Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Hakuna abwabwajae ila wewe, hakuna ateteae ufisadi hata kidogo, bali kwenye ukweli ni ukweli tu. JK anafanya kazi zake vyema kabisa na zinaonekana mpaka IMF na kwa Bush na mafisadi wanashughulikiwa kisheria na si kwa kukurupuka na waambie wakae mkao wa kula JK anakuja systematically. JK unanikuna mpaka ndani ya loho.

Wakati viongozi wengi duniani wanakwepa hata kuhusisha majina yao na kichaka na IMF wewe ndio unayaleta hapa! naona inabidi mafisadi watafute mtetezi mwingine mwenye kisomo kidogo!
 
Usiwe na shaka na hilo hata hao wanaokwepa kujihusisha na Kichaka na IMF wamemkubali JK, si unaona chuo kikuu kipya kule Dom. Si unajuwa nani anakifanya kiwe? basi ujuwe anakubalika pande zote. Unalo?

Na sijui kama ulibahatika kumuona balozi wa Iran jana kwenye TV? kama hujabahatika basi pole sana, nao pia wanamkubali JK. Unalo?
 
Usiwe na shaka na hilo hata hao wanaokwepa kujihusisha na Kichaka na IMF wamemkubali JK, si unaona chuo kikuu kipya kule Dom. Si unajuwa nani anakifanya kiwe? basi ujuwe anakubalika pande zote. Unalo?

Nadhani unahitaji kukumbushwa kuwa hata Karl Peters alitoa nguo na vipesa kidogo kwa machifu wakati wa kusaini mikataba ya kuleta ukoloni Tanzania!
 
Wakati viongozi wengi duniani wanakwepa hata kuhusisha majina yao na kichaka na IMF wewe ndio unayaleta hapa! naona inabidi mafisadi watafute mtetezi mwingine mwenye kisomo kidogo!

Thanks African lady,

Huyu jamaa nafikiri something is wrong upstairs! Hata kama ni mtetezi wa mafisadi, hajui kucheza game kabisa!! will ignore him/her completely from now.
 
Pole Mw Kike naona imekuchukua muda kujua mshikaji yupo kwenye payroll ya kusafisha mafisadi ...Dar Es Salaam nadhani anakesha hapa JF kujibu tuhuma...sehemu ya Job description yake pole pole hapa hafagiliwi boss wako!!

Ulijuwaje kama hatukeshi pamoja humu? hakuna cha boss wangu kufagiliwa, ukweli unaonekana na unajifagilia wenyewe mpaka mtakubali wenyewe, katizame thread ya kibaki ulole huyo mwanamke anavyo mfagilia JK.
 
Thanks African lady,

Huyu jamaa nafikiri something is wrong upstairs! Hata kama ni mtetezi wa mafisadi, hajui kucheza game kabisa!! will ignore him/her completely from now.

Ukweli unauma! hayooo yanaona haya. Waswahili wanasema "akunyimae kunde akupunguzia mashuzi" hiyo ndio itanipa wasaa wa kupambana na wengine humu wanaompinga JK kwa chuki binafsi na agenda za siri.
 
Good thinking,

mimi huyu ninaye tu mpaka kieleweke. Kazi yangu hapa ni pamoja na kupambana na mafisadi na watetezi wao kama huyu ambao nia yao ni kuharibu threads ili watu wachoke kuchangia!

The game has just started!
 
Ulijuwaje kama hatukeshi pamoja humu? hakuna cha boss wangu kufagiliwa, ukweli unaonekana na unajifagilia wenyewe mpaka mtakubali wenyewe, katizame thread ya kibaki ulole huyo mwanamke anavyo mfagilia JK.

Uwe unakesha au unafanya nini na fisadi mwenzako Rostam Azizi haya ni historia. For now ufisadi hapa haupiti hata kwa dawa!
 
Nadhani unahitaji kukumbushwa kuwa hata Karl Peters alitoa nguo na vipesa kidogo kwa machifu wakati wa kusaini mikataba ya kuleta ukoloni Tanzania!

