Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Lakini mkuu hii si ilikuwa kazi ya Kamati ya Mwakyembe au?

Mkuu Kitila,

Kama utakumbuka Hadidu Rejea za Kamati ya Bunge kuchunguza suala la Richmond,ya kwanza ilikuwa ni Kubainisha Richmond Development Company LLC ni kina nani, na ni kampuni ya shughuli zipi na hivyo kupima uwezo wake kupatiwa zabuni ya kuleta nchini na kujenga mtambo wa umeme wa gesi wa MW 100.

na moja majibu kuhusiana na hoja hiyo,Mhe. mwakyembe alitayabaanisha haya



na wakati Mhe. ajahitimisha alisema haya kuhusu nani mmiliki wa RDC


Hapa walieleza Meneja wa RDC tu ila wamiliki wa RDC ni kina nani,sababu Rostama alikuwa anafanya nao Biashara lazima atakuwa akifahamu ni nani mmiliki wa RDC.Hivi kwa maneno ya Msabaha,Kampuni ya Bwana Mkubwa ni nani??Kubene alaienda kutoa Ushahidi kuhusu RDC,na anajua fika RDC ni kampuni ya kitapeli inayomilikiwa na Bwana Mkubwa.

Kuna haja sasa Kwa Dr. Msabaha(kama Sheria ya Bunge ikipindishwa) aje atuambie huyo Bwana Mkubwa ni nani??Je ni kitila au Gembe??
 

Yes Kitila,
Unajua Rostam ndiyo anajua ni kiasi Gani ambacho RDC wanlipwa kwa siku,sababu mpaka sasa serikali haijajitokeza hadharani kukiri kwamba RDC inalipwa hiicho kiasi cha pesa,na huu ndio uzandiki na usiri ambao utamgharimu JK.

Kimsingi na kwa ukaribu inawezekana 152m. inajumuaisha na Capacity charge,malipo ya ziada na jinsi Biashara ilivyokuwa imepangwa,Rostam anayajua Mengi kuhusu RDC Mie namuombea apewe nafasi ayazungumze tena Mahakamani.

Kuhusu Suala la Kamati kufanya kazi baada ya Muda,Angalia kanuni za bunge utaona uwezo wanaopewa,iko mbali nami ila nitasema ni wapi panawapa ruhusa ya kufanya hivyo
 
Mkuu Kitila,


[/COLOR]RDC ni kampuni ya kitapeli inayomilikiwa na Bwana Mkubwa.

Kuna haja ya sasa Kwa Dr. Msabaha(kama Sheria ya Bunge ikipindishwa) aje atuambie huyo Bwana Mkubwa ni nani??Je ni kitila au Gembe??

Sasa mimi ndio hapo nashangaa, kama ushahidi upo, kwa nini kamati nayo ilijiumauma katika kumtaja huyo mkubwa, kwa nini tuzungushane?

Wasiwasi wangu ni kwamba tutasubiri JK atoke madarakani ndipo tuseme kwamba alihusika na Richmond. Ndivyo tulivyofanya kwa Mkapa; alikuwa akijichotea tunamwangalia. Tulimuona akijiuzia ile nyumba pale Upanga kwa bei poa lakini tukafunga macho. Tulinusa, tukasikia na kuona Mkapa akijipa Kiwira lakini tukaamua kuziba pua, macho na masikio yetu na tukayafungua alipotoka madarakani.

Tunajua JK ndiye aliyeitetea vizuri sana na kuikingia kifua kampuni ya Richmond na utetezi wa Rais ulinukuliwa kwa kirefu na kwa mbwembwe katika gazeti la Guardian la tarehe 21 Desemba 2006. Sasa kwa nini kamati ilikwepa kumtaja Rais na kwa nini na sisi hapa tumebaki kuhangaika na Rostam na tunaelekea hatutaki hata kusoma vizuri maelezo yake? Au ndiyo ileile kasumba yetu ya woga na unafiki ambao pia Mwakyembe kaeleza vizuri kwenye ripoti yake?
 

Alitaka ushahidi hapa kwani hapa ni mahakama au polisi?
 
Kwa nini alisubiri mpaka aitwe?? Kama kweli alikuwa anajua atahitajika kwa namna moja ama nyingine kwa nini hakujipeleka mwenyewe akahojiwe au ndo na yeye anataka kutuambia natural justice haikufanyika????

