Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Mimi naona tuendelee kuwa makondoo tu, kwani tutafanya nini?

Rostam ndio amemweka JK madaralani... Kwa hiyo serekali ameiweka mfukoni mwake.. Cha msingi watanzania tuendelee Kumwomba Mungu amwuue, Chenge, Rostam, Lowasa, Karamagi, Sitta, Mkapa.. kwani naona kila kukicha hutuachi kusikia haya majina kwenye vyombo vya habari mara Fisadi.... Wakishakufa walau tutapumua tutafuta historia za maisha yao mahali popote zilipoandikwa Tanzania.. Tutawasahau kabisa. Watakuwa ni majivu tuu
 
Na kwa kuzingatia ukaribu wa watatu hao (Kikwete, Lowassa na Rostam) kisiasa na kifamilia,

Mimi nilifikiri hao watatu wana uhusiano wa kisiasa tu, kumbe kuna na familia involved, how? Hapa nahisi kuna kitendawili hapo,

1. yaani Lowassa na muungwana wana uhusiano wa kifamilia? no way, mmoja Mmeru, mwingine Mkwere, hawaoleani kwa hiyo sio hawa.

2. muungwana na Rostam, uhusiano wa kifamilia sijawahi kusikia, au kuna more zaidi kwenye uhusiano wao mpaka kufikia kifamilia?
 
Mimi nilifikiri hao watatu wana uhusiano wa kisiasa tu, kumbe kuna na familia involved, how? Hapa nahisi kuna kitendawili hapo,

1. yaani Lowassa na muungwana wana uhusiano wa kifamilia? no way, mmoja Mmeru, mwingine Mkwere, hawaoleani kwa hiyo sio hawa.

2. muungwana na Rostam, uhusiano wa kifamilia sijawahi kusikia, au kuna more zaidi kwenye uhusiano wao mpaka kufikia kifamilia?

Mkuu Tanzania unajua siyo kenya.

Uhusiano wa kifamilia Tanzania unaweza kuunganisha makabila Tofauti. Na hii naona mimi ni hatari kwa maendeleo ya taifa ambapo unakuta familia ya karamagi na Rostamu ni marafiki sana.

Tuombe mungu yasitukute haya huuu ni utapeli.

Hii story inatukumbusha mbali CCM inatakiwa kujipanga upya kutoka midomoni mwa mamba.

Suala hili ni mtihani wa mkubwa kwa watanzania na CCM kwa ujumla hila cha maana wale walio wazuri ndani ya CCM hawana budi kuanzisha CCM B yao.
 
I am sure most of us we still have the question lingering in our mind as to how this man RA become so familar with dirty deals and how and when he managed to forge relationship with Tanzanian top most leader.

He RA with the help of another prominent member EL he became an adviser,trouble-shooter and financer during the election process,he engeneered 'dirty' smear campaign as well as illegal funds to help Jakaya clinch the CCM's nomination.

They went on, they grabed funds illegally from external debt payment account popularly known as EPA,the account supposedly created by the president himself when he was a finance minister in Ruksa government.Other deals used to sweep funds from national treassure mentioned includes but not limited to TANGOLD,MEREMETA & Deep Green

Through this funds and from many other illegal deals like IPTL and mining contracts when he was energy minister,he was propelled to power. This was a land slide victory which they call 'Ushindi wa tsunami' . Indeed RA was a Kingmaker.

As usual if the lion tests human blood will not stop from geting another human flesh.Using the pretext of power blackout they designed Richmond and continued to bleed already highly impoverished country.

Now things seems not to be going well.Whistles are now blown everywhere and very close allies have been recently sacrificed to cover the dead.The fact is clear you cannot cover the dead with flesh hoping that you will prevent the dead to give a disturbing smell because that will be just a temporary measure,as flesh will soon decompose too and add to the smell.

