Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 164
Lakini mkuu hii si ilikuwa kazi ya Kamati ya Mwakyembe au?
Mkuu Kitila,
Kama utakumbuka Hadidu Rejea za Kamati ya Bunge kuchunguza suala la Richmond,ya kwanza ilikuwa ni Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina nani, na ni kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa gesi wa MW 100.
na moja majibu kuhusiana na hoja hiyo,Mhe. mwakyembe alitayabaanisha haya
Mheshimiwa Spika, matokeo haya yanaonesha hali halisi iliyopo Tanzania, hali ya uoga na ya kutojiamini inayowakumba Watanzania walio wengi wanapotakiwa kuelezea kwa uwazi maneno yale yale wanayoyanong'ona pembeni kwa hamasa kubwa. Kwa mtindo huu Taifa letu linaweza kuishia kuwa la walalamishi wasio na ujasiri wala dhamira ya dhati ya kukemea maovu pale inapobidi.
na wakati Mhe. ajahitimisha alisema haya kuhusu nani mmiliki wa RDC
Mheshimiwa Spika, Mkataba wa uzalishaji umeme wa dharura unaielezea kwenye utangulizi Richmond Development Company LLC kuwa ni kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Jimbo la Texas, Marekani na yenye anuani ifuatayo: 5825 Schumacher, Houston Texas 77057, Marekani. Aidha, kifungu cha 5.1 (a) cha Mkataba huo kinatoa maelezo ya ziada kuhusu Richmond Development Company LLC kuwa ni kampuni yenye ukomo wa hisa (limited by shares) ambayo uwepo wake Tanzania haukinzani na sheria za nchi. Kifungu hicho kidogo kinamalizia kwa kutamka bayana kuwa kampuni hiyo ina nguvu na mamlaka yote stahili ya kikampuni (all requisite corporate power and authority) ya kumiliki au kukodisha na kutumia mali zake na kuendesha biashara zake kama ilivyokusudiwa nchini Tanzania.
Mheshimiwa Spika, hiyo ndiyo sura ya Richmond Development Company LLC kama ilivyoainishwa katika Mkataba huo wa kisheria uliotiwa saini kwa upande wa TANESCO na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa TANESCO, Johannes G. Lottering na kushuhudiwa na aliyekuwa Kaimu Katibu (Ag. Company Secretary) wa TANESCO, Godson Makia na kwa upande wa Richmond na Meneja wake, Mohamed Gire na kushuhudiwa na wakili maarufu nchini, Dr. Ringo Tenga ambaye alijitambulisha katika mkataba huo kama Katibu wa Richmond Development Company LLC.
Hapa walieleza Meneja wa RDC tu ila wamiliki wa RDC ni kina nani,sababu Rostama alikuwa anafanya nao Biashara lazima atakuwa akifahamu ni nani mmiliki wa RDC.Hivi kwa maneno ya Msabaha,Kampuni ya Bwana Mkubwa ni nani??Kubene alaienda kutoa Ushahidi kuhusu RDC,na anajua fika RDC ni kampuni ya kitapeli inayomilikiwa na Bwana Mkubwa.
Kuna haja sasa Kwa Dr. Msabaha(kama Sheria ya Bunge ikipindishwa) aje atuambie huyo Bwana Mkubwa ni nani??Je ni kitila au Gembe??