Rosti viazi na samaki wa kukaanga

farkhina

Platinum Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
14,568
Reaction score
16,917
Mahitaji
Kwa ajili ya supu

  • Viazi 4 vikubwa katakata round
  • Nyanya 2 kubwa katakata
  • Kitunguu maji 1 kikubwa
  • Kitunguu saumu 1 tablespoon...
  • Tangawizi 1 tablespoon..
  • Bizar ya pilau 1/2 teaspoo.
  • Mdalasini 1/2 teaspoon
  • Curry powder 1/2 teaspoon (sio lazima)
  • Nyanya ya kopo 1..
  • Pilipili mboga 1
  • Karot 1
  • Chumvi kiasi
  • Limau 1

Namna ya kutaarisha
  • Kaanga viazi vikiwiva weka pembeni..
  • Katika sufuria kaanga kitunguu maji Kwa dakika 10
  • Weka pilipili mboga na karot
  • Kaanga vikivaribia kuwiva weka nyanya kaanga vizuri
  • Weka nyanya ya kopo na limau
  • Ikiwiva weka viazi vichanganyike na rosti...taratibu viazi visivurugike
  • Epua
Samaki wa kukaanga

Mahitaji
  • Samaki wa vipande
  • Pilipili ya kuwasha kiasi upendacho
  • Pilipili manga 1 teaspoon
  • Tangawizi 1 teaspoon
  • Kitunguu saumu 1 teaspoon
  • Chumvi kiasi
Namna ya kutayarisha
  • Safisha vizuri samaki wako
  • Mueke viungo vyote...muaxhe 30 min _-1 hour ili akolee viungo
  • Weka pan yako mafuta
  • Kaanga samaki
  • Akiwiva weka kwenye bakuli lako la mchuzi mimina roasti ya viazi juu yake...
  • Tayari kwa kuliwa.


Michango ya wadau

----
 
Ahsante, nitalifanyia kazi hili somo nikipata wasaa.
 
Yaani ni cha kawaida sana.. Thanx my dear..
 
Thanks da fa. Apo kwa kuongezea wanaopenda mabilingani, pia unakata round bila kumenya maganda.

Na samaki wa vipande au hata mzima sio mbaya. Km changu.

Mie hupenda changu au nguru
 

Da #farkhina asante kwa mapishi, mie hupika sana mbatata jap hupenda kuzila na rosti la nyama ila leo nimejifunza style mpya!

Nauliza pale mwanzoni viazi unavikaanga na mafuta si ndio au sijaelewa??nimependa upishi huu

Miye huwa nakaanga rosti vizuri halaf viazi sikaangi huviweka baada ya rosti kukaribia kuiva kisha nikafunika hadi vyote vikaiva.ila ntajaribu hii style ya kukaanga kwanza viazi nimeipenda
 
Thanks da fa. Apo kwa kuongezea wanaopenda mabilingani, pia unakata round bila kumenya maganda.

Na samaki wa vipande au hata mzima sio mbaya. Km changu.

Mie hupenda changu au nguru

Yeah na mabiringani sema mie siku nayo hapo ikikaribia kuwiva ukitupia kotmir inazidi kupendeza
 


Yeah unakaanga viazi na mafuta kwanza then unaweka pembeni
 
Mamie na huu mwezi wa Ramadhani unavyokaribia, yani sijui hata umejuaje kama hiyo ndo futari pendwa yangu, yani napenda mbatata balaa...nashukuru kwa kuniongezea ujuzi wa kuchanganya na samaki.
 
Asante sana
Naandikaje...kazi kwangu kurejea kwenye hii note...
Leo taandaa hili pishi
Karibuni
 
Swadakta da shosti.........na mi nitajaribu na fish maana sikuzote inakuwaga na nyama tu. Nakupendaje sasa my dia!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…