With this nation in dilema,he the president is expected to take action.The people pretend to present themselves as if they know nothing with the involvement of the commander in-chief in dirty deals.They present faith in their face with dismay in their heart.They demand action from the presida on financial worms who stole funds from public coffers.

This is an extremely bitter pill for the bwagamoyo man to swallow let alone to chew.Recent statement by his left handman the PM wa kupinda can prove this.He said the culpits of BoT are untouchable.He simply said the truth.Because he know for sure that the government can do nothing.

Indeed they are untouchable because if you touch them whether it is RA or EL they will have no choice other than to spill the beans!.This certainly will be suicidal to the government.

With this fact now it is clear the King maker now has turned to be the Hangman's noose.No one will dare to put his neck there,I insist no one.

What does this imply?.Possibly you have your own answer but mine is that the fate of the country now lie in the hands of wananchi not the sirikali.
Think about it Mabibi na Mabwana
 
Mtu mzima,

Ina maana Mfalme anatembea kwenye joho jipya kumbe yupo uchi?
 
Mimi sioni mantiki yoyote kumzuia huyu Bwana kutoa maelezo yake mbele ya Bunge otherwise kama kuna jambo ambalo 6 na wenzake hawataki livuje nje ya CCM.

Kama Rostam atashindwa kutoa maelezo yake Bungeni suala bado ni rahisi; aende Maelezo na aweke wazi mambo yote kwa waandishi wa habari na ujumbe utafika.
 
Rostam amejiandalia anguko la pili?



Ansbert Ngurumo




**** mambo mawili hapa. Kwanza, hoja ya Rostam ina nia ya kufichua udhaifu fulani ambao anadhani utamsaidia kusafisha jina lake na la Lowassa. Pili, hoja hiyo hiyo itafichua kingine asichokusudia, ambacho kitamvua nguo yeye, Lowassa na Kikwete; CCM na serikali.




ansbertn@yahoo.com
+447847922762
www.ngurumo.blogspot.com


Mkuu Nadhani kwenye Redhapo hukumaanisha hivyo nadhani ulitaka kuandika kuna.

Vinginevyo taarifa vinzuri assumption nyingi na uzuri ,umeshauri tushubiri tuone zipi kati ya hizo zita work.

Maelezo yako ambayo ni marefu umefanya vyema kuyaweka yote kwa kuwa yametoa mwanga ya jambo hilo amblo kwa kifupi ni mchezo mchafu tu.

Ni juu yetu to reverse haya .
 
With this fact now it is clear the King maker now has turned to be the Hangman's noose.No one will dare to put his neck there,I insist no one.

What does this imply?.Possibly you have your own answer but mine is that the fate of the country now lie in the hands of wananchi not the sirikali.
Think about it Mabibi na Mabwana

Duh!
Surely but as 80% wananchi are just sitting down and complaining who's to decide the fate of this Peaceful Country Tanzania???
 
Nakumbuka kazi aliyoifanya RA wakati ule JK anaonesha nia ya kugombea urais, RA alikuwa akitoa mapesa mengi katika matawi ya chama na pale tabora aliwahi kutoa zaidi ya milioni 10 alitoa hizi kama mtu binafsi anayechangia chama. Sasa naelewa kwanini jamaa hawezi kuguswa japokuwa usanii wake unajulikana mpaka chumbani

MUGABE MALIZIA KAZI ULIYOTUMWA NA WANANCHI
 
Kwa kweli mambo bado ni magumu sana Rostam kwa namna yoyote ile ameiweka Serikali mfukoni mwake pamoja na CCM yake Makala hii imenifanya niamini kuwa Rostam alikuwa na ajenda yake kuingia kwenye siasa.
Rostam ndio chimbuko la siasa za maji taka kwani yeye ni muasisi wa kundi la mtandao.
Rostam ndie ataefanikisha anguko la CCM
Rostam ndie aliyefanikisha kumweka JK madarakani na ndiye atakae sababisha JK atoke pale alipo sasa.
Rostam, Rostam, Rostam
Mfanyabiashara mkuwa mwenye hisa 30% Vodacom Tanzania Ltd, yeye kuonana na Rais, Mkuu wa Usalama wa Taifa na top wa serikali wala ahitaji appointment. allaa awaweke yeye walipo halafu aombe apontment uliona wapi?


sawa point zako ni nzuri, sasa ulikuwa na haja gani ya kuquote dude lote hili kama si kuleta uvivu na kutumia memori vby
 
Rostam amejiandalia anguko la pili?



