazi vijavyo vingewahukumu wabunge kwa uamuzi huo. Leo kamati ya Madini ya Rais, chini ya Jaji Mark Bomani, imeipitia sheria hii. Si ajabu matokeo yatakuwa sawa na alivyokuwa amependekeza Rostam.

Mwaka 1999 Rostam huyu huyu ambaye mwandishi hakumbuki iwapo aliwahi kusema lolote bungeni, aliweka historia katika chama tawala. Akiwa mbunge wa chama tawala, aliongoza kundi la wabunge 50 kupinga iliyoitwa kesi ya uhaini dhidi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF).

Kumbuka CUF ni chama cha upinzani. Kesi hii ilikuwa imepandikizwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, akidai wabunge hao walikuwa na njama za kumpindua. Baada ya hoja ya Rostam, muda mfupi baadaye watuhumiwa wote waliachiwa.

Mwaka huo huo, kwa ujasiri mkubwa, Rostam aliongoza mapambano dhidi ya Dk. Salmin aliyetaka kubadili Katiba ya Zanzibar na kuongeza muda wake wa kuwa madarakani.

Yapo mengi, ila nikumbushe hata hili. Rostam huyo huyo anayebezwa, mwaka 2001, alisimama kidete kupinga mabadiliko ya Katiba yaliyokuwa yakimpa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka makubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kuteua wabunge 10.

Lakini si vibaya nikakumbusha kwamba pamoja na mengi yaliyozungumzwa na Rostam bungeni, na ambayo yamekuwa na manufaa kwa Taifa ni pamoja na lile la mwaka 2004 bungeni.

Katika mkutano wa Bunge la Bajeti, Rostam alimbana vilivyo aliyekuwa Waziri wa Uchumi na Mipango, Dk. Abdallah Kigoda juu ya kazi za wizara hiyo.

Nakumbuka vizuri sana suala hili. Hasa kutokana na ujasiri wake wa kuzuia shilingi, akitaka apewe majibu ya hoja kadhaa. Mosi, ilikuwa akitaka ahakikishiwe kuwa wizara hiyo inaachana na mpango wa kukusanya takwimu za uchumi, badala yake ibuni mipango thabiti ya uchumi na kuisimamia ipasavyo.

Akapendekeza Wizara ya Uchumi na Mipango iunganishwe na Wizara ya Fedha, kwani kazi zake zilikuwa pacha na zilizohitaji kuwa chini ya kiongozi mmoja. Leo suala hilo limetekelezwa na Seriakali iliyo madarakani.

Akataka uwepo udhibiti wa hali ya juu ili shilingi isiporomoke kila uchao, kwani athari za kushuka kwa thamani kulikuwa kunayumbisha uchumi.

Mjadala ulikuwa mkali mno, na wote walioshuhudia wanakumbuka vizuri hoja za Rostam ambazo baadaye zimetekelezwa.

Sipendi kuendelea zaidi ya hapo. Natumaini mwenye macho haambiwi tazama. Wapo wabunge wa kubezwa, lakini Rostam Aziz si mmoja wao, mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.

Nimjuavyo Rostam Aziz, kwa ujasiri aliouonyesha ni kweli angetikisa nchi. Hata hivyo, hoja zinazopenyezwa kuwa angeweza kukiumbua chama chake, Chama Cha Mapinduzi, inaelekea wanaozitoa hawamfahamu vilivyo.

Kwa jinsi anavyojulikana, Rostam atakuwa mtu wa mwisho kukiumbua chama chake, hofu inayoonekana inatokana na ujasiri uliowekwa wazi na sehemu ya historia niliyoonyesha hapo juu.

