Usichanganye fiber na 5G mkuu, nchi hizo unazozitaja mobile data kama 5G ni ghali sana ila wana Fiber network nzuri. Fiber ni rahisi kusambaza eneo dogo ila nchi kubwa kama yetu ngumu, ila mobile network kama 5G it's possible ku cover maeneo mengi.
India ndio hao 6,000-9000 unapata unlimited, Indonesia Around $6 unapata Unlimited, Ufilipino na nchi nyingi za Asia zenye watu wengi 5G unlimited ni bei rahisi.
Jinsi tutakavyoongezeka kwenye 5G ndio jinsi bei itakavyoshuka, miundombinu tayari ipo na mkonga upo under utilised, mfano Airtel backbone yao ya 5G ni 180 terabytes per second, hapo inahitaji watu kama milioni 18 kwa speed ya 10mbps kujaza hio capacity, wanachaji 70,000 kwa capacity ya sasa ila watu wakiongezeka gharama ya backbone ni ile ile na wao watashusha bei.