Kati ya Rostam na Mwakyembe nani anastahili kuitwa msanii?? Rostam acha kutuletea maneno mengi ya kibombay hapa!!! Hivi unatuambia nini hapo? Kwamba ripoti nzima imepotoshwa? na kama wewe ndo unaujua ukweli kwa nini haukuutoa kabla...??

Hivi huyu Rostam ana advisors kweli au yeye anaongea tu kile kinachomjia kichwani??
 
Nadhani watu bado mnachanganya kampuni ya RDC ya Houston ambayo wamiliki wake ni Mohammed Gire na the other Mohammed, wamiliki wa RDC Tanzania hawajulikani; why? kwa sababu kampuni yenyewe haipo.
 
Yes Kitila,

Kuhusu Suala la Kamati kufanya kazi baada ya Muda,Angalia kanuni za bunge utaona uwezo wanaopewa,iko mbali nami ila nitasema ni wapi panawapa ruhusa ya kufanya hivyo

Sasa issue hapa ni kwa nini Mwakyembe alikanusha bungeni kwamba kazi yao hawakufanya nje ya muda waliopewa, what was he is trying to conceal? Au hakukanusha?

Unajua hapa ninachokiona kuna loop holes za kijinga kiasi kwenye ripoti ya kamati ambazo zinawapa hawa mafisadi sababu za kujitetea unnecessarily. Lest we forget, it has been said many time here and elsewhere, corrupt people are not stupid; they are very smart. In order to deal with them effectively we must be many times smarter than them. Sasa inaonekana bado tuna shida na namna ya ku-deal na hawa jamaa sawasawa.

At the end of the day, tutakuja gundua kwamba kamati ya mwakyembe ilimsaidia zaidi JK kuondokana na watu ambao alikuwa hawataki kwenye serikali yake, ambao pengine alikuwa hana uwezo wa kuwatoa, kuliko kuliokoa taifa na mtandao wa ufisadi. Sasa kama mpaka dakika hii tunaendelea kuilipa Dowans kwa kazi ambayo hawakuifanya na hata baada ya kugundua kwamba mkataba wenyewe ulikuwa hewa in the first place, utasema sisi tupo smarter kuliko mafisadi?
 
Nadhani watu bado mnachanganya kampuni ya RDC ya Houston ambayo wamiliki wake ni Mohammed Gire na the other Mohammed, wamiliki wa RDC Tanzania hawajulikani; why? kwa sababu kampuni yenyewe haipo.
Sio kwamb Kampuni haipo,ipo sana,Mohamed Gire ndiye aliyesaini mkataba kwa niaba ya RDC huku shahidi akiwa Ringo Tenga.

Kampuni ipo ila sema File lake ndilo alionekani,Kuna maneno ameyasema Kitila Hapo juu yana uzito wa khali ya juu sana,tusisubiri tuje tuyasemehe baada ya mtu kutoka madarakani.

Mzee Mwanakijiji unamkumbuka Githongo?yule aliyekuwa Katibu wa Tume ya Maadili ya Kenya,alisema hadharani kuhusu uovu uanofanywa na viongozi wa serikali,Hatuhitaji wajerumani waje watuchape viboko ile tutatumbue hili,tunahitaji viongozi shupavu na wasio waoga kusema jambo kama Marehemu Mwalimu J.k Nyerere.
 

Hii ndiyo ilikuwa point ya kuwa na hiyo kamati.na kama unakumbuka Mwanakijiji alishasema hilo lilikuwa ni bao la kisigino tulilopigwa
 
Mzee wa vimada AKA Six AKA mzee wa kukurupuka AKA mzee wa kwenda USA kwenye mwaliko wa kidini wakati bunge likiendelea AKA mzee wa busara za spika amechemsha sana kutumika kwenye PR ya mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata Rostam Azizi.

Angempa nafasi atoe hii hoja bungeni kisha wabunge wa ccm wawe kwenye record ili ijulikane kama wako na sisi (with us) au wako na wezi na mafisadi wakubwa wanaonyonya nchi (with them/against us).
 
