figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za Taifa Group, Rostam Azizi
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA
MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za Taifa Group, Rostam Azizi anapenda kuuhakikishia umma kwamba hana uhusiano wowote na asingependa kuhusishwa kwa namna yoyote na mtu anayejiita Kigogo katika mitandao ya kijamii.
Sambamba na hilo, ndugu Rostam hakubaliani na tuhuma kadha wa kadha zisizo za msingi wala ukweli ambazo huyu bwana amekuwa akizielekeza kwake binafsi na wakati mwingine kwa viongozi wa serikali na Watu wengine kadhaa.
Hatua ya mtu huyo, kufuatilia kazi za kampuni yetu ya Taifa Gas na wakati mwingine kupongeza utendaji wake kazi haipaswi kuonekana kwamba Taifa Gas inafahamiana naye au pengine kumtumia.
Ikumbukwe kwamba, wakati fulani mtu huyo huyo alipata kumjeruhi ndugu Rostam na mke wake wakati ule wa mlipuko wa COVID 19 kwa kuandika taarifa ambazo baadaye zilikuja kubainika hazikuwa na ukweli wowote.
Kwa sababu hiyo basi mwenyekiti wetu ndugu Rostam Azizi, anawasihi Watanzania wanaotumia na kufuatilia mitandao kuzingatia misingi ya utu, uwajibikaji na kuwa makini na yale wanayoandika au yanayoandikwa huko.
Pia kupuuzia uzushi na uongo unaoenezwa mitandaoni.
Mara kadhaa kumekuwa na taarifa katika mitandao za kuua na kufufua watu zinazotengenezwa mithili ya hadithi za kufikirika za Alfu Lela Ulela na wakati mwingine kuwatuhumu watu kwa wizi huku wengine wakitengenezwa waonekane ni malaika.
Haya ni mambo ya kukemea kwa nguvu zetu zote.
Imetolewa na
Ofisi ya Mwenyekiti Mtendaji
Taifa Group
Mei 5, 2023
Plot No. 77, Kipawa Kiwalani
Nyerere Road, P.O. Box 75627
Dar es Salaam Tanzania