Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Mh.Tukae mkao wa kula au kupigwa machanga ya macho. Make usishangae kusikia kuwa kutakuja big news lakini si chochote zaidi ya kumsafisha. Na tungoje tuone
 
kale ka nzi ka kijijini kamepata fununu kuwa siri haiwezi kuwa ni siri ya watu wawili kamwe... hivyo nasikia mojawapo ya magazeti itafunua siri ya Rostam kesho.. Ningependa kukutajia gazeti gani..lakini it won't be fair to others... so come wednesday angaza angaza macho!!

Mwanzo mzuri na nina hakika kuwa hili suala la RA kubaniwa nafasi ya kutoa duku duku lake ndani ya Bunge litaweza kuibua siri nyingine ambazo hazikutegemewa.

Sisi yetu macho manake siasa yetu imefikia mahali patamu panapoweza kuboresha Demokrasia.

Cha muhimu iwepo fair Play, kutoana macho hakuna haja. Mtu akishindwa atoke akajipange upya kama EL anavyopanga mashambulizi yake kimya kimya. Tutegemee kushuhudia mengi mpaka ifikapo 2010 siri itakuwa hadharani kuhusu nani Adui na nani Rafiki wa kweli kwa Tanzania na Watanzania.
 
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Nyrere alikuwa anaweka watu kizuizini hata kama walikuwa marafiki. Ni mambo kama haya ya kujuana na kutishiana maisha, JK anatakiwa kuwasweka RA na EL nadani mara moja. Otherwise watamsumbua sana

Hahahaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!! JAMANI JAKAYA AFANYE NINI NDIO MUMUELEWE,NI SISI WA KUMLINDA NA MADHIRA,TUSISAHAU KUWA 2005 TULIFUNGA NA KUOMBA KWA AJILI YAKE,TUOMBE SASA ILI AREJEWE NA NGUVU ZILE KABALA YA KUINGIA IKULU,KUMLAUMU HAISADII ,TUTIMIZE WAJIBU WETU
 
Habari ndiyo hiyo,ila Mwanakijiji kwanini haukukaa kimya kwanza??au ulishazoea speculation??

Je Gazeti litatoka?

Mzee Ruhinda??kuna thread moja kuna nimeweka picha ta Ruhinda na Rostam..
 
kutoana macho hakuna haja. Mtu akishindwa atoke akajipange upya kama EL anavyopanga mashambulizi yake kimya kimya. Tutegemee kushuhudia mengi mpaka ifikapo 2010 siri itakuwa hadharani kuhusu nani Adui na nani Rafiki wa kweli kwa Tanzania na Watanzania.


hata akijipanga vipi hatumchagui sababu ni moja kubwa,Yeye si kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu na zaidi ya yote tunamuomba ajibu swali la Marehemu Baba wa taifa,Utajiri wote alionao ameutoa wapi na aliupataje?
 
Amani haiji ila kwa ncha ya upanga, hili nimeliona pale kenya na kwingineko duniani, mfano mwingine ni pale Mkoani Mara wilayani Tarime,wote tunaufahamu mgodi wa North Mara, wale jamaa(wakulya)kila kukicha wanachukua kilichochao, na yoyote anayejipendekeza halali yao, sasa kama Viongozi wanataka tufike huko tutafika tuu,kisha tujiulize kuishi kwetu sisi kuna maana gani kama watoto wako na wajukuu wako watateseka huku watoto wa viongozi wakila neema? Iko siku itatimu na si Kitambo
 
kuna mtu alikuwa anauliza leo kufunuliwa kama anaumbuliwa au kuelezea alichokuwa anataka kusema? Kesho magazeti yanasubiriwa kwa hamu kama unayosema ni kweli au ni zile "stori" zako.

thanks, and I'm out.. time is up
 
Sitegemei hiyo issue kutoka , kwa sababu , alichosema Kijiji, kitasababisha hiyo story kuzuiwa kistaarabu kwa watu kupewa pesa yao , kwa usalama wa taifa, na kama ikitoka itakuwa imepunguzwa makali.
 
FUMBA MACHO ALAFU USOME


""""""""RAIA MWEMA""""""""""
 
kuna mtu alikuwa anauliza leo kufunuliwa kama anaumbuliwa au kuelezea alichokuwa anataka kusema? Kesho magazeti yanasubiriwa kwa hamu kama unayosema ni kweli au ni zile "stori" zako.

thanks, and I'm out.. time is up

Be senti 50,

Achaneni na huyu Rostam maana atawaharibia chama. The guy ni mchafu sana na hawezi kusafishika hata kwa damu ya kigagula toka Bagamoyo!

Ni ushauri tu .....
 
MTANDAO wa ufisadi wa EPA unawajumuisha pamoja wafanyabiashara kadhaa akiwemo mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam.

Wengine katika mtandao huo ni pamoja na Salleth Vithlani, yule wakala wa uuzaji wa rada, vifaa vya kijeshi na ndege ya Rais aliyekuja kutoroka baadaye.

