Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Ukisoma post zangu a nyuma nilishawahi kusema kuwa wewe, mtu wa pwani na kibunango ni mtu mmoja na nikatoa hoja zangu ni kwa nini. Kwa hiyo sishangai kwa nini umeingilia ujumbe haraka haraka bila ya kuutafakari.

Ujumbe wangu kwa wewe na hao ndugu zako ni kwamba tunazikaribisha hoja zenu lakini at least ziwe na nguvu na research za kutosha. Lakini kama mkiendelea kukurupuka kama hivi na kuleta hoja za kishabiki tutawa-fire tu kama tulivyomfanyia baba yenu bungeni. Hapa JF haogopwi mtu hapa hasa watu wenye hoja nyepesi kama zenu. Nadhani itabidi kufanya IQ test kabla ya kupewa uwanachama hoja za kusema ccm ndicho chama imara bila ya kutuambia kuwa ni kwa nini ni imara hazina nafasi humu labda kwenye majukwaa.

Wasalimie pwani

Kwa hiyo post yako hapo juu hiyo IQ test wewe usha fail yaani yako imezidiwa na kidogo na ya kuku.

Kama Masatu = Mtu wa Pwani = Kibunango unahitaji kukumbiziwa mirembe haraka sana as the matter of urgency...
 
2008-02-16 09:23:21
By Guardian Reporter, Dodoma

The Speaker of the National Assembly, Samuel Sitta has said that he will ask the Igunga MP, Rostam Aziz, who was accused by the House select committee of refusing to testify when summoned, to respond to the allegations in the next sitting.

Rostam Aziz has been implicated in the Richmond scam during the just-ended House session as one of the key players.

Speaking before the winding up of the House session by Prime Minister Mizengo Pinda, the Speaker informed the House that he had received a letter from Rostam Aziz complaining that he was not fairly treated by the select committee when collecting evidence with regard to the ownership of Richmond Development Company, LLC.

``Since Rostam is not in the House today I will ask him to clarify his claims in the next session that he was not given a chance to plead his case,`` said Sitta.

In his presentation, the select committee chairman, Harrison Mwakyembe said a summons was delivered to Rostam Aziz`s Oyterbay home in Dar es Salaam on December 24, last year by an official from the Parliament office.

In his letter, he claimed that the summons was delivered to him on a day that he could not be easily available in Dar es Salaam.

One of Rostam`s relatives apparently received the summons on his behalf saying that Rostam was out of the country.

The committee had requested him to appear before the committee on December 27, 2007, but didn?t turn up.

Parliament had been told that Rostam Aziz had arrogantly refused to appear before the select committee and that he should be penalized.

Several MPs who spoke on Thursday directly linked Rostam Aziz with Richmond as the proprietor of the controversial firm.
SOURCE: Guardian
 
I think government should do something soon as they can because most of Tanzanians now hate this unforgoten fraud which done by our leaders,while thousands of people left helpless in their villages
 
Huyu jamaa si tunaambiwa vilevile yumo kwenye sakata la EPA ya BoT?
 
Huyu anapatikana kila kona yenye pesa ama wizi yeye ni mwizi na deals chafu na JK analijua hili tangia zamani na ni mshikaji wake wa karibu sana .
 
Kwa hiyo post yako hapo juu hiyo IQ test wewe usha fail yaani yako imezidiwa na kidogo na ya kuku.

Kama Masatu = Mtu wa Pwani = Kibunango unahitaji kukumbiziwa mirembe haraka sana as the matter of urgency...

KInachonifanya niseme nyie ni watu wamoja ni kutokana na vitu vifuatavyo:-

(i)Kujibu kwa kukurupuka
(ii)Kuandika haraka bila ya kuedit ulichoanndika
(iii)Ushabiki wa vyama bila ya hoja ya msingi
(iv)Kupenda kutukana watu (matusi)
(v)Kuwa JF 24 hrs (sijui hamja ajiriwa au kujiajiri)
(vi)Kutoipenda Tanzania
(vii)na kutoelewa kuwa ccm ni chama tu siyo malaika

Hayo hapo yamenifanya niwaweke group moja. Mimi sijui kama ni mtu mmoja au ni watu watatu tofauti ila nachojua ni kuwa nyie mko class moja. Sasa kama unawakana wenzio kuwa ni tofauti na wewe mimi siko.

Cha msingi hapa ni kubadilika na kuanza kuja na hoja za msingi ambazo umezifanyia utafiti. Kuwa tayari kupingwa kwa sababu tuko watu wenye mtizamo tofauti. Uandike hoja zako kiufasaha na kujaribu kuedit unachoandika ili tunaosoma tuelewe unasema nini. Hapo nitakutoa kwenye kundi hilo usilolitaka. Kuanzia sasa nitakuwa ninakuchunguza thread zako na nitakupa majibu nitakaporizika kuwa umejirikebisha.

