1. Rwanda vivutio vya utalii ni aina na wajihi wa watu walopo hapo (Tutsi, Hutu & Watwa), eneo dogo, utawala wa kifalme uliohamishiwa kuwa utawala wa nchi, na mauaji ya kimbari
2. Utalii wa Israel ni kiimani, miundo mbinu iliyotumika na mitume pamoja na nabii Issa au Yesu kuwepo hadi sasa na kingine ni kubadili jangwa kuwa la kijani kwa kuhamisha udongo kutoka maeneo yenye udongo wenye rutuba kisha kuendesha kilimo kikubwa kuliko mataifa mengine ya kiarabu ambayo yako eneo moja la kijiogrofia na Israel (recreational)
3.Utalii wa Tanzania (Bara na Visiwani) ni wa vitu vya asili (mafuvu ya binadamu wa kale kuvumbuliwa huko Ngorongoro-Olduvai Gorge, makabila zaidi ya 123 bila kuwepo hata moja kutumia nguvu ya wingi kutawala nchi kama ilivyotokea Rwanda kisa cha mauaji ya rais Juvenal Habyarimana mwaka 1994 yakifuatiwa na mauji ya kimbari, mbuga za asili za wanyama na mimea, mito, maziwa na fukwe kongwe za bahari, miji mikongwe kwa historia ya utawala wa kijerumani, waarabu, himaya za kitemi kwa makabila mbalimbali, madini kama Tanzanite iliyogunduliwa na Mtanzania (mzee Ngoma) huko Mererani Manyarak Almasi huko Shinyanga, Dhahabu huko Mwanza, Geita, Shinyanga, Mara, Singida, Tabora na Morogoro, madini ya chuma, makaa ya mawe, madini ya ulanga, madini ya bati, madini ya nikeli, ajali ya meli MV Bukoba mwaka 1996 huko ziwa Viktoria, njia za misafara ya watumwa huko Kigoma, Ngome za kiutawala za kitemi huko Iringa-Mkwawa, Tabora-Isike, Mirambo, Shinyanga, Kilimanjaro-Mangi, Tanga-Kimweri, Kagera-Rumanyika, Ruvuma-Songea, Morogoro-Kingalu, Kigoma-Mwami Riyami wa Bayungu au Heru juu, nk