Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

mi hata sielewi kinachoendelea nahisi kidhungudhungu, swali langu ni pinda, ambaye anakaimu nafasi, sitta ambaye ndo spika wa Bunge na rostam ambaye ni mbunge, intetions zao ni nini? kati yao kuna maslahi binafsi na ya taifa so far sioni chochote katika maslahi ya taifa kila mtu anajaribu kuhakikisha upande anaosimamia huko salama, hadi hapo kikwete na serikali yake watakapokuja na msimamo unaoeleweka, in meantime siwezi hata kuanza kumhukumu rostam kwasababu sijui chui yupi, kondoo yupi, mi nawaona wote machui tu! yaani am furious kupita maelezo, at the end of it all i dont know how kikwete na ccm na wote wanaohusika na madaraka ktk nchi wakavyoanza kujustify yote haya i mean this is too much, good thing yanaanza kujitokeza.
 
Sina hakika kama kutakuwa na jipya. RA anataka kujisafisha bila kujua kwamba anachotaka kufanya ni kurusha jiwe wakati yeye yupo ndani ya nyumba ya kioo
 
Naona Spika na Naibu Spika wameamua kumpa RA ushindi wa chee ili akiingia mtaani atambe kwamba ikiwa angepewa nafasi ya kuwasilisha utetezi wake angelitikisa Bunge na Taifa. Yale yale ya EL kwamba hakupewa nafasi ya kujitetea (natural justice).

Watu kama hawa haitakiwi uwape leeway ya kujionyesha mbele ya jamii kwamba serikali inawaogopa. Ilitakiwa apewe nafasi ya kujitetea na sisi wananchi tungeweza kuchambua mchele na pumba. Sasa kama Spika na Naibu Spika wanafanya kazi ya kuchambua inawezekana wakawa wanachambua kinyume maana thinking yao iko biased kwa kuwa wote ni wana CCM na ile ibara iliyopigiwa kelele ndiyo inayowaongoza kwenye uchambuzi wao. Sisi wengine hatuna mrengo wa CCM wala upinzani tungeweza kugeuza pande zote mbili na kuona ukweli uko wapi.

Mpaka hapa naona RA amepewa ushindi wa mezani wa magoli 2 kwa bila dhidi ya Spika/Naibu Spika na Bunge kwa ujumla. Hili akitumia vizuri magazeti yake ku-spin litakuwa ni kovu kubwa sana na litawasumbua akina Sitta na Bunge lake na kujenga hisia kwa jamii kwamba aidha RA anaogopwa ama alionewa na Tume ya Mwakyembe.
 
Sasa kama hakuwa na jipya mbona alimfunga mdomo? 😕
Si tayari yote yako hadharani basi Watanzania tungependa kuyasikia amwache azoze ili tuendelee kukusanya ushahidi dhidi ya mafisadi.
 
Sina hakika kama kutakuwa na jipya. RA anataka kujisafisha bila kujua kwamba anachotaka kufanya ni kurusha jiwe wakati yeye yupo ndani ya nyumba ya kioo

HATUNA HAJA YA KUJUA KAMA NI MAPYA AU YA ZAMANI BALI TUNATAKA AZIMIO LA BUNGE KUWA ra ASIMAME NA KUJIBI HOJA BUNGENI LITEKELEZWE.KWANI SIKU ILE SPIKA ALIPOSEMA HAMUONI MH RA BUNGENI NA KWAMBA ANGEKUWEPO ANGESIMAMA KUJIBU HOJA ALIKUWA ANAMAANISHA NINI.NA ANGEMZUIAJE KUYASEMA HAYO KAMA ANGEKUWEPO SIKU ILE???MWENYE WAJIBU WA KUJUA KAMA HAKUWA NA JIPYA NI HUYO MAMA MAKINDA??TUACHE HOJA NYEPESI HAPA.
 
Na mwandishi wetu.
Mwanahalisi.

Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, ametishia kujiuzulu ubunge kutokana na hatua ya kamati ya Uongozi ya bunge kumzuia kuwasilisha hoya yake bungeni, Mwanahalisi limedokezwa.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, zinasema Rostam alitoa tishio hilo mbele ya wajumbe wa kamati ya uongozi ambao pamoja na Spika wa bunge, Samweli Sitta na Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Inaelezwa kwamba baada ya Rostam kutoa kauli hiyo, Waziri Mkuu na Spika pamoja walimtaka afanye hivyo haraka.

"Kabla rostam hajamaliza kulalama, Spika hakumkawiza. Alisema, "Andika barua ya kujiuzulu sasa hivi. Hatuwezi kupeleka matusi haya ndani ya Bunge....." alinukuliwa na mjumbe mmoja wa Kamati.