Mimi si mwanachama wa ccm, wala sikubariani nao na jinsi wanavyoendesha nchi hii. lakini naweza kuandika hoja ya kukipamba chama kuliko wewe unavyofanya humu. Cha kujiuliza sasa wewe unafanya nini humu? week end njema
 
KUTOKA MAKTABA YA JAMBOFORUMS

Pressure on Kikwete to act on graft

When the gathering political storm in Tanzania reaches a crisis, President Jakaya Kikwete might be forced to do the unthinkable - sacrifice bosom friend, Prime Minister Edward Lowasa.

The public views the premier as the embodiment of graft in the Government, which the president cannot tame.

Jakaya has come under pressure in the past two months to purge "rotten eggs" from his stable.

Among the donor community, he is anything but not in charge..

The Government was last week thrown into panic after Western development partners demanded action on runaway corruption, failing which they threatened to withhold financial support pending the arrest and prosecution of the culprits.

Donors have warned that Tanzania, which has a hole in its $5.8 billion budget, risks aid cuts for failing to rein in graft.

The prospect of aid cutback elicited angry response from Foreign Minister, Mr. Bernard Membe, who demanded that the envoys stop meddling in Tanzanias affairs.

Matters were worsened whenhe threated to expel foreign envoys who recently threatened to halt development funding pending investigation of fraud allegations.

The standoff between Tanzania and donors had a ring of the controversy between Kenya and its development partners, during which aid was withheld for more than 14 years from 1992.

Sourcestold the Sunday Standard that a Cabinet reshuffle looms in which key Kikwete allies, including Lowasa, are likely to be relieved of their duties.
He added that the public is concerned that the Government has failed to quell ethnic cleansing in the West where scores of people have been killed. (????)

The media have been directed not to report the blood bath in Kagera "to maintain a good image of the country abroad." (?????)

The opposition has taken the cue from the public and given the Government one-month ultimatum to institute investigation into fraud allegations and quell ethnic cleansing or risk countrywide civil disobidience.

Opposition parties - Chadema, Tanzania Labour Party (TLP), NCCR-Mageuzi and Civic United Front (CUF) - announced on Monday plans to organize demonstrations to force the Government to come clean on graft allegations.

President's son in financial rip offs???

Word on the streets in Dar has it that the reshuffle could be on the cards soon after the national elections of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) next month.

To cushion himself againstpotential retribution, opposition leaders said, Lowasa involved the president's son in one of massive financial ripoffs in which the taxpayer lost huge sums of money through faulty tendering of Tanzania Electric Supply Company (Tanesco for the procurement of emergency power generators last year.

The expensive equipment turned out to be second-hand. They stalled just months after they were commissioned,(???)plunging the country into darkness and limited production hours.

The public is also concerned over dumping of the junk presidential jet for which the Exchequer paid $44 million - more than twice the actual cost of a new aircraft.(?????)The jet is not in use, barely six years since it was bought.

There is also the matter of the Bank of Tanzania (BOT) that is set to cost the taxpayer $340 million; which experts saying the figure is 10 times above the actual cost. The president is accused of being aware of the scams but failing to act as his henchmen have huge stakes in them.

This is a new experience for Dar es Salaam, which is beginning to feel the heat after donors demanded transparency in public expenditure.

The demand was prompted by the compilation and circulation of a 'List of shame'by the Opposition, which indicts Lowasa, Kikwete's son and wife (????), businessman and MP Rostam Aziz - who bankrolled Kikwete's election in 2005).

But the Director of Communications Salva Rweyemamu dismissed the 'List of shame' as 'A List of Lies'. Rweyemamu, a journalist, who used his position as a managing editor at Habari Corporation to Campaign for Kikwete, admitted on Tuesday that BOT was indeed under investigation.

Civil disobidience is an alien concept in Dar and would never have been contemplated as a means of protesting at State culpability. Political unrest is also rare, save for occassional flare-ups at election time.

But this time round, senior Cabinet members are under scrutiny as an increasingly restless public question the Kikwete administration's inability to fight poverty and corruption.

As a sign of the gathering storm, Cabinet ministers going round the country to 'explain' the budget to the electorate were heckled as wananchi complained of rising cost of food, fuel and unemployment.

The level of public discontet is unpresidented and the opposion has rolled out civil education to sensitise the public.

Source: Sunday Standard (Kenya) of October 14, 2007.
Repoter: Ernest Mpinganjira
 
KUTOKA MAKTABA YA JAMBOFORUMS:MICHANGO YA BAADHI YA WANACHAMA KUHUSIANA NA HIYO HABARI:

Pressure on Kikwete to act on graft: Ernest Mpinganjira, Sunday Standard (Kenya) of October 14, 2007.

Mtanganyika: 15th October 2007, 07:23 AM
The author has point, however me and you we don't have enough facts to prove some of his points. I can't declare all of his points are false, but i can't accept some of them because i don't have enough evidence to accept them.

All in all, i like his article.

--------------------------------------------------------------------------------

Mzee Mwanakijiji: 15th October 2007, 07:36 AM
Ernest si Mtanzania huyo ama?

--------------------------------------------------------------------------------

FDR Jr: 15th October 2007, 10:45 AM
Atajibiwa humuhumu JF na hata kwenye makaratasi cha muhimu tusubiri ni majibu gani hususani hli la Bukoba huko

--------------------------------------------------------------------------------

Mtanzania: 15th October 2007, 10:53 AM
Huyu mwandishi anatumia ukweli kidogo kufanya madai ambayo
hana data za kuyathibitisha.

