Kaniki1974
JF-Expert Member
- Dec 2, 2008
- 352
- 22
Watanzania si wakulaumiwa bali wanaokichagua CCM chama kisicho na dira.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba Wana JF mnielimishe na kunifahamisha.
Mhe Rostam Aziz aliwekeza sana ili JK aingie ikulu...na sasa ni wakati wake wa kuvuna...Kwa nini mnamlaumu.????..Je ingekuwa wewe umewekeza hivyo ungepeleka mambo yaendaje???
Je alaumie RA au JK au WaTanzania waliomchagua JK???
NAOMBA JIBU BILA JAZBA....
RA Hakuwekeza, bali makampuni yake yalitumika kuchota fedha za umma zilizomweka JK, isitoshe si fedha zote zilizopitia kwenye makampuni yake fake zilitumika kumweka JK, bali nyingine alibaki nazo na bado anazo, hakuna wa kumdai, kwani ana siri nyingi juu ya uhuni wa kuibia umma ulivyofanyika, huyuu ni kumkolimba tu au mnasemaje wadau
Sasa ndo tunamkumbuka Nyerere alipokuwa akikemea kuchagua viongozi wenye makundi. Tatizo kubwa lililo jitokeza kwa kikwete ni kuanza kulipa fadhila, wat kama Thomas Apson Mwang'onda, Husna Mwilima, Betty Mkwasa ndugu zanguni hawa ukitafuta mchango wao mkubwa mpaka wateuliwe kwenye nyadhifa hizo ulikuwa upi kama siyo fadhila.Hilo ndo tatizo ambalo litazidi kutuandama na hakuna jinsi ya kujikwamua kwani watanzania tumezid woga.Leo mashambulizi aliyopewa DR.Slaa kwa kufunua maovu hakuna watu wanaosimama naye kwa nguvu zote na kuiambia serikali kwamba isidhubutu kumgusa kwa lolote.Tatizo kubwa ni watu waliojipandikizakatika chama baada ya chama cha mapinduzi kuondoka na mwasisi wake Nyerere.Leo hii chama kina mamuluki watupu.
Watanzania tujifunze kwamba Kaunda na chama chake walipong'olewa zambia mpaka leo imedumu hasa wakati wa marehem Mwanawasa.Kwa hiyo Tanzania bila CCM nayo inaweza kuwepo.Amerika imeng'oa upuuzi pale wananchi hasa wale ambao walikwisha kata tamaa walipo hamasishwa wakapige kura ili wagoe upuzi huo.Sasa wasomi wacho kikuu mnaofukuzwa kla siku,machinga, walimu mnaonymwa mishahara yenu huku kuna watu wanapata posho ya mshahara wa mwalimu wa mwaka mzima muko wapi kuungana ili kuondoa aidha wana mtandao waltufikisha hapa tulipo au kukiondoa chama kizima maana kimeshindwa kujisafisha tutaimba hadi lini.
JK kuingia Ikulu kwa fedha ya RA na Kagoda yake sio issue kwa sasa. Issue ni baada ya kuingia anafanya nini.
Kwa upande wangu, ile pesa ni kama sadaka. Ukitua sadaka kanisani/msikitini, hiyo sadaka itafanya kazi ya Mungu, haijalishi hiyo pesa wewe uliipata wapi, uliiba, umeokota au umeitokea jasho.
Kwa kawaida, anayekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, kwa vile CCM imepokea ufadhili wa RA, sio kosa kwa CCM wala haina haja ya kujua RA alitoa wapi fedha hizo kama ilivyo kwa UV-CCM kupokea milioni 400 za Tanil Somaiya, ili kufanyia uchaguzi wake mkuu. Sio issue ya UV-CCM kujua Tanil, katoa wapi pesa.
Baada ya ufadhili wote wa RA na Tanil, baadaye ndiipo ugandua kuwa walituibia, hata kama ni wewe ndio JK, ungefanya nini?.
Inabidi anyamaze tuu kama alivyojinyamazia na mwakani ni kwa kishindo tena, this time bila fedha ya RA, bali kwa kura yako, yangu, yake, yenu, yetu, zetu, hata kama mimi na wewe hatutampigia, yeye na yule watampigia, 'the winner takes it all' ndio atakuwa rais wako kwa kura yako na yangu, au bila kura yako na yangu.
Unawaibia watu maskini wanaokufa kwa njaa--yet duniani ukipata kuishi miaka 70 au 80 ni bahati ya Mungu!
Mstahiki hapa kinachouma sio kua alitumia pesa zake kumuweka madarakani JK bali kitendo cha kuiba pesa zetu au kutumiwa kuiba pesa zetu HILI LINAUMA ZAIDI .Mfano chukulia ya kwamba mwizi kakuibia shilingi 1000 alafu mwizi huyohuyo anakusaidi shilingi 200 kama nauli kukufikisha nyumbani ni wazi utamshukuru na kumkumbuka kwa msaada wake,lakini ukija kugundua ya kua ni yeye ndie mwizi aliekuibia ni wazi mtazamo wako utakua mwingine.Kitu kingine ambacho naweza kukubaliana nawe inawezekana RA sio mwizi bali ametumiwa na CCM pamoja na JK kutuibia kwa maana nyingine mwizi hapa ni CCM pamoja na JK hii inadhihilishwa na ukimya na kumkingia kifua kwa CCM na JK MUNGU IBARIKI TANZANIAMimi nafikiri RA si wa kumlaumu kabisa...kama muwekezaji yoyote anataka pesa yake irudi na faida....Wa kulaumiwa ni JK na WaTanzania...
....
Sina kumbukumbu tu ni lini Marehemu Salome Mbatia alishika nafasi ya Rostam na kisha kurudi tena kwa Rostam kwa sababu marehemu hayupo tena duniani ......