Router za TTCL

Unauhakika hizo nchi mobile data ni ghali? Au unataka kudanganya watu hapa?? Unajuwa kama kuna watu wengi humu wanaishi hizo nchi,mambo ya ghali walishaachana nayo labda huko India sijawahi fika.
 
Kuna muda hii router huwa natamani niipige ngumi vifurushi ghali afu internet connection ina sua sua,kazi ya kufanya dakika sifuri unatumia nusu saa. Hiyo mitandao ya simu wanafikiri kila mtu anaishi city center.Hapa najichanga niagize zangu star link kit hapo nairobee.
 
Kwani inafungwaje mkuu? Inafungwa kama nyaya za simu ya upepo?
Fiber ni miundombinu mingine, sometime inakuja kama mashimo ya maji ya Ardhini, sometime inakuja na nguzo etc. Ukiangalia nje kwako unaweza jua kama wamepita ama La kwenye nguzo za kawaida ama za umeme utaona waya Extra.
 
Ila hao halotel huduma zao mbovu sana mkuu. Sitaki hata kuwasikia.
5G sasa advantage yake ndio hio, ina uwezo hata wa kuhudumia uwanja kama Taifa ukiwa umejaa, unless huo ubovu wa Halotel sio wa Kimtandao.
 
TTCL Ni ipo slow sana na Kuna muda inakata kabisa nimeitoa inazingua...kwanza hadi waje kukufungia umeimba nyimbo zote...kama upo mbweni na maeneo ya jirani bora uchukue fiber ya tigo au ufunge dedicated japo ni expensive kidogo ila it's worthy
 
Inategemea, kila mtu anaangalia matumiz yake na gharama.

Mfan kuna mtu anawz jiunga unlimited lakin mwez mzima hamalizi hata gb 10.. na analipa sawa na mtu anaetumia TB 2.
 
Ndio lipi hili bundle la unlimited la mwaka.
Sio Unlimited in terms of matumizi.. ni unlimited interms of expiration.. kingine unaweza topup ina jirenew kulingana na tarehe ya mwisho ya kujiunga.

Hii nzuri kwa wale wanaosurf kawaida mtandaoni kwa ishu za kawaida kama kuingia YouTube, Jf, IG etc..

Ila kwa wale wanaodownload movie na games si rafiki.
 
Sisi bongo internet serikali yetu imetuminya aisee toka walivyotoa unlimited data za usiku nili walaani sana
 
Alianza Vodacom 115,000 kwa 20mbps, akaja 120,000 kwa 30mbps, Airtel akashusha hadi 110,000 30mbps na akatoa 70,000 kwa 10mbps, Tigo nao wakajibu 70,000 10mbps. Tetesi Halotel naye anakuja na 5G soon na wao wanakuja Kuvunja bei.
Leo watu wa halotel wamenitembelea nyumbani(kigamboni/mjimwema) wamenitangazia huduma hii, 20MBPS ni 79k, 40mbps ni 95k kwa mwezi.
 
India huwezi compare na bongo, daah nilikuwa pande hizo nina unlimited calls na watu wa kupigia sina🤣🤣
 
Coverage yao unaifahamu hawa mkuu?
Almost Nchi nzima Halotel ana fiber, walipokuja walitandaza fiber kote, lakini wakawa wanazitumia tu na minara yao. Jumla wana km 18,000 za fiber kwa wakati huo wanaweka nafkiri hata TTCL alikua hawafikii. Naona wanaanza kuuza sasa hivi sijajua eneo gani na eneo gani wanauza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…