Kwa kutumia Kanuni za Bunge, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ameyazuia maelezo ya Rostam kwa kwa kile kinachoelezwa na watoa habari wetu kwamba ni kulinda maslahi na hadhi ya Bunge, lakini pia kulinda mshikamano ndani ya Bunge na ndani ya CCM.
Uamuzi wa kumzuia Rostam kuwasilisha maelezo yake ulifikiwa baada ya vikao vya wabunge wa CCM wakiongozwa na Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa chama hicho na baadaye kamati ya wabunge wote wa CCM. Rostam ni mjumbe wa vikao vyote kutokana na wadhifa wake wa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM.
Pamoja na kutowekwa hadharani kwa maelezo ya Rostam, yeye mwenyewe amenukuliwa katika baadhi ya vyombo vya habari akisema kwamba alikuwa na maelezo yenye nguvu na ambayo yangebainisha kuwa yeye ni mtu safi ambaye hakuhusika kwa namna yoyote na mkataba wa Richmond pamoja na kuwa na uhusiano wa kibiashara na kampuni iliyorithi mkataba huo ya Dowans.
Wana JF Haya maelezo ya RA yaelekea ni mazuri kuyapata hapa "tutayapataje mwenye nukunuku ayaweke hapa tayachambue Fisadi kiongozi huyu"