Huyo Bwana anayeishi karibu na Slipway Hotel ndiye anayesimamia mtandao mdogo unaohushisha makampuni kadhaa yaliyochota fedha za EPA. Inadaiwa pia kuwa ana hisa katika Benki M.

Wengine wenye hisa katika benki hiyo inaaminika kuwa ni pamoja na Jeetu Patel (alijitoa baadaye), Daudi Balali, Vima Meha, Sanjeer Kumar, Bhasker Narayan, Anna Muganda na wengineo.

Pia mtandao wa Jeetu Patel unamhusisha mfanyabiashara mmoja aishie nchini Kenya aliyewahi kumiliki Benki tata nchini humo “Delphis Bank”
iliyowahi kuwapora wateja zaidi ya dola milioni 90.

Aliwahi pia kumiliki nchini humo kampuni ya kuuza magari iitwayo “Marshalls Kenya Limited” na kuliuzia Jeshi la Kenya magari kwa mkataba wenye utata kama ilivyotokea hapa nchini kwetu kwa Sailesh Vithlani na Serikali yetu (mauzo ya rada).

Ni mfanyabiashara huyo pia ambaye amewahi kuwapora wateja wa Benki ya “Trust Bank” iliyosimamiwa na BOT chini ya dhamana ya Delphis Bank mwaka 1999, na hadi sasa angali anasakwa na polisi.

Wengine katika mtandao huo ni Bharat Patel, raia wa Uingereza ambaye ni mdogo wake Jeetu Patel anayeishi mjini London mwenye kumiliki kampuni iitwayo Motorsense. Yupo pia mtoto wa Bharat Patel, raia wa Uingereza anayeishi hapa nchini aitwaye Mitul Patel ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa baadhi ya makampuni yanayodaiwa kushiriki kuchota fedha za EPA.

Pengine sakata la pesa za EPA lisingejulikana na kulipuka kama mmojawao aitwaye Jitesh Ladwa asingewashambulia na kuwararua wenzake kwa kusahau kufuta pua na midomo yao!

Mapema 2005, Jitesh Ladwa, mfanyabiashara na mdaiwa mkubwa wa vyombo vya fedha hapa nchini, alisambaza ujumbe kwa njia ya E-mail duniani kote kuibua ufisadi uliokithiri BOT. Inasemekana Jitesh alikuwa anadaiwa na EuroAfrican Bank kiasi cha Sh. bilioni moja, IFC Sh. bilioni 7 na Barclays Bank Sh. bilioni 2.5, ambapo hoteli za Golden Tulip na Karibu Hotel zilikuwa chini ya rehani.

Hapo Machi 7, 2005 Jitesh Ladwa aliomba mkopo kutoka BOT kwa ajili ya kupanua Hoteli yake iitwayo Indian Ocean Hotels kwa lengo la kuvutia watalii nchini. Ombi lake lilikataliwa na BOT kwa barua ya Septemba 1, 2005 kwa maelezo mafupi tu kwamba Benki hiyo haikuwa na uwezo wa kushughulikia ombi lake.

Kabla ya hapo, Jitesh alikuwa “mteja mzuri” na mahiri wa EPA na alinufaika kwa kiasi kikubwa yeye na “Mbwa mwitu” wengine. Sababu kubwa ya kukataliwa kwa maombi ya Jitesh ni utata wa baadhi ya hati alizowasilisha Benki kwa kudhaniwa kwamba hazikuwa halisi.

Kunyimwa mkopo kwa Jitesh kulizua vita kali kati yake na uongozi wa BOT, chini ya Daudi Ballali, pamoja na wafanyabiashara wenzake (Mbwa mwitu) wenye asili ya Kiasia na akaanza kuanika nje uozo ndani ya Benki na sakata zima la pesa za EPA ambazo yeye alikuwa mnufaika pia.

Jitesh alimshambulia pia Jeetu Patel kwa kushindwa kumwokoa alipowasilisha kwake ombi la mkopo binafsi kufuatia BOT kumwekea ngumu.

Inasemekana baada ya kugonga mwamba BoT na kwa Jeetu Patel, Jitesh Ladwa alimwendea mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliweza kumpatia mkopo aliotaka. Inadhaniwa pia kuwa, pengine ni kwa sababu ya kumsaidia Jitesh, kwamba Rostam Aziz hakutajwa katika E-mails alizosambaza Jitesh duniani pamoja na kuwa mbunge huyo naye alinufaika na pesa za EPA.

Kuokolewa kwa Jitesh na Rostam Aziz kulijenga kambi mbili za “Mbwa mwitu” katika ufisadi wa EPA, kati ya kundi la wafanyabiashara “wapendwa” walioendelea kunufaika na BOT na kundi la “walioteuliwa” likiongozwa na Jitesh ambalo liliapa kuwalipua wale wa kundi la “wapendwa” isipokuwa Rostam Aziz kwa sababu ya umaarufu wake.