Mjumbe huyo alisema kauli ya Rostam iliwaudhi wajumbe wa Kamati ya Uongozi kwani haraka Waziri Mkuu alitoa tamko la kuungana na Spika Sitta kumtaka Rostam ajiuzulu ubunge.

wiki iliyopita, Spika alimzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake bungeni, baada ya kubaini kuwa aliyoyaeleza katika kile alichoita "Hoja yake" hayakustahili kuwasilishwa bungeni.

Katika Mkutano wa bunge uliopita (wa kumi) bunge lilimtaka Rostam kuwasilisha maelezo yake katika mkutano unaolendelea sasa mjini Dodoma, baada ya kusikika akituhumu kwamba kamati teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond, " aliendelea na kazi zake hata baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa Spika"
Rostam kwa mujibu wa taarifa yake kwa spika.

Rostam kwa mujibu wa taarifa alitaka Spika kwa kutumia hoja za Rostam , amwamuru Dr. Mwakyembe kumsafisha ndani ya bunge.

Hata hivyo shinikizo lake hilo lilikataliwa na kamati ya Uongozi.

Taarifa za ndani ya bunge zimesema kukataliwa kwa maelezo binafsi ya rostam kumetokana na konekana yamejaa tuhuma, shutuma na dharau kwa bunge na kamati teule ya Mwakyembe.

Spika wa Bunge amekiri kupokea hoja binafsi ya Rostam, lakini alisema ameshindwa kuruhusu iwasilishwe bungeni kutokana ka kwend kinyume na kanuni za bunge.

Mjumbe mmoja wa Kamati ya uongozi amemkariri Spika akisema Bunge halikujadili hoja ya Rostam, siyo kwa kumwogopa, kama baadhi ya magazeti yanavyotaka kuonyesha, bali kwa sababu hoja yenyewe inakiuka kanuni za Bunge.

Alipopigiwa simu na gazeti hili kupata undani wa taarifa hiyo, Sitta aliekeza mwandishi awasiliane na Rostam mwenyewe ambaye Spika alisema tayari amejulishwa uamuzi huo.

Mwanahalisi halikuweza kuwasiliana na Rostam kupata upande wake.

Katibu wa wa wabunge wa CCM, alli Ameir Mohammed, alipoulizwa juu ya suala hili alisema, "sijui kilichojajiliwa. Sifahamu kamati ya Uongozi wa wabunge wamesema nini. Sikuwepo Dodoma na wala sijakutana na mwenyekiti wangu, wala Rostam"

Hata hivyo, imefahamika kuwa wajumbe wa kamati teule walikuwa wamejiandaa vilivyo kulithibitishia taifa kuwa Rostam ndiye mwenye Richmond na Dowans.

Uchunguzi wa Mwanahalisi umeonyesha kuwa wajumbe walikuwa wamekamilisha kile kilichoitwa misumari ya mwisho wa kumpigilia Rostam.

Wiki iliyopita Rostam alimweleza spika wa bunge, nia yake ya kutoa maelezo binafsi kuhusu madai ya kamati teule kuwa ilihuka na njama za kufisadi za kuibeba Richmond.

Taarifa za Bunge zimesema hakukubaliwa kw amujibu wa kanuni za 53(8) na 54(4) za kanuni za kudumu za bunge, toleo la 2007 zinazopinga kuwa "Mbunge yeyote hataruhusiwa kufufua jambo lolote ambalo bunge lilikwisha kuliamua ama katika mkutano huo au ule uliotangulia.

Imefahamika kuwa Rostam katika hoja iliyokataliwa na Spika, aliwaita wabunge kuwa ni wasanii na wababaishaji kwa babau tu walimshuku kwenye taarifa yao kuhusika na mkataba wa kuisadi wa Richmond/Dowans.

Uchunguzi wa gazeti hili umethibitisha kuwa Rostam aligawa fedha nyingi kwa baadhi ya wabunge, hasa wa viti maalum(Majina tunayo) ili wampigie makofi ya nguvu wakati wa kusasilisha maelezo yake.

Kuna madai pia kuwa aligawa fehda nzuri kwa baadhi ya waandishi wa habari (Majina tunayo) ili kuipunguza makali ripoti ya kamati teule.

Pamoja na jitihada zote hizo, bado zaidi ya asilimia 95% ya wabunge wanaiunga mkono kamati teule na wangetaka wahusika wote katika kashfa ya Richmond wachukuliwe hatua kali.

"Hawa watu hawajui kusoma mood ya wabung. wengi tuna hasira nae; tungemchanachana baada ya kuwasilisha utumbo wake, sauti za viti malum zingemezwa na sauti za wabunge wazalendo" amesema mbunge kijana na machachari.