Ansbert Ngurumo



NILITARAJIA kwamba Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ingemfunga mdomo Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi, ili asijitetee kuhusu alivyohusishwa na kashfa ya Richmond.


Ni kawaida ya kamati hii kuziba watu (wabunge wake) midomo wanapokaribia kuibua mambo mazito yatakayoivua nguo. Lakini yawezekana kwamba katika hili, sasa ndiyo inamzibua mdomo Rostam Azizi.

Rostam Azizi hakuzuka tu. Alijipanga na alidhamiria. Anaijua kamati hiyo, na amekuwa akiitumia kuziba mengine. Alijua analeta mambo mazito dhidi ya Bunge na CCM yake; na alifanya mikakati na wadau wenzake kabla ya kwenda bungeni.

Alijua waziri mkuu angeitisha kikao hicho kumdhibiti. Nimeshangaa kwamba amekubali kudhibitika!

Zaidi ya hayo alijua kwamba Spika wa Bunge, Samuel Sitta, asingeipokea na kuipitisha hoja yake moja kwa moja. Anajua madhara yake. Hata Sitta alijua kuwa Rostam Azizi anaandaa mashambulizi, kwani ni mwendelezo ule ule wa utetezi wa kambi ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujitetea na kusafisha majina yao.

Sitta alijua fika kuwa wanaosafisha majina yao ndio hao wanaosababisha kile alichokiita ‘siasa za maji taka,’ za kuibua kashfa zake.

Baadhi yetu tulishaonya kuwa suala hili la Richmond halikuwa la Lowassa na Rostam pekee; na kwamba haliwezi kwisha sasa. Tulisema pia kwamba kama Lowassa asingejiuzulu, tungejua mengi makubwa, iwapo wangeanza kutajana.

Lowassa alitunyima fursa hii. Alikataa kujitetea. Alikataa kusema anachokijua. Akajiuzulu. Naamini sasa kambi yake imejizatiti upya, na hoja zake zitapatikana katika utetezi wa Rostam Azizi.

Hapa katikati yametokea mengi ndani na nje ya CCM, ambayo hata Spika wa Bunge anayajua.

Kwanza, Rostam Azizi na Lowassa wamekuwa wakilalamika kwamba walihusishwa kimakosa. Alianza Lowassa, baadaye wakubwa wakamzima kama kibatari, baada ya kuona wana Monduli wamemwekea zulia jekundu!

Sasa ni zamu ya Rostam Azizi; na ujumbe wao ni ule ule. Napenda kusema kwamba si vema kuwaziba midomo. Waachwe waseme walichonacho. Wana haki ya kujitetea.

Imesemwa sana chini chini, sasa iachwe iwekwe wazi; kwani kina Rostam na Lowassa wanadai kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Richmond iliwaonea, na ilipewa maagizo maalumu; tena nje ya muda wake.

Katika hili, kambi hiyo inamtuhumu Spika wa Bunge moja kwa moja. Si siri kwamba wakati Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, anawasilisha ripoti ya kamati yake bungeni, na kutoa hitimisho lililolazimisha Baraza la Mawaziri kuvunjwa; tayari kambi ya Rostam na Lowassa ilikuwa na mafaili ya ripoti mbili mkononi.

Kwa mujibu wa kambi hiyo, ripoti ya kwanza ya kamati ya Bunge haikuwahusisha kabisa Rostam na Lowassa.

Wanadai kwamba ilipowasilishwa kwa Spika, akaikataa kwa maelezo kwamba Bunge lisingeweza kupokea ripoti ‘isiyokamilika.’

Ripoti ya pili, iliyowahusisha, ndiyo iliyowasilishwa bungeni; na wao wanadai ilitengenezwa ‘nje ya muda’ waliopewa, ikaongezewa vikolezo na ‘majina’ yaliyokusudiwa.

Haya ni madai ya kambi ya Rostam na Lowassa. Na ndipo hapa wanapoanzia kudai kwamba muda unaodaiwa kutumika kukamilisha ‘ripoti’ ya pili haukuwa rasmi!

Tuwaamini Rostam na Lowassa? Tuiamini ripoti ya kamati ya Bunge? Lakini hatuwezi kujibu vema maswali haya hadi kwanza utetezi wa Rostam uwasilishwe na usikilizwe.

Sana sana, kambi ya kina Rostam inatufanya tujiulize leo. Mbona wanataka kujitetea leo wakati walikuwa na muda wa kufanya hivyo na kutoa vielelezo wakati wa mjadala wa ripoti hiyo katika kikao kilichopita? Je, baada ya miezi miwili kupita, jamii itaamini maelezo wanayokuja nayo sasa? Utetezi wao utaaminika kwa Bunge na mamlaka nyingine zinazohusika? Utawasafisha?

Hata hivyo, habari za kuaminika zinasema kwamba muda huu waliopewa, umewasaidia kuwasilisha vema utetezi wao kwa Rais Jakaya Kikwete, kabla ya kuupeleka bungeni.

Ni wazi kwamba rais naye ni mhusika mkuu katika mradi wa Richmond tangu mwanzo, bali hapa katikati mawimbi ya kisiasa yalimzidi nguvu.

Na kwa kuzingatia ukaribu wa watatu hao (Kikwete, Lowassa na Rostam) kisiasa na kifamilia, rais amewasikiliza na kuahidi ‘kusaidia’ kuwasafisha. Kisichojulikana ni kama walidhani njia mwafaka ya kujisafisha ni kupitia bungeni.

Maana, ili wajisafishie bungeni, inabidi Bunge lifike mahali likiri kwamba liliwaonea. Maana yake, kamati ya Bunge ilikosea; hivyo hata mapendekezo iliyotoa, ambayo serikali iliahidi kuyatekeleza yalivyo, yasitishwe.

Je, watawala wako tayari kulidhalilisha Bunge kuwasafisha marafiki wa wakubwa? Lakini wengine wanasema katika siasa za Tanzania lolote linawezekana.

Kwa maana hiyo, yawezekana hata jitihada za sasa za kambi ya Rostam na Lowassa zina baraka kutoka juu. Maana baadhi ya wachunguzi na wafuatiliaji wa mambo wamegundua kuwa katika siku za karibuni, uhusiano kati ya Kikwete na Sitta umechafuka kwa sababu ya Richmond.

Niliandika suala hili kwa kifupi huko nyuma, kwamba sasa Kikwete ameogopa athari ya kujitenga na kina Lowassa na Rostam, kwa hiyo anawatafutia fursa wajisafishe; na kwamba ndiyo maana hata vikao vya CCM Butiama vilikwepa kabisa kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

Hili liliwaudhi baadhi ya wajumbe; na liliwagawa wastaafu kila mtu akajitengenezea sababu ya kutokwenda Butiama.

Walitaka Kikwete achukue msimamo wa Bunge, asikilize maoni na hisia za wananchi juu ya ufisadi.

Alikataa, kwani alishapewa dozi ya ‘siri’ ambayo ilikuwa katika mafaili ya Rostam na Lowassa, akajua akiruhusu chama kiwaguse tu, watakitesa; maana wana mengi ya kuanika.

Lakini hili linawatia watawala katika mtihani mgumu. Yawezekana ni kweli kwamba hoja ya Rostam na Lowassa dhidi ya kamati ya Bunge ni kweli. Na kama ni kweli, hasira za rais dhidi ya Spika zitathibitishwa siku si nyingi.