Kwa vyovyote iwavyo, Mwananzela hakumtendea haki Rostam. Uandishi wa aina hii ni hatari kwa ustawi wa Taifa. Ninashauri bora kutoandika pale tusipokuwa na taarifa sahihi, vinginevyo tunaishia kujiumbua na kulipotosha Taifa.








http://raiamwema.co.tz/08/04/23/23.php
 
Kufikiri kwamba wasomaji wa gazeti ni "timu" ya gazeti hilo si sahihi, unaweza kuwa supporter na mwanaharakati wa gazeti fulani lakini ultimately kama kuna litigation atakayekuwa responsible ni mhariri labda na wandishi wake.

Unachoweza kufanya ni kuwaelewa, ku protest kwa njia nyingi ikiwa pamoja na barua za wasomaji au barua personal kwa mhariri/muandishi au kuonyesha kutoridhika publicly kama unavyofanya hapa.Kama yote unaona hayafai unaweza kuacha kununua hilo gazeti au hata kuanzisha lako.

Walioandika habari hiyo ni waandishi/ timu ya gazeti na wenye wajibu wa kuomba au kutoomba radhi ni wao wenyewe, sisi wengine ni waangaliaji na kama tutawajudge itakuwa ni kwa wallets zetu.

Tatizo la sheria, kwa mtu anayeelewa sio kweli kwamba mara zote inasimamia ukweli.Unaweza kusema ukweli kwamba fulani ni mwizi lakini kama huna ushahidi wa kuthibitisha hivyo anaweza kukupiga libel charges ikabidi uombe msamaha.Wenye kuelewa wataelewa nini kinachoendelea.

Tanzania ingawa tunahitaji "exposee journalisms" pia tunahitaji a balanced approach na responsible journalism ili tusiwape hawa mafisadi ushindi unaotokana na legal technicalities.Kitu kikiandikwa watu wawe tayari kwenda mahakamani kukitetea, ama sivyo hata kama tuna habari za nguvu hapa, na tunajua ni za kweli, lakini kama tunakosa ushahidi unaoweza kusimama mahakamani hatuchapishi ng'o!


Lets hope haya uliyo sema na mengineyo katika kuepusha madhila ambayo yangetokea mbele(kortini)kua ni sababu ya kuomba radhi.

Ukichulia ukweli gazeti Lenu bado jipya that means hata its fanancial status bado kuweza kusimama mahakamani na FISADI kama RA obviously atawashinda tu.
Lakini mkubali au mkatae Histiria hapa inawahukumu kwani humuwezi kuzuia watu ku-speculate mahusiano yale ya mwanzo (na Rostam)na jinsi mambo sasa yanavyo kwenda.
Vinginevyo,kama laivosema mchangiaji aliye tangulia kwamab all in all the massege is SENT,kuomba radhi ni formality tu.

ALUTA CONTINUE.....
 
Sipendi
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa wanataaluma wanaweza kuzitetea taaluma zao. Lakini pia watu wanaweza kutumia taaluma zao kuwazuia wengine wasipate nafasi ya kuongea na kusikilizwa. Sasa RA anaona kachafuliwa anaenda mahakamani kumshtaki aliyemchafua, wahariri wanasema watamvaa huoni hapa wanazuia mtu asisikilizwe hata kama ni kwa kisingizio cha taaluma yao. Simtetei RA kwamba ni msafi suala hapa ni haki yake kama binadamu ambaye anahisi amekosewa. Sasa wahariri hawajui kama ana haki ya kwenda mahakamani? Kama wanajua kwa nini wakasirike mtu anapokwenda mahakamani kutafuta haki yake? Tukiacha media yetu iendelee na haka kautamaduni kakatuchagulia nani aongee na nani asiongee tutajikuta kila siku tunapata viongozi wabaya. Maana kwa kipindi cha miaka 10 wanamtandao waliviteka vyombo vya habari na wakatuchaguliwa nani apambwe na nani achafuliwe. Tunaona matokeo yake sasa. Kwa hiyo wahariri waache kabisa tabia za kutisha watu ambao hawakubaliani na walivyoviandika na wawe tayari kuutetea ukweli kwa misingi ya uwazi na katika misingi ya kuheshimu wale waliondikwa kwa kuwapa nafasi ya kusikilizwa
 
kuombwa radhi kaka RA siyo ishu maana mchele tayari umesha mwagika kwenye kuku wengi
 
Very interesting.
So, according to Joseph Wambura, Rostam ni mhimiri wa uzalendo!

Ironically. mzalendo huyu haoni tatizo lolote katika chama chake kitukufu anachokipenda sana? This fact in itself negates the entire defence of Rostam's umahiri.
 
Kalamu rudi tena na kuisoma hiyo makala ya "Joseph Wambura" halafu badilisha hilo jina na andika "Rostam Aziz" then it'll hit you like BAM!!
 
Si Nasikia Kuna Wahariri Wengine Wako Kwenye Paycheck Ya Mafisadi!? Sasa Ni Kweli Wahariri Wa Bongo Wanaweza Kuungana? Kwa Sababu Pesa Ya Mafisadi Inaweza Kuwanunua Baadhi Yao. Cha Muhimu Ni Kumtatutia Hata Kumsaidia Kulipa Lawyer Mzuri, Ingawa Kwa System Zetu Za Afrika Mtu Aliye Kwenye Power Anaweza Kuwa-influence Majaji. Labda Kama Kungekuwa Na Jury System Na Hao Ma-jury Wenyewe Wasinunuliwe. Ila Namtakia Kila La Heri Jamaa Na Ni Kweli Wahariri Inabidi Ku-stand Up Kwa Mwenzao. Goodluck Wahariri All I Can Do Is Pray 4 U

Point kubwa sana Lusajo.

Wahariri wengi wako kwenye payroll ya mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata Rostam Azizi. Kinachofanyika hapa ni mazingaombwe until wakifanya kwa vitendo wanachokisema.
 
Hebu tuangalie kilichoandikiwa na lugha iliyotumika:

MTANDAO wa ufisadi wa EPA unawajumuisha pamoja wafanyabiashara kadhaa akiwemo mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam.

Wengine katika mtandao huo ni pamoja na Salleth Vithlani, yule wakala wa uuzaji wa rada, vifaa vya kijeshi na ndege ya Rais aliyekuja kutoroka baadaye.

Huyo Bwana anayeishi karibu na Slipway Hotel ndiye anayesimamia mtandao mdogo unaohushisha makampuni kadhaa yaliyochota fedha za EPA. Inadaiwa pia kuwa ana hisa katika Benki M.

Wengine wenye hisa katika benki hiyo inaaminika (Ni imani tu, na huwezi kumzuia mtu kuwa na imani)kuwa ni pamoja na Jeetu Patel (alijitoa baadaye), Daudi Balali, Vima Meha, Sanjeer Kumar, Bhasker Narayan, Anna Muganda na wengineo.

Pia mtandao wa Jeetu Patel unamhusisha mfanyabiashara mmoja aishie nchini Kenya aliyewahi kumiliki Benki tata nchini humo “Delphis Bank”
iliyowahi kuwapora wateja zaidi ya dola milioni 90.

Aliwahi pia kumiliki nchini humo kampuni ya kuuza magari iitwayo “Marshalls Kenya Limited” na kuliuzia Jeshi la Kenya magari kwa mkataba wenye utata kama ilivyotokea hapa nchini kwetu kwa Sailesh Vithlani na Serikali yetu (mauzo ya rada).

Ni mfanyabiashara huyo pia ambaye amewahi kuwapora wateja wa Benki ya “Trust Bank” iliyosimamiwa na BOT chini ya dhamana ya Delphis Bank mwaka 1999, na hadi sasa angali anasakwa na polisi.