Article kama hii angeandika huku kwao wangemaliza mara moja.

Kwasababu anajua hatuna watu wa kukabiliana naye kwa hoja basi anaandika uchafu wowote aliowahi kuusikia karibuni bila kufanya uchunguzi wa kina.

--------------------------------------------------------------------------------

Halisi: 16th October 2007, 01:35 AM
Pamoja na kukosa baadhi ya facts ama kuwa nazo ambazo hazijafanyiwa kazi, lakini mwandishi anatupa picha moja mbaya sana kwamba kuna PENGO KUBWA KATIKA MEDIA ZA TANZANIA.
1. Media za Tanzania haziwezi moja kwa moja kumuandika Lowasa na Rostam Aziz, jambo ambalo mwandishi hapa kawaandika. Thisday wamejaribu naona wanabanwa sasa na mumeona Nguba katoa statement.
2. Media ya Tanzania imekua na woga na upenzi ambao hausaidii Taifa.
3. Media ya Tanzania haina umoja kwa mambo yanayogusa maslahi ya Taifa, habari ikiandikwa na gazeti moja mengine hayafuatilii kama ilivyo Kenya na Uganda.

--------------------------------------------------------------------------------

Dua: 16th October 2007, 01:45 AM
Brown envelopes zinafanya kazi.

--------------------------------------------------------------------------------

Kalamu: 16th October 2007, 04:16 PM

Halisi:
Sote tunaelewa udhaifu wa vyombo vya habari hapa nchini kwetu. Hivyo vinavyomilikiwa na serikali, wao hawana lolote na pengine hatuwezi kuwalaumu kwa kuogopa kuukata mkono wa asali. Vile vinavyomilikiwa na wafanya biashara, mambo ni yale yale, wako katika biashara. Lengo sio kupasha habari kama zinavyotokea.

Lakini....., bado siamini kabisa kwamba 'ethnic cleansing' huko Kagera itokee na pasiwe hata na chombo kimoja tu cha kutoa habari hiyo, eti kwa kuogopa kulipaka tope taifa. Huo ni uzushi wa huyo mwandishi wa habari wa Sunday Standard; na sitaamini mpaka niambiwe kuwa ni kweli hayo yapo, na yanaendelea kutokea na vyanzo vinavyoaminika.
Mbona hapa JF kuna watu toka sehemu mbalimbali nchini; nao kweli wanaogopa kutoa habari kama hizo? Sababu ikiwa ni nini!
 
KUTOKA MAKTABA YA JAMBOFORUMS:MICHANGO YA BAADHI YA WANACHAMA KUHUSIANA NA HIYO HABARI:

Pressure on Kikwete to act on graft: Ernest Mpinganjira, Sunday Standard (Kenya) of October 14, 2007.

-----------------------------------------------------------------

Mtanzania: 15th October 2007, 10:53 AM
Huyu mwandishi anatumia ukweli kidogo kufanya madai ambayo
hana data za kuyathibitisha.

Article kama hii angeandika huku kwao wangemaliza mara moja.

Kwasababu anajua hatuna watu wa kukabiliana naye kwa hoja basi anaandika uchafu wowote aliowahi kuusikia karibuni bila kufanya uchunguzi wa kina.

-----------------------------------------------------------------

Halisi: 16th October 2007, 01:35 AM
Pamoja na kukosa baadhi ya facts ama kuwa nazo ambazo hazijafanyiwa kazi, lakini mwandishi anatupa picha moja mbaya sana kwamba kuna PENGO KUBWA KATIKA MEDIA ZA TANZANIA.
1. Media za Tanzania haziwezi moja kwa moja kumuandika Lowasa na Rostam Aziz, jambo ambalo mwandishi hapa kawaandika. Thisday wamejaribu naona wanabanwa sasa na mumeona Nguba katoa statement.
2. Media ya Tanzania imekua na woga na upenzi ambao hausaidii Taifa.
3. Media ya Tanzania haina umoja kwa mambo yanayogusa maslahi ya Taifa, habari ikiandikwa na gazeti moja mengine hayafuatilii kama ilivyo Kenya na Uganda.

--------------------------------------------------------------------------------

Dua: 16th October 2007, 01:45 AM
Brown envelopes zinafanya kazi.

Sasa imebainika kuwa ni kweli Lowasa alihusika katika deal ya Richmond

Ukisoma article ya Saed Kubenea,Salva Rweyemamu mkurugenzi wa habari ikulu,anakili kuwa alipewa kazi ya kuhakikisha nini kinaandikwa na media za Tanzania na nini hakiandikwi

Maswali kwa wana JF: Je kama yote haya ndani ya habari hii ni kweli,kwa nini mimi nisiamini kuwa Rizwani Kikwete alihusishwa na Lowasa kwenye deal kama mwandishi alivyosema? ni kwa nini nisiamini kuwa ni kweli kuna mauaji yalitokea huko Kagera na habari zikazimwa?
Kwa nini Lowasa,Aziz na Yona wameonyesha viburi hata kwa Bunge?
 