Alipoulizwa Dk. Mwakyembe kama kweli kamati yake ilikuwa na ushahidi wa ziada unaoonesha Rostam ndiyoe Richmond/Dowans, alisema kwa ufupi " Tumbuombee tu mwenzetu aruhusiwe kutoa dukuduka lake. Tutakayoyasema yatajulikana palepale ulingoni"
 
JAPO HII POSTI HAINA TOFAUTI NA BAADHI YA POSTI AMBAZO TAYARI ZIPO LAKINI ACHA TUCHANGIE............RA anao uwezo wa kutikisa kiberiti kwa kuwa ata wakina Sita wanagwaya atawaumbua kwa kukosa kwa uaminifu na ukweli ni kuwa wanamuogopa sana atawazidi na kutoa mapungufu ya tume na makosa na usanii wa tume ya mwakyembe.
 
mi hata sielewi kinachoendelea nahisi kidhungudhungu, swali langu ni pinda, ambaye anakaimu nafasi, sitta ambaye ndo spika wa Bunge na rostam ambaye ni mbunge, intetions zao ni nini? kati yao kuna maslahi binafsi na ya taifa so far sioni chochote katika maslahi ya taifa kila mtu anajaribu kuhakikisha upande anaosimamia huko salama, hadi hapo kikwete na serikali yake watakapokuja na msimamo unaoeleweka, in meantime siwezi hata kuanza kumhukumu rostam kwasababu sijui chui yupi, kondoo yupi, mi nawaona wote machui tu! yaani am furious kupita maelezo, at the end of it all i dont know how kikwete na ccm na wote wanaohusika na madaraka ktk nchi wakavyoanza kujustify yote haya i mean this is too much, good thing yanaanza kujitokeza.

...mama Poroko chukua tano! hii naona ndio ile inayoitwa spin-machine 'at its best', yaani 'wanatuchezesha' mduara weeee kisha haoooo wanatuachia vumbi! ama kweli Tanzania eeh, nchi yangu eeeh!!!...
 
tatizo ni CCM haitaki kuwawajibisha wanachama wake

...na wanaopenda mpaka chongo wakaita kengeza, yaani wale wanaowapa ushindi wa kishindo hata wale wabunge wanaoonekana dhahiri hawakutufaa, hawajatufaa na wala hawatakuja tufaa huko tunapokusudia kwenda...

2010 sio mbali, sitaona ajabu hawa hawa 'wabunge' leo hii tunaowaita mafisadi wakapita tena kwa kishindo, maana wapiga kura kwa kusahau siye, mnh!!!
 
Ajiuzulu tu! Kwanza kuna lipi la maana ambalo amewafanyia watu wake wa Igunga? Spika amwajibishe? Ampe adhabu ya kuzuiwa kushiriki kwenye vikao vya bunge kwa mkutano mzima, kama alivyofanya kwa Zitto! La sivyo tutasema ni upendeleo! Ndani ya bunge hakuna 'huyu ni mbunge wa CCM' au 'huyu ni mbunge wa CUF" au 'huyu ni mbunge wa TLP'! Wote ni wabunge!

Mbona wabunge wenyewe hawabaguani?

Spika anawajibika kumsimamisha kushiriki vikao vya bunge. Au ni lile suala la mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa binadam haramu?

./Mwana wa Haki
 
Nadhani tuwe objective ili tupate habari kamili hapa,sasa kama fisadi anatupa upande mwingine wa shilingi then tunaonyesha wazi kumpinga na kumwambia anamsemea muiran pamoja na kuita magazeti yake kuwa ni new habari corruption haiondoi haki yake ya kusema ukweli.....Mimi nachojua ni kuwa kwa taratibu za ccm ni ngumu sana kwa mtu kama rostam kuzungumza nje ya bunge kama Slaa kwa kuwa ule ni uamuzi wa kamati ya uongozi ambayo ni ya chama,naye ni mjumbe wa kamati kuu ya ccm.Hivyo hatua aliochukua ni sahihi...hapo msaliti ni Sita kwa nini hakupeleka kwa wabunge hoja na akaipeleka ccm.aliogopa kuumbuliwa.???????????

Kwa kwa Dr. Slaa urahisi ulikuwa wapi?Kinachohitajika ni nia tu ya kusema kilicho kweli.Tusidanganyane.Rostam Aziz hana jipya lolote la kusema isipokuwa kijaribu kusalvage his political career for his personal gain.Kama angekuwa anasukumwa na uzalendo na upendo wa kweli kwa wananchi angekuwa bold enough na kusema enough is enough akamwaga mambo hadharani.Mbona Mrema alithibutu kipindi kile?


Don't that much cheap.tafadhali jaribuni kutazma mambo kwa uhalisia.
 
Mpuuzi mkubwa huyu, amechangia sana kudestabilize nchi yetu, ashukuru mungu hatuna jazba kama za waganda, yeye angekuwa wa kwanza kutimuliwa. Anadhani anaweza kuwanunua watanzania wote!
 
