Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Jamani mimi naona sawa hawa Raia Mwema kuomba radhi,lakini ukweli ni kwamba RA ni mla rushwa,Fisadi,Mhujumu Uchumi ni mtu asie na uchungu na Nchi hii,ingawa ushahidi haupo mahakamani lakini huyu Muirani ni mtu mbaya sana huo ndio ukweli wenyewe.
 
Wahariri, gate keepers! Kutokana na habari wanazozihariri katika baadhi ya magazeti yao, sitashangaa kama wataamua kumuacha SK ahangaike na RA.

Wahariri wa Tanzania wana dhiki na ndiyo maana baadhi yao wamo ndani ya payroll ya RA.


Mama mjinga na mwenye njaa hamkumbuki mwanae anpoona chakula
 
Point kubwa sana Lusajo.

Wahariri wengi wako kwenye payroll ya mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata Rostam Azizi. Kinachofanyika hapa ni mazingaombwe until wakifanya kwa vitendo wanachokisema.
Watu wanadandia magari sio maneno
 
Nadhani hii ingeunganishwa na ile ya Mwanakijiji, kwamba Raia Mwema wataomba radhi
 
Kwa maoni yangu wamefanya haraka mno kuomba samahani. Wangeutumia ushahidi huu hapa kwa kutafuta hiyo email iliyosambazwa na huyu jamaa na yeye kutakiwa kutoa ushahidi kuhusiana na email hiyo.

Mapema 2005, Jitesh Ladwa, mfanyabiashara na mdaiwa mkubwa wa vyombo vya fedha hapa nchini, alisambaza ujumbe kwa njia ya E-mail duniani kote kuibua ufisadi uliokithiri BOT. Inasemekana Jitesh alikuwa anadaiwa na EuroAfrican Bank kiasi cha Sh. bilioni moja, IFC Sh. bilioni 7 na Barclays Bank Sh. bilioni 2.5, ambapo hoteli za Golden Tulip na Karibu Hotel zilikuwa chini ya rehani.

Hapo Machi 7, 2005 Jitesh Ladwa aliomba mkopo kutoka BOT kwa ajili ya kupanua Hoteli yake iitwayo Indian Ocean Hotels kwa lengo la kuvutia watalii nchini. Ombi lake lilikataliwa na BOT kwa barua ya Septemba 1, 2005 kwa maelezo mafupi tu kwamba Benki hiyo haikuwa na uwezo wa kushughulikia ombi lake.

Kabla ya hapo, Jitesh alikuwa "mteja mzuri" na mahiri wa EPA na alinufaika kwa kiasi kikubwa yeye na "Mbwa mwitu" wengine. Sababu kubwa ya kukataliwa kwa maombi ya Jitesh ni utata wa baadhi ya hati alizowasilisha Benki kwa kudhaniwa kwamba hazikuwa halisi.

Kunyimwa mkopo kwa Jitesh kulizua vita kali kati yake na uongozi wa BOT, chini ya Daudi Ballali, pamoja na wafanyabiashara wenzake (Mbwa mwitu) wenye asili ya Kiasia na akaanza kuanika nje uozo ndani ya Benki na sakata zima la pesa za EPA ambazo yeye alikuwa mnufaika pia.

Jitesh alimshambulia pia Jeetu Patel kwa kushindwa kumwokoa alipowasilisha kwake ombi la mkopo binafsi kufuatia BOT kumwekea ngumu.

Inasemekana baada ya kugonga mwamba BoT na kwa Jeetu Patel, Jitesh Ladwa alimwendea mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliweza kumpatia mkopo aliotaka. Inadhaniwa pia kuwa, pengine ni kwa sababu ya kumsaidia Jitesh, kwamba Rostam Aziz hakutajwa katika E-mails alizosambaza Jitesh duniani pamoja na kuwa mbunge huyo naye alinufaika na pesa za EPA.


Pia wangeitumia ripoti ya Mwakyembe kumgeuzia kibao huyu jamaa ili ajibu tuhuma hizo na labda kuyasema yale aliyokataliwa kuyasema bungeni. Je alimpa mkopo huyo jamaa? wa kiasi gani? kwa uhusiano gani aliokuwa nao na huyo jamaa?
 
nnaamini raia mwema walipima upepo kabla ya kuamua, walishauriana na watu wa sheria na nnaamini walihadharishwa na hatari ilio mbele yao.


kwa hio waliamua kufata msemo wa kiswahili usemao "bora lawama kuliko fedheha"
 
Habari ikishakuwa na "inasemekana" tu inakuwa yale yale....