Idiots ni kipaji na bahati nzuri na wewe una qualify hivyo na wewe unacho... hongera sana..

...This is to say JF inaruhusiwa kutukana bila onyo wala nin.
Ngoja niende kutafuta kamusi yangu na mie nitafungulia bomba very sooon ila kama hairuhusiwi kutukana basi mnaofanya hivyo acheni mara moja.

Toa hoja na tetea hoja bila kutoana macho

Ninaunga mkono kukaangwa kwa Rostam na anatakiwa awe roasted kweli kweli ili iwe fundisho kwa wenye tamaa mbele
 
Mkuu Msanii,

Usipoteze muda wako mkuu, humu JF tunabeba kila aina ya watu ndio demokrasia at work, si unajua bin-adam huwa tunajisema who we are kwa maneno yetu, sasa hayo maneno si clear jamaa ni mtu wa aina gani!
 
Response yangu in blue font:
huenda ukawa unazungumza sana kishabiki, kuliko kuzungumza kiuhalisia.

CCM ni chama cha mapinduzi ni chama ambacho kinabadilika kutokana na hali na wakati na sio conservative.

Kunabadilika hasi na Chanya, kwa hili nakubaliana na wewe kuwa CCM inabadilika lakini in a negative way.

suala hili lililetwa bungeni na mbunge wa CCM Shekilengo na unajua ila mkuu akawa anatumia kutisha na mengine lkn chini kwa chini viongozi wakawa wanalizungumza.

Kwanini iwe chini kwa chini? Kama siyo Ufisadi mwingine. Wapinzani walilizungumza kwa uwazi na wanachi walio wengi hata sisi tulioko Sitalike, Mpanda tukalifahamu. Hivyo kwa kulizungumzia chini chini ilikuwa ishara nyingine ya kuficha ufisadi kwa gharama za wananchi.

na nnaamini kama si baraka za CCM hakuna lolote lingekuwa ila walifika pahala wakasema sawa ukweli uwe ukweli na tulifatilieni na aliehusika achukuliwe hatua.

Hii ni pressure kutoka kwa wanachi na siyo baraka za CCM kama unavyotaka kutafanya tuamini. Insingekuwa zomea zomea mikoni JK asingefanya lolote.

sikatai mchango wa upinzani upo tena mkubwa, lakini sio kujilabu na kutaka kuonesha kuwa wabunge wa CCM wamelala na wao ndio pekeee wenye uchungu wa nchi hii na wao pekee ndio waliofichua mambo hayo.

Wabunge wa CCM hawajalaa isipokuwa walikuwa macho kutetea Ufisadi, kwani huoni Zitto alivyotimuliwa bungeni katika scam ya Buzwagi?

ukweli utabakia wazi ndani ya CCM wako wengi kuliko upinzani wenye uchungu na nchi yao na wanaumia kuona wenzao wachache wanaharibu kwa maslahi ya nafsi zao.

Hakuna ukweli wowote, nchi imeingia mikataba mingapi ya kifisadi? Siku zote hizo wabunge wa CCM wenye uchungu si wangeachia ngazi?

CCm ni chama pekeee tanzania chenye utaratibu mzuri na sheria zilizonyooka, sio kama wapinzani wengi wanaganga njaa.

It is just a matter of time kabla hujaona CCM inasambaratika. CCM ilikomaa wakati wa CHama kimoja kwa sababu ya sintofahamu ya Wadanganyika na vilevile mawasiliano yalikuwa hafifu, yaani ili kupata habari za kitaifa mpaka mtu asome mzalendo, uhuru au asikilize Radio Tudanganyane Daima.Sasa hivi kuna namna nyingi ya kupata habari kitu ambacho ni mwiba kwa Sisiemu.

kweli una uchungu wa nchi baada ya kuhimiza wananchi kaitka maendeleo ww unawashawishi ktk mambo ambayo hayaleti faida yeyote ya nchi?

hivi upinzani hawawezi kuleta maendeleo hadi wawe na serikali?

Kuleta maendeleo kuna maana nyingi sana. lakini jukumu kubwa linabakia kuwa la Sirikali kwa sababu wao ni wanakusanya Kodi na kuratibu misaada na mikopo kutoka kwa Donors. Wapinzani wanapokemea ufisadi na kuokoa mamilioni ya shillingi huo ni mchango mkubwa wa maendeleo. Kama EL et al watafikishwa Kizimbani, Tanesco ikaokolewa na mzigo wa kulipa milioni 152 kwa siku gharama ya Umeme itapungua and as a result watu wanaojiri kwa kutegemea umeme wataongezeka. Lakini sifahamu wewe una-define vipi mchango wa kuleta maendeleo ya nchi.
hivi hamuwezi kuwahimiza alau kwa kuanzia wanachama wenu kusoma kwa bidii kujitolea wilaya zao kuboresha maendeleo yote yakiwemo ya elimu?

na kiteto mkishindwa mtasema watanzania hawana mwamko.