JAPO HII POSTI HAINA TOFAUTI NA BAADHI YA POSTI AMBAZO TAYARI ZIPO LAKINI ACHA TUCHANGIE............RA anao uwezo wa kutikisa kiberiti kwa kuwa ata wakina Sita wanagwaya atawaumbua kwa kukosa kwa uaminifu na ukweli ni kuwa wanamuogopa sana atawazidi na kutoa mapungufu ya tume na makosa na usanii wa tume ya mwakyembe.

Huyu Rostam hana chochote ila hapa ni strategy ya sisiemu ya kumpa sifa za bure Rostam. Kama ana mambo kwa nini asitumie magazeti yake ya Rai, mtanzania, majira na mengine kujisafisha?

Kwani zile pesa alizompa Balile na wenzake kumsafisha zimeishia wapi?
 

Kwa kwa Dr. Slaa urahisi ulikuwa wapi?Kinachohitajika ni nia tu ya kusema kilicho kweli.Tusidanganyane.Rostam Aziz hana jipya lolote la kusema isipokuwa kijaribu kusalvage his political career for his personal gain.Kama angekuwa anasukumwa na uzalendo na upendo wa kweli kwa wananchi angekuwa bold enough na kusema enough is enough akamwaga mambo hadharani.Mbona Mrema alithibutu kipindi kile?


Don't that much cheap.tafadhali jaribuni kutazma mambo kwa uhalisia.

UWEZO WAKO NI MDOGO SANA WA KUCHANGANUA NA KUTOFAUTISHA MAMBO,SLAA ALIWEZA FANYA VILE KWA KUWA ALIEMZUIA NI SPIKA NA SIYO CHAMA CHAKE,RA NI TOFAUTI KABISA HAPA KWA KUWA ALIEMZUIA NI KIKAO CHA CHAMA CHAKE THEN WABUNGE WAKAPEWA TAARIFA..MFANO WAKO WA MREMA NI MDOGO SANA NA MREMA ANA MATATIZO MAKUBWA YA AKILI.
 
Na wewe unaona uwezo wako wa kuchanganua mambo ni mkubwa.....acha kuchekesha watu hapa
 
MFANO WAKO WA MREMA NI MDOGO SANA NA MREMA ANA MATATIZO MAKUBWA YA AKILI.

Mkuu,

Unapaswa kuwa mwangalifu unapoangamiza kinadharia uwezo wa kiakili wa Mrema hata kama una mawazo ya kidikteta ambayo huwa ni ya mwisho.

Sasa unaweza kutoa ufafanuzi wenye vielelezo kuthibitisha hoja yako hio kwamba Mrema ana matatizo (makubwa) ya akili?
 
Inashanga saana kuona kwamba vipi Spika ameogopa hoja ya Rostam iwasilishwe,inaonyesha wazi jinsi Serikali haitaki wananchi tuelewe ukweli wa yaliotokea kuhusu uisadi wa EPA.
 
mama Anna makinda is equal to PIUS.This equivalent to vodacom..where VODACOM is the SI UNIT Of relationship btn EL,RA..kama kunakuwa na wabunge wa viti maalum kama hawa nashawishika kutoa pendekizo wasiwepo sababu anawakilisha mawazo mgando siku zote
 
UWEZO WAKO NI MDOGO SANA WA KUCHANGANUA NA KUTOFAUTISHA MAMBO,SLAA ALIWEZA FANYA VILE KWA KUWA ALIEMZUIA NI SPIKA NA SIYO CHAMA CHAKE,RA NI TOFAUTI KABISA HAPA KWA KUWA ALIEMZUIA NI KIKAO CHA CHAMA CHAKE THEN WABUNGE WAKAPEWA TAARIFA..MFANO WAKO WA MREMA NI MDOGO SANA NA MREMA ANA MATATIZO MAKUBWA YA AKILI.

Kaka naona umeamua kutukana Taifa, mrema ni mtu makini sana na ndo maana alipoona ufisadi umemzidi akamua kuondoka CCM, NCCR aliondoka wakati mapandikizi ya mafisadi yalipomzidi mfano Mabere marando, TLP aliweza kuwafukuza mafisadi mwenyewe mfano Ngawaiya. kuwa makini unapotaja majina ya watu, kama anaweza ajitoe katika chama na aweke wazi maelezo yake kama anamini yeye ni safi kama anavyofikiri.
Jamani hii ni makusudi wananchi wasijue kilichokuwamo kwenye maelezo ya RA, kama yalikuwa maelezo yaleyale aliyotoa kwa mdomo kwanini walimkalia kikao cha kamati ya uongozi. Tusikubali mpaka tuone maelezo ya RA kuna siri kubwa kwenye maelezo hayo, inawezekana ikawa ndo ukombozi wa Mtanzania.
 
Back
Top Bottom