Hapana Rostam amesema na kuonyesha kwa mbali kuna watu wamefichwa na wao wametolewa kama kafara ,kilicho zuia habari hii kufikishwa Bungeni ni maswali ambayo Rostam alikuwa na uhakika yatazuka na hapo ndipo atakapopata nafasi kutoa lile alilonalo rohoni,naamini kabisa majibu aliyoyatayarisha ambayo hayamezeki alikusudia kwenda kuyatapika hapo amwache spika azowe ila kilichomwagika hakizoleki tena ,hapo ndipo walipopaona wakwasi wanaojua mitego ya kina ,ukisoma utaona kitu very simpo lakini kwa undani kuna jipu limeiva.CCM wamekwepa jipu hilo kwenda kutumbuka mbele ya Bunge.
Na hasira zake sasa ameenda kukamua waandishi akijua huko wanaelekea mahakamani na kwa vile jipu halikutumbuka Bungeni sasa analipeleka huko kaeni mkao wa kusikia harufu mbaya nani na nani watanuka au watanukia huko.
Nionavyo CCM kama hawakuamka mapema basi jamaa ataenda kuwaumbua huko.
 
Hivi huyu Mkoloni andhani ataweza kututawla na kuamrisha mahakama zetu kama anavyotaka yeye?

Na mahakama zetu kama kweli ni mkondo wa haki,basi zichambue kwa makini hoja za huyu fisadi bila kupinda pinda.

Pia naamini hata kama atatumia pesa kuhonga mahakama (maanke mfumo wetu wa kimahakama nao unanuka rushwa) ili ifute matakwa yake kama tajiri,basi JF tujue tuna jukumu kubwa la kupambana na mtu kama huyu.maanke sidhani kama mahkama wataweza kutuzuia sisi wananchi kummulika.


Jamani,pia mwenye details za uraia wake plz atoe ili tujue pia jinsi ya kumpa moyo Mtikila kushughulika na huyu Mpuuzi.Maanake kuna siku alisema atafuatilia kuibua uchafu wa huyu punguani.
 
Da!! hii mpaka mtu aichambue, ama watayamaliza pale mahakamani, sisi watanzania tukae kimya, kama kuna ukweli ktk hili litajulikana tu. let we take the time.
 
Mahakamani jama!!! Kwenye vyombo vya habari nini tena!!! Tuachie mahakama Kubenea au Aziz mkutane huko tutajua nani mkweli!!!

Kubenea: Ati ile kesi yako ni ya Nyumba nd*g* au ni ya Mafisadi? Which is which I'm confused bro.


Sasa hapo ndipo mtu atakapopindisha mjadala.Hapa ni kubenea na wananchi VS RA na mafisadi.Lazima tuanze kuwazomea kabla hata hawjaenda huko mahakamani.

Kesi ni ya kumwagiwa Tindikali
 
Huyu Rostam ni mpuuzi.Kwanza kwenye hizi hoja zake lengo lake ni kumshambulia na kumuumbua mwakyembe.anataka kupambana na Mwakyembe na si kupambanisha hoja.

Keep it up speaker,ulifanya vyema kutupilia mbali huu utumbo.

Halafu anasema anatusaidia watanzania kubaini ukweli.Mimi namuomba autusaidie kwa kurudisha Fedha zetu na ku-resign ubunge.Atakua ametusaidia sana pia akirudi kwao huko iran au ajisajili kama foreign investor
 

Rostam doesn't have that kind of thinking.... alichokisema ndio hicho hicho!!! Kama kweli angekuwa na busara kiasi hicho sidhani kama angethubutu kusafiri nje ya nchi makusudi ili aje atoe lawama kwa tume!!!
Waandishi watamtoa nishai tu na asipojiangalia that will be his end!!! Pole sana Rostam ila kwa kuwa wewe ni fisadi you can't change that!!!
 


Huyu spika nae wakati huo huo tukisubiri ripoti ya matumizi tata ktk ofisi ya Bunge,pia aandae utetezi juu ya ufisadi wake.

Ila kweli Rostam hajui kujitetea.Yaani hapo karusha mipasho tu,hakuna hoja ya msingi.
 


He thought that wil be the best way of expressing his anger.Bado angetakiwa kufanya lililo bora zaidi
 

Kitila,
Ahsante kwa kutuwekea kumbukumbu tena. Hatimae, hata wasiopenda kuamini kuwa mfalme yuko uchi watauona ukweli ulivyo. Tunabaki kuzunguka zunguka tu mbuyu kama wendawazimu, sijui kwa nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…