Sishangai kwa CCM kushinda Kiteto kwa sababu wanaweza kutumia Emilio Kibaki's style,kwa sababu TUME ni yao na wasimamizi ni wao.

kama kuna haja ya mabadiliko kuiondoa CCM basi mtanzania mbado hajajua ni chama kipi ambacho kinafaa kuiongoza Tanzania.

maana vyote ni vyama ambavyo havijawiva.

Heri kuongozwa na Chama chochote kile kuliko CCM iliyojaa ufisadi na wamewiva katika kubaka uchumi wa Taifa.

nnamalizia ktk vyama vya upinzani wako watu wachache makini na nnawakubali na kuwaheshimu lkn wengi wao wanafata mkumbo tu

Tanganyika ilipata Uhuru baada ya mtu makini mmoja JK Nyerere(R.I.P) kuuunganisha nguvu za Watanzania. Hivyo mapambano ya kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini yanahitaji Viongozi wachache makini wenye uwezo wa ku-articulate issues, Kudhibiti ufisadi, kuhakikisha maliasili inatumika kuinua maisha ya mtz na kuwaunganisha Watanzania katika kujilete maisha bora.
 
Kikwete aanza kujuta

na Charles Mullinda

MTIRIRIKO wa matukio na kauli za Rais Jakaya Kikwete katika kipindi cha wiki moja iliyopita, vinaonyesha kuwa ameanza kujutia hatua ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu wadhifa wake.
Tofauti na mtizamo wa awali uliokuwa ukionyesha kuwa Kikwete aliridhia kujiuzulu kwa Lowassa baada ya kutajwa kuwa mhusika mkuu katika kashfa ya Richmond, sasa imedhihirika kuwa alilazimika kukubaliana na uamuzi huo kwa vile hakuwa na njia nyingine ya kumnusuru.

Kikwete, ambaye alikuwa Dodoma kwa takriban wiki moja akikabiliana na misukosuko iliyokuwa ikiiandama serikali yake, alikuwa kimya kwa kipindi kirefu na hata kukataa kuonana na baadhi ya maswahiba wake baada ya Lowassa kujiuzulu na yeye kulazimika kulivunja baraza la mawaziri.

Hatua hiyo ya kukataa kuonana na baadhi ya watu wake wa karibu inaelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa, ilitokana na mshtuko alioupata baada ya Lowassa, ambaye ni swahiba wake mkubwa katika maisha ya kawaida na hata ya kikazi, kuachia ngazi.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wameeleza kuwa Kikwete sasa anakabiliwa na mtihani mgumu wa kurejesha umoja na mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni mwenyekiti wake, kufuatia kuibuka kwa mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho, uliosababishwa na kujiuzulu kwa Lowassa.

Tanzania Daima Jumapili ilidokezwa hivi karibuni na watu wa kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kuwa kishindo cha kujiuzulu kwa Lowassa kimewagawa vigogo na makada maarufu wa CCM, jambo linalotishia uhai na uimara wake.

Mgawanyiko huo unamgusa pia Rais Kikwete, ambaye hotuba zake mbili alizozitoa baada ya kuapisha baraza lake jipya la mawaziri zinaonyesha kuwa hakubaliani moja kwa moja na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura, ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya Marekani, iliyomtia matatani Lowassa.

Hili linapewa uzito na hatua ya Rais Kikwete kutowateua katika baraza lake jipya la mawaziri wajumbe wa Kamati ya Mwakyembe pamoja na wabunge wote wa CCM waliomshambulia Lowassa na wenzake waliotajwa ndani ya ripoti ya kamati hiyo.

Wadadisi wameeleza kuwa hatua hiyo inaonyesha jinsi ambavyo rais hakufurahishwa na namna kamati hiyo ilivyofanya kazi yake.

Sambamba na hayo, hatua ya Rais Kikwete kukiri kuwa kujiuzulu kwa Lowassa kulikuja wakati usiotarajiwa na kumwelezea kama ni kiongozi aliyelitumikia taifa hili kwa ujasiri na uzalendo mkubwa katika kipindi chote cha uongozi wake, licha ya kulazimika kuachia ngazi kwa tuhuma, kunaonyesha jinsi alivyosononeshwa na ulazima wa rafiki yake huyo kujiuzulu.

Wakati wabunge wengi waliojadili ripoti hiyo wakionyesha hasira dhidi ya Lowassa na wengine wakieleza kuwa anapaswa kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutolipwa marupurupu ya uwaziri mkuu mstaafu, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa kupitia kwa wazee wa Dar es Salaam, alieleza kuwa anaamini Lowassa ameacha alama ya kudumu katika uongozi wake na kwamba yaliyotokea hadi kulazimika kujiuzulu ni ajali katika maisha ya kisiasa.

Kauli nyingine zinazoonyesha jinsi Rais Kikwete alivyosononeka, ni kukiri kuwa Lowassa, mtu aliyeongoza harakati za kuhakikisha kuwa Kikwete anakuwa rais wa nne wa Tanzania mwaka 2005 alikuwa na uhusiano naye kikazi na kimaisha kwa muda mrefu na kwamba kama mambo fulani fulani yangefanyika, basi yaliyotokea yasingefikia kuwa yalivyo.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa Lowassa, hali pia si shwari kwa swahiba wake mwingine, Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga, ambaye mbali na kutajwa katika kashfa ya Richmond pamoja na ile ya kuchotwa kwa mabilioni ya fedha kutoka Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) sasa anakabiliwa na kitimoto bungeni anakotakiwa kwenda kuthibitisha au kufuta kauli yake kuwa kamati iliendelea na kazi hata baada ya muda wake wa Desemba 30 kwisha.

