Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Rostam Aziz of New Habari Corporation: The facts

Kuwekeza kwa RA ili kumsaidia JK kuingia ikulu hakutoshi kuhesabiwa kuwa uovu. Ila kinachogomba ni namna anavyoramba rasilimali za nchi akilindwa na serikali tunayoilipa kwa k odi zetu.

Kinachoongeza uchungu ni uhakika kuwa sehemu kubwa sana ya fedha anazochhuma Tanzania anazikimbiza nje ya nchi haraka sana. Fedha hizo zingekuwa hapa nchini katika mzunguko zingesaidia wengi.

Kibaya zaidi mtizamo wa namna anavyopoka unaowapa watanzania wenye uwezo wa kawaida wa kufikiria na kutathmini hisia kuwa wao wamezaliwa watumwa katika nchi yao.

nk nk nk nk
 
Mimi nafikiri RA si wa kumlaumu kabisa...kama muwekezaji yoyote anataka pesa yake irudi na faida....Wa kulaumiwa ni JK na WaTanzania...
 
Naomba Wana JF mnielimishe na kunifahamisha.
Mhe Rostam Aziz aliwekeza sana ili JK aingie ikulu...na sasa ni wakati wake wa kuvuna...Kwa nini mnamlaumu.????..Je ingekuwa wewe umewekeza hivyo ungepeleka mambo yaendaje???
Je alaumie RA au JK au WaTanzania waliomchagua JK???

NAOMBA JIBU BILA JAZBA....

RA Hakuwekeza, bali makampuni yake yalitumika kuchota fedha za umma zilizomweka JK, isitoshe si fedha zote zilizopitia kwenye makampuni yake fake zilitumika kumweka JK, bali nyingine alibaki nazo na bado anazo, hakuna wa kumdai, kwani ana siri nyingi juu ya uhuni wa kuibia umma ulivyofanyika, huyuu ni kumkolimba tu au mnasemaje wadau
 
Sasa ndo tunamkumbuka Nyerere alipokuwa akikemea kuchagua viongozi wenye makundi. Tatizo kubwa lililo jitokeza kwa kikwete ni kuanza kulipa fadhila, wat kama Thomas Apson Mwang'onda, Husna Mwilima, Betty Mkwasa ndugu zanguni hawa ukitafuta mchango wao mkubwa mpaka wateuliwe kwenye nyadhifa hizo ulikuwa upi kama siyo fadhila.Hilo ndo tatizo ambalo litazidi kutuandama na hakuna jinsi ya kujikwamua kwani watanzania tumezid woga.Leo mashambulizi aliyopewa DR.Slaa kwa kufunua maovu hakuna watu wanaosimama naye kwa nguvu zote na kuiambia serikali kwamba isidhubutu kumgusa kwa lolote.Tatizo kubwa ni watu waliojipandikizakatika chama baada ya chama cha mapinduzi kuondoka na mwasisi wake Nyerere.Leo hii chama kina mamuluki watupu.
Watanzania tujifunze kwamba Kaunda na chama chake walipong'olewa zambia mpaka leo imedumu hasa wakati wa marehem Mwanawasa.Kwa hiyo Tanzania bila CCM nayo inaweza kuwepo.Amerika imeng'oa upuuzi pale wananchi hasa wale ambao walikwisha kata tamaa walipo hamasishwa wakapige kura ili wagoe upuzi huo.Sasa wasomi wacho kikuu mnaofukuzwa kla siku,machinga, walimu mnaonymwa mishahara yenu huku kuna watu wanapata posho ya mshahara wa mwalimu wa mwaka mzima muko wapi kuungana ili kuondoa aidha wana mtandao waltufikisha hapa tulipo au kukiondoa chama kizima maana kimeshindwa kujisafisha tutaimba hadi lini.
 
Vyama vya upinzani viungane na kumsimamisha mugombea urais mmoja na pia kila jimbo asimame mbunge mmoja tu wa upinzani anayekubalika eneo hilo na vyama vyote viwe nyuma yake hapo bila shaka CCM itaaga dunia, bila hivyo tutaendelea kupiga kelele
 
JK kuingia Ikulu kwa fedha ya RA na Kagoda yake sio issue kwa sasa. Issue ni baada ya kuingia anafanya nini.
Kwa upande wangu, ile pesa ni kama sadaka. Ukitua sadaka kanisani/msikitini, hiyo sadaka itafanya kazi ya Mungu, haijalishi hiyo pesa wewe uliipata wapi, uliiba, umeokota au umeitokea jasho.

Kwa kawaida, anayekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, kwa vile CCM imepokea ufadhili wa RA, sio kosa kwa CCM wala haina haja ya kujua RA alitoa wapi fedha hizo kama ilivyo kwa UV-CCM kupokea milioni 400 za Tanil Somaiya, ili kufanyia uchaguzi wake mkuu. Sio issue ya UV-CCM kujua Tanil, katoa wapi pesa.

Baada ya ufadhili wote wa RA na Tanil, baadaye ndiipo ugandua kuwa walituibia, hata kama ni wewe ndio JK, ungefanya nini?.
Inabidi anyamaze tuu kama alivyojinyamazia na mwakani ni kwa kishindo tena, this time bila fedha ya RA, bali kwa kura yako, yangu, yake, yenu, yetu, zetu, hata kama mimi na wewe hatutampigia, yeye na yule watampigia, 'the winner takes it all' ndio atakuwa rais wako kwa kura yako na yangu, au bila kura yako na yangu.
 