Out of point, si tusiwaite basi. Au na wewe ndio uko huko unagawa pipi kidogo ili uwa koloni?
 
Ukweli unauma! hayooo yanaona haya. Waswahili wanasema "akunyimae kunde akupunguzia mashuzi" hiyo ndio itanipa wasaa wa kupambana na wengine humu wanaompinga JK kwa chuki binafsi na agenda za siri.

Utapambana na nani wakati uko very paranoid na accusations za kitoto kuwa mwafrika wa kike ni mwanakijiji? hoja ndio husimama hapa JF na sio umbea!
 
Mahakamni hawataki kwenda? si uwashitaki tu, ushahidi wote wa kuwafikisha mahakamani si unao? unangoja nini? mie nashangaa. Au ndio hakuna cha kusema tena.

Wacheni tume zilizoundwa zifanye kazi, na kila mmoja alietenda dhambi atahukumiwa kisheria na ambae hana dhambi ameingizwa kimazingira nae atajulikana. Au unaona waliounda zile tume na wale waliopo kwenye hizo tume ni wajinga? Ya nini kuandikia mate na wino upo?
Dar-es-salaam,nakubaliana na wewe kwa theory yako ya debe tupu, ni kweli "ninyi ccm mmetugeuza wananchi debe tupu,nasi hatuachi kutika" kwani hatuna silaha nyingine zaidi ya kutika.Majeshi ninyi ndio mnayo,mnatupiga,tukitika sana hapa jf mnatufungia wewe na wenzako,tukiandamana mnatupiga.Hivyo we have nothing to loose except our labour power,nasi hatutaacha kutika.Maana debe likitika sana hata mwenye nalo anaona ghasia itabidi tu alitulize na kututuliza ndio mnavunja baraza la mawaziri,mnakubali shingo upande na mnakiri hadharani kuwa tuliwalazisha kwa kuwa tulichonga sana
Naam mnatuuliza namba za viatu mwaka huu miaka mitano baadaye mnatwambia tulitaka viatu gani?Kilimo mnatuambia uti wa mgongo wa maisha yetu,lakini bajeti mnayotupa ni ya kununua matrekta matatu nchi nzima. Yote haya tusiache kutika?
Hat mkisema kwa kusupport kwamba Richmond haijui,sisi tunapoona ukweli hatutaacha kutika,kwani hata richmond mlituzima sana,na maji mkatumwagia mkasema there is nothing wrong there,hata bot vilevile lakini tulipotika sanaaaaaaaaaaaa mkasikia mkakiri,mkajifanya RAIS amekasirishwa sana....hahaha

Kweli mnatuchezea
 
Hakuna abwabwajae ila wewe, hakuna ateteae ufisadi hata kidogo, bali kwenye ukweli ni ukweli tu. JK anafanya kazi zake vyema kabisa na zinaonekana mpaka IMF na kwa Bush na mafisadi wanashughulikiwa kisheria na si kwa kukurupuka na waambie wakae mkao wa kula JK anakuja systematically. JK unanikuna mpaka ndani ya loho.

Wewe kaa kimya inaelekea hufahamu ministerial responsibility manaake nini wala administrative law au wala governonce. Hivi unaelewa watu wanaposema serikali ya dar-es-salaam imesema wana maana gani? au wanaposema tanzania imesema? laiti ungejua maana ya haya maneno wala usingeeendelea kubishana,watu hapa wanaposema kiwete haimaanishi kikwete kama individual yeye ndio kabeba dhamana ya serikali nzima.Huwezi kumtofautisha yeye na mabaya ya watendaji wake,watendaji wake wanapofanya vizuri tunasema kiwete kaboresha hili kaboresha lile,wanapofanya vibaya tunasema kikwete kashindwa hili kashindwa lile.
Kwa ufupi,hadi sasa kuna ahadi nyingi kuliko vitendo.Hivi miaka miwili sasa kwenye uchumi serikali imewekeza kitu gani kipya zaidi ya kuendeleza ya beny?kuna barabara gani mpya ambayo imejengwa kwa plan ya serikali iliyopo sasa?je,makusanyo ya TRA yameongezeka kiasi gani toka awamu ya nne iingie madarakani?kama sio wananchi kukamuliwa zaidi kujenga shule zenye mwalimu mmoja?Mtaifa makubwa yanatusifia kwa mipango,lakini ispotekelezeka hayohayo kesho yatatukejeli.Kwa mipango tu aah hiyo serikali inaweza sana,njoo kwenye kutekeleza.Muhimbili ndio hizo zinaua watoto,zina pasua watu ndivyo sivyo yote haya tusitike?
 