Lakini kikubwa kinachoonekana kutishia sifa na heshima aliyonayo Rostam katika jamii ni madai ya kuhusishwa kwake katika kashfa ya EPA ambapo inadaiwa kuwa moja ya kampuni zilizochotewa fedha hizo ni Kagoda anayodaiwa kuimiliki.

Pamoja na kupenda kukaa mbali na vyombo vya habari, Rostam, mwanasiasa mwenye mvuto na ushawishi na pia anayeheshimika ndani ya CCM sasa alazimika kujitokeza mbele ya vyombo vya habari kuzungumzia tuhuma zinazoelekezwa kwake ili kuondoa picha mbaya inayoanza kujengaka dhidi yake.

Iwapo kamati iliyoundwa na Rais Kikwete kuchunguza kampuni zilizotajwa kuhusika katika kashfa hiyo itamtaja kuhusika na Kagoda, mbali na kuchafua sifa yake, atachafua pia sifa ya Rais Kikwete, ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja wa wanamtandao walioshiriki kwa karibu kufadhili kampeni za CCM za mwaka 2005.

Kama ilivyokuwa kwa Lowassa, Rostam naye amekuwa akitajwa tajwa sana kuhusika katika kashfa hiyo kutokana na ukwasi wa kutisha alionao, unaodaiwa kutoendana na maelezo ya historia ya alikotokea kibiashara tangu wakati akiwa mfanyabiashara wa ngozi.

Wakati huo huo, fukuto la kashfa ya Richmond bado linaonekana kuwa bichi kutokana na kutofahamika, hasa kwa wamiliki wa kampuni hiyo na nguvu ilizonazo katika kunasa tenda kubwa kubwa za serikali licha ya sifa yake ya kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi inazoomba.

Kushindwa kwa kamati teule ya Bunge iliyochunguza upatikanaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kampuni hiyo kubaini wamiliki wake, kumezidisha kuwapo wingu la mashaka dhidi ya baadhi ya vigogo kuhusika nayo.

Aidha, baadhi ya wachambuzi na wadadisi wameonyesha mashaka ya wazi kuhusu usiri unaoizunguka Richmond, wakirejea hatua ya Rais Kikwete kulazimika kuchomoa sehemu ya hotuba yake aliyoitoa kwa taifa Desemba mwaka 2006 iliyokuwa ikizungumzia masuala ya Richmond.
 
Tunasubiri kikao kijacho cha bunge atakapokuja kujitetea tutajua ukweli huko wapi
 
Kikwete aanza kujuta

na Charles Mullinda

MTIRIRIKO wa matukio na kauli za Rais Jakaya Kikwete katika kipindi cha wiki moja iliyopita, vinaonyesha kuwa ameanza kujutia hatua ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu wadhifa wake.
Tofauti na mtizamo wa awali uliokuwa ukionyesha kuwa Kikwete aliridhia kujiuzulu kwa Lowassa baada ya kutajwa kuwa mhusika mkuu katika kashfa ya Richmond, sasa imedhihirika kuwa alilazimika kukubaliana na uamuzi huo kwa vile hakuwa na njia nyingine ya kumnusuru.

Kikwete, ambaye alikuwa Dodoma kwa takriban wiki moja akikabiliana na misukosuko iliyokuwa ikiiandama serikali yake, alikuwa kimya kwa kipindi kirefu na hata kukataa kuonana na baadhi ya maswahiba wake baada ya Lowassa kujiuzulu na yeye kulazimika kulivunja baraza la mawaziri.

Hatua hiyo ya kukataa kuonana na baadhi ya watu wake wa karibu inaelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa, ilitokana na mshtuko alioupata baada ya Lowassa, ambaye ni swahiba wake mkubwa katika maisha ya kawaida na hata ya kikazi, kuachia ngazi.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wameeleza kuwa Kikwete sasa anakabiliwa na mtihani mgumu wa kurejesha umoja na mshikamano ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho yeye ni mwenyekiti wake, kufuatia kuibuka kwa mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho, uliosababishwa na kujiuzulu kwa Lowassa.

Tanzania Daima Jumapili ilidokezwa hivi karibuni na watu wa kuaminika kutoka ndani ya chama hicho kuwa kishindo cha kujiuzulu kwa Lowassa kimewagawa vigogo na makada maarufu wa CCM, jambo linalotishia uhai na uimara wake.

Mgawanyiko huo unamgusa pia Rais Kikwete, ambaye hotuba zake mbili alizozitoa baada ya kuapisha baraza lake jipya la mawaziri zinaonyesha kuwa hakubaliani moja kwa moja na ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa zabuni ya uzalishaji umeme wa dharura, ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development ya Marekani, iliyomtia matatani Lowassa.