Ukitembea na mwizi utaitwa mwizi.
 
RA na wengineo hawakutoa pesa zao (japo wachache wametoa zao-akiba zao). Kilichofanyika ni kufacilitate kuchukua pesa za umma kupitia kwao(EPA, contracts nk) na kugawa kidogo kwa ajili ya uchaguzi kuanzia mchakato!!! wa kupata wagombea !!! Kwa hiyo si kweli wali-invest pesa !!!!!!! labda muda wao tu-na amabao baada ya deals walikeep pesa yao na ku-release kiasi kwenye uchaguzi, hivyo muda wao walijilipa upfront.
 
Unawaibia watu maskini wanaokufa kwa njaa--yet duniani ukipata kuishi miaka 70 au 80 ni bahati ya Mungu!

yani umeongea,ingekuwatunaishi atleast 500 yrs inge-sound kidogo to me but....bp and other stuff....ukifika 60-70 unabahati kweli.wapumbavu sana-wizi wa kijinga! unatia kizazi umaskini wa kutisha kwaajili tu familia mmoja!
 
hatuwezi kumwacha kamwee, mpaka atakapoacha ufisadi wake katika nchi yetu.
 
Duh! Master, umefanikiwa kuwa divert.......

Ila sisi tunarudi kule kule kwa NSSF na Kapuya na RA!!
 
Itakuwa ajabu tukimsifia mtu anayedhulumu kwa kigezo kuwa nchi jirani ya Kenya imepitiliza kwa vitendo hivyo. Unajuaje kama akiachiwa aendelee kufanya huu uharamia atawapiku Kenya wiki mbili zinazokuja? Naona watu wameshamchoka jamaa mana hadithi zake kila kukicha ni zile zile za kuiharibu nchi yetu. Hatuwezi kumpumzisha kwa kazi ambayo hatujamtuma..ameianza mwenyewe na aminia ataimalizia.
Duuh! Kweli anayelala usimwamshe mana ukimwamsha utalala wewe.
 
Hivi sheria ya vyombo vya habari ndiyo basi? TUNAZUNGUKA KAMA "TENGALUZI" YA DR(???) MZINDAKAYA!
 
Tunaamini vyombo vya habari ni nguzo ya nne ktk kuendesha nchi. Je navyo vikitiwa mfukoni km bunde letu ktk mwaka 2006/2008 tutafika? Mie sijui labda tumwulize mzee wa CCM Makwaia Wa Kuhenga
 
Mimi nafikiri RA si wa kumlaumu kabisa...kama muwekezaji yoyote anataka pesa yake irudi na faida....Wa kulaumiwa ni JK na WaTanzania...
Mstahiki hapa kinachouma sio kua alitumia pesa zake kumuweka madarakani JK bali kitendo cha kuiba pesa zetu au kutumiwa kuiba pesa zetu HILI LINAUMA ZAIDI .Mfano chukulia ya kwamba mwizi kakuibia shilingi 1000 alafu mwizi huyohuyo anakusaidi shilingi 200 kama nauli kukufikisha nyumbani ni wazi utamshukuru na kumkumbuka kwa msaada wake,lakini ukija kugundua ya kua ni yeye ndie mwizi aliekuibia ni wazi mtazamo wako utakua mwingine.Kitu kingine ambacho naweza kukubaliana nawe inawezekana RA sio mwizi bali ametumiwa na CCM pamoja na JK kutuibia kwa maana nyingine mwizi hapa ni CCM pamoja na JK hii inadhihilishwa na ukimya na kumkingia kifua kwa CCM na JK MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Rostam alikuwa Mweka Hazina wa CCM tangu lini; na JK alimchukua lini kuwa Meneja wa kampeni yake ya urais?
 
Mwanakijiji,

Mkuu wangu navyofahamu mimi Rostam alikuwa mweka hazina wa CCM toka wakati wa Mkapa na ndiye aliyeshughulika na kampeni za uchaguzi..

Nakumbuka vizuri sana wakati FMES alipokuwa akitupa data za huyu jamaa kabla ya uchaguzi wa Kikwete, how powerful he is, na sisi wote humu tulikuwa tukimbishia sana FMES kuwa mtu mmoja hawezi kuwa na nguvu kama hizo kwa kutumia fedha..nikaingia site ya CCM na kuona alikuwa party treasurer..

Sina kumbukumbu tu ni lini Marehemu Salome Mbatia alishika nafasi ya Rostam na kisha kurudi tena kwa Rostam kwa sababu marehemu hayupo tena duniani kukana lolote linalohusiana na madai ya Rostam...Bila aibu mtu huyu yuko radhi kumlaumu marehemu kuwa ndiye mhusika mkuu wa mikopo ya EPA inapofikia swala la chama na kibaya zaidi chama kimemtupa kabisa marehemu, wameshindwa kumtendea haki kwa kuweka rekodi sawa...

Taarifa hizi zimefutwa kabisa na sii rahisi kuzipata tena isipokuwa through watu wa CCM wenyewe..
 
....
Sina kumbukumbu tu ni lini Marehemu Salome Mbatia alishika nafasi ya Rostam na kisha kurudi tena kwa Rostam kwa sababu marehemu hayupo tena duniani ......

Lahaulawalakuwata, msalie mtume shehe, unapotosha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom