Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Kama nilivyokwishasema ingawa ukweli huo unaogopwa, RA ni nguvu kubwa ambayo inahitaji umoja kuishinda. Ukisema RA unamgusa moja kwa moja Lowassa, Karamagi na Vijisenti ambao kwa pamoja wanamiliki sehemu kubwa ya media nchini na wanawaandishi wa habari na wahariri wao! Hivyo, bila kumsaidia Kubenea, bwana mdogo huyo ataenda na maji! Ijabu
 
Hebu tuangalie kilichoandikiwa na lugha iliyotumika:.

Ah kweli "the article is full of sweeping statements". Hii inaashiria kweli iliandikwa kukiwa na some elements of "jazba" ingawa sio kali kama zile "jazba za kipemba". This is no good for- a responsible journalism.
 

Hakuna haja ya kuwapongeza mafisadi! RA apati sifa kwa vile amekuwa na uongo wa kueleza umma wa Tanzania!

Kwa heshima nyingi nakuomba moelex23 ufute kauli yako?
 
Ukifuatilia porojo za ugoni wa Kubenea na jinsi zinavyoungwa mkono na baadhi ya wanaJF, utaelewa kwa nini kila kiongozi sasa anataka kuwa na gazeti lake! Anaongoza RA ambaye mbali na Mtanzania, Rai, The African na Mwananchi (ambako ana shares), ameanzisha msururu wa vijigazeti vya udaku kumsafisha yeye na rafiki yake kipenzi Lowassa. Wanafuatia wengine: Diallo, Seif Khatib, Mbowe n.k. Sababu iko wazi: anzisha uongo wowote ule gazetini kwako, sehemu kubwa ya Watanzania watauamini bila tafakuri. Kubenea "mgoni", wataamini; Spika Sitta "kagushi risiti ya dawa", wataamini; Mwandosya "anataka Urais 2010", wataamini; Lowassa "kaonewa" licha ya kushindwa kujitetea Bungeni, wataamini; Lowassa "kaonewa" kwa kuwa ni "Mmasai" wa Monduli, wataamini; Msabaha "kaonewa" kwa kuwa ni Mwislamu, wataamini; Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge "ameiba" maji ya DAWASCO, wataamini n.k. Tumekosa utamaduni wa uchambuzi, wa kupembua taarifa ili kutenganisha pumba na mchele! Mafisadi wanataka tupoteze lengo, tuache kuwamulika tujishughulishe na porojo za ngono za Kubenea! Mafisadi wamejeruhiwa vibaya na taarifa ya Richmond ambayo imeandikwa kwa ustadi, ufasaha na umakini mkubwa, sasa wanataka tuelekeze macho kwenye porojo na risiti za hospitali na nyumba ndogo ya Spika! Hawataki tuendelee kuiangalia taarifa ya Kamati Teule, wanataka tujadili porojo za kitoto za Mwakyembe kuiba maji ya DAWASCO! Tunaomjua Mwakyembe kwa karibu tunawashangaa wanaoamini taarifa za washikaji wa Lowassa - CEO wa DAWASCO ni ndugu yake na Meneja Uhusiano ni Bibi yake (pengine wawe wameachana leo), na wote tulio kwenye media tunaliojua hilo! Wahariri, waandishi wote wa habari tumsaidie Kubenea kwa nguvu zetu zote ama sivyo kenda na maji huyo! Anapambana na nguvu kubwa! Ijabu
 
Ni afadhali wamfunuwe huo mdomo wake ili abwabwaje! Akifanya hiyo ataweza kumwaga MCHELE KWENYE KUKU WENGI.
Mpka sasa wote watuhumiwa hawajaweza kumwaga huo mchele.Kuna vitu vingine ni vya siri mno kwani wengine serikalini pia nao wamenyamaza kimya kama kwamba wamefungwa kauli.
WEKENI MAMBO WAZI HADHARANI.

AU MNATAKA rais Kikwete atunge tena TUME maalum ya ROSTAM !
 
Hamna lolote hapa,
Wote SPIKA,RA,SYSTEM,MWANAHALISI(Saidi Kubenea na wanzake)lao mmoja.
Kwenye ile Taarifa iliyo chwapishwa kwenye MWANAHALISI la jana hakukua nakitu cha SPIKA kumfungia RA kuzungumza.
i get this wield feeling kwamba bado tunaongopewa huu wote ni mpango hakukua na lolote kwenye ile taarifa ambayo supposely ilikua ya RA kwa SPIKA na BUnge na hayo matusi kwa DK.Mwakyembe hayakua moja kwa moja na kwa kuhesabu yapo kama matatu kama sio 4 na naomba niseme ni YAKUTENGENEZA.

w
Well,kwa mtazamo wangu Jamaa (Aliye juu i mean aliye juu kwenye Uongozi) ameamua kumrudishia HISA ZAKE ROSTAM ndio maan wakaamua kutu fix na hilo Mwanahalisi kama hivyo sivyo basi then we could have RA spred the beans.

MTAZAMO TU....!
 
Ni kitu gani kinachomfanya huyo jamaa (wa ngazi ya juu katika Uongozi) kumrudishia RA hisa zake?
Kuna fununu kwamba huyo RA si raia wa Tanzania kwa hivyo ilikuwaje awe na cheo cha UBUNGE?
Huku kuogopana na na kukingana (kirafiki) ndiko kunakoharibu maendeleo ya Tanzania.