Hili linapewa uzito na hatua ya Rais Kikwete kutowateua katika baraza lake jipya la mawaziri wajumbe wa Kamati ya Mwakyembe pamoja na wabunge wote wa CCM waliomshambulia Lowassa na wenzake waliotajwa ndani ya ripoti ya kamati hiyo.

Wadadisi wameeleza kuwa hatua hiyo inaonyesha jinsi ambavyo rais hakufurahishwa na namna kamati hiyo ilivyofanya kazi yake.

Sambamba na hayo, hatua ya Rais Kikwete kukiri kuwa kujiuzulu kwa Lowassa kulikuja wakati usiotarajiwa na kumwelezea kama ni kiongozi aliyelitumikia taifa hili kwa ujasiri na uzalendo mkubwa katika kipindi chote cha uongozi wake, licha ya kulazimika kuachia ngazi kwa tuhuma, kunaonyesha jinsi alivyosononeshwa na ulazima wa rafiki yake huyo kujiuzulu.

Wakati wabunge wengi waliojadili ripoti hiyo wakionyesha hasira dhidi ya Lowassa na wengine wakieleza kuwa anapaswa kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutolipwa marupurupu ya uwaziri mkuu mstaafu, Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa kupitia kwa wazee wa Dar es Salaam, alieleza kuwa anaamini Lowassa ameacha alama ya kudumu katika uongozi wake na kwamba yaliyotokea hadi kulazimika kujiuzulu ni ajali katika maisha ya kisiasa.

Kauli nyingine zinazoonyesha jinsi Rais Kikwete alivyosononeka, ni kukiri kuwa Lowassa, mtu aliyeongoza harakati za kuhakikisha kuwa Kikwete anakuwa rais wa nne wa Tanzania mwaka 2005 alikuwa na uhusiano naye kikazi na kimaisha kwa muda mrefu na kwamba kama mambo fulani fulani yangefanyika, basi yaliyotokea yasingefikia kuwa yalivyo.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa upande wa Lowassa, hali pia si shwari kwa swahiba wake mwingine, Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga, ambaye mbali na kutajwa katika kashfa ya Richmond pamoja na ile ya kuchotwa kwa mabilioni ya fedha kutoka Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) sasa anakabiliwa na kitimoto bungeni anakotakiwa kwenda kuthibitisha au kufuta kauli yake kuwa kamati iliendelea na kazi hata baada ya muda wake wa Desemba 30 kwisha.

Lakini kikubwa kinachoonekana kutishia sifa na heshima aliyonayo Rostam katika jamii ni madai ya kuhusishwa kwake katika kashfa ya EPA ambapo inadaiwa kuwa moja ya kampuni zilizochotewa fedha hizo ni Kagoda anayodaiwa kuimiliki.

Pamoja na kupenda kukaa mbali na vyombo vya habari, Rostam, mwanasiasa mwenye mvuto na ushawishi na pia anayeheshimika ndani ya CCM sasa alazimika kujitokeza mbele ya vyombo vya habari kuzungumzia tuhuma zinazoelekezwa kwake ili kuondoa picha mbaya inayoanza kujengaka dhidi yake.Iwapo kamati iliyoundwa na Rais Kikwete kuchunguza kampuni zilizotajwa kuhusika katika kashfa hiyo itamtaja kuhusika na Kagoda, mbali na kuchafua sifa yake, atachafua pia sifa ya Rais Kikwete, ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja wa wanamtandao walioshiriki kwa karibu kufadhili kampeni za CCM za mwaka 2005.

Kama ilivyokuwa kwa Lowassa, Rostam naye amekuwa akitajwa tajwa sana kuhusika katika kashfa hiyo kutokana na ukwasi wa kutisha alionao, unaodaiwa kutoendana na maelezo ya historia ya alikotokea kibiashara tangu wakati akiwa mfanyabiashara wa ngozi.

Wakati huo huo, fukuto la kashfa ya Richmond bado linaonekana kuwa bichi kutokana na kutofahamika, hasa kwa wamiliki wa kampuni hiyo na nguvu ilizonazo katika kunasa tenda kubwa kubwa za serikali licha ya sifa yake ya kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi inazoomba.

Kushindwa kwa kamati teule ya Bunge iliyochunguza upatikanaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kampuni hiyo kubaini wamiliki wake, kumezidisha kuwapo wingu la mashaka dhidi ya baadhi ya vigogo kuhusika nayo.

Aidha, baadhi ya wachambuzi na wadadisi wameonyesha mashaka ya wazi kuhusu usiri unaoizunguka Richmond, wakirejea hatua ya Rais Kikwete kulazimika kuchomoa sehemu ya hotuba yake aliyoitoa kwa taifa Desemba mwaka 2006 iliyokuwa ikizungumzia masuala ya Richmond.