Ukweli ni kuwa, ilifika mahali kulikuwa na Serikali mbili ndani ya Serikali ya Tanzania, yaani Serikali halali chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na “Serikali nyingine” chini ya wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rostam Aziz.

“Serikali” hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.

Inadhaniwa kwamba ni “Serikali” hii ya pili (ya Rostam Aziz) iliyohamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kupigania nafasi za kisiasa ili kupata habari toka ndani ya Serikali ya namna ya kutoa ushawishi jinsi ya kufikiwa maamuzi yaliyopendelea tabaka la wafanyabiashara, ubepari wa kimataifa na kikundi kidogo cha watawala waliotekwa nyara na ubepari huo.

Kwa hili, kwa nini umma usiamini unapoona kwamba mafisadi hawakamatiki ambapo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act), Sheria ya Udhahidi (Evidence Act) na Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) zimesitishwa dhidi ya mafisadi ili waonekane kama wadaiwa wa kawaida chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Act), tena bila kutozwa riba?
Kwa nini umma usiamini hivyo unapoona kwamba fedha za ufisadi zinarejeshwa na mizuka (ghosts) isiyoonekana, lakini Serikali inakiri kuzipokea kutoka kwa “watu” (“serikali ya pili”) wasiojulikana?
Je, zinatupwa na kuokotwa barabarani?

Ajabu, yote haya yanatendeka mbele ya Tume iliyoundwa na Rais, ikijumuisha Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, na Mkuu wa TAKUKURU ambao wote ni wanasheria kwa taaluma.

Sakata la EPA ndani ya BoT liliibuka kutokana na Mbwa mwitu kuraruana wao kwa wao kiasi kwamba minyukano yao iliwaamsha wananchi wenye mali kutoka usingizini na kujionea jinsi wanavyoporwa mali zao.

Rais Kikwete aliunda Tume kuchunguza uporaji huo baada ya umma kupiga yowe muda mrefu kuwa unaibiwa. Ukichunguza kwa makini huwezi kushindwa kubaini kuwa wale wanaounda Tume, baadhi yao ni wale wale wanaonufaika na mizoga iliyoachwa na Mbwa mwitu wawindaji. Je, fisi anaweza kumhukumu mbweha anayempa chakula? Ili iweje na akale wapi?

Na kwa kuwa umma wa Kitanzania umeamshwa na minyukano ya mbweha mafisadi na kukuta umeporwa mali zake kwa muda mrefu kabla ya hapo, je kuna sababu gani kunyamazia uporaji wa kale iwapo ushahidi upo? Kwa nini Rais asiunde Tume kama ile ya EPA kufuatilia uporaji wa kale?

Tuna Serikali ya wananchi moja tu ambayo tumeambiwa haina ubia na mtu au kikundi chochote cha watu katika kuongoza nchi. Kama hivyo ndivyo, hatutarajii kuona “Serikali” ya kikundi cha mafisadi walio juu ya dhana ya utawala wa sheria wanaoweza kupora na kuyeyuka “kimiujiza” wasiweze kuguswa na mkondo wa sheria.

Inapokuwa hivyo, umma hauwezi kujizuia kuamini kwamba baadhi ya viongozi wetu wananufaika na mizoga inayotemwa na kundi la mmbwa mwitu wawindaji ndani ya nchi yao.
http://www.raiamwema.co.tz/08/04/09/mihangwa.php
 
Sasa mimi sioni habari nyingine na leo ni jumatano hapa Bongo. Mimi ndo nimeshafungua ka hardware kangu natafuta weee sioni.

Mwanakijiji ni PM basi mzee mwenzangu.
 
Habari iko katika Gazeti la Mwanahalisi ,litafute..Ni kuhusu Rostam kutishia kamati ya uongozi kwamba kama wasipomruhsuu atoe hoja yake Bungeni basi anajiuzuru Ubunge.

wakati Rostam akitoa maneno hayo Mhe. Spika alimwambia jiuzuru sasa hivi na Mhe. Pinda ambaye kwa sasa ndiye amri jeshi mkuu akamuunga mkono Mhe. Sitta.

Habari ndiyo hiyo.RA alitaka asafishwe na Mwenyeketi wa kamati ya kuchunguza mkataba wa RDC,Dr. MWakyembe na inasemekana kuna baadhi ya wabunge wa viti maalum CCM walikuwa wameongwa ili wakati RA anatoa Hoja yake wampigie makofi.

Now i understand why and why Jk left Chenge and he is still let RA do his own bussines,alishawapa meno spika na Pinda na nina uhakika yule mkaramba atawapeleka puata kwa sasa.

No more Ufisadi and pesa infront of PINDA na ndio maana laisema kama mtu akimuona au kuhusu kwamba yeye ni fisadi Mungu amchukue,alikuwa anaa maanisha

Mungu Mbariki Mizengo k. Pinda,Mungu ibariki Tanzania,Mungu Tuepeushe na Mafisadi wasio na huruma nasi.
 
Back
Top Bottom