WATAKINGANA MPAKA LINI? AKHERA!
 
Kama ufisadi ni huo waliofanya RA na Mkapa mimi kwangu nauita ufisadi endelevu kwa maana kuwa wamewekeza ndani ya nchi na watu wamepeta ajira,leo tunafaidika na bank m amabayoinalipa mishahara watoto wa walalahoi mizuri kuliko bank yeyote ndani ya nchi,kiwila mine imetoa ajira mpya zaidi ya mia tatu kwa watanzania,gazeti kubwa nchini la mwananchi limetoa ajira ngapi?habari corporation ilikuwa inakufa nasasakaifufua na wananchi wamepata ajira tena.Tunapinga tabia kama za kina mobutu au sani abacha ambao wanaweka mapesa nje ya tanzania.Kwa nchi yeyote ilioendelea hakuna namna unaweza pata maendeleo bila accumulation of capital.ulaya walitumia ukoloni.sisi tutpata wapi nchi ya kuinyonya,hivyo watu wenye akili kam RA wachukue hio bank kuu na kuwekeza...bravo Rostam Aziz,God bless u.
 


Fisadi mkubwa,
Ufisadi ni ufisadi tu kwa sababu at the end of the day atakayelipia madhambi aliyoyafanya Mkapa na RA ni wewe, mimi, mjomba wangu, shangazi yangu na wote
ambao wameshindwa kupata matibabu stahili kwa sababu hela zetu zinakwenda kulipia riba kubwa ya madeni ambayo mafisadi hao wenzako wametuingizia. Huwezi ku- accumulate capital kwa migongo ya wakulima na wafanyikazi wa Tanzania. Huo ni uhaini. Na ningekuwa na mamlaka hao mashujaa wako unaowatetea ningewatia wote KITANZI!
 
Na ningekuwa na mamlaka hao mashujaa wako unaowatetea ningewatia wote KITANZI!

Mkuu Jasusi,

Heshima mbele mkuu, tupo ukurasa mmoja hapo!

By the way vipi huko anga zako huko nasikia kuna habari za kifo, vipi hizo?
 
Haya tena, yaelekea Rostam hakuwa na skadi la maelezo ya kuhatarisha maslahi ya CCM au SiriKali... kama isemavyo hapo chini


 
Mkuu mbona unakosea tena!!!?? CCM mtu safi ni Mmoja tuu!!(Dr.).Na hata wao wanalijua hilo,hao wengine ni kina nani haswa?
**sanasana Mh.Shamsi Vuai Nahodha wa kulee upande wa pili.
 
Kila chama kina taratibu zake na wla sio pinda kama unavyodhani ccm inaongozwa na katiba yake hata jk hawezi kuamua mwenyewe ni kikao ndicho kinachoamua unafikiri ccm ni chama kama vyama vingine mtu yuko BWEJUU atakalo sema ndiyo chama kimesema Mzee mwanakijiji hebu wafafanulie hiyo ibala uliyonakili
 
Huyu Rostam ni gabachori na magabachori wengi wana matatizo ya pesa maana wana msemo wao unaosema "MALI BILA GENDO AWEZI KUWA MALI" kwa maana hiyo nafikiri jk alishauriwa vibaya kumuteua huyo gabachori na ndiyo maana alivyoona tume imeundwa akakimbilia uk kujificha na wala siyo kupuzika jk naomba uwe macho na hawa magabacholi
 
Duh hii kali eti 'hospitality' to share an email account...kweli he must think tanzanians are soooo stupid..ni ufinyu wa mawazo..it takes 20mins to set up ...@dowans.co.tz lol...naona ata kuiba nako wanabahatisha...Anyway ndo siasa zetu hizi...naona sasa tukubali matokeo tuu...
 
Fisadi anapoamua kupambana na washika kalamu nani mshindi??? Tusije kusikia mtu mzima yuko LUGALO???
 
Huyo ameshakuwa fisadi koko. Kuna msemo wa kiswahili usemao mfa maji haachi kutapatapa. Hiyo mitaji aliyoiwekeza Dubai kwa nini asingewekeza bongo? Sasa akianza kuchokoza watu watamuumbua mimi sitaki kumfanyia character assassination fisadi huyu hasha sisi tunahitaji kilichokuwa chetu kama watanzania.
 
We Fisadi Mtoto, mdogo, sijui kuna kitu gani ambacho wame-invest Tanzania ambacho kinaendelea vizuri? yaani mradi wowote ambao mafisadi wameanzisha na uko fresh kabisaa. Hawa jamaa walikuwa na Tamaa mbaya tuu, kila kitu walitaka wao na sasa yanawashinda. Mradi wa Richmond Ovyoo, Bandari ovyoo, Kiwira Ovyoo, na mengineyo. Yaani kwa kifupi ni tamaa tuu. Na hao wahindi waliowatumia hao viongozi wetu wako wapi sasa hivi, si ajabu wanakula kuku na wakati kina Mkapa kila mtu anawaponda sasa hivi. Kuna kitu kinaitwa "Common Sense" ambacho naona hao ndugu zangu hawana, wana tamaa tu.
Back to the Topic. Keep it up Kubenea, at the end the truth will prevail
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…