Huyu mwandishi atariharibu gazeti la TANZANIA DAIMA kila anapoandika makala inaymhusu rostam mara zote anatoa sifa za kijinga! rostam ana mvuto gani na kwa nani??? labda kwake mwandishi!
rostam ana ushawishi gani ccm!! kuwa na fedha za wizi kuwahonga watu kireja reja siyo ushawishi! ni lini mwandishi amewahi kusikia rostam akizungumza bungeni?

rostam hastahili sifa hizo anazojaribu kumpa mwandishi! huyu ni mwizi, tapeli na laghai, hana sifa hata moja ya kuwa kiongozi wa nchi hii, achilia mbali ubunge hata uenyekiti wa mtaa hawezi!!

Mwalimu Nyerere alisema kama wewe unampenda mtu kwa mvuto mkaribishe chai nyumbani kwako, lakini usijaribu kushawishi wengine wafikiri kama wewe!

nahisi huyu mullinda ni kati ya waandishi walionunuliwa na rostam, don;t be cheap kijana, njaa yako itakuja kukupeleka pabaya!!

Sioni haja ya kusubiri hadi kikao kijacho eti rostam ajitetee, yafunguliwe mashtaka dhidi yake ya uhujumu uchumi, wala huko bungeni asiende tena!!
 
Na "nikiahidi kutofanya tena reaction ya JF, Slaa na wengine itakuwaje?!" Kikwete akipata ushauri wako utamvutia sana lakini atakuwa na mawswali kama hayo hapo juu. Atatamani mkutane ili umpe details zaidi na ikiwezekana umfanyie forecasts yatakoyojiri baada ya hapo.

tik tak tik tak.............

Green29,

Mimi naamini kuwa Kikwete akiamua kukata mzizi wa fitina hapa na akaamua kubadili moyo na kufutilia mbali ufisadi katika serikali yake ataweza na wananchi watamuunga mkono kwa hilo bila kujali itikadi na sera zao za vyama.

Yakifanyika mambo nusunusu hivi inakuwa inaonyesha kuwa JK hayuko serious na hii issue nzima. Alipata nafasi nzuri sana hapa ya kubadili mambo na kila kitu alikuwa ametengewa kama zile pass za Jayson Kidd na yeye ilikuwa ni ku-dunk tu!
 
Huyu mwandishi something is wrong na maandishi yake, kwa sababu anasahau kuwa Kiwete, alitoa hotuba nzito Zanzibar kabla ya kwenda Dodoma, akikaripia sana viongozi wasiofuata maadili ya uongozi, ambao alisema wamelihujumu sana taifa letu,

exactly, Kiwete alikuwa anamuongelea nani? Kama Lowassa ni bora na Kikwete alikuwa anampenda sana kama muandishi anavyotaka tuamani then why alimnyima umakamu wa ccm? Ilikuwaje Rostam akatolewa kwenye uweka hazina kama Kikwete anawapenda sana hawa?

Ukweli ni kwamba Lowassa na Rostam ni marafiki wa karibu sana wa Kikwete, sio siri, lakini pressure za wananchi ndio zimemfanya Kikwete kuwafanyia ambayo hakutaka kabisaa, na wao hawamkusaidia au kujisaidia wenyewe kutokana na mambo waliyoyafanya ya uwizi, muandishi ninaaamini kuwa anajaribu kuwafagilia hao watu lowassa na rostam, nilisema siku nyingi kuwa hawa wawili wana mtu huko Tanzania Daima, maana mara nyingi huyu mkuu huchukua mpango toka kwa hawa wakuu na kuua articles za kuwatwanga.

Kikwete, kama ana huzuni sana basi na yeye aoondoke awafuate wenziwe, kikwete, hawezi kushindana na bunge, na hasa sasa baada ya Kingunge, na lowassa kuondoka, it is over, six na lowassa ilikuwa paka na panya, kwa sababu lowassa alikuwa akimtisha sana six, sasa ni six ndiye mwenye ubavu ndani ya bunge, kwa hiyo kama kikwete akiendelea na kucheza na taifa letu itakuwa ni bad news kwake toka bungeni kila siku, maana hana mtu tena mle Makamba hawezi tisha mtu, baraza alilochagua sasa ukweli ni temporary tu, mimi ninaamini kuwa bado kuna viongozi ambao kikwete angependa kuwatema anasubiri wakanyagwe na bunge tena,

Rostam should understand kuwa mwisho wake kisiasa, unakaribia sana, so far anashikilia uzi wa sindano tu, serikali imepewa miezi mitatu kujibu mapendekezo ya kamati ya Mwakyembe, na pm ameahidi kiyajibu, wakati tunasubiri hayo hatuhitaji kudanganywa na hawa waandishi uchwara!
 
Mkuu FMES
Nimekusoma na nikikandamizia zaidi waelewe kuwa enzi za uhuru na mzalendo zishapita loong time. oni kisha he chombHmtumbwi uivi sasa matundu kibao yanaingiza maji. lazima wazame safari hii

ingawa bado nina mashaka sana na bunge maana ccm wameanza kwa mbwembwe ila naamini kuwa wanatafutiwa timing halafu watapigwa jeuri ya chama kisha utaona watakavyonywea.

Kuna mtu anaweza kunikumbusha kuwa ni lini RA aliwahi kuuliza swali bungeni? ni swali gani na kikao gani?

MWAKA WA MUNGU HUU
 
Back
Top Bottom