Wengine katika mtandao huo ni Bharat Patel, raia wa Uingereza ambaye ni mdogo wake Jeetu Patel anayeishi mjini London mwenye kumiliki kampuni iitwayo Motorsense. Yupo pia mtoto wa Bharat Patel, raia wa Uingereza anayeishi hapa nchini aitwaye Mitul Patel ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa baadhi ya makampuni yanayodaiwa kushiriki kuchota fedha za EPA.

Pengine sakata la pesa za EPA lisingejulikana na kulipuka kama mmojawao aitwaye Jitesh Ladwa asingewashambulia na kuwararua wenzake kwa kusahau kufuta pua na midomo yao!

Mapema 2005, Jitesh Ladwa, mfanyabiashara na mdaiwa mkubwa wa vyombo vya fedha hapa nchini, alisambaza ujumbe kwa njia ya E-mail duniani kote kuibua ufisadi uliokithiri BOT. Inasemekana (watu wanazungumza mtu, hakuna ushahidi)Jitesh alikuwa anadaiwa na EuroAfrican Bank kiasi cha Sh. bilioni moja, IFC Sh. bilioni 7 na Barclays Bank Sh. bilioni 2.5, ambapo hoteli za Golden Tulip na Karibu Hotel zilikuwa chini ya rehani.

Hapo Machi 7, 2005 Jitesh Ladwa aliomba mkopo kutoka BOT kwa ajili ya kupanua Hoteli yake iitwayo Indian Ocean Hotels kwa lengo la kuvutia watalii nchini. Ombi lake lilikataliwa na BOT kwa barua ya Septemba 1, 2005 kwa maelezo mafupi tu kwamba Benki hiyo haikuwa na uwezo wa kushughulikia ombi lake.

Kabla ya hapo, Jitesh alikuwa “mteja mzuri” na mahiri wa EPA na alinufaika kwa kiasi kikubwa yeye na “Mbwa mwitu” wengine. Sababu kubwa ya kukataliwa kwa maombi ya Jitesh ni utata wa baadhi ya hati alizowasilisha Benki kwa kudhaniwa kwamba hazikuwa halisi.

Kunyimwa mkopo kwa Jitesh kulizua vita kali kati yake na uongozi wa BOT, chini ya Daudi Ballali, pamoja na wafanyabiashara wenzake (Mbwa mwitu) wenye asili ya Kiasia na akaanza kuanika nje uozo ndani ya Benki na sakata zima la pesa za EPA ambazo yeye alikuwa mnufaika pia.

Jitesh alimshambulia pia Jeetu Patel kwa kushindwa kumwokoa alipowasilisha kwake ombi la mkopo binafsi kufuatia BOT kumwekea ngumu.

Inasemekana (once again, yaweza kuwa kweli au ni porojo tu)baada ya kugonga mwamba BoT na kwa Jeetu Patel, Jitesh Ladwa alimwendea mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliweza kumpatia mkopo aliotaka. Inadhaniwa [/B](kudhania siyo kosa na watu wanadhania vingi tu!)pia kuwa, pengine(yaani yaweza kuwa au isiwe) ni kwa sababu ya kumsaidia Jitesh, kwamba Rostam Aziz hakutajwa katika E-mails alizosambaza Jitesh duniani pamoja na kuwa mbunge huyo naye alinufaika na pesa za EPA (mahakama ingeamua kama ni kweli au la)

Kuokolewa kwa Jitesh na Rostam Aziz kulijenga kambi mbili za “Mbwa mwitu” katika ufisadi wa EPA, kati ya kundi la wafanyabiashara “wapendwa” walioendelea kunufaika na BOT na kundi la “walioteuliwa” likiongozwa na Jitesh ambalo liliapa kuwalipua wale wa kundi la “wapendwa” isipokuwa Rostam Aziz kwa sababu ya umaarufu wake.

Ukweli ni kuwa, ilifika mahali kulikuwa na Serikali mbili ndani ya Serikali ya Tanzania, yaani Serikali halali chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na “Serikali nyingine” chini ya wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rostam Aziz.