Maana kama si kamati ya Bunge, Baraza la Mawaziri lisingevunjwa; rais asingeingizwa katika wakati mgumu unaotishia kukigawa chama chake na serikali yake.

Hata hivyo, itabidi achague moja; ama kuwasikiliza kina Rostam na Lowassa au kulisikiliza Bunge. Je, yuko tayari kutosa taasisi za utawala na kuwakumbatia marafiki? Yuko tayari kuliaibisha Bunge na kujenga heshima ya watu binafsi?

Lakini wapo watu wanaodhani kwamba lolote linawezekana. Wanaosema hivi wapo ndani ya mfumo wenyewe, na wanakumbuka kwamba miaka miwili iliyopita, Rais Kikwete alishauriwa na kuonywa kuhusu uhusiano wa serikali yake na Rostam.

Waliomuonya waliona mbali juu ya ukweli ambao sasa ndio umedhihirika. Walitaka ‘amshukuru’ Rostam kwa msaada wake kwao katika kampeni za urais, lakini asimweke karibu mno katika masuala ya utawala wa nchi.

Lakini Rais Kikwete alitaka kuwa muungwana kwa waliomsaidia. Ilifikia wakati, ingawa Rostam hakuwa serikalini, alikuwa akijihusisha moja kwa moja katika mipango ya serikali, hata katika mambo ambayo kimsingi yangefanywa na mawaziri.

Baadhi ya wanahabari wanakumbuka, na kumbukumbu bado zipo, kwamba hata baadhi ya taarifa za mikutano ya viongozi wa serikali na wanahabari kuhusu maamuzi kadhaa ‘mazuri’ kwa serikali zilitoka kwake kwenda vyumba vya habari.

Ajabu, zipo taarifa za baadhi ya mawaziri ambao walifanikiwa kirahisi kumfikia rais kupitia ‘nje ya serikali.’ Mtu mmoja aliyemuona kigogo mmoja wa usalama wa taifa ofisini kwa Rostam, tena wakijadili masuala ya taifa, aliwahi kudokeza kwamba sasa tunakoelekea ‘utabiri wa Nyerere unakaribia kutimia, Rostam ataiweka nchi mfukoni.’

Waliotaka kumtenga Rostam na Kikwete mwanzoni mwa utawala wa Awamu ya Nne, walijua kuwa Rostam ni mfanyabiashara mtafutaji na ana malengo mengi katika siasa, ambayo hawakutaka yamguse rais.

Kwa sababu hiyo, baadhi ya wanaojua vema uhusiano wake na Kikwete, waliokerwa na ukaribu wao huo, wanamuunga mkono mtu yeyote anayeweza kuwatenganisha – kwa masilahi ya taifa.

Sasa leo yanapoibuka masuala nyeti kama haya, ni dhahiri rais anakumbuka ushauri aliopewa akaupuuza. Lakini anaona pia amechelewa kumtema Rostam, maana tayari anajua mengi yanayoweza kumuangusha Kikwete mwenywe. Amfanyeje?

Inaonekana kwamba hata katika sakata hili la Richmond, kama madai ya kina Rostam ni kweli, Sitta alidhamiria kutimiza azima ya kuwatenganisha Rais Kikwete, Rostam na Lowassa, kwa sababu binafsi au hizo hizo zilizotajwa hapo juu. Kwa muda sasa amefanikiwa. Je, utengano huu utadumu hadi lini?

Jambo linalojulikana pande zote ni kwamba Kamati ya Mwakyembe haikukuta faili la usajili wa Richmond; ikahitimisha kwamba Richmond ni kampuni feki.

Lakini wajuzi wa mambo wanajua kwamba faili hilo lilikwapuliwa muda mfupi baada ya kamati ya Bunge kuundwa na kupewa hadidu za rejea.