Out of point, si tusiwaite basi. Au na wewe ndio uko huko unagawa pipi kidogo ili uwa koloni?

Kinachonifurahisha sana kuhusu nyie watetezi wa mafisadi ni kwamba mafisadi hawakawii kuwageuka na kuwanyang'anya wake zenu halafu mnabaki mnalialia tu
 
Jamani mi naomba tuanzishe TROLL alert! Maana trolls wa mafisadi wako humu kwa wingi, just copy paste the bs they get from their bosses!
Huyo Rostam mi naomba akajinyamazie tu maana hii ya kusema eti hawajui Richmond itamlipukia sasa hivi! Kama wenzangu mmebahatika kusoma ile ripoti ya tume ya Richmond na viambatanisho kuna barua moja kutoka unnamed source from BRELA iliyoeleza wazi kuwa mchezo mchafu ulichezwa BRELA kufuta majina ya wakurugenzi original wa Richmond na jamaa aliyeifanya hiyo kazi BRELA sasa amepewa nyumba! Sasa taarifa kwa Rostam: if you have something against you, just keep quiet. Kwa hiyo Salva Rweyemamu ambaye ndiye mshikaji wake na RA alimpa kazi Ikulu 'amempakazia?' Maana kama ni hivyo Salva alisema uongo chini ya kiapo na ANALO! Also email ya Caspian kutumika na Dowans ni very weak excuse eti waliforge.
Huyu rafiki yetu kama anataka kujisafisha asimame bungeni ajitetee siyo kuongea uchochoroni na waandishi makanjanja! Naomba apeleke hoja zake kwa Spika ili akina Mwakyembe wajibu vyema hoja hizi, na Salva naye aitwe bungeni wakalumbane!
 
Kweli kabisa Susuviri! Kama kawaida hapa JF mafisadi na wawakilishi wao (ukianza na huyu Dar es salaam) ni kuwamulika tu ili hizo pesa wanazolipwa wazione chungu. Na uhakika kabisa huyu Salva anatamani kama angerudisha tarehe nyuma na kuanza upya ila ndio hivyo tena yuko late!
 
Mahakamni hawataki kwenda? si uwashitaki tu, ushahidi wote wa kuwafikisha mahakamani si unao? unangoja nini? mie nashangaa. Au ndio hakuna cha kusema tena.

Wacheni tume zilizoundwa zifanye kazi, na kila mmoja alietenda dhambi atahukumiwa kisheria na ambae hana dhambi ameingizwa kimazingira nae atajulikana. Au unaona waliounda zile tume na wale waliopo kwenye hizo tume ni wajinga? Ya nini kuandikia mate na wino upo?
Poor Dar-es-salaam
Mwananchi wa kawaida hawezi kuanzisha mashtaka ya jinai dhidi ya kiongozi wa serikali,anaweza tu kuanzisha mashtaka ya madai na ndio maana kesi za jinai huandikwa hivi R.v. John Smith ikimaanisha kuwa jamhuri au Regina kwa huko uingereza(queen) dhidi ya john smith.Ukishwaona kesi imeandikwa Dar-es-salaam v. Mahalu hizo ni dili zenu binafsini madai hayo.Ndio maana watu wanasema serikali iwashtaki,yenyewe ndiyo yenye jukumu chini ya katiba,na chini ya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai
 
Kweli kabisa RA hawezi kuifahamu Richimonduli kwa sababu hata hivi sasa ukimuuliza kama anamfahamu EL atakwambia hamfahamu. Ujanja ule ule wa wenzetu wakihindi unapokuwa madarakani mambo shwari.
 
Back
Top Bottom