“Serikali” hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.

Inadhaniwa kwamba ni “Serikali” hii ya pili (ya Rostam Aziz) iliyohamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kupigania nafasi za kisiasa ili kupata habari toka ndani ya Serikali ya namna ya kutoa ushawishi jinsi ya kufikiwa maamuzi yaliyopendelea tabaka la wafanyabiashara, ubepari wa kimataifa na kikundi kidogo cha watawala waliotekwa nyara na ubepari huo.
(Hiki ndicho kifungu ambacho naamini kilikuwa na madai mazito zaidi na ambayo aidha unayathibitisha mahakamani vinginevyo unayakanusha. Kosa la Mihangwa hapa ni kutumia neno "Ukweli ni kuwa" kwani kwa kufanya hivyo anajaribu kuashiria kile kinachofuatia ni factual)

Kwa hili, kwa nini umma usiamini unapoona kwamba mafisadi hawakamatiki ambapo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act), Sheria ya Udhahidi (Evidence Act) na Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) zimesitishwa dhidi ya mafisadi ili waonekane kama wadaiwa wa kawaida chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Act), tena bila kutozwa riba?

Kwa nini umma usiamini hivyo unapoona kwamba fedha za ufisadi zinarejeshwa na mizuka (ghosts) isiyoonekana, lakini Serikali inakiri kuzipokea kutoka kwa “watu” (“serikali ya pili”) wasiojulikana?
Je, zinatupwa na kuokotwa barabarani?

Ajabu, yote haya yanatendeka mbele ya Tume iliyoundwa na Rais, ikijumuisha Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, na Mkuu wa TAKUKURU ambao wote ni wanasheria kwa taaluma.

Sakata la EPA ndani ya BoT liliibuka kutokana na Mbwa mwitu kuraruana wao kwa wao kiasi kwamba minyukano yao iliwaamsha wananchi wenye mali kutoka usingizini na kujionea jinsi wanavyoporwa mali zao.

Rais Kikwete aliunda Tume kuchunguza uporaji huo baada ya umma kupiga yowe muda mrefu kuwa unaibiwa. Ukichunguza kwa makini huwezi kushindwa kubaini kuwa wale wanaounda Tume, baadhi yao ni wale wale wanaonufaika na mizoga iliyoachwa na Mbwa mwitu wawindaji. Je, fisi anaweza kumhukumu mbweha anayempa chakula? Ili iweje na akale wapi?

Na kwa kuwa umma wa Kitanzania umeamshwa na minyukano ya mbweha mafisadi na kukuta umeporwa mali zake kwa muda mrefu kabla ya hapo, je kuna sababu gani kunyamazia uporaji wa kale iwapo ushahidi upo? Kwa nini Rais asiunde Tume kama ile ya EPA kufuatilia uporaji wa kale?

Tuna Serikali ya wananchi moja tu [/B](kauli hii ina negate hoja ya uwezekano wa kuwepo shauri mbili kwa hiyo hizi kauli mbili zina 'cancel each other)ambayo tumeambiwa haina ubia na mtu au kikundi chochote cha watu katika kuongoza nchi. Kama hivyo ndivyo, hatutarajii kuona “Serikali” ya kikundi cha mafisadi walio juu ya dhana ya utawala wa sheria wanaoweza kupora na kuyeyuka “kimiujiza” wasiweze kuguswa na mkondo wa sheria.

Inapokuwa hivyo, umma hauwezi kujizuia kuamini kwamba baadhi ya viongozi wetu wananufaika na mizoga inayotemwa na kundi la mmbwa mwitu wawindaji ndani ya nchi yao.
 
Kupambana na RA ni gharama kubwa, kuomba msamaha si kosa, kuijipanga ni muhimu kupambana na hali kama hii.


UKWELI HATA UKIFICHWA, UTAIBUKA
 
Back
Top Bottom