Kama una ushahidi unaweka "ThisDay can reveal"

Halafu wabishe unawatolea document mahakamani, habari za kusemekana hata huko Scotland inasemekana kuna "Loch Ness Monster" inasemekana pia kuna parallel universes with different laws of physics and particles such as tachyons with the speed of light as lowest speed barrier.

Key world ni "inasemekana"
 
nnaamini raia mwema walipima upepo kabla ya kuamua, walishauriana na watu wa sheria na nnaamini walihadharishwa na hatari ilio mbele yao.


kwa hio waliamua kufata msemo wa kiswahili usemao "bora lawama kuliko fedheha"

Email hiyo hiyo iliyoandikwa na huyo jamaa ndiyo ilianika hadharani ufisadi uliofanywa pale BoT, na ukweli umedhihirika. Kwa hiyo huyu jamaa alichoandika kina ukweli ambao unaweza kutumika dhidi ya RA.
 
Hicho ki email hakiwezi kusimama mahakamani, labda kama wana document za nguvu za kuki back.

Mtu yeyote anaweza kuchonga email yoyote kuhusu kitu chochote, tatizo ni document zinazoweza kusimama in a court of law.
 
Je kwa vile RA anawajua wakuu wa Raia Mwema ambao wamewahi kufanya kazi chini yake yawezekana alijua anaujiko wa aina fulani wa kuwatikisa? just thinking...
 
Joseph Wambura Aprili 23 said:
...Kilichonisikitisha zaidi, mwandishi wa makala hiyo naye ameangukia katika mkumbo. Anamwagia matope Rostam, bila kuchunguza na wala sijui kilichomtuma afanye hivyo.

- Mwaka 1994 ...
- Mwaka 1977 Rostam alikuwa...
- Mwaka 1999 Rostam huyu huyu...
- Mwaka huo huo, kwa ujasiri mkubwa, Rostam
- Rostam huyo huyo anayebezwa, mwaka 2001, ...
- mwaka 2004 Rostam alimbana vilivyo aliyekuwa Waziri wa Uchumi na ...
- Akataka uwepo udhibiti wa hali ya juu ili shilingi isiporomoke ...
- Sipendi kuendelea zaidi ya hapo. Natumaini mwenye macho haambiwi tazama.
Hivi wajibu wa Mbunge kwa kiapo chake unaweza kufunika makosa anayoyafanya? Ni kweli kwamba wabunge uongea ili kulipwa fadhira tofauti na kiapo (kama kupata uwaziri au kuchota pesa EPA)?
Kwa vyovyote iwavyo, Mwananzela hakumtendea haki Rostam.
Katika hili, huyu Bw. Wambura ndio hakumtendea haki RA kwa kumuweka katika kundi la wabunge ambao hutekeleza wajibu wao Bungeni ili fadhira ziwarudie!

Mwananzela amejaribu kumtetea RA alipoonyesha kushangazwa na Bunge kuzima hoja

Uandishi wa aina hii ni hatari kwa ustawi wa Taifa. Ninashauri bora kutoandika pale tusipokuwa na taarifa sahihi, vinginevyo tunaishia kujiumbua na kulipotosha Taifa.
Hapa nashindwa kuelewa nani analipotosha Taifa, Wambura anayeshawishi uozo wa RA ufunikwe (na wajibu aliofanya Bungeni), au Mwananzela aliyehoji RA kutopewa nafasi ya kufichua mengi zaidi?

Ningekuwa mimi ndiye RA ningemwambia huyu jamaa (Bw. Wambura) arudishe pesa maana makala imekosa nguvu kunisafisha!
 
John.. what if... Joseph Wambura ndiye Rostam Aziz? .... Hivyo vyote alivyovitaja hapo ni watu wangapi wanavikumbuka... isipokuwa..
 
sasa hivi ni Raia Mwema, Uuungwana si Vitendo
 
Ngurumo Ni Fimbo Ya Mbali Anapiga Kelele Weee Halafu Mwaka 2010 Atakuja Hapa Kuomba Uanachamahalafu Mwaka 2011 Tutampa Ukuu Wa Wilaya Au Aendeshe Kipindi Fulani Katika Tbc

Mkuu Shy, maneno hayo makali kweli kweli. lakini unamjua Ngurumo au unamsikia? naona hapa umemwonea saaaaaaaaaaana.
 
Back
Top Bottom