Bahati nzuri, waliolipoteza wanajulikana, na walidhani wangetumia kumbukumbu hizo kuonyesha udhaifu wa kamati ya Bunge, kuwatetea waliohusishwa na kashfa; jambo ambalo sidhani kama litasaidia sasa.

Haya yote yakiibuka, Bunge litapaswa kujadili na hatimaye kujua nani aliiba faili la usajili wa Richmond, na alitaka kuficha nini!

Bahati nzuri nyingine ni kwamba wenye Richmond wanajulikana. Hata Rostam Azizi anawajua. Lakini sidhani kama kwa ukweli wote wa moyo wake, anaweza kuwataja bungeni, ingawa ana vielelezo vya kuwachoma wengine.

Katika hili, Rostam hana ujasiri wa kunywa sumu! Hawezi. Hatathubutu! Sana sana, atakachofanya ni kujaribu kuonyesha kwamba yeye hayumo.

Lakini lolote atakalosema Rostam sasa, likijadiliwa vema na hadharani, likachunguzwa kwa macho ya akili ya watu makini na wazalendo, litaivua nguo serikali na CCM.

Na kama linaivua nguo CCM ili wananchi wapone, kwanini Rostam anazuiwa kusema? Kwani CCM ni bora kuliko Watanzania? Kwani wizi wa wakubwa ni baraka kwa taifa?

Hii ni fursa nyingine kwa wananchi kujua makubwa zaidi kuhusu Richmond; si kwa kusikia tu hoja ya Rostam, bali kwa kuifanyia pia uchambuzi wa kina na kuona kilichomo na kinachokusudiwa.

**** mambo mawili hapa. Kwanza, hoja ya Rostam ina nia ya kufichua udhaifu fulani ambao anadhani utamsaidia kusafisha jina lake na la Lowassa. Pili, hoja hiyo hiyo itafichua kingine asichokusudia, ambacho kitamvua nguo yeye, Lowassa na Kikwete; CCM na serikali.

Hapo ndipo utamu ulipo; mtego ambao kamati ya CCM inakusudia kuuruka. Hilo la kwanza, linalenga kutoboa matundu kwenye nguzo ya Bunge, kuonyesha udhaifu wa Spika na kamati zake, na kuwajenga waliohusishwa na kashfa ya Richmond.

Spika yupo tayari kudhalilisha Bunge kwa ajili ya kuwajenga washindani wake? Hapa ndipo ulipo woga wa Spika. Je, rais atamtosa Spika katika hili?

Hili la pili ndilo linalomsumbua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Ndio wasiwasi wa Kamati ya Uongozi ya CCM. Kwa sababu za kisiasa, ni wasiwasi wa Rais Kikwete pia. Sasa akae upande upi? Tusihukumu leo. Tusubiri.

Na inawezekana Rostam akafungwa mdono. Lakini je, Bunge litaikalia hoja yake hadi lini? Je, baada ya CCM kuingilia kati kumfunga mdomo asiliaibishe Bunge na CCM, ambalo Spika anaweza kulitumia kumnyima fursa ya kujieleza, Rostam atakuwa na ujasiri kama wa Dk. Willibrod Slaa, aliyechomoa hoja yake bungeni na kuimwaga hadharani?

Na je, hata akipewa muda atakuwa tayari kusema ukweli wote kuhusu Richmond na kujibu maswali yatokanayo? Kama ana uchungu na uwezo huo, kwa nini aliikwepa Kamati ya Mwakyembe, ndani ya muda iliopewa?

Mbona analeta utetezi wake nje ya muda wa kamati? Au aliamini kwa kuwa upotevu wa mafaili ‘kilikuwa kisiki tosha kwa kamati ya Bunge kuhitimisha kazi yake?’

Na je, anadhani iwapo Bunge litaruhusu hoja yake ijadiliwe kwa uwazi, hayatazuka mengine ambayo wajumbe wa kamati waliyafunika ili ‘mwanaharamu apite’ na ambayo wanaweza kuyaibua leo kudhoofisha kabisa utetezi wa Rostam? Je, yuko tayari kwa anguko la pili? Tunasubiri matokeo.

ansbertn@yahoo.com
+447847922762
www.ngurumo.blogspot.com

Kuna rafiki yangu mmoja niliwahi kumwambia mara tu baada ya uteuzi wa mgombea wa ccm mwaka 2005 kuwa ataongoza miaka mitano tu na kuukabidhi uongozi kwenye upinzani ambao bado haujaundwa ila utakuwepo tukikaribia 2010.Tuombe uzima kuona hayo yatakapotokea kwani hakika yatatokea.lakini lazima watu wajitoe mhanga wanahitajika wazito kama kumi tu wataungwa mkono na uma wa watanzania waliochoka kudanganywa lakini hawana jinsi imebaki yao ni macho tu.
 
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Nyrere alikuwa anaweka watu kizuizini hata kama walikuwa marafiki. Ni mambo kama haya ya kujuana na kutishiana maisha, JK anatakiwa kuwasweka RA na EL nadani mara moja. Otherwise watamsumbua sana
 
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Nyrere alikuwa anaweka watu kizuizini hata kama walikuwa marafiki. Ni mambo kama haya ya kujuana na kutishiana maisha, JK anatakiwa kuwasweka RA na EL nadani mara moja. Otherwise watamsumbua sana

Hata mimi nimekuwa nafikiria hili karibuni. Option nyingine ni kuwaweka pale mnazi mmoja na kuwachapa risasi za miguuni toka kwa shap shutaz kama mia moja huku TV zote zikionesha live!

Na baada ya hapa inabidi Rostam awe deported kwenda kwao Iran maana imeanza kuthibitika kuwa uraia wake ni wa kufoji!
 
Duh!
Surely but as 80% wananchi are just sitting down and complaining who's to decide the fate of this Peaceful Country Tanzania???

You are absolutely right.This is our immediate challenge we are facing but we need solution and a way forward urgently.

IMPOSSIBLE CAN BE MADE POSSIBLE IF AND ONLY IF YOU HAVE THE WILL AND COURAGE,DESPAIR AND GIVING UP HAVE NO CHANCE IN THE WAR IF YOU ARE FOR THE VICTORY.
 
kale ka nzi ka kijijini kamepata fununu kuwa siri haiwezi kuwa ni siri ya watu wawili kamwe... hivyo nasikia mojawapo ya magazeti itafunua siri ya Rostam kesho.. Ningependa kukutajia gazeti gani..lakini it won't be fair to others... so come wednesday angaza angaza macho!!
 
kale ka nzi ka kijijini kamepata fununu kuwa siri haiwezi kuwa ni siri ya watu wawili kamwe... hivyo nasikia mojawapo ya magazeti itafunua siri ya Rostam kesho.. Ningependa kukutajia gazeti gani..lakini it won't be fair to others... so come wednesday angaza angaza macho!!



Umh! afadhali tujue kitakachojiri maana nilidhani hii ishu ya RA ndio imeshazimika like a candle in the wind. Toa hata hint tu Mwana, ni gazeti linalopatikana mtandaoni?
 
kale ka nzi ka kijijini kamepata fununu kuwa siri haiwezi kuwa ni siri ya watu wawili kamwe... hivyo nasikia mojawapo ya magazeti itafunua siri ya Rostam kesho.. Ningependa kukutajia gazeti gani..lakini it won't be fair to others... so come wednesday angaza angaza macho!!

Tunasuburi mkuu ingawa sina imani kama anaubavu wa kujifunua mwili mzima
 
Umh! afadhali tujue kitakachojiri maana nilidhani hii ishu ya RA ndio imeshazimika like a candle in the wind. Toa hata hint tu Mwana, ni gazeti linalopatikana mtandaoni?

Bora asitaje ka gazeti kenyewe maana RA anaweza kuka-Kabenea na TINDIKALI
